Dr Harrison Mwakyembe atua Tabora kwa gari moshi leo

Dr Harrison Mwakyembe atua Tabora kwa gari moshi leo

treni za mwendo kasi haziko marekani?
haziko ulaya? au unazungumzia nchi gani? unazungumzia mwendo kasi upi zaidi ya unaotumika kwa sasa na treni kama siemens nk?
kumbe bila kuwa na mipango ya baadae tutakuwa na maendeleo?
upeo wako wa kufikiri ndio huu?
wenzetu wana mipango ya zaidi ya miaka 50 ijayo wewe unawaza hapo ulipo
tutaendelea vipi?
Mkuu Ritz
Angalia watu wengine walivyokuwa na vichwa duni ni mahodari wa kugoogle hizi treni wananoziongelea hata taifa tajiri kama Marekani hawana hivi sasa ndio wanafikiria kuwa na hizi treni za mwendo wa kasi; hivi sasa ndio wanafanya study kuwa na treni ya kasi kati ; Tanzanian hatujachalewa dizeli injini zinatumika mpaka leo sasa tatizo lipo wapi kwa sisi Tanzania kuendelea kuzitumia?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Sikonge unamaanisha kuwa treni letu halitumii mafuta linatumia umeme unaojizalishia wenyewe?
kwani hata treni la mafuta linazalisha umeme
ila umeme ninaozungumzia hapa sio huo unaozalishwa na dizeli ni umeme kama wa Tanesco
ambao ndio tunataka uwe unatumika kwenye tren zetu kama nchi za wenzetu
haya tunayotumia yameshapitwa na wakati na usitegemee yakimbia zaidi ya spid ilivo sasa hata kama wakirekebisha reli bado vichwa ni vile vya kizamani ambavo kwa wenzetu hawavitumii tena
what we need is a new and modern railway
kuhusu shule yangu mkuu ni field ingine kabisa ndio namalizia kadegree ka tatu
kusoma nimesoma hilo ondoa shaka niko upande wa mafuta na gesi kwa upande wa sheria
Mkuu Lokissa,

Naona una mwanga kidogo wa mambo ila bado hujapiga shule ya KUJISOMEA. Nafikiri hizi ni Story umekuwa unapewa tu na watu na nafurahi kuwa unazikumbuka vizuri. Au tuseme umekaa majuu na kupata mwanga kidogo.

Tanzania ni nchi kubwa nakubaliana na wewe ila kwa Train bado si kubwa sana. Kwa ndege nilishasafiri hadi Kigoma kutoka Tabora ni saa moja. Ila inategemea unatumia ndege gani maana speed zinapishana.

Kigoma Tabora ni karibu sana kwa Train na ilitakiwa tusafiri kwa masaa SITA yaani nusu ya muda aliosafiri Mwakyembe. Inawezekana kabisa kwa Train za Tanzania kwa sababu na ZENYEWE NI ZA UMEME.

Hahahaa, naona unatoa macho kusoma neno TRAIN ZA UMEME wakati hujaona waya za umeme na hapo unafikiri mie ninakudanganya. Hapana, nakuambia ukweli kabisa. Vile vichwa vya Train siyo kama yalivyo maroli au magari. Lile dubwana ni GENERATOR ya UMEME na linazalisha umeme ambao unatumika kuendesha Train na wakati huo huo kwa matumizi ya ndani ya Mabehewa kama umeme, kupikia, kuwasha vifaa vya Umeme(electronics) nk.

Ndiyo maana ukiangalia vizuri, baadhi ya mabehewa utaona MOTORS ambazo huzungushwa na umeme kusaidia dubwana lipande milima. Na utajua ni TRAIN la umeme kwa sababu, kutoka Speed 0 km/hr hadi 40 km/hrs linapoondoka Railway Station kama Dodoma, huchukua muda mfupi sana .

Kwa maana hiyo, likiwa kama TRAIN LA UMEME, linaweza kabisa kwenda hadi 80 km/hrs na huo nina uhakika kabisa ila tatizo ni RELI na Mabehewa yetu yatahilimi? Ile Reli ni Nyembamba sana na train haiwi STABLE inapotembea maana ina upana wa 1 meter na kwa kawaida kwa sasa duniani wengi wanatumia upana wa Mita kama moja na robo hivi. Na wengine huenda hata 1.4**meters.

