Dowans: Another Richmond in making?

Dowans: Another Richmond in making?

Watu waeshindwa kumuelewa Zitto. simpo. Na sababu za kuto-muelewa zinajulikana kwa wenye kutafakari. Zitto Hana kosa alilotenda.
 
Nheshimiwa Zitto Kabwe kaitia hasara kambi nzima ya upinzani kwa msimamo wake wa kijinga wa kupenda kuropoka jambo bila kuangalia athari zake.Zitto kaunga mkono ununuzi wa mitambo mtumba wa Downs wakati uchaguzi mkuu unakaribia.

Mbaya ni pale wajumbe wa kamati yake walipoanza kumruka kwamba baadhi ya hoja anazozitetea mheshimiwa Zitto ni zake binafsi wala hakutumwa na kamati ya bunge kusema anayoyasema.

Ukisikiliza kwa makini hoja za mheshimiwa Mwakyembe na mheshimiwa Zitto unatagundua kwamba Mheshimiwa Zitto alivutiwa kitu kidogo au alikuwa promised atavutiwa baada ya deal kufanikiwa.

Ningependa kumshauri Mheshimiwa Zitto kujiuzulu nafasi ya naibu katibu mkuu na asigombee ubunge kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2010 ili kulinda heshima ya chama na upinzani kwa jumla.

Naomba kuwasilisha.
 
========

Issue nzima ilikuwa emotional. Hakuna haja ya kujiuzuru. Hata mimi niliudhika kuona Zitto anajitungika kitanzini kisiasa. Lakini Zitto bado anapenda kutembea kwenye tight line. Afanye Mea Culpa yaishe, twende mbele. Mafisadi ulimi nje.
 
Wewe unaandika hapo kama msemaji wa chadema na huo ndio msimamo wa chadema , chama kilikaa kikao na kuamua kuja na kichwa hicho cha habari au unaongea wewe kama wewe huna jina , huna anwani
 
Mimi kama mwana chadema ambaye nimejitahidi kuhamasisha vijana wengi walioko nje na ndani ya nchi ujiunga na chadema nimekatishwa tamaa kiasa kikubwa na Zito kabwe na ushabiki wake wa kununua dowans.

Unapigania CHADEMA ama ufuasi wako ni mtu/watu?
 
Kinepi siamini kama umewahi kuchangia chochote chadema zaidi ya hayo mauza uza unayojaribu kuelezea hapo juu tunaomba uje na jina lako kamili na taarifa yako kamili kama wewe ni mwanachama hai wa chadema na unakitakia chama hicho maisha marefu mbeleni
 
Mimi kama mwana chadema ambaye nimejitahidi kuhamasisha vijana wengi walioko nje na ndani ya nchi ujiunga na chadema nimekatishwa tamaa kiasa kikubwa na Zito kabwe na ushabiki wake wa kununua dowans.

Sasa ndugu unakata tamaa mapema namna hiyo kana kwamba Zitto ndiyo alikuvutia ili ujiunge na Chadema,,ungekuwa CCM ungekata tamaa mara ngapi,, mara ya Chenge, mara ya Lowasa,mara ya Kara, Rostam, nk

Ndugu zangu tuanze kujiunga ktk vyama kwa kuangalia sera za vyama si kuvutiwa na mtu mmoja ndani ya chama. Tukubali kuwa watu huingia ndani ya chama na kutoka lakini msingi wa chama hubakia palepale. Chadema si Zitto, si Slaa na wala si Mbowe na ukishajua hilo huna haja ya kukata tamaa anapechemka mmoja wao,, tujitahidi kuplani namna ambavyo tunaweza kuinua chama si kulaumu chama kwa mtu mmoja kuchemka.

Mwacheni Zitto akafie mbali na ubishi wake wa kimsimo ambao yeye mwenyewe ameshasema ya kuwa "I am Zitto Zuberi Kabwe, i here stand......" hakusema "I am the Dep Secret of Chadema....." yaani inamaanisha kuwa huo ni msimamo wake pekee na si wa chama na hana lazima ya kusema maneno haya akiwa mwanachama wa chadema tu,, angeweza kusema hata akiwa TLP, UDP, DOWANS, CCM, EPA, VIJISENTI au CUF. (maana nasikia siku hizi hata dowans, epa na vijisenti ni vyama vya siasa)
 
Watu waeshindwa kumuelewa Zitto. simpo. Na sababu za kuto-muelewa zinajulikana kwa wenye kutafakari. Zitto Hana kosa alilotenda.

Kwa kweli ilikuwa ni vigumu kwa wengi wetu kumuelewa, lakini kwa sababu tofauti kabisa. kwa hiyo inabidi upanue kidogo wigo wa sentesi yako. Binafsi zikumuelewa si kwa sababu alikosea kwa HOJa. Ni kwa sababu alikosea kama mwanasiasa. Angekuwa katika taaluma nyingine kama mwalimu anayefundisha, ningeona hana kosa kabisa, lakini kwa hili amekosea kisiasa. Kama mwanasiasa kijana angepima upepo wa kisiasa ulivyo. Hebu shangaa, Rostam Aziz anasema haifahamu Dowans, halafu anakuja anasema anaifahamu lakini si yake, anasema alifanya nao biashara, anasema walitumia anuani yake ya biashara, lakini leo hii watu wanauliza Dowans ni nani? Wanakwenda mahali wanakuta wafanyakazi wa Dowans wamiliki hawaonekani. Tulielezwa ni wawekezaji wa kigeni, lakini siku zinahesabika tutaambiwa VINGINEVYO tena kwa KISHINDO.

Kwa hiyo, kwa utata wa Dowans na mama yake Richmond, kwa jina baya la Richmond na mwanae Dowans, ni kunywa sumu kuwa karibu na kampuni hizo. Hizo kampuni zimefunikwa na siri nzito ambayo Dk. Rashidi hajawaambia kamati ya Zitto wala ya MWakyembe.

Jambo la pili, Zitto hajatofuatiana na kamati na nina hakika na hilo kwa asilimia mia moja. Tatizo la Zitto ni kuwaamini mno waandishi wa habari wengi ambao baadhi wamemuumiza sana katika suala hili. Gazeti la Mwananchi, Tanzania Daima, TBC wamepotosha kwa viwango tofauti kauli ya Zitto. Mutashangaa ni kwanini hajakanusha, mutashangaa ni kwanini Tanzania Daima, mutashangaa na wengine (pengine hata yeye) wakaibuka na kubisha kwamba si wote walipotosha.

habari inayotokana na tafsiri mara nyingi kila mtu huwa na tafsiri yake.

Zitto asingeweza kuzungumza nje ya yale waliyokubaliana ndani ya Kamati. Kosa lake ni kuitaja Dowans katika mtiririko wa maelezo yake yanayoonyesha anaihurumia Tanesco na mtu asiye makini ataona kwamba anaunga mkono kila kitu (ikiwamo Dowans) wanachotaka Tanesco. Kosa lingine ni pale aliposema "Hata kama ni kununua Dowans, iwe ni baada ya kamati zote mbili kujiridhisha na bila kukiuka sheria na taratibu", hapo mtu anakuja na kusema Zitto anaunga mkono kununua Dowans. Ukirudia hiyo sentensi (si waandishi wote wanarudia walichosikia, au kurekodi).

Kosa lingine ni pale mtu anapouliza, "inaonekana sheria ni kikwazo, je, sheria inaweza kubadilishwa?" jibu kwa yeyote litakuwa, "ndio, sheria si msahafu, kama kuna ulazima wa kufanya hivyo kwa maslahi ya taifa, itabadilishwa"... sasa leading questions na kutokuwa makini kutafsiri kauli za watu, ni mambo ambayo yamemponza Zitto.

Bahati mbaya sana Chadema (hata CCM) wanasiasa wetu hawana wasaidizi wa kudumu ambao kila jambo wanalifanyia uhakiki kabla halijawafikia waandishi wa habari, vinginevyo Zitto angetumia hoja hii hii ambayo imemgeuka kuzidi kuwabana CCM na Tanesco, lakini sasa ni kinyume.

Kwa mwanasiasa kijana, Zitto ana nafasi kubwa na nyepesi zaidi kujijenga na kupasua katikati ya wingu zito la sakata la Dowans na kufanya maajabu zaidi kisiasa. Ana uwezo huo na wengi wanamkubali na ninaamini WATAMUELEWA.

Ni bahati mbaya sana, watu hawakumsikiliza alipozungumza na ITV, na bahati mbaya sana TBC hawakumuacha azungumze kile wasiochata kisikike kwa umma na matokeo yake watu wakapata nusu nusu na nusu ingine wakaipika wao kwa kusema, "Kamati ya Zitto imeishauri serikali inunue DOwans" wakati huo ulikuwa ni UONGO wa dhahiri. Hakusema na hatosema hivyo.
 
Sasa ndugu unakata tamaa mapema namna hiyo kana kwamba Zitto ndiyo alikuvutia ili ujiunge na Chadema,,ungekuwa CCM ungekata tamaa mara ngapi,, mara ya Chenge, mara ya Lowasa,mara ya Kara, Rostam, nk

Ndugu zangu tuanze kujiunga ktk vyama kwa kuangalia sera za vyama si kuvutiwa na mtu mmoja ndani ya chama. Tukubali kuwa watu huingia ndani ya chama na kutoka lakini msingi wa chama hubakia palepale. Chadema si Zitto, si Slaa na wala si Mbowe na ukishajua hilo huna haja ya kukata tamaa anapechemka mmoja wao,, tujitahidi kuplani namna ambavyo tunaweza kuinua chama si kulaumu chama kwa mtu mmoja kuchemka.

Mwacheni Zitto akafie mbali na ubishi wake wa kimsimo ambao yeye mwenyewe ameshasema ya kuwa "I am Zitto Zuberi Kabwe, i here stand......" hakusema "I am the Dep Secret of Chadema....." yaani inamaanisha kuwa huo ni msimamo wake pekee na si wa chama na hana lazima ya kusema maneno haya akiwa mwanachama wa chadema tu,, angeweza kusema hata akiwa TLP, UDP, DOWANS, CCM, EPA, VIJISENTI au CUF. (maana nasikia siku hizi hata dowans, epa na vijisenti ni vyama vya siasa)

I want to state here in explicit terms that, I, Kabwe Zuberi Zitto (MP), Chairman Public Investments Committee of Parliament of Tanzania, stand with TANESCO on their desire to acquire gas fired turbines to improve electricity generation to the country. I stand firm to my decision and ready to be held accountable to that. I do this in good faith. I am genuine and honest. People can say all what they want to say, so long as this decision is mine based on the information i have, technical information. So long as i reached to this decision without any influence whatsover, i stand by it.

Kama nilivyosema hapo mwanzo, hakusema anaunga mkono Dowans, na hapo soma vizuri utaona kwamba anataka wanunue mitambo mipya. Mwakyemba, Selelii, Shellukindo wamesama hayo hayo na ndio maana wakaja na bei mbadala kwamba zipo za bei nafuu. Kwa mantiki hiyo Zitto anasisitiza umuhimu wa Tanesco kupata mitambo mipya, na kamati yake ilisema si lazima Dowans tu, wakasema njia mbadala na zitakazozingatia sheria zifuatwe.
 
Kwa kweli ilikuwa ni vigumu kwa wengi wetu kumuelewa, lakini kwa sababu tofauti kabisa. kwa hiyo inabidi upanue kidogo wigo wa sentesi yako. Binafsi zikumuelewa si kwa sababu alikosea kwa HOJa. Ni kwa sababu alikosea kama mwanasiasa. Angekuwa katika taaluma nyingine kama mwalimu anayefundisha, ningeona hana kosa kabisa, lakini kwa hili amekosea kisiasa. Kama mwanasiasa kijana angepima upepo wa kisiasa ulivyo. Hebu shangaa, Rostam Aziz anasema haifahamu Dowans, halafu anakuja anasema anaifahamu lakini si yake, anasema alifanya nao biashara, anasema walitumia anuani yake ya biashara, lakini leo hii watu wanauliza Dowans ni nani? Wanakwenda mahali wanakuta wafanyakazi wa Dowans wamiliki hawaonekani. Tulielezwa ni wawekezaji wa kigeni, lakini siku zinahesabika tutaambiwa VINGINEVYO tena kwa KISHINDO.

Kwa hiyo, kwa utata wa Dowans na mama yake Richmond, kwa jina baya la Richmond na mwanae Dowans, ni kunywa sumu kuwa karibu na kampuni hizo. Hizo kampuni zimefunikwa na siri nzito ambayo Dk. Rashidi hajawaambia kamati ya Zitto wala ya MWakyembe.

Jambo la pili, Zitto hajatofuatiana na kamati na nina hakika na hilo kwa asilimia mia moja. Tatizo la Zitto ni kuwaamini mno waandishi wa habari wengi ambao baadhi wamemuumiza sana katika suala hili. Gazeti la Mwananchi, Tanzania Daima, TBC wamepotosha kwa viwango tofauti kauli ya Zitto. Mutashangaa ni kwanini hajakanusha, mutashangaa ni kwanini Tanzania Daima, mutashangaa na wengine (pengine hata yeye) wakaibuka na kubisha kwamba si wote walipotosha.

habari inayotokana na tafsiri mara nyingi kila mtu huwa na tafsiri yake.

Zitto asingeweza kuzungumza nje ya yale waliyokubaliana ndani ya Kamati. Kosa lake ni kuitaja Dowans katika mtiririko wa maelezo yake yanayoonyesha anaihurumia Tanesco na mtu asiye makini ataona kwamba anaunga mkono kila kitu (ikiwamo Dowans) wanachotaka Tanesco. Kosa lingine ni pale aliposema "Hata kama ni kununua Dowans, iwe ni baada ya kamati zote mbili kujiridhisha na bila kukiuka sheria na taratibu", hapo mtu anakuja na kusema Zitto anaunga mkono kununua Dowans. Ukirudia hiyo sentensi (si waandishi wote wanarudia walichosikia, au kurekodi).

Kosa lingine ni pale mtu anapouliza, "inaonekana sheria ni kikwazo, je, sheria inaweza kubadilishwa?" jibu kwa yeyote litakuwa, "ndio, sheria si msahafu, kama kuna ulazima wa kufanya hivyo kwa maslahi ya taifa, itabadilishwa"... sasa leading questions na kutokuwa makini kutafsiri kauli za watu, ni mambo ambayo yamemponza Zitto.

Bahati mbaya sana Chadema (hata CCM) wanasiasa wetu hawana wasaidizi wa kudumu ambao kila jambo wanalifanyia uhakiki kabla halijawafikia waandishi wa habari, vinginevyo Zitto angetumia hoja hii hii ambayo imemgeuka kuzidi kuwabana CCM na Tanesco, lakini sasa ni kinyume.

Kwa mwanasiasa kijana, Zitto ana nafasi kubwa na nyepesi zaidi kujijenga na kupasua katikati ya wingu zito la sakata la Dowans na kufanya maajabu zaidi kisiasa. Ana uwezo huo na wengi wanamkubali na ninaamini WATAMUELEWA.

Ni bahati mbaya sana, watu hawakumsikiliza alipozungumza na ITV, na bahati mbaya sana TBC hawakumuacha azungumze kile wasiochata kisikike kwa umma na matokeo yake watu wakapata nusu nusu na nusu ingine wakaipika wao kwa kusema, "Kamati ya Zitto imeishauri serikali inunue DOwans" wakati huo ulikuwa ni UONGO wa dhahiri. Hakusema na hatosema hivyo.

Mkuu Halisi, heshima mbele sana.

Je wewe ndiye Zitto au msemaji wake?

Imekuwaje wananchi wengi wasimwelewe Zitto, imekuwaje wakati huu wa Dowans tu ndio wasimsikilize na kumwelewa vyama au tofauti? Na ni kwa nini wasimwelewe? Ametumia kanuni za Calculus ama za Bernoulli hadi asieleweke kirahisi? Huko nyuma alikuwa akitumia kanuni gani zilizomfanya aeleweke kwa urahisi? Na kwa nini amebadilisha kanuni wakati wa sakata hili?

Kama ametumia kanuni ngumu, namshauri akiri makosa na atumie kanuni rahisi na mifano hai kama vile kufundisha biology topic ya reproduction.
 
Wengi wetuhumu ni watu wazima wanauelewa .

Kila mmoja ameelewa nini Zito alichokisema na vizuri tumemsikia kwa kauli yake kutoka ktk radio Kenedy.Na nafikiri Zito sio nabii au mnajimu ya kwamba anachokisema watu hawamwelewi mpaka wahitaji tafsri kama ilivyokuwa kwa Nabii Yesu na Mohammed ama wanajimu wengine waliofunuliwa kumwelewa Zito ana maanisha nini akisema kile ama hiki.

Mimi nafikiri watu wazima kama sisi hatuhitaji kuelimishwa Zitto alimaanisha nini bali ni sisi kuchukuwa hatuwa stahiki kwa kile tulichokisikia .
 
Mkuu Halisi, heshima mbele sana.

Je wewe ndiye Zitto au msemaji wake?

Imekuwaje wananchi wengi wasimwelewe Zitto, imekuwaje wakati huu wa Dowans tu ndio wasimsikilize na kumwelewa vyama au tofauti? Na ni kwa nini wasimwelewe? Ametumia kanuni za Calculus ama za Bernoulli hadi asieleweke kirahisi? Huko nyuma alikuwa akitumia kanuni gani zilizomfanya aeleweke kwa urahisi? Na kwa nini amebadilisha kanuni wakati wa sakata hili?

Kama ametumia kanuni ngumu, namshauri akiri makosa na atumie kanuni rahisi na mifano hai kama vile kufundisha biology topic ya reproduction.

Kama ungesoma na kunielewa na kurudi katika magazeti ya Mwananchi utaelewa ninachokisema. Sijasema hajakosea, lakini makosa yake sio yanayozungumzwa. Kama mtu akikosea leo, si sahihi kuuliza kwanini jana alifanya kwa usahihi. Kwamba mbona wakati wote alieleweka, ndio maana tunasema safari hiii amekosea.

Binafsi napingana na Zitto kwa kiwango kikubwa kwa sababu namjua Idris Rashidi kuwa anatumikia waliomuweka pale. Nilishasema, Dk. Rashidi ametokea Vodacom, Ngeleja ametokea Vodacom. Huhitaji Sheikh Yahaya kukufanyia utabiri hapo. Tanesco ( na wanaowatuma) walichofanya ni kuwakoroga ili mugombane wao wapete, lakini WATANZANIA SI MABWEGE TENA, na hapa HOJA SI ZITTO hoja ni DOWANS na HAITAFUTIKA
 
Halisi: Zitto hana kosa alilotenda? Umetumwa kumtetea? Katika thread moja humu ndefu aliingia kichwa kichwa kutetea msimamo wake, tena kwa kubishana na wana-JF wengine kwa hasira kweli kweli. hayo unayosema ni baadhi ya yale aliyokuwa akikandamiza katika thread ile.

Kwa yeye, Dowans ilikuwa ni mada ambayo angepishana nayo kwa mbali sana, wala asingeikaribia, na kama angetaka kujiingiza, angefanya hivyo kwa njia ya uwakala -- kwa kumtumia mtu mwingine.

Kuna ripoti alionekana Habari Corporation Sinza wiki mbili zilizopita akizungumza faragha kwa masaa kadha na swahiba mmoja wa Riostam aliyemfanya kuwa Mhariri Mkuu wa magazeti yake -- Muhingo Rweyemamu? Na baada ya hapo tu ndio akaanza sekeseklana msimamo wake wa kutetea Dowans.

Angekuwa na mapenzi kwa wananchi wanaotishiwa kukosa umeme, angetetea kwa nguvu zake zote ununuzi wa mitambo mipya, siyo hiyo mitumba iliyojaa harufu ya hujuma kwa wananchi.
 
Binafsi napingana na Zitto kwa kiwango kikubwa kwa sababu namjua Idris Rashidi kuwa anatumikia waliomuweka pale. Tanesco ( na wanaowatuma) walichofanya ni kuwakoroga ili mugombane wao wapete, lakini WATANZANIA SI MABWEGE TENA, na hapa HOJA ni ZITTO na DOWANS na HAITAFUTIKA

Mkuu Halisi, nakusoma na ninasoma kama ilivyo hapo juu, sio kama ulivyoandika.

Zitto kachemsha, aombe radhi.
 
Kama umenisoma hapa, ukisoma toka mwanzo nimekuwa wazi, kwamba kuna makosa ya kisiasa, ambayo naamini hata yeye akiwa makini atayaona. Lakini katika kila mafanikio kuna hatari zake na hivyo anaweza kupanda chati kwa hili badala ya kuwa anguko lake kama baadhi ya watu wanavyotaka kuliweka.
 
Halisi: Zitto hana kosa alilotenda? Umetumwa kumtetea? Katika thread moja humu ndefu aliingia kichwa kichwa kutetea msimamo wake, tena kwa kubishana na wana-JF wengine kwa hasira kweli kweli. hayo unayosema ni baadhi ya yale aliyokuwa akikandamiza katika thread ile.

SIjasema hana kosa, nimesema makosa yake kwa sasa (hadi tutakapoletewa ziada) ni ya kisiasa kwa kujiingiza kichwa kichwa katika kuitaja Dowans mdomoni.

Kwa yeye, Dowans ilikuwa ni mada ambayo angepishana nayo kwa mbali sana, wala asingeikaribia, na kama angetaka kujiingiza, angefanya hivyo kwa njia ya uwakala -- kwa kumtumia mtu mwingine.

Uko sahihi, hapo ndio mwanzo wa kosa lake

Kuna ripoti alionekana Habari Corporation Sinza wiki mbili zilizopita akizungumza faragha kwa masaa kadha na swahiba mmoja wa Riostam aliyemfanya kuwa Mhariri Mkuu wa magazeti yake -- Muhingo Rweyemamu? Na baada ya hapo tu ndio akaanza sekeseklana msimamo wake wa kutetea Dowans.

Jamani kwa mwanasiasa kwenda TBC 1 kuongea na Tido ambaye ni swahiba wa kina Lowasa, ama kwenda Mtanzania kuongea na Muhingo wa Rai si kosa, tena nadhani ni sahihi na ndio maana Mrema na Lipumba wanazungumza na waandishi wa uhuru na wanapewa covarage kama ambavyo kina Makamba na Kikwete wanaandikwa vizuri na Tanzania Daima na wanakwenda pale Bilicanas. Kama kuna ushahidi wa jambo baya utolewe. Lakini pia newsroom si mahala pa kufanyia dili na kwa kweli Muhingo hawezi kutumwa na RA hata mara moja tena kwa mwanasiasa kama Zitto. Tuache siasa za MAJI TAKA

Angekuwa na mapenzi kwa wananchi wanaotishiwa kukosa umeme, angetetea kwa nguvu zake zote ununuzi wa mitambo mipya, siyo hiyo mitumba iliyojaa harufu ya hujuma kwa wananchi.

Ninavyojua na umesoma stamement yake hapo juu, hajatetea Dowans, amesema mitambo mipya ya umeme.. Mwakyembe na Selelii wote wamesema mitambo mipya na wanajua bei yake, hapo tofauti yao nini? Kosa mwanzo aliweka mdomoni Dowans kwa kurejea hoja za Tanesco katika kamati
 
Kama ungesoma na kunielewa na kurudi katika magazeti ya Mwananchi utaelewa ninachokisema. Sijasema hajakosea, lakini makosa yake sio yanayozungumzwa. Kama mtu akikosea leo, si sahihi kuuliza kwanini jana alifanya kwa usahihi. Kwamba mbona wakati wote alieleweka, ndio maana tunasema safari hiii amekosea.

Binafsi napingana na Zitto kwa kiwango kikubwa kwa sababu namjua Idris Rashidi kuwa anatumikia waliomuweka pale. Nilishasema, Dk. Rashidi ametokea Vodacom, Ngeleja ametokea Vodacom. Huhitaji Sheikh Yahaya kukufanyia utabiri hapo. Tanesco ( na wanaowatuma) walichofanya ni kuwakoroga ili mugombane wao wapete, lakini WATANZANIA SI MABWEGE TENA, na hapa HOJA SI ZITTO hoja ni DOWANS na HAITAFUTIKA

Halisi,

Zitto amesema ana-stand na TANESCO wanunue mitambo ya gas fired turbines............na awali ya yote.............TANESCO desire wanasema wanunue mitambo ya DOWANS (ambayo pia ni gas fired turbines)

pamoja na kwamba maneno yake Zitto hayakutaja Dowans.....lakini ame/wame-support nini sijui!!
 
Zitto ameboa, basi...wakati upepo wa dowans na richmond unavuma kwa nguvu, alipaswa kujua nini aseme kwa umma..ameboa na ataboreka
 
Halisi,

Zitto amesema ana-stand na TANESCO wanunue mitambo ya gas fired turbines............na wali ya yote.............TANESCO wanasema wanunue mitambo ya DOWANS (ambayo pia ni gas fired turbines

pamoja na kwamba maneno yake hayakutaja Dowans.....lakini ame/wamesupport nini sijui!!

Nimebahatika kuzungumza na wajumbe wengi wa kamati ya Zitto, nimebahatika pia kuzungumza na wajumbe wengi wa kamati ya kina Mwakyembe, nimebahatika pia kuzungumza na watu wa ofisi ya Bunge, nimebahatika pia kusoma nyaraka za kamati ya Zitto na ile ya Mwakyembe, nimebahatika pia kusoma nyaraka za Waziri Ngeleja na mawasiliano yake na....... (nitaweka wazi siku mwafaka)... Nimebahatika pia kupata nyaraka zote muhimu na ambazo nadhani zitaanikwa JF soon.

Kwa maelezo hayo hapo juu, hakuna ambaye haiungi mkono Tanesco (si Dk. Rashidi) kupata mitambo mipya, hiyo iko katika mipango yao ya muda mrefu na mfupi. Hata wewe utapenda Tanesco wapate mitambo. Zitto anakosea kutosema asichosema na hivyo kutoa nafasi ya kuwachanganya watu, na kuna mahali alisema anafanya makusudi. Sijui anateka kutuambia nini. Pengine huu mjadala umesaidia sana kuwabana Tanesco mpaka wamekwama. Zitto amefanikiwa lakini amekuwa KAFARA wetu. Kama si Zitto suala hili lisingekuwa HOT kama ilivyo sasa na ndio maana limekuwa na wasemaji wengi na limesaidia mjadala kupaaa na kuwatisha kina Dk Rashidi am baya akageuka kuwatisha Watanzania.

Soma maandiko yake. Sikiliza matamshi yake ya SAUTI si ya kunukuliwa, utaona hakusema anaunga mkono kwamba lazima kunuliwa kwa DOwans. Kuna mahala amesema (narudia) kwamba kaama kuna ulazima wa kununua Dowans basi sheria zizingatiwe. na Kuwepo mjadala ili uamuzi ufanyike kwa HOJA si kwa JAZBA. Hapo sioni kosa la kimantiki ila kuna kosa la KISIASA kwam ba Dowans/Richmond ni alama ya mafanikio ya vita ya UFISADI kwa hiyo hatuwezi kukubali kwa gharama yoyote mtu yeyote (hata Zitto) kuuvunja huu MNARA wa vita ya UFISADI
 
Back
Top Bottom