Dr. Batilda Amsalimia Mhe. Ruto "Shikamoo"

Dr. Batilda Amsalimia Mhe. Ruto "Shikamoo"

Batilda na Ruto wamepishana mwaka mmoja, ingawa Batilda ni mkubwa, ila kwa heshima ya kiafrika, Mwanamke ataamkia shikamoo kwa mtu yoyote alkiyemzidi umri au cheo!, hivyo Dr. Batild did the right thing kumwamkia Ruto Shikamoo!.

Hata ikitokea mke ni mkubwa kuliko mume, bado atamwamkia shikamoo kicheo cha ndoa tuu!. Mimi nina baba zangu wadogo, nawaamkia wake zao shikamoo, huku nimewazidi umri kwa hoja mke wa baba ni mama yako, regardless ana umri gani!.

Siku ukipata fursa, hudhuria ziara yoyote ya JK, sikilizia shikamoo anazozipata kwa watu ambao kwa macho tuu utawajua wamemzidi umri!, shikamoo hizo ni za heshima kwa mkuu wa nchi, na sio za umri!.
Dr. Batilda ni mama wa heshima sana ya kiafrika na kidini, sikumbuki kuwahi kumuona bila hijab!, mimi ni wa late 60's, nilipokutana nae kwa mara ya kwanza, sikumwamkia nikimdhania ni wa 70's, alikuwa na mwalimu wangu fulani wa Tambaza tukimwita Miss Juma!, ndipo mwalimu akaniambia "nyie watoto siku hizi mnajidai mmekuwa, mwamkie huyu shikamoo, huyo ni mama yako!, nilipigundua ni wa early 60's sasa ndio natoa shikamoo ya heshima ya umri!.

NB!, Shikamoo ni salam ya kitumwa ikimaanisha niko chini ya miguu yako!. Wakoloni Waarabu nao wametifanya vibaya, kama valivyotufanya wazungu na kasumba ya kizungu!.

Pasco.

Ondoa mfumo dume wako katika karne hii, nyie ndo mnawafanya wanawake hawajiamini wanasubiria kuwezeshwa tu.
 
Sifahamu vizuri historia ya salamu ya ''Shikamoo/marahabaah" ila ilivozoeleka kwa waTz mara nyingi shikamoo hutolewa kwa mtu anayekuzidi at least miaka 5 and above. Kwa watu mnaolingana au kutofautiana angalau miaka 4, husalimiana habari yako/habari, kwa hiyo Dr Batlida angemsalimia 'habar yako mkuu'. Nashangaa kuna wanajf wanasema et ni kawaida tu kwa mtz. Nakubali ni kawaida kwa waTz kumsalimia unayemzidi umri kwa upande wa utamaduni wa makabila na sio lugha ya kiswahili. Ni bora na sie watz tukapromote 'salamu kuu' tofauti na 'shikamoo' ambayo hata mkubwa anaweza akaanza kumsalimia mdogo, mfano wenzetu wazungu yeyote mkubwa/mdogo anaweza kuanza kumsalimia mwenzake, make salamu ya shikamoo ishakuwa kero unakuta mtu anakuzidi umri ukimsalimia anakujibu aaah! Usinizeeshe mwenzio!
 
Kwa takwiimu hizo yamkini Ruto alitakiwwa amsalimu Batilida shikamoo dada au wangesalimiana kwa Batilida kumwambia Ruto, habari, hujambo au mambo?

Tukubali kiswahili chetu kwenye salam kimepwelea
 
Dr Batrida ni mwanasiasa
Sasa kazoe wakati wa Kampeni huwa wana
toa shikamoo hata kwa watoto wa Shule
lengo ni kupata kura.

Nadhani ndiyo maana anamwaga shikamoo
kama yuko kwenye kampeni Arusha alikomwagwa.
 
Daah! Sijui ndo kukosa kujiamini ama ni nini. nilikuwa naangalia KTN TV taarifa ya habari ya saa 3 usiku leo (4/4/2013) wakati Mhe. Dr. Baloz Batilda akimpa mkono Naibu Raisi wa Kenya Mhe. Ruto akaangusha na Shikamoo daah! nilichoka hivi kweli Batilda ni wa kumpa Shikamoo Ruto? au ndo confidence ilipotea kabisa. Mama jiamini wewe Dr wa PhD unaogopa namna hiyo??

Update:



Sasa akikutana na LEMA itakuwaje hapo!! Si ndo atahara kabisa!!!
 
Wajamenii,

Mmekomaliapo hapaaaaaaaaaaa kwa Bati na Rutoz..... MBONA way back hapa home ile Midingi inayopangaga FOLENI kumpokea FAST JET a.k.a VASCO DA GAMA akirudipo matembezini huwa wanamwamkia shikamoo Mheshimiwa wakati wememzidi Umri? MADARAKA Wanawane, chezea CHEO.

Shkamoooooo CHEO!
 
..utumwa wa kifikra (infiriority complex)ni mbaya sana...Mimi hata mke kumwamkia mmewe(hata kama mume kamzidi umri)sikubaliani nako...huu ni utumwa pia..
 
Pasco, mmmh. Batlida ni Baloz wa tz kenya, chochote afanyacho kenya na hasa katika diplomatic table kama hilo la kuonana na ruto imply tz yote imefanya. Najua unampeeenda yule mama, but tendea haki fikra je NI SAHIHI TZ YOOTE KUMPA SHKAMOO RUTO? or ni failure katika diplomatic communication and statutory behaviours?
Au waona sawa tu balazi wetu na wengini sitawataja kupetiwa mgongoni na mkuu fulan wa nchi na kuambiwa GOOD BOY,, GOOD LADY... Hapana Pasco

Amekosea sana kwa etiquette ya kidplomasia na amejishushia hadhi na ya serikali ya Tanzania pia!
 
Nikiona thread kama hii inafika kurasa sta na inaendelea kupamba moto halafu watu wanalalamika kuwa wana maisha magumu napata maswali mengi sana.

Kuna vitu ambavyo huwezi kuvijadili kama njaa inakuuma au huna uhakika wa sehemu ya kulala...
 
Nikiona thread kama hii inafika kurasa sta na inaendelea kupamba moto halafu watu wanalalamika kuwa wana maisha magumu napata maswali mengi sana.

Kuna vitu ambavyo huwezi kuvijadili kama njaa inakuuma au huna uhakika wa sehemu ya kulala...

Kwa hiyo mkuu kupitia hii thread unataka kujenga hoja maisha Tz ni rahisi sana? Tuache bana tujadili tamaduni zetu!!
 
No sio dharau, bali ni kutokana na ile traditional position ya mwanamke katika "yale" siku zote huwa chini!, hii mitindo ya kisasa ya wao kuja juu ni katika manjonjo tuu!, ndio maana hata Mungu, ameiweka pale chini!, katika uumbaji, angeweza tuu kuiweka pale kwenye kitovu, ili "somo" lifanyike while standing on equal basis!, lakini kaiweka pale, ili mmoja awe juu na mwingine awe chini!.
Hapa nazungumzia tuu position!, ndio maana kwa makabila mengine, hata mtoto wa kiume anakazwa kulia lia kama mwanamke, tena ukiambia usiwe kama mwanamke, kwa wengine ni umetukanwa!.

Ni ukweli ki baolojia mwanamme na mwanamke tuko sawa, ila Mungu alianza kwanza kumuumba Adamu, Eve aliumbwa tuu ili kumtumikia Adamu, hivyo hao wanawake tumeumbiwa sisi, watutumikie!.
Pasco.


Pasco, ni lazima utambue ya kuwa watu hawawezi kuendelea kuwa watumwa wa mila na desturi. Na itakuwa ni kosa kubwa kutumia imani fulani kutetea hoja yako, kwani sio watu wote wanaoamini katika dini. Zaidi ya yote, kitendo chako cha kutumia lugha ya kificho pale uliposema traditional position mwanamke anatakiwa kuwa chini, kuimply ya kuwa mwanamke ni mtu wa chini, ni kitendo cha kishamba na kilichopitwa na wakati. Nadhani kama hauna la kuchangia ni bora ukae kimya kuliko ku-expose ulimbukeni wako. Shame on you.
 
kuhusu huyo Batilda sijui but hapo kwenye mzee kumwambia mtoto shikamoo NAKATAA.Nimeishi moshi muda mrefu but ndio naona hiki kitu kwako.
Hapo kwenye nyekundu na bluu nimecheka sana....nimekumbuka mbali.....hizo rangi zinaoana sana
 
Huku kwa ndugu zangu usukumani mwanamke anakupa shikamoo kidume hata kama amekuzidi umri, lakini hii ni kwa watu wakoo moja yaani kidume is always superior to mwanamke!! Lakini kwa Dr Batilda duh hapo sina comment!!

Ha ha haaa! Kule Uchagani kama una cheo kikubwa au una fedha ya kutosha una uhakika wa kupata shikamoo regardless your age. Ndiyo maana watoto wadogo wanaamkiwa. :yo:
 
Daah! Sijui ndo kukosa kujiamini ama ni nini. nilikuwa naangalia KTN TV taarifa ya habari ya saa 3 usiku leo (4/4/2013) wakati Mhe. Dr. Baloz Batilda akimpa mkono Naibu Raisi wa Kenya Mhe. Ruto akaangusha na Shikamoo daah! nilichoka hivi kweli Batilda ni wa kumpa Shikamoo Ruto? au ndo confidence ilipotea kabisa. Mama jiamini wewe Dr wa PhD unaogopa namna hiyo??Update:
Hiyo shikamoo ina mengi. UHURUTO si mchezo ndugu yangu.
 
Daah! Sijui ndo kukosa kujiamini ama ni nini. nilikuwa naangalia KTN TV taarifa ya habari ya saa 3 usiku leo (4/4/2013) wakati Mhe. Dr. Baloz Batilda akimpa mkono Naibu Raisi wa Kenya Mhe. Ruto akaangusha na Shikamoo daah! nilichoka hivi kweli Batilda ni wa kumpa Shikamoo Ruto? au ndo confidence ilipotea kabisa. Mama jiamini wewe Dr wa PhD unaogopa namna hiyo??

Update:
Bila kuangalia tofauti za kiitikadi...mwanaume na mwanamke...kwa tamaduni nyingi shikamoo ni salam ya heshima japo umri ndiyo kigezo lakini ni kawaida kwa wanawake kujihisi bado wadogo na wanaume kupenda ukubwa. Si ajabu kwa mke kumwamkia mume hata kama wanatofauti ya mwaka 1. Ni utaratibu tuu usio rasmi
 
Daah! Sijui ndo kukosa kujiamini ama ni nini. nilikuwa naangalia KTN TV taarifa ya habari ya saa 3 usiku leo (4/4/2013) wakati Mhe. Dr. Baloz Batilda akimpa mkono Naibu Raisi wa Kenya Mhe. Ruto akaangusha na Shikamoo daah! nilichoka hivi kweli Batilda ni wa kumpa Shikamoo Ruto? au ndo confidence ilipotea kabisa. Mama jiamini wewe Dr wa PhD unaogopa namna hiyo??

Update:

kwa makabila ya kaskazini mwa Tanzania kwa maana Kilimanjaro na Arusha ni kawaida kwa Mwenye umri mkubwa kumwamkia mwenye umri mdogo ambaye ana nyadhifa fulani ama cheo hivyo alichofanya Mhe Balozi ni kawaida sana wala usishangae kabisa
 
Daah! Sijui ndo kukosa kujiamini ama ni nini. nilikuwa naangalia KTN TV taarifa ya habari ya saa 3 usiku leo (4/4/2013) wakati Mhe. Dr. Baloz Batilda akimpa mkono Naibu Raisi wa Kenya Mhe. Ruto akaangusha na Shikamoo daah! nilichoka hivi kweli Batilda ni wa kumpa Shikamoo Ruto? au ndo confidence ilipotea kabisa. Mama jiamini wewe Dr wa PhD unaogopa namna hiyo??

Update:
Loooh, hiyo hata mimi siipendi. Kwa Mugabe, Mandela, sawa kwa sisi waafrika.
 
HATA KAMA ANGEKUWA AMEMZIDI KWELI!
DIPLOMASIA NA TAMADUNI WAPI NA WAPI?
huwa nashangaa kweli napowaona wanawake viongozi wakiwapigia magoti wenzao!
hv ulishawahi kuona siku salma kikwete akipokea wageni pale airport?jamani huwa anakunja goti mpka huruma!usikute hapo anasema ''good morning,welcome in tanzania'' af na goti!mweeh !mweeeh!

Watu mna visa? dah!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom