Dr. Helen Kijo Bisimba wa LHRC apata ajali

Dr. Helen Kijo Bisimba wa LHRC apata ajali

Hivi lowassa hajaondoka na hawa vijana wake? sijaona mantiki ya kumtukania mzazi kwa kuulizwa swali lile, mods mko wapi? Invisible Paw

Onesha tusi hata kwa kubold tu sio unatokwa povu kama koki ya ki,.bof..u imeachia unavyoamka asbh, Lowasa unayemtaja katika mazingira haya hana watoto?
 
Last edited by a moderator:
LHRC kinaendeshwa na hela za wafadhili, sio kodi zetu. Pia, ukiliona hata jengo lao pale Mwenge pia utasema ni mafisadi. Siipendi dhana hiyo. Tuilaumu serikali yetu inayokusanya kodi toka kwa raia na matumizi yake hayaendani na umaskini wetu. Vinginevyo tutamchukia kila mtu hata asiyehusika. Ni jukumu la serikali kutufanya sote kuwa na vipato vya kati na vikubwa. LHRC wanasaidia tu kutusemea.

hoja yangu tunapowanyoshea vidole mawaziri kuwa wanatumia mashangingi yanayotunyonya wakati nanyie mnatumia hayohayo mantiki inakosekana, hao wafadhili wanawaletea mashangingi wanajua munayahitaji kwa shughuli zenu huku mukitaka igp na cdf watumie noah!

lazima sisi wenyewe tuwe mfano kabla hatujawanyoshea vidole wengine, huyu mama sijawahi kusikia ameenda hata kibaha hilo V8 mjini la kazi gani? kumbuka serikali inatumia fedha chache za kigeni tulizonazo kuagiza mafuta ya diesel huku wengine wakitumia mafuta hayo kwa mambo ya anasa. leo jumapili umuhimu wa hilo gari kuwa barabarani siuoni hata kama ni la mtu binafsi.
 
Huyu mama alikuwa anapinga matumizi ya mashangingi kumbe na yeye analo, mungu kamuumbua.
Kwani hilo limenunuliwa kwa kodi zetu au ni misaada ya wafadhili? Mbona mnaharakia kuhukumu haraka hivyo? Je kama alipewa lift?
 
Pole Mama Bisimba ,inshallah Mwenyezi Mungu atakunusuru!Mleta habari hebu nyyoosha maelezo yako ili yaendane na picha ulizobandika,Nanukuu "....Walikuwa kwenye mataa, wamegongwa na gari kwa nyuma gari lao lika-overturn."mwisho wa kunukuu.
Sasa tukiangalia vielelezo picha tunaona gari husika imegongwa ubavuni! hapo sijui kipi sahihi!
 
hii nchi tuache tu kuhubiri ufisadi, sikutegemea huyu mama angekuwa na gari kali namna hii, sasa naamini kuwa nchi hii masikini ni wachache mno wengine wanajifanyisha tu. Mleta story hebu tueleze alikuwa anaendesha mwenyewe kama nape? basi asijekuwa kajitoa muhanga zile computer zilizochukuliwa na kova zilikuwa na mambo mazito sana.

Nani alilyekuambia ufisadi ni utajiri? Au kuwa na gari la thamani ni utajiri au ufisadi? Wivu utakuua, tumia maarifa zaidi zaidi ya kuongozwa na emotions.. Unataka kuwahamishia matajiri vita vyako vya kukosa? Ni chi gani duniani, au hata katika ukoo wako kwamba watu wote mmlingana kimapato, mipango na vipaumbele? Kama kazi yake inalipa kwa nini asinunue gari la gharama? Kamwibia nani?

Au kwa akili yako unadhani wewe kama huna uwezo ama sifa ya kuwa na kazi nzuri, hpashwhi kuwaonea wivu wenye kazi nzuri. Kama vipi nawewe soma, au utafute kazi nzuri. Kinachokatazwa ni mapato yasiyo ya haki. Huyu mama kakwibia lini?
 
naona gari nusura iingie kwenye jingo la NHC inawezekana ilikuwa inatokea barabara ya Hassan mwinyi kuelekea aghakhan hospital, lakini tulishasema hizi V8 hazina balance barabarani ukilinganisha na hardtop au Nissan patrol. ingekuwa hardtop hapo angekunja na kusepa bila tatizo.

Hata mimi pale ofisini kwetu nimegundua hilo kuwa haya ma vx au v8 balance yao ni mashaka, nakubali nissan patrol jinsi ilivyo kupinduka si rahisi. Ila sijui kwa nini vibosile hupendelea haya ma landcruiser kuliko nissan patrol.
 
hii nchi tuache tu kuhubiri ufisadi, sikutegemea huyu mama angekuwa na gari kali namna hii, sasa naamini kuwa nchi hii masikini ni wachache mno wengine wanajifanyisha tu. Mleta story hebu tueleze alikuwa anaendesha mwenyewe kama nape? basi asijekuwa kajitoa muhanga zile computer zilizochukuliwa na kova zilikuwa na mambo mazito sana.

Hivi akili zenu mnazifungia wapi... Hivi ukiwa tajiri kwa mfano mengi hawezi kupinga utumiaji wa magari mashangingi serikalini japo na yeye anayo tena ya zaidi ya hayo...
 
Kwani hilo limenunuliwa kwa kodi zetu au ni misaada ya wafadhili? Mbona mnaharakia kuhukumu haraka hivyo? Je kama alipewa lift?

kwani hao wafadhili walilileta likiwa na mafuta? silinatumia mafuta yaliagizwa kwa fedha zetu za kigeni?
 
Uguwa pole.

Labda ukiwa hospitali utazifikiria dhambi zako vizuri za kujifanya mtetezi wa haki za binaadam kumbe ni mnafik.
 
hoja yangu tunapowanyoshea vidole mawaziri kuwa wanatumia mashangingi yanayotunyonya wakati nanyie mnatumia hayohayo mantiki inakosekana, hao wafadhili wanawaletea mashangingi wanajua munayahitaji kwa shughuli zenu huku mukitaka igp na cdf watumie noah!

lazima sisi wenyewe tuwe mfano kabla hatujawanyoshea vidole wengine, huyu mama sijawahi kusikia ameenda hata kibaha hilo V8 mjini la kazi gani? kumbuka serikali inatumia fedha chache za kigeni tulizonazo kuagiza mafuta ya diesel huku wengine wakitumia mafuta hayo kwa mambo ya anasa. leo jumapili umuhimu wa hilo gari kuwa barabarani siuoni hata kama ni la mtu binafsi.

Mfano upiii....hili ni jasho la mtu kwa mshahara wake...na hilo gari lina private number...kwani sisi tumewakataza mawaziri kumiliki hata hammer?? Kinachopingwa na serikali kutumia magari ghari si kwa mtu binafsi... Hii haitaji elimu kubwa kuelewa hili...
 
Hata mimi pale ofisini kwetu nimegundua hilo kuwa haya ma vx au v8 balance yao ni mashaka, nakubali nissan patrol jinsi ilivyo kupinduka si rahisi. Ila sijui kwa nini vibosile hupendelea haya ma landcruiser kuliko nissan patrol.

nadhani hili ndo jambo tunalopaswa kulizungumza, mfano Mercedes Benz G series ziko stable sana barabarani na hata ikipigwa pasi haiwezi rushwa juu hivyo na hata fuel consumption yake iko chini ukilinganisha na Toyota V8. Ukiangalia hiyo ni Gx series na sio VX series kula mzinga ni kufikia tu, katika highway ndo haifai kabisa.
 
baada ya hawa majambazi kuchukua vifaa vyake vya kazi wameona haitoshi wanataka kuchukua roho ya mama yetu. washindwe na walegee kama mtele!

.....

...nasiku wakifa Mungu wadrop jehanamu !!!

very sad....
 
ukiona nchi wananchi wanawachukia watetezi wa haki za binadamu. Nchi hiyo inatatizo kubwa la ubaguzi either rangi, dini, kabila au siasa. Hapa ni siasa.

Wale wa chama kinachotawala wote wanajiona kama watawala. Wanasahau shida zao zote kwa gharama ya chama. Hivyo wapo tayari kuona binadamu mwingine hatendewi haki, wapo tayari kuteswa na kusulubiwa kwa kila namna ilimradi tu chama chao ndiyo kinatawala.

Hizi ni dalidali za nchi changa kabisa yenye watu wanaokuwa taratibu mno kifikra. Watu walio wanafiki. Wanaojiona ni watawala kwa kuwa chama chao au kabila lao linatawala.

Anae tawala ni yule aliyepo madarakani. Wengine wote ni watawaliwa bila kujali upo chama gani. Watetezi wa haki za binadamu wanakutetea.
 
Uguwa pole.

Labda ukiwa hospitali utazifikiria dhambi zako vizuri za kujifanya mtetezi wa haki za binaadam kumbe ni mnafik.

FF
maneno yako ni makali lakin huo ndio ukweli
hawa watu ni wanafiki kwa kweli . hayo mashangingi ya milion 120 . ni project mbali mbali ambazo kwa bahat mbaya sana hizo hela haziwafikii walengwa
 
Mfano upiii....hili ni jasho la mtu kwa mshahara wake...na hilo gari lina private number...kwani sisi tumewakataza mawaziri kumiliki hata hammer?? Kinachopingwa na serikali kutumia magari ghari si kwa mtu binafsi... Hii haitaji elimu kubwa kuelewa hili...

wakati wa nyerere ukitaka kuagiza gari ilibidi upate kibali cha ikulu na ueleze hilo gari ni kwa kazi gani, leo watu wanajiagizia tu magari yanatafuna fedha za kigeni kuyawekea mafuta na vipuri. kwa jasho gani anamiliki gari ya mil500 kama hajawaibia wajane tu, matajiri tunawajua na wanapata kipato halali wanakula jasho lao.
 
Tizama gari ya nape, nyumba ya deo, sasa gari la dr! hapana hii nchi mtetezi kabaki magufuli tu, nae akitutosa basi tena.

Roho na akili za kimasikini ni mbaya sana!
Hii komenti inadhihirisha jinsi wengi wetu tulivyo na mtazamo na fikra finyu!
Fanya kazi kwa bidii upate lako na kuacha kujadili mafanikio ya watu wanaojituma pengine kabla hata hujazaliwa!
 
Back
Top Bottom