Heshima kwako mkuu na Hepi New Year!
Japo haijakamilika doc inatupa japo nini kiliendelea nyuma ya pazia. Mawazo au maswali yangu katika hili ni haya:
1. Mkataba na Richmond ulikuwa for emergency purpose baada ya ukame 2005 mwishoni lakini Tanesco wameendelea kuhangaika na zigo hilo mwezi December 2006 kipindi hicho tunatapisha mabwawa. Hii inapingana na kinachosemwa kuwa ni public interest.... providing much-needed power to the national grid (509)
2. Ni wazi PPA Act ya 2004 haijitoshelezi ama imeachwa hivyo makusudi as far as void or avoidance of contract is concerned. (510)
3. CRDB imeendelea kutumika kupitisha uoza kama ambayo imeonekana kuikingia kifua Dowans. Mkuu wa hii benki kwa vyovyote vile ni mmoja wa genge hili la wahujumu (514 sec17.6)
4. Hapa unaona makosa ya makusudi kabisa ama makosa yanayotokana na shinikizo. No Due dilegence kabisa maana kampuni inaonekana kuelea kati ya anga la Rica na U.A.E (514 sec 17.10)
5. (514 sec 17.11) Hapa unamtambua Rostam kuwa ni zaidi ya mafia walotikisa dunia miaka ya nyuma. Ana power of Attorney tu kukamua mamilioni yetu. With all the businesses he is believed to run, hakuna hata moja utakuta jina lake which is to say No legal proceedings can find him guilty of wrong doings. Kuna mwana JF mmoja aegusia kulipuka nae, pengine hiyo pekee ndio inaweza kumzuia kutenda anayotenda kwa sasa.
Maisha ya wana Igunga ni ya kupigika ile mbaya lakini jamaa wanampa political haven toka alipokufa Kabeho miaka ya Tisini. Angalau anachoiba angekuwa anakipeleka kule.
6. Pale kwenye 519 wanaongelea competitive bidding, wakati mkataba unafaulishwa kutoka Richmond kwenda Dowans was that a competitive bidding???
Kwa ujumla ni kwamba Tanesco walikuwa na hoja lakini kwa makusudi hawakuwa na vielezo matokeo yake inaonekana Dowans ndo walikuwa wameshika ng'ombe (Bull) kwa pembe zake. Kama mzee wa kikofia (gwiji wa sheria) ndo alikuwa upande kwa Dowans na anajulikana kwa fitna za kisheria sioni mahali Tanesco wangefurukuta.
Kesi hii tukubali kwamba tumeliwa na kama serikali isingekuwa inamilikiwa na kina RA basi tungeweza kusema tugome kulipa tu based on moral grounds. Mbona kesi ya Chavda (kama sikosei) mpaka leo serikali imeweka mguu chini???
Tuwekee na hiyo Part II ili tujue moja.