DOWANS: Slaa ulituongopea! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DOWANS: Slaa ulituongopea!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by wimbi la mbele, Jan 7, 2011.

 1. w

  wimbi la mbele JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 647
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Majina ya owners wa Dowans jana yametolewa na sijaona jina la JK kama ilivyodaiwa na Slaa. Slaa kama kiongozi wangu shupavu amenivunja sana moyo. I need a leader I could trust na sio kiongozi mwenye Jazba na anyezungumza bila ya kuwa na facts

  Hizi si zama za abuniasi kuambia uwongo ili mradi uandikwe kwenye magazeti

  Unasema JK own DOWANS lete ushahidi

  This is disgusting na mimi sitaki kuwa na kiongozi ambaye alikuwa ni Mchungaji na mtu wa Mungu

  Unless ana ushaidi mwingine so i stand to be corrected lakini majina ya waliotajwa jana sijaona jina la JAKAYA MRISHO KIKWETE!!!!!
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,267
  Likes Received: 19,410
  Trophy Points: 280
  kuna mtu wa serikalini anayeweza kusimama na kupanua domo lake na kusema JK owns dowans? Dont swallow everything..kwa hiyo una uhakika gani kuwa hao waliotajwa ni changa la macho?
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Hahahahahah,katumwa huyo,na ni mamluki!kwani KIWIRA ilikua ya nani?si ya MKAPA?alishawah kutoka hadharani akakubali?mbona huyo anakua na akili kama za dagaa?
   
 4. n

  niweze JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wewe Kweli ni Kichwa Maji Kweli.

  Huyu JK unayemwita Kiongozi Wenu wa CCM Hujiulizi Maswali Kabla ya Kuelekeza kwa Watanzania Wenzako Wanaotafuta Ukweli wa Dowans. Kitu Gani Kiliwafanya CCM Kusubiri Kutoa Majina Wanao Own Dowans?
  Kwanini CCM Wamesubiri Mpaka Wananchi Wanataka Kupindua Hii Nchi na Kwa Kuandamana na Kufanya Mikutano Ndio Majina Yanatolewa? Unataka Kutueleza CCM Walikuwa Wanatafuta Majina ya Wanao Own Dowans Kwenye Google?

  Mkataba Ulisaini Mwaka Gani? na Hayo Majina Yametolewa Lini? Swala Lilipotolewa Bungeni Mwaka Sasa Mbona Hao Kwenye Majina Wananchi Hatukuwaona Wakitetea services na dhamana ya huu mkataba? Kweli acha ujinga na uuwaji wako.

  Mnapiga Risasi Wananchi Halafu Mkisikia Wananchi Wanajipanga Mnakwenda Kurodhesha Majina ya Foreigners Mitaani na Kuwalipa Pesa ili Wakubali Wao ni Watu Miliki. Tutajua Ukweli Sio Kutoka Kwa CCM. Dowans na Kashfa Zote za TAIFA Letu Ndizo Zitamng'oa JK na Sio Vingine, JK Hafiki 2015 Wananchi Mashahidi. This Time No More.

  "Muda wa Kucheze Watanzania Akili Umekwisha na Wajinga ni Nyie Sio Wananchi"
   
 5. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2011
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Si kosa lako bali la aliyekuroga
   
 6. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #6
  Jan 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Shame to you and Ngeleja!!!!!!!!
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Jan 7, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Unajua dola milioni 2 za JK mwaka 2005 zilitoka wapi na kwa nani? Ukijua jibu la swali hilo utajua kuwa Dr. Slaa hakusema uongo na utaelewa ni kwanini Dowans ilikuwa ni lazima walipwe kwa mbinde au kwa upinde.
   
 8. Mbwiga_Plus

  Mbwiga_Plus Senior Member

  #8
  Jan 7, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na kwa taarifa yake huyu wa kuja ni kwamba hata hawa waliotajwa ni mpango uliosukwa fasta ili kumsafisha JK...KWANI SIKU ZOTE WALIKUWA WAPI KUWATAJA?...HUONI KWAMBA KITENDO CHA SLAA KUSEMA VILE KIMEHARAKISHA SERIKALI KUWATAJA HAO WATU.?..JAPOKUWA wa hakika ni changa la macho!
   
 9. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #9
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,446
  Likes Received: 5,833
  Trophy Points: 280
  Usiri wote uko kwa DOWANS SA ya Costa Rica...nani mmiliki?
   
 10. m

  mams JF-Expert Member

  #10
  Jan 7, 2011
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 616
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Maskini nchi yangu Tz, siijui hatima yako.
   
 11. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #11
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,446
  Likes Received: 5,833
  Trophy Points: 280
  Halafu Ngeleja haonyeshi hata uchungu wa kushindwa TANESCO kwenye kesi....anaonyesha kabisa yuko upande gani...yaani mtu akuibie mkeo halafu unamtetea?
   
 12. mzozaji

  mzozaji JF-Expert Member

  #12
  Jan 7, 2011
  Joined: Jul 28, 2010
  Messages: 257
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Weka basi hayo majina au na wewe unatuongopea????
   
 13. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #13
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,446
  Likes Received: 5,833
  Trophy Points: 280
  Raymond Kaminyoge
  SERIKALI imeamua kuilipa kampuni ya Dowans Tanzania Ltd, Sh 94 bilioni kama ilivyoamuliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi (ICC) na kuwataja wamiliki na wakurugenzi wa kampuni hiyo ambao wote si Watanzania.

  Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alisema hayo jana jijini Dar es Salaam, katika mkutano wake na waandishi wa habari.
  Alisema Sh.185 bilioni zilizokuwa zikitajwa kwenye vyombo vya habari ndizo ambazo kampuni ya Dowans iliiomba ICC ilipwe fidia kwa Tanesco kwa kukatiza mkataba walioingia wa kufua umeme, lakini mahakama iliafiki ilipe dola 65 milioni za Marekani.

  Alisema fedha hizo zitalipwa baada ya pande hizo zitasajili uamuzi huo katika mahakama kuu.

  " Serikali tumekwishaamua kuwa tutailipa Dowans dola za Marekani 65 milioni, kama ilivyoamuliwa na ICC ambazo ni sawa na Sh 94 bilioni, kuchelewa kuwalipa kutatufanya tulipe riba ya asilimia 7.5," alisema.

  " Siyo kwamba kiasi tunachotakiwa kulipa ni kidogo, ila tumeona ni muhimu Watanzania wakafahamu kiasi halisi ambacho tunatakiwa kuilipa Dowans," alisema.

  Alisema wameamua kulipa baada ya mwanasheria mkuu wa serikali, kusema kuwa hukumu hiyo ilikuwa halali na kuipinga kungeizidishia serikali gharama.

  "Mwanasheria mkuu wa serikali ameshauri kutekeleza uamuzi wa mahakama ya usuluhishi endapo uamuzi huo utasajiliwa katika mahakama kuu ya Tanzania," alisema Ngeleja.

  Aidha Ngeleja aliwataja wamiliki wa Dowans Tanzania Ltd, na hisa wanazomiliki katika mabano kuwa ni Dowans Holding S.A ya Costa Rica (81) na Portek Systems and Equipment (PTE) LTd (54).

  Aidha Waziri Ngeleja huku akirejea barua ya Wakala wa Usajili wa Kampuni (Brella), aliwataja wakurugenzi na nchi wanazotoka kuwa ni Andrew James Tice (Canada) na Gopalakrishnan Balachandaran (India).

  Wakurugenzi wengine kwa mujibu wa Waziri Ngeleja ni Hon Sung Woo (Singapore), Guy Picard (Canada), Sulaiman Al Adawi (Oman) na Stanley Munai (Kenya).

  Kiini cha sakata hilo kilianza mwaka 2006, wakati Tanesco ilipoingia mkataba wa mauziano ya umeme wa Tanesco na kampuni ya Richmond Developmen LLC.

  Miezi sita baadaye mkataba huo ulihamishiwa kwa kampuni ya Dowans Holdings ya nchini Costa Rica na baadaye kwa Dowans Tanzania Ltd,
  Wakati wa utekelezaji wa mkataba huo, ilizuka hoja kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo wabunge kwamba mkataba baina ya Tanesco na Richmond haukuwa halali kisheria hivyo usingeweza kurithiwa na Dowans.

  Suala hilo lilizua mjadala mkubwa hali ambayo Tanesco kwa kuwatumia mawakili wa kampuni ya Rex Attorneys ya jijini Dar es Salaam walivunja mkataba huo.

  Baada ya kuvunjwa kwa mkataba huo, ndipo kampuni hiyo ikalipeleka suala hilo ICC kama walivyokubaliana na Tanesco kwenye mkataba.
  Uamuzi huo wa ICC ulizua mjadala katika siku za hivi karibuni baada ya viongozi wa serikali kutofautiana kuhusu kuilipa kampuni hiyo au kutoilipa.

  Wakati Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Samwel Sitta, akiitaka serikali kutolipa Dowans kwa kuwa kufanya hivyo ni uhujumu wa nchi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema akitaka kampuni hiyo ilipwe.
   
 14. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #14
  Jan 7, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Inasikitisha sana yaani wanachakachua mpaka majina?
   
 15. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #15
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,446
  Likes Received: 5,833
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  The Portek Group, established in 1988, and headquartered in Singapore, is a turnkey provider of equipment, services and solutions to ports globally, as well as an operator of medium sized container and multipurpose ports.

  As a provider, we are able to deliver both capacity and productivity solutions to port operators by enabling them to gear up quickly to meet their demand surge in cargo traffic. Our range of competencies includes port equipment modernisation, modification, mobilisation and maintenance, equipment leasing and sale, accident recovery and repairs, consultancy services, and distribution of components and parts.

  Portek also provide IT based productivity enhancement solutions through its Portek IT & Automation Pte Ltd. Its offerings include software for Container Terminal Management System, Terminal Planning and Simulation software, Automation solutions such as Container Position Determination Systems, and Optical Character Recognition System for gate automation, Radio Data Terminal Systems, among others.

  [​IMG]

  Significantly, Portek operate and manage a portfolio of 7 medium sized container and multipurpose terminals in Indonesia, Algeria, Malta and Gabon. Portek's in-house ability to deliver equipment, implement IT systems, and provide port management is a compelling factor in it's been selected by port authorities or terminal operators as a trusted partner to operate those concessions. Also important is our ability to fast-track port modernization and transformation, and hence significantly shorten "time to market".

  Mimi sijaona DOWANS ikitajwa na hawa wakuu kama moja ya biashara zao pamoja na kumiliki 54% shares za DOWANS kwa mujibu wa mwanasheria Ngeleja
   
 16. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #16
  Jan 7, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Dowans kosa lao lipi? Rostam kosa lake lipi? JMK kosa lake lipi?

  Jee, hamkuona yale madege yakishusha hii mitambo?
  Jee hamkuona hiyo mitambo pale Ubungo?

  Jee ni haki Tanesco kuvunja mkataba?

  Jee mawakili wa Tanesco wamelipwa kiasi gani?

  Jee mawakili wa Dowans wamelipwa kiasi gani?
   
 17. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #17
  Jan 7, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  So you believe everything you hear!!
  I wish you all the best
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  Jan 7, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Ukisema kazi zao una maana gani? Kwani walishindwa kuifanya kazi walioahidi?
   
 19. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #19
  Jan 7, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135


  Utakuwa na matatizo ya mtindio wa ubongo
   
 20. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #20
  Jan 7, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  umetumwa wewe.

  katika akili zako mbovu ulizani serikali hii ya kifisadi ingemtaja kikwete.

  subiri. atatajwa na Mungu.
   
Loading...