Unajua slogan ya Jamiiforums ni "Forum for great thinkers". Tatizo la Forum hii sasa kuna hata vihiyo nao wanataka kuwa thinkers! Dr. Slaa kusema Dowans ni ya Kikwete ana maana zaidi ya hiyo. Ni kweli ni ya JK kwa maana bila serikali yake kukubali kampuni ambayo dalili zote ni ya kitapeli ina maana ni "yake". Hao waliotajwa hapo wote ni geresha wenyewe wapo na wanajulikana kma alivyosema Samuel Sitta. Mbona Kagoda ilisemekana ni kampuni ya kina Komuhendo lakini ni ukweli nyuma yao kuna kigogo mmoja? Nini tofauti ya Dowans na Kagoda? Nauliza.