Dr. Batilda Amsalimia Mhe. Ruto "Shikamoo"

Dr. Batilda Amsalimia Mhe. Ruto "Shikamoo"

Hayo mambo ya Pwani au ulikuwa hujui.....shikamooo naomba mia!!!!!! sasa si mama anataka msaada hapo
 
Hayo mambo ya Pwani au ulikuwa hujui.....shikamooo naomba mia!!!!!! sasa si mama anataka msaada hapo

Wachagga je? Hujawahi kusikia mzee anasema "Shikamoo Mwanangu" . Hapo unakuta kijana ana umatemate wa kutosha na hivyo kinachopewa shikamoo si mtu bali alichonacho mtu.
 
Kwanza wakenya wa bara hawajui salamu ya shikamoo. Ruto ni Mkalenjin sijui hiyo shikamoo aliitikiaje! Kenya shikamoo inatumika Mommbasa
 
mkuu unaniacha hoi. mwenzako lema alikuwa anamtangaza waziwazi kuwa huyo ni gaidi kwa sababu anavaa kilemba. wewe unaongea opposite, kuwa ni waheshima. akikusikia lema huenda ukawepo kwenye ile list ya lwak....

Batilda na Ruto wamepishana mwaka mmoja, ingawa Batilda ni mkubwa, ila kwa heshima ya kiafrika, Mwanamke ataamkia shikamoo kwa mtu yoyote alkiyemzidi umri au cheo!, hivyo Dr. Batild did the right thing kumwamkia Ruto Shikamoo!.

Hata ikitokea mke ni mkubwa kuliko mume, bado atamwamkia shikamoo kicheo cha ndoa tuu!. Mimi nina baba zangu wadogo, nawaamkia wake zao shikamoo, huku nimewazidi umri kwa hoja mke wa baba ni mama yako, regardless ana umri gani!.

Siku ukipata fursa, hudhuria ziara yoyote ya JK, sikilizia shikamoo anazozipata kwa watu ambao kwa macho tuu utawajua wamemzidi umri!, shikamoo hizo ni za heshima kwa mkuu wa nchi, na sio za umri!.
Dr. Batilda ni mama wa heshima sana ya kiafrika na kidini, sikumbuki kuwahi kumuona bila hijab!, mimi ni wa late 60's, nilipokutana nae kwa mara ya kwanza, sikumwamkia nikimdhania ni wa 70's, alikuwa na mwalimu wangu fulani wa Tambaza tukimwita Miss Juma!, ndipo mwalimu akaniambia "nyie watoto siku hizi mnajidai mmekuwa, mwamkie huyu shikamoo, huyo ni mama yako!, nilipigundua ni wa early 60's sasa ndio natoa shikamoo ya heshima ya umri!.

NB!, Shikamoo ni salam ya kitumwa ikimaanisha niko chini ya miguu yako!. Wakoloni Waarabu nao wametifanya vibaya, kama valivyotufanya wazungu na kasumba ya kizungu!.

Pasco.
 
Ha ha haaa! Kule Uchagani kama una cheo kikubwa au una fedha ya kutosha una uhakika wa kupata shikamoo regardless your age. Ndiyo maana watoto wadogo wanaamkiwa. :yo:
kitu cha shikamoo mwanangu sio?
aahahahhahha
cc Nicas Mtei
 
Last edited by a moderator:
huyo si ashazoea kuwa small house, nadhani alikuwa akimtega Ruto
 
Kwanza wakenya wa bara hawajui salamu ya shikamoo. Ruto ni Mkalenjin sijui hiyo shikamoo aliitikiaje! Kenya shikamoo inatumika Mommbasa

Mkuu arap Ruto anaijua shikamoo. Huyu ni miongoni mwa Wanandi (Mkalenjin) anayekijua vizuri kiswahili
 
Hakuna justification yoyote ile kuh Batilda kumuamkia Ruto ambaye ni mdogo kwake kiumri kwa 'shikamoo'.
Amechemka big tym. Hakuna cha jinsia, mapokeo, utamaduni, madaraka (tarajiwa) ya Ruto, wala nn.

Simply ni kuwa Batilda amekosa confidence.
Pity on her & us (Tz).
Ataweza kutetea maslahi ya Tz huko Ke?
Sidhani.

Tuache kutetea makosa. Hiki ndicho kinachotugharimu waTz.
 
Jana nilishangaa Dialo alimwamkia Rais wa nch shikamoo. Hivi dialo na kikwete nani mkubwa?
 
Ni kawaida ya magamba ndo maana hata wameshindwa hata kuliletea taifa maendeleo
 
...Namuona Dr. Batilda kama mtu asiye na majivuno. Nilikutana naye anatoka ktk booth ya ATM, akawa wa kwanza kunipa salam, wakati hanijui, na kama kawaida alikuwa amejisitiri vizuri. Sasa hii sio 'gesture' ndogo kwa aina ya wanasiasa tulio nao, ambao kila mahali walipo wanataka watambuliwe kuwa wapo juu kuliko raia wengine.

Hata hivyo, nadhani alishikwa na kiwewe cha ghafla alipokutana na makam wa rais mtarajiwa. Si mtaalam wa diplomasia, lakin nadhani hata Ruto angemzidi miaka 5, bado haikuwa sahihi kumpa 'shikamoo'. Angemwambia 'Salam Aleikum'. Haya mambo yana maana kubwa kidiplomasia-yana maana upo submissive, unaweza kupewa ndoana ukameza. Kuna video moja maarafu kati ya rais wa USSR na Kennedy, ambapo kila mmoja wao anamtegea mwenzake awe wa kwanza kuingia ndani, mmojawapo anaenda mbali zaidi na kumshika bega mwenzake akimtanguliza ndani! Yote hiyo ni ktk kuonyesha supremacy!
 
Hivi JK akikutana na Wassira wanasalimianaje?au JK na Josee Kabila wa Kabange?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom