Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,987
MKURUGENZI wa Mashitaka nchini ( DPP), Sylvester Mwakitalu, amesema kwa sasa hakuna mwalifu atakayenufaika na mapato ambayo ameyapata kwa njia ya rushwa au uharifu, kwa maana hiyo fedha na mali zitataifishwa.
Amesema Rushwa ni janga kubwa na athari zake zinaonekana katika ngazi ya taifa na Kimataifa.
DPP Mwakitalu, ameyasema leo Mkoani Dar es Salaam, wakati wa kongamano Maalumu kuhusu mapambano dhidi ya Rushwa iliyowahusisha Jeshi la polisi, Takukuru na Taasisi nyingine 11
Amesema kati ya mambo ambayo yanafanyiwa msisistizo kuhakikisha kwamba rushwa na makosa yoyote ya kupangwa yanakabiliwa kikamilifu na si kwa waalifu wanapewa adhabu tu làkini wanakwenda zaidi kutafuta mali na fedha zilizopatikana kwa njia ya uharifu .
," Natoa meseji kwamba uhalifu haulipi bali unapewa adhabu na pia mali ambazo zimepatikana kwa njia ya rushwa zitataifishwa," amesema
Ameongeza kwamba lengo kubwa la kongamano hilo ni kuimalisha mapambano dhidi ya Rushwa na kuhakikisha hakuna mwalifu atakayenufaika na uhalifu.
Akizungumza kuhusu hatua kadhaa zilizochukuliwa kisheria ni pamoja makosa yote ya Rushwa yalikuwa lazima kufika Makao Makuu na DPP mwenyewe lazima kuyaona kisha kusaini vibali làkini.
DPP alisema baada ya kuona umuhimu wa jambo hilo kwa sasa wametatua kwa kutoa sheria ndogo ambayo imewezesha wakuu wa mashitaka wa mikoa na Wilaya kupewa vibali isipokuwa kwa makosa machache yale ambayo yanafedha nyingi au yanayogusa viongozi wa Serikali.
"Kuna makosa machache ambayo natakiwa kuyaona ili niweze kutoa maagizo làkini kwa sasa kesi nyingi zinaishia mkoani mkuu wa mashitaka wa mikoa wanakaa na vyombo vya uchunguzi wanapitia majalada kwani kwa sasa hakuna ucheleweshwaji tena kesi zinasikilozwa," amesema
DPP Mwakitalu, amezungumzia mafanikio ambayo yanapatikana baada ya kuwa na kongamano ni pamoja na kuwajengea uwezo na kisha uchunguzi unafanyika kwa weledi na mashitaka kwa weledi kwani kesi ikichukuwa muda mrefu bila kuisha yako mambo yanajitokeza,
"Kesi ikichukuwa muda mrefu haijafika mwisho yapo mambo yanajitokeza hapa Kati ya mashahidi kwani ni binadamu wanafariki wanahama, wanapotea, hivyo kuna kuwepo na athari nyingi zinaweza kusababisha kesi nyingi zisifike mwisho
" Sio kwa sababj hakukuwa na kosa au ushaidi làkini pengine mashahidi hawapo tena na ushahidi wake haupo tena, hivyo kusikiliza kesi kwa haraka na kufika mwisho inatupa matokeo mazuri," amesema.
Nae mgeni rasmi katika kongamano hilo Naibu Waziri wa nchi, ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora, Deogratius Ndejembi, amesema mapambano dhidi ya rushwa yanahitaji ushiriki mpana wa wananchi, wadau mbalimbali na mbinu imara na endelevu.
Ndejembi ambaye ndiye mgeni rasmi katika kongamano ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kongamano maalumu kuhusu mapambano dhidi ya rushwa.
Amesema kutokana na umuhimu wa kupambana na Rushwa Serikali imetunga sheria kanuni na miongozo mbalimbali na kwa sasa mapambano dhidi ya rushwa yanaratibiwa na kusimamiwa na ofisi ya Rais Ikulu kupitia mkakati wa Taifa dhidi ya rushwa .
Ameongeza kuwa Serikali inatambua uwepo wa changamoto nyingi katika kupambana na rushwa kama ambavyo imekuwa ni changamoto ya maendeleo nchi nyingi duniani.
"Hata hivyo juhudi za Serikali kupambana na Rushwa zimeonesha mafanikio makubwa licha ya changamoto tunazozipata ambazo nina Imani kuwa nazo zitatatuliwa kupitia mikakati ya Serikali," amesema.
Kwa upande wa mwakilishi wa Takukuru, Dk. Emmanuel Kiyabo, alitaja changamoto wanazokabiliana nazo kiwa ni wananchi wanakuwa wagumu kutoa ushirikiano wa kutoa ushahidi
Pia Takukuru wanakabiliwa na changamoto ya kifedha kwa ajili ya kufanya kongamano mbalimbali
Katika kesi 100 mwaka 1995 tulikuwa tunafikia asilimia 40! kwa sasa ni asilimia 60 na tunatarajia kufikia asilimia 80 hadi 90 kwa malengo yajayo