Mkuu sexon 2000, siwezi kukudai ushahidi kwa issues za NSSF wala hizo za PPF manake inawweza kukuwea ngumu hata kama issue ulizoongea ni kweli. hata hivyo, nimefarijika ki2 kimoja kwa maelezo yako kuhusu PPF wakati umenikatisha tamaa kuhusu NSSF. Ulipoongea kuhusu PPF, unaonesha umeongea kwa kujiamini kupita kiasi kwavile umeweza kutaja hata majina ya wahusika bila kuuma uma meno. Hata hivyo, umeshindwa kufanya hivyo kwa upande wa NSSF.....hii unanishawishi niamini kwamba una uhakika unachoongea kuhusu PPF lakini huna unachoongea kuhusu NSSF na badala yake umetawaliwa na dhahania. Ikiwa umeweza kuwataja hata MODS wa JF kwamba ni CORRUPTS, umeshindwa nini kutaja kwa majina hao wa NSSF?! Ni akina nani wameajiriwa NSSF kwa sababu tu ya dini zao?! Una uhakika kwamba hao ambao walihamishwa walifanywa hivyo kwa sababu tu ya dini zao na si vinginevyo? Umsema kwama aliwahamisha wakurugenzi wawili kwenda mikoani kwa sabau ni wakristo....je, ina maana NSSF ilikuwa na wakurugenzi wawili tu ambao ni wakristo?!