Nilitegemea Mwakyembe kama msomi, aanze na mabadiliko kama hayo ya kupanua reli ila na yeye anatafuta WASHANGILIAJI na Wapambe ambao naona kawapata wengi kama Kumbi kumbi.

Asante kwa picha ya TRAIN nzuri ya Mgeruman, ICE.
 
nataka kujua, amelipa nauli? alikaa daraja gani? alienda kigoma kwa kutumia usafiri upi? ndege? bus? au gari la ofisini? kama ni ndege au bus ,sina shaka nampongeza lkn kama alienda na gari la ofisi yaani serikali kisha akaamua yy kurudi na train ,huku gari likimfuata kwa barabara ni ufujaji.hapaswi kupongezwa. kama amepanda train hiyo kwa lengo la kujionea yy mwenyewe uendeshaji wake, vituo vya njiani kubaini matatizo yao nivyema saana. je? alishirikisha watendaji, hakika mimi si mshabiki wa siasa za kutaka sifa. kujijengea umaarufu kwa kufanya utalii.huku gari la serikali likiunguza mafuta kukufuata.
 
Kwani unafikiri mie sijasafiri na hizo za German?

Watu tumeshapanda hadi TGV ya Mfaransa, wewe sijui unaandika upuuzi gani. Kaa huko USA na kula Marehemu Kuku wa KFC tu ili unenepeane kama watoto wa Antonio LA Reid.

Nimeshakutana na hao Wataalamu kutoka USA nchi fulani huko Europe wakiwa wanafanya utafiti jinsi ya kutumia na kuyaweka kwenye RELI hayo Matrain ya Speed kali. By the way, hata South Africa wanajenga kuunga mji wa Pretoria na J'burn na Oliver Tambo International Airport...... walijua hilo Mla KFC?

Walipofika Ulaya, Wamarekani hao nilikuwa ni mmoja ya watu niliowapa shule na nikaondoka zangu kujirudia Sikonge maana baridi la Ulaya lilinishinda. Wewe sikiliza tu News na kusoma kwenye Internet hizo habari wakati wenzio tuliongea hadi na watu watakaoshughulika na hii habari nzima.

Pana wakati kuna State moja pia walifika kutaka kujifunza jinsi ya ku-organise Public Transport in Urban areas. Wakaja tukawapa shule na wakajiondokea. Masikini USA, walikuwa wamelala kwa vitu vingi sana, kisa MAFISADI. Poleni.
Mkuu endelea kokopy na kupaste Marekani hawana treni za kasi kama walizonazo Europe na China; hivi sasa ndio kwanza wanafanya utafiti wa awali treni ya kwanza ya mwendo wa kasi ya umeme itakuwa kati ya San Franscisco Bay area na Los Angeles Carlifornia gharama nzima ya mradi itakuwa $9.95 bilioni mradi utakamilika 2030 mkuu sipo Sikonge nakueleza vitu ambavyo ndiyo vinatawala kwenye vyombo vya habari. Mkuu Ritz jamaa anahangaika kugoogle lakini habari nzima Marekani hawana treni za umeme za Mwendo wa kasi; mwaka 2000 Amtrak ndio walianzisha treni Acela kati ya Boston na Washington DC hii kwa hapa USA ndio inaonekana ya kasi ila kwenye viwango vya dunia haimo; Acela top speed yake ni 150mph wakati China wao wana treni inapiga 302mph; mkuu Sikonge nimeshafiri na Acela na nimeshafiri na hizi train Germany siongei kwa kugoogle.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Tupongeze tu pale treni itakapofikia angalau utendaji wa miaka ya sabini/themanini. Mnakumbuka ilifikia kuanza safari mbili kwa siku kwenda MWANZA/Kigoma. Sasa tunashangilia waziri kufanya public relations! Ebu tuwape Mawaziri wetu real challenge siyo kuwasifia kwa kisichokuwepo. Usafiri wa treni ni muhimu sana kwa uchumi wetu na maendeleo ya nchi yetu tunapaswa kuwapa changamoto ya kweli na kuwashinikiza waupe kipaumbele. Tunataka waupe kipaumbele Kama wanavyotoa kwenye mabarabara (ambayo bahati nzuri yanawapa kura ndio maana utoana macho bungeni kupigania kila mbuge ajengewe barabara Jimboni kwake)
 
Ninachosema mie hapa ni kuwa TRAIN la Tanzania linatumia UMEME pia. Ila umeme huo unazalishwa na GENERATOR inayotembea ambayo imeundwa na kuonekana kama KICHWA CHA TRAIN.

Ndiyo maana linakuwa kubwa mno kwa sababu linabeba mafuta ya kutosha humo ndani. Lingelikuwa ni Train la umeme tu, basi ni Motors kibao humo ndani zinakuwpo na mchezo umekwisha.

Hivyo, unaposema UMEME, inabidi uende zaidi na kusema ni umeme upi. Kama ni wa TANESCO jibu ni HAPANA. Ila kama Umeme wa TRAIN yenyewe, jibu ni YES. Yaani Kichwani cha train hakitengenezi Torque (Mzunguko) wa kuendesha Train ila linatengeneza umeme na umeme huo ndiyo unaendesha Train nzima kasoro hiyo Generator ambayo inatumia DIESEL.

Kwa Tanzania, inabidi kwanza tuanze na upana wa reli Starndard. Tukishapanua Reli hapo ndiyo tuanze kufikiri kuongeza speed ya Train. Ukileta Train ya Mjapan leo ya Mwaka 1967 iitwayo Shikansen, bado haitaenda na speed yake ya juu ingawa ni train la zamani sana na kisa ni Ubovu wa reli.
Hayo ndiyo mambo ambayo wengine tulitegemea Mwakyembe aanze kuyafanyia kazi. Ila kaanza kivyake na watu wanamshangilia, OK.

Mengine NAKUBALIANA na wewe kabisa kuwa inabidi tuwe na Modern Railway maana ni AIBU sasa.

Mwishoni: Hongera kwa NONDO nzito. Nategemea utakuwa unaPanda hadi Darini hivi karibuni kama sikosei. Angalia tu badala yake hiyo PhD isiwe ile wanasema Permanent head Damage kama Madokta wengi wa Tanzania kwa sasa waliofumuka kama uyoga. Ni heri umalize hiyo sheria ili mje mtulindie Mafuta na Gas yetu maana akina chama na wazazi wao wanauza kila kitu 🙂

Ila kusema ukweli, hata uandishi wako ulivyojibu, utaona mtu kaenda shule huyu, SAFI SANA.
Sikonge unamaanisha kuwa treni letu halitumii mafuta linatumia umeme unaojizalishia wenyewe?
kwani hata treni la mafuta linazalisha umeme
ila umeme ninaozungumzia hapa sio huo unaozalishwa na dizeli ni umeme kama wa Tanesco
ambao ndio tunataka uwe unatumika kwenye tren zetu kama nchi za wenzetu
haya tunayotumia yameshapitwa na wakati na usitegemee yakimbia zaidi ya spid ilivo sasa hata kama wakirekebisha reli bado vichwa ni vile vya kizamani ambavo kwa wenzetu hawavitumii tena
what we need is a new and modern railway
kuhusu shule yangu mkuu ni field ingine kabisa ndio namalizia kadegree ka tatu
kusoma nimesoma hilo ondoa shaka niko upande wa mafuta na gesi kwa upande wa sheria
 
Mwakyembe hana tofauti na wauza sura wenye kutembelea bajaji na wakati mwingine bodaboda... CCM Miaka hamsini ya uhuru bado tunachechemea kwa merikebu ya nchi kavu!!! eti mnapongezana kwenye upuuzi wa kuuza sura...grrrrr...Uzuzu mtupu!
 
Mkuu,

USA zipo High Speed train ila ni LINE moja tu ya hii train inaitwa ACELA Express iliyo chini ya AMTRAK. Hili dude linakwenda hadi speed Maximum 250km/hrs ila Avarage yake ni chini ya hapo.

Unajua kitu kinachopunguza Speed kwenye reli kama hizi ni MIJI na KONA. Ndiyo maana inabidi wazibadilishe ujenzi wa Reli hasa kwenye Kona na kujenga SLOPES ili kusaidia Centrifugal Forces kulirusha train nje ya rail. Kuna baadhi ya Train za high speed kwa sasa, zinaji-TILT zenyewe ili hiyo nguvu kwenye train isidhuru watu na train bila ya kubadili ujenzi wa Rail.

300px-DC283_hokuto_001.jpg
images
TILTING TRAIN.

Ahh, hizi Train za Umeme kwa Tanzania ni kujitumbukiza kwenye matatizo tu. Ni sawa na ujenge Metro Dar, itaingia maji kila siku, Almost 🙂 Kutokana na ukubwa wa Tanzania na udogo wa miji yetu (Idadi ya watu) na uchache wa Train, Train za Umeme wa TANESCO siyo Economical. Kuna factor nyingi sana zinatumika. Ndiyo maana ukiwa UK, chini reli za train kibao ila kule Juu Scotland ni Diesel Engine zinatawala maana idadi ya train ni chache na watu pia wachache.

treni za mwendo kasi haziko marekani?
haziko ulaya? au unazungumzia nchi gani? unazungumzia mwendo kasi upi zaidi ya unaotumika kwa sasa na treni kama siemens nk?
kumbe bila kuwa na mipango ya baadae tutakuwa na maendeleo?
upeo wako wa kufikiri ndio huu?
wenzetu wana mipango ya zaidi ya miaka 50 ijayo wewe unawaza hapo ulipo
tutaendelea vipi?
 
Tunategemea wataalamu kama Sikonge wawepo kwenye wizara ya miundo mbinu
nadhani mwakyembe atapata mbinu mbadala
Mkuu kuwa na degree tatu sio lazima phd.
ni vile videgree vya kuunga unga,undergraduate na postgraduate(masters) 2
 
Kwani unafikiri mie sijasafiri na hizo za German?

Watu tumeshapanda hadi TGV ya Mfaransa, wewe sijui unaandika upuuzi gani. Kaa huko USA na kula Marehemu Kuku wa KFC tu ili unenepeane kama watoto wa Antonio LA Reid.

Nimeshakutana na hao Wataalamu kutoka USA nchi fulani huko Europe wakiwa wanafanya utafiti jinsi ya kutumia na kuyaweka kwenye RELI hayo Matrain ya Speed kali. By the way, hata South Africa wanajenga kuunga mji wa Pretoria na J'burn na Oliver Tambo International Airport...... walijua hilo Mla KFC?

Walipofika Ulaya, Wamarekani hao nilikuwa ni mmoja ya watu niliowapa shule na nikaondoka zangu kujirudia Sikonge maana baridi la Ulaya lilinishinda. Wewe sikiliza tu News na kusoma kwenye Internet hizo habari wakati wenzio tuliongea hadi na watu watakaoshughulika na hii habari nzima.

Pana wakati kuna State moja pia walifika kutaka kujifunza jinsi ya ku-organise Public Transport in Urban areas. Wakaja tukawapa shule na wakajiondokea. Masikini USA, walikuwa wamelala kwa vitu vingi sana, kisa MAFISADI. Poleni.

Ungekuwa umeishi viwanja akili yako ingetulia kidogo endelea kugoogle; na usisahau wikipedia; sidhani hata Dar umewahi kuishi; nina uhakika wewe anga zako ni Sikonge; Urambo; Nzega na Tabora mjini kama ulitoka sana basi itakuwa Shinyanga mjini au Kahama; nina uhakika wewe una wazimu hebu nitajie huo waliotaka kujifundisha namna ya kuo-organize Public Transportation

Chama
Gongo la mboto DSM
 
treni za mwendo kasi haziko marekani?
haziko ulaya? au unazungumzia nchi gani? unazungumzia mwendo kasi upi zaidi ya unaotumika kwa sasa na treni kama siemens nk?
kumbe bila kuwa na mipango ya baadae tutakuwa na maendeleo?
upeo wako wa kufikiri ndio huu?
wenzetu wana mipango ya zaidi ya miaka 50 ijayo wewe unawaza hapo ulipo
tutaendelea vipi?

Treni iliyopo ya kasi Marekani Acela inakwenda 150mph; China inakwenda 302mph Marekani hawana treni ya kasi hivi sasa ndio California wameanza kuuza Bonds ili kupata pesa za kugharimia ujenzi wa treni ya kati ya San Fransisco na Los Angeles; Marekani hawana treni ya mwendo kama zilizopo ulaya na Asia; kichwa hakipo barabara mipango ya maendeleo ipo ; huku kuifufua treni ya abiria ni moja kati ya mipango ya serikali; usiwe unakifikiria kama vile kichwa kimejaa uyoga badala ya ubongo; watanzania wanachohitaji ni usafiri wa uhakika kati ya point A na B; hizi porojo na pumba tafuteni sehemu nyingine mzitapike

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Sijui kwa nini baadhi ya wazazi hawakutumia DUREX enzi zao........

Wazazi wangu ni wana ndoa halali hawana haja ya kutumia Durex; labda ungemhoji yule anayeishi na kimada!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Hata nikikuambia unawafahamu? Wahandisi wewe utawajulia wapi na umefika USA kwa Mgongo wa Mtoto wa Kigogo?

Wengine tumetoka Sikonge na tukafika hadi Ulaya kwa kutumia VICHWA vyetu.

Kwenye mambo ya Transport, waweza hata kwenda DEEP zaidi na kujadili mambo ambayo hayapo ndani ya GOOGLE na tutajadiliana vizuri tu. Kwa mfano swala la USA kuuwa Train zake na kuanza kujenga na kutumia Highways, hebu litafute kwenye Google na ukilipata ninakutumia Matobolwa 🙂

Mie Dar sijawahi kuishi zaidi ya kupita tu. Mie Mshamba nitaishije huko? Ni kweli mitaa yangu ni ya SIKONGE na huko majuu muishi nyie tu.

Haya kama wewe ni mtaalamu wa Train: What means Combined Transport in Railway Cargo? Why it's so useful in Country like Switzerland? (Kama ku-google unapata majibu yote, haya mwagika sasa Mzee wa Marehemu kuku wa KFC).
Ungekuwa umeishi viwanja akili yako ingetulia kidogo endelea kugoogle; na usisahau wikipedia; sidhani hata Dar umewahi kuishi; nina uhakika wewe anga zako ni Sikonge; Urambo; Nzega na Tabora mjini kama ulitoka sana basi itakuwa Shinyanga mjini au Kahama; nina uhakika wewe una wazimu hebu nitajie huo waliotaka kujifundisha namna ya kuo-organize Public Transportation

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Sikuwa na maana hiyo. Anyway, kama hukuelewa JOKE yangu basi poa, yaishe 🙂

Wazazi wangu ni wana ndoa halali hawana haja ya kutumia Durex; labda ungemhoji yule anayeishi na kimada!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Kumbe kukabidhiwa WIZARA NI TUZO!!!! Ndio maana eti........ eeh!! Watu wanafaidika kutokana na "tuzo", sio wanawajibika.
Hapa ndipo hoja zinazosemwa siku nyingi kuwa "jk anatoa vyeo kama tuzo/zawadi kwa anaowapa" ZIMETHIBITISHWA na RIZ. ​That's why I like magamba's portofolio.
Sasa inabidi zipunguzwe hizo wizara ili "tuzo zipungue" kwakuwa zinafilisi nchi.

Mkuu mimi nilifikili tunampongeza JEMBE letu kwanza, mambo ya itikadi tuyaweke pembeni KWANZA!
 
.....yeye si abiria ....kama...wewe...kwanini..ushangae?????.....hili...nalo..unalitengenezea bangoooooooooooooooooooo!!!.
....wakati majangili..wameli smash?

...makamanda tuchukue...nchi...
wasifuri..ni ...wengi...sikuaminini hata...mw.....naye ..ni......
.

..heri umiliki sifuri..... maana ni .....kubwa zaidi ya.... -100,000....
 
.....Napenda sana kulinganisha .... Dr. Mwakyembe vs Nundu.... Kagasheki vs wafuatao Maige, Shamsa Mwangunga na Zakhia Megji......... Prof. Muhongo vs wafuatao Ngeleja na Karamagi ..............!!!!!

Magufuli Vs Kawambwa............
 
Sasa mtu kuanda train nako imekuwa hoja?? Wananchi wanataka maendeleo na si mazingaombwe yasiyokuwa na tija!!
 
Back
Top Bottom