Batilda na Ruto wamepishana mwaka mmoja, ingawa Batilda ni mkubwa, ila kwa heshima ya kiafrika, Mwanamke ataamkia shikamoo kwa mtu yoyote alkiyemzidi umri au cheo!, hivyo Dr. Batild did the right thing kumwamkia Ruto Shikamoo!.
Hata ikitokea mke ni mkubwa kuliko mume, bado atamwamkia shikamoo kicheo cha ndoa tuu!. Mimi nina baba zangu wadogo, nawaamkia wake zao shikamoo, huku nimewazidi umri kwa hoja mke wa baba ni mama yako, regardless ana umri gani!.
Siku ukipata fursa, hudhuria ziara yoyote ya JK, sikilizia shikamoo anazozipata kwa watu ambao kwa macho tuu utawajua wamemzidi umri!, shikamoo hizo ni za heshima kwa mkuu wa nchi, na sio za umri!.
Dr. Batilda ni mama wa heshima sana ya kiafrika na kidini, sikumbuki kuwahi kumuona bila hijab!, mimi ni wa late 60's, nilipokutana nae kwa mara ya kwanza, sikumwamkia nikimdhania ni wa 70's, alikuwa na mwalimu wangu fulani wa Tambaza tukimwita Miss Juma!, ndipo mwalimu akaniambia "nyie watoto siku hizi mnajidai mmekuwa, mwamkie huyu shikamoo, huyo ni mama yako!, nilipigundua ni wa early 60's sasa ndio natoa shikamoo ya heshima ya umri!.
NB!, Shikamoo ni salam ya kitumwa ikimaanisha niko chini ya miguu yako!. Wakoloni Waarabu nao wametifanya vibaya, kama valivyotufanya wazungu na kasumba ya kizungu!.
Pasco.