DR. Jakaya Kikwete: Mnyonge Mnyongeni!

Nini maana ya demokrasia huru? si kupiga kura kupitia boksi la kura bali pamoja na kuhakikisha utekelezaji wa ahadi 'manifesto' au ahadi zinazotolewa na chama tawala. Sasa ikiwa chama tawala kimeshindwa kutekeleza ahadi zake ktk uchaguzi 'wa-kidemokrasia' basi hapo demokrasia yetu haipaswi kupata hata chembe 'kiduchu' ya kusifiwa wala kujitambia.

Mfano, mfano matatizo makubwa katika sekta ya elimu (tazama video hapo chini) ni aibu kubwa kwa utawala wa Mh. Jakaya Mrisho Kikwete, tizama clip hii ya mwezi huu wa March 2012 na watoto wa shule na waalimu wao wanavyoteseka ktk mazingira magumu , tunasubiri chenji za ununuzi wa radar kuwapatia watoto hawa mazingira mazuri ya elimu.

Video kwa hisani ya Tangibovu wa YouTube

Wazo langu:
CCM na mwenyekiti wao taifa Mh Jakaya Mrisho Kikwete wangolewe kupitia sanduku la kura 2015, kwaniutawala wa CCM umeshindwa kutawala nchi(kuleta maendeleo ya wengi) pamoja ya kuwa inakusanya fedha nyingi za kodi na kugharamia matumizi ya anasa kama ununuzi wa magari ya kifahari 'mashangingi' n.k
 
Last edited by a moderator:
Hiyo ya Uvumilivu wa Demokrasia nakuunga mkono!

Uvumilivu wake umechanganyika na kutazama pembeni na kutojali. Tanzania inazidi kudidmia kwa tatizo la rushwa na uvunjifu wa sheria. Serikali yake imepata kigugumizi cha ajabu sana. Wanashindwa kabisa kukemea rushwa wakti wanaiona kila siku. Kwa mfano, ukienda Wizara ya Ardhi kupata Title Deed inakubidi utoe siyo chini ya milioni mbili ili faili lako litembee la sivyo sahau. Wafanyakazi wa serikali, wanaolipwa mishahara kutumia kodi za Watanzania wanatumia ofisi za serikali kuwanyonga Watanzania. Wao ni maconsultant wamepanga kwenye jengo la Wizara ya Ardhi lakini badala ya kulipa rent wanalipwa mshahara na Serikali.

Mimi sina kinyongo na Kikwete, lakini siupendi kabisa kabisa msimamo wake kuhusu rushwa. Wale akina Patel wa EPA wapo wapi? Majaji wa akina Mramba na Mgonja walijiuzuru? au wamekufa?
 
Hivi bila ya demokras ya jk Sabodo angeweza wapi kupata ujasiri wa kuwahonga wachagga mamillion?
 
UVUMILIVU wa demokrasia ndio kitu gani mkuu wangu?.. Una maana JK anatakiwa kupambana na adha za Demokrasia? au unachotaka kusema ni uvumilivu ktk uhuru na haki za watu kuhabarishana. Na akipiga vita uhuru wa habari sii ndio atajiharibia zaidi, wewe huoni kwamba toka mwaka 2005 duniani kote, uhuru huu umepewa kipaumbele zaidi kuliko miaka ya nyuma?. Wakati wa Mkapa vita kubwa ilikuwa Rushwa kwa nchi maskini lakini hapakuwepo nguvu kubwa ktk uhuru wa habari, waandishi wengi walifungwa ama kuuliwa na ndio maana imesisitizwa zaidi kutokana na watu kama Mkapa na wengineo.

Kama wewe FMES unatembea na mke wa mtu na watu wanakusema sana kwa kutembea na mke wa mtu. Je, utavulimia lawama hizo au utapambana nazo? Kwa mtazamo wangu JK anakubali yote yanayozungumzwa kwa sababu yana ukweli na makosa yapo vile vile isipokuwa hajui afanye nini maana kashindwa kujizuia na Ufisadi. Ubabae wa kina Mkapa ulisaidiwa sana na kutokuwepo mkazo mkubwa ktk uhuru wa habari na ndio maana aliweza kunyamazisha watu. Miaka yake ndio ilikuwa mwanzo wa hizi Blog, Hi5, facebook na kadhalika lakini sasa hivi hawezi kuzuia tena hata Assad akashindwa.

2. Middle class gani FMES watu wanaishi mjini kiujana ujanja tu. Wee unaweza kuamini ya kwamba wakati wa Nyerere asilimia kubwa ya wananchi walikuwa na ajira kuliko leo hii?..Sasa utaweza vipi create middle class ikiwa asilimia kubwa ya wananchi hawana kazi na waliokuwa nayo ni vipanga hawanunui vitu kwa fedha yao mfukoni bali waliyopiga mishemishe. Hakuna mtu anaishi kwa mshahara wake bali kufisadiana, unapigwa panga hapa na wewe unaelekeza mashambulizi yako sehemu nyingine. Na kweli mkulu amekaa kimya akitazama sinema inavyoendelea.
 
Kama kile wanachodai wananchi au vyama vya upinzani ni haki yao, then sioni sababu ya kumpa credit JK kwamba mvumilivu wa demokrasia. Kama kile kinachoandikwa magazetini kina ukweli kwa 100%, then sioni kama kuna sababu ya kumpa credit JK.

Tukubaliane kwamba zama za u-dictator zimepita, sasa hivi kiongozi yeyote akijaribu u-dictator anaweza kuishia kuua watu na akajisogeza The Hague. Wananchi wa Tanzania wamepigika sana wamefika mahali wakibanwa kidogo tu mlipuko wake unaweza kuwa na athari kubwa sana. Ndio maana unaona watu wanapigwa risasi leo na bado wengine wanarudi barabarani kesho yake. Mifano ni Mby, Songea na Arusha. Ogopa mtu aliyepoteza matumaini, he/she has nothing to loose hata akifa!

Sijui ni Middle class gani unayoiongelea, maana kama ni waajiriwa asilimia kubwa ya waajiriwa ni wafanyakazi wa serikalini ambao wengi wao mishahara yao tunaijua, kuna waajiriwa wa serikalini ambao mishahara yao ni midogo kuliko vipato vya wamachinga au mama lishe. Na huko serikalini wanaochipukia wengi wao ni wajanja wajanja wanaoishi kwa mishemishe tu [ufisadi].

Creation ya middle class inaendana na sera nzuri za kuvutia wawekezaji genuine na sio hawa wanaoletwa na wana siasa halafu wanakuwa na kiburi kwa kuwa serikali haiwezi kufanya kitu. Serikali inapanga kima cha chini cha mshahara halafu hao wawekezaji wanagoma kulipa na baadaye serikali inaufyata. Ni kwa kuwa serikali yenyewe imekuwa muwekezaji indirectly kwa kutumia watu walio serikalini ambao nao wana hisa au walishapewa mshiko ili kulinda maslahi ya wawekezaji na ndio maana wawekezaji wengi hawafuati sheria na hakuna anayewachukulia hatua.
 
UVUMILIVU wa demokrasia ndio kitu gani mkuu wangu?.. Una maana JK anatakiwa kupambana na adha za Demokrasia? au unachotaka kusema ni uvumilivu ktk uhuru na haki za watu kuhabarishana. Na akipiga vita uhuru wa habari sii ndio atajiharibia zaidi, wewe huoni kwamba toka mwaka 2005 duniani kote, uhuru huu umepewa kipaumbele zaidi kuliko miaka ya nyuma?. Wakati wa Mkapa vita kubwa ilikuwa Rushwa kwa nchi maskini lakini hapakuwepo nguvu kubwa ktk uhuru wa habari, waandishi wengi walifungwa ama kuuliwa na ndio maana imesisitizwa zaidi kutokana na watu kama Mkapa na wengineo.

Kama wewe FMES unatembea na mke wa mtu na watu wanakusema sana kwa kutembea na mke wa mtu. Je, utavulimia lawama hizo au utapambana nazo? Kwa mtazamo wangu JK anakubali yote yanayozungumzwa kwa sababu yana ukweli na makosa yapo vile vile isipokuwa hajui afanye nini maana kashindwa kujizuia na Ufisadi. Ubabae wa kina Mkapa ulisaidiwa sana na kutokuwepo mkazo mkubwa ktk uhuru wa habari na ndio maana aliweza kunyamazisha watu. Miaka yake ndio ilikuwa mwanzo wa hizi Blog, Hi5, facebook na kadhalika lakini sasa hivi hawezi kuzuia tena hata Assad akashindwa.

2. Middle class gani FMES watu wanaishi mjini kiujana ujanja tu. Wee unaweza kuamini ya kwamba wakati wa Nyerere asilimia kubwa ya wananchi walikuwa na ajira kuliko leo hii?..Sasa utaweza vipi create middle class ikiwa asilimia kubwa ya wananchi hawana kazi na waliokuwa nayo ni vipanga hawanunui vitu kwa fedha yao mfukoni bali waliyopiga mishemishe. Hakuna mtu anaishi kwa mshahara wake bali kufisadiana, unapigwa panga hapa na wewe unaelekeza mashambulizi yako sehemu nyingine. Na kweli mkulu amekaa kimya akitazama sinema inavyoendelea.

- Bob mimi nimefika Colombia, huko ukiisema Serikali vibaya au matajiri, unapigwa risasi mchana na inakubalika na jamii, sisi hapa magazeti yetu sio tu yanashambulia ila yanafika mahali yanatukana mpaka matusi ya nguoni, lakini hakuna lolote wanalofanyiwa, sasa kwa maoni yangu kulinganisha sisi na nchi kama Colombia, tunanafuu sana na isingewezekana kama sio Rais wa sasa.

- Hapa bongo ninajionea vijana wadogo sana kiumri ambao wanaendesha mashirika ya private na ya serikali, wanalipwa mahela makuwba sana, wanaishi vizuri sana sawa sio wengi sana kulinganisha hesabu yetu ya wananchi ya taifa, lakini please sisi tulioishi Awamu ya kwanza tunaheshimu sana hii new generation power, sina namba za kitafiti of where we are kitaifa na namba, lakini hata mikoani nimeona hawa vijana wakiishi vizuri, sasa hii imeondoa ile gap ya umasikini kabisa na matajiri, kwa maoni yangu kwa ninayoyaona hapa bongo, kwenye hizi Club za starehe hukuti wazee siku hizi kama zamani unakuta vijana tu inatia moyo sana kwa sisi tulioisho under Awamu ya kwanza! Siku hizi kwenda majuu imekwua mchezo tu, kwenda South Africa ndio usiseme, I mean kuna wakati haya yote yalikwua ni ndoto wka vijana!

- NDIO NINASEMA MNYONGE MNYONGENI!
 
2. CREATION OF MIDDLE CLASS.:
FMES,mbona huonyeshi data za hao walioingia kwenye middle class katika miaka yake madarakani na wewe ni "mzee wa data"?ie parcentage etc.

Pia nadhani umekosea, ukisema ame "create", ina maana there wasn't a middle class before?
 
- Mushi ni kweli middle class haikuwepo sasa ipo, na pia namba za kisayansi sijazipata lakini kwa kuona tu najua kwamba sasa tuna middle class na haikuwepo siku za nyuma!, na infact most of my friends wanatokea humo ndio imekwua rahisi sana kwangu kuelewa hili!

Es!
 
Mkuu mi bado nipo gizani hasa katika kujua mantiki ya thread hii. Je imejikita zaidi katika kuendeleza yaleyale ya kujionesha mbele ya wagawa ulaji ili nawe ufikiriwe, lakini hili nadhani haliwezi kuwa kwako wewe. Je ni kuonesha kuwa ni mwenzao? Je unaposema middle class unamaanisha ni watu wenye kipato gani kwa Tanzania?, Maana at least US wanaweza sema mtu wa below $1m but more than $0.1 m a year, others between $0.1m to $0.25m but at least kuna discussion ya kipato.

Je Tanzania ni watu wa kipato gani?. Je kipimo cha maendeleo ni kuangalia wale ulio karibu nao kama wameendelea au wananchi wote kwa ujumla?. Hivi Mtanzania anayelala bila kujua kesho atakula nini kwa kukosa fedha naye unamuweka wapi hata kama atakula kesho?.

JK ni kweli anastahili sana pongezi katika baadhi ya maeneo na mimi hili huwa nalisema kila siku (mfano, mmoja ni kitengo cha uhamiaji hasa kwenye pass za kusafiria, hapo nyuma ilikuwa ni ngumu kupata pass kuliko kupata visa ya UK au US, ila katika miaka ya mwanzo ya utawala wake sijui sasa, alibadilisha hilo kwa ziara zake za wizarani)

Ila JK anastahili lawama na hatasahaulika kwa hili (Japo kwangu mimi ninaliona kama kuelemewa na mzigo wa kikatiba kwa kuwa ni mwoga) katika kuwalinda mafisadi japo ushahidi upo ila anaogopa kuonekana mmbaya mbele ya maswahiba wake. Hili ni moja ya mambo ambayo ymemfanya JK aonekane ni worse president aliyeanza as the best. Leo hii anaogopa hata interviews zitakazomuuliza maswali magumu kuhusu wizi uliofanywa na jamaa zake wa karibu.

Haya yote uliyoandika FMES katika thread hii hayapo supported na facts, ila inaweza kuwa ni Political move.

- Bob mimi nimefika Colombia, huko ukiisema Serikali vibaya au matajiri, unapigwa risasi mchana na inakubalika na jamii, sisi hapa magazeti yetu sio tu yanashambulia ila yanafika mahali yanatukana mpaka matusi ya nguoni, lakini hakuna lolote wanalofanyiwa, sasa kwa maoni yangu kulinganisha sisi na nchi kama Colombia, tunanafuu sana na isingewezekana kama sio Rais wa sasa.

- Hapa bongo ninajionea vijana wadogo sana kiumri ambao wanaendesha mashirika ya private na ya serikali, wanalipwa mahela makuwba sana, wanaishi vizuri sana sawa sio wengi sana kulinganisha hesabu yetu ya wananchi ya taifa, lakini please sisi tulioishi Awamu ya kwanza tunaheshimu sana hii new generation power, sina namba za kitafiti of where we are kitaifa na namba, lakini hata mikoani nimeona hawa vijana wakiishi vizuri, sasa hii imeondoa ile gap ya umasikini kabisa na matajiri, kwa maoni yangu kwa ninayoyaona hapa bongo, kwenye hizi Club za starehe hukuti wazee siku hizi kama zamani unakuta vijana tu inatia moyo sana kwa sisi tulioisho under Awamu ya kwanza! Siku hizi kwenda majuu imekwua mchezo tu, kwenda South Africa ndio usiseme, I mean kuna wakati haya yote yalikwua ni ndoto wka vijana!

- NDIO NINASEMA MNYONGE MNYONGENI!

Ungetoa na mfano wa USA pia ungekuwa ume balance hasa. Huwezi fananisha Colombia na Tanzania. Kuhusu vijana wadogo kulipwa mahela makubwa ukifuata sana utakuwa majority wamewekwa na baba zao ambao ni wanasiasa wenye ushawishi serikalini.

Mtoto wa mkulima kufikia hatua hiyo si kazi rahisi kwa Tanzania ya leo. Nepotism is at best in Tanzania you know that. Ndiyo maana wewe utasemea unaowajua tu kwa kuwa ndiyo waliokaribu na upendeleo.

Tumsifie JK kwa mengine lakini si haya uliyoyaandika.
 
- Mushi ni kweli middle class haikuwepo sasa ipo, na pia namba za kisayansi sijazipata lakini kwa kuona tu najua kwamba sasa tuna middle class na haikuwepo siku za nyuma!, na infact most of my friends wanatokea humo ndio imekwua rahisi sana kwangu kuelewa hili!

Es!
Are you sure hatukuwahi kuwa na middle class hata kwa level yetu ya umasikini? Middle class kwetu ni watu wa aina gani?

What makes someone a middle class in Tz?

Ntashukuru tukielimishana hapa.
 
To me Kikwete is hopeless and spineless head of the state! Hajui kwanini taifa lake ni maskini . Uswahili na uislam umemjaaa
 
ES! Middle class ameijenga vipi? Labda ungetuelewesha! Naona kama maisha yamekuwa magumu zaidi kwa watu wa maisha ya kati na chini. Ingawa ni kweli ukiondoa wachache wanaotamba hajajenga kabisa kundi la kina bwana mkubwa kama ilivyokuwa awamu iliyopita
 
- Mushi ni kweli middle class haikuwepo sasa ipo, na pia namba za kisayansi sijazipata lakini kwa kuona tu najua kwamba sasa tuna middle class na haikuwepo siku za nyuma!, na infact most of my friends wanatokea humo ndio imekwua rahisi sana kwangu kuelewa hili!

Es!
Are you sure mkuu?what gets you a "middle class" status in Tz?
Nadhani middle class ilikuwepo kama kuna kiwango cha mapato kinachomfanya mtu kuwa kwenye middle class, je ni kipi hicho?

Ina maana kuwa hakukuwahi kuwa na watu wenye viwango hivyo vya mishahara/mapato ambao tungeweza kuwaita "middle class"? kabla ya JK kuingia madarakani?
 
Wewe umetawaliwa na wivu na choyo!!Sasa we ulitakaje?kama mtu hafanyi shughuli ya kumuingizia kipato asitegemee nafuu ya maisha.Mungu hapendi wavivu
 
hao hawawezi kuukubali ukweli hata siku moja juu ya mazuri ya jakaya, wamekunywa komunio na sakramenti hao
 
Kwani hao kina middle class ndio kina nani? Wanaishi hapa hapa tz?
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom