Hashpower7113
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 1,353
- 2,137
Criminal Case No.208/2016 iliyokuwa ikimkabili Tundu Lissu na wenzake watatu katika Mahakama ya Kisutu, imefutwa na DPP kwa mujibu wa Kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo ya Makosa ya Jinai. Watuhumiwa wote wako huru.
Mbali na Lissu washtakiwa wengine walikuwa ni Mhariri wa Gazeti la Mawio, Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehbooh
Washtakiwa hao kwa pamoja Walikuwa wanakabiliwa na mashtaka matano likiwamo la kuandika habari za uchochezi kinyume na sheria ya magazeti ya mwaka 2002.
Patrick Mwita wakili wa serikali mbele Thomas Simba Hakimu Mkazi Mkuu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alisoma shitaka la kwanza na tano.
Mwita alidai kuwa shitaka la kwanza ni la kupanga njama za kutoa chapisho la uchochezi, kosa linalodaiwa kutendwa kati ya tarehe 12 na 14 Januari mwaka 2016 ambapo;
Idrissa, Mkina na Lissu katika eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam walipanga njama za kuchapisha taarifa za uchochezi.
Katika kosa la tano, mshitakiwa namba moja (Idrissa), namba mbili (Mkina) na namba nne (Lissu), wanatuhumiwa kuchochea hofu miongoni mwa wananchi kwa kuchapisha habari “Machafuko yaja Zanzibar” na kwamba, ingeweza kuzua vita au umwagaji damu.
Shitaka pili likimkabili Jabir, Mkina na Lissu, wakidaiwa kuchapisha chapisho la uchochezi katika Gazeti la MAWIO, toleo Na. 182 la tarehe 14-20 Januari 2016.
Shitaka la tatu linamuhusu Ismail akidaiwa kuchapisha chapisho la uchochezi katika gazeti hilo lenye kichwa cha Habari ‘Machafuko yaja Z’bar’.
Shitaka la nne linamkabili Ismail akidaiwa kuchapisha gazeti bila kupeleka kiapo kwa Msajili wa Magazeti.
Zaidi, soma;
Thread 'Lissu, Mhariri wa Mawio wafikishwa kizimbani leo' Lissu, Mhariri wa Mawio wafikishwa kizimbani leo