Sheria inazuia kumtaja kwa jina, makazi au anwani ya mtu aliyetoa taarifa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
Rushwa 1.jpg
Kifungu cha 39 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya Mwaka 2007 kinatamka kila mtu mwenye taarifa kuhusu kufanyika kwa vitendo vya rushwa au mpango wa kufanyikwa kwa vitendo vya Rushwa anawajibika kutoa taarifa kwa TAKUKURU.

Ukikosa huduma katika mazingira ya Rushwa, Sheria hiyo inaeleza wazi kuwa kuna umuhimu wa kutoa ulinzi kwa Watu wanaotoa taarifa, mfano, kifungu cha 51(1)(a) kinazuia kutajwa kwa jina, makazi au anwani ya mtu aliyetoa taarifa.

Kifungu cha 51(1)(b) kinazuia shahidi kujibu swali ambalo jibu lake laweza kusababisha kujulikana kwa mtu aliyetoa taarifa juu ya vitendo vya rushwa ambavyo vimepelekea kuwepo kwa mashitaka mahakamani.

Wajibu wa Mwananchi katika Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini
Kama ilivyokwisha kuelezwa hapo awali, Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007 imedhamiria kuushirikisha umma katika mapambano dhidi ya rushwa nchini. Hii inatokana na ukweli kwamba mapambano dhidi ya rushwa nchini yanaweza yasifanikiwe kama umma wa Watanzania hautashirikishwa kikamilifu.

Kwa mantiki hiyo, Kifungu cha 39 cha sheria hii kinatamka bayana kwamba kila mtu mwenye taarifa kuhusu kufanyika kwa vitendo vya rushwa au kuhusiana na mpango wa kufanyikwa kwa vitendo vya rushwa unaopangwa na mtu au kundi la watu anawajibika kutoa taarifa kwa TAKUKURU.

Aidha, sheria imeeleza bayana kwamba ili kufanikisha wananchi kutoa taarifa kwa TAKUKURU kwa urahisi zaidi, kanuni au utaratibu wa kufanya hivyo utaandaliwa.

Ulinzi kwa Watu Wanaotoa Taarifa Kuhusiana na Rushwa au Mashahidi
Ili kuhakikisha kwamba wananchi wanashiriki kikamilifu na bila hofu katika vita ya rushwa, Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007 imeanzisha mpango wa kutoa ulinzi kwa watu wanaotoa taarifa kwa TAKUKURU kuhusiana na vitendo vya rushwa na pia mashahidi katika kesi za rushwa.

Kwa mfano, kifungu cha 51(1)(a) cha sheria hii kinazuia kutajwa kwa jina, makazi au anwani ya mtu aliyetoa taarifa kuhusiana na vitendo vya rushwa kwa shahidi anayetoa ushahidi mahakamani.

Hali kadhalika, kifungu cha 51(1)(b) kinazuia shahidi kujibu swali ambalo jibu lake laweza kusababisha kujulikana kwa mtu aliyetoa taarifa juu ya vitendo vya rushwa ambavyo vimepelekea kuwepo kwa mashitaka mahakamani.

Ili kutoa ulinzi kwa mtu anayetoa taarifa za kufanyika vitendo vya rushwa au mpango wa kufanyika vitendo hivyo, kifungu cha 51(3) cha sheria hii kinafafanua kwamba kama mtoa taarifa atatishiwa kuumizwa au kulipiziwa kisasi na watu aliowataja

Yajue Makosa ya Rushwa au maswahiba wao, basi serikali itafanya mambo au jambo moja kati ya haya:
(a) itampa mtu huyo ulinzi wa kutosha kulingana na vitisho anavyopata;
(b) itamlipa fidia inayolingana na madhara aliyoyapata; au
(c) itampatia msaada wa aina nyingine unaolingana na mahitaji halisi.

Angalizo:
Ni vema ikumbukwe kwamba fidia, msaada au ulinzi kwa mtoa taarifa anayetishiwa vitatolewa na serikali pale tu TAKUKURU itakaparidhishwa na kuwepo kwa vitisho hivyo, na pia ukubwa wa vitisho hivyo.

Aidha, kifungu cha 52 cha sheria hii kinatoa ulinzi kwa mtu yeyote anayetoa taarifa au ushahidi kuhusiana na kufanyika kwa vitendo vya rushwa. Ulinzi huo ni pamoja na

(a) kutounganishwa kwenye mashitaka ya rushwa mahakamani; ou
(b) kutofunguliwa kesi ya madal au ya jinai mahakamani kwa sababu ya kutoa taarifa hizo.

Mambo Mengine ya Msingi katika Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini
Ni vema pia kufahamu kwamba Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007 imeanzisha mambo kadhaa ya msingi na ambayo yanasaidia kuongeza nguvu katika vita dhidi ya rushwa nchini. Mambo haya ni pamoja na:

Mahakama kutoa amri ya kukamata na kutaifisha mali zilizopatikana kwa njia au vitendo vya rushwa (kifungu cha 38);

TAKUKURU ikishirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) au mahakama yenyewe, kuwa na uwezo wa kukamata na kufilisi mali iliyopatikana kwa njia au vitendo vya rushwa (kifungu cha 40);

Mwajiri au idara ya serikali ambayo mtumishi wake alitoa rushwa anaweza kufungua kesi ya madai na kuiomba mahakama itoe amri ya kurejeshewa pesa au mali hizo dhidi ya mtu aliyepokea rushwa (kifungu cha 44);

TAKUKURU imepewa nguvu na uwezo wa kushirikiana na idara nyingine, hasa zile zinazosimamia utekelezaji wa sheria, katika vita dhidi ya rushwa nchini (kifungu cha 45);

TAKUKURU imepewa nguvu na uwezo wa kushirikiana na sekta binafsi katika vita dhidi ya rushwa nchini (kifungu cha 46);
 
Back
Top Bottom