Dowans: Another Richmond in making?

Dowans: Another Richmond in making?

Kasheshe,
Hivi tukikubali kuwa tumlipe Dowans hiyo hundi tutampa nani?

Jasusi, hili la kutojua wamiliki wa Richmond/Dowans ni akina nani linaonyesha ni jinsi gani serikali yetu isivyokuwa makini katika kuweka maslahi ya nchi mbele. Eti wanaingia mkataba wa shilingi bilioni 200 na kampuni ambayo ildai ina HQ yake Houston, Texas bila kujua wamiliki wake ni nani!!!! Kila anayeulizwa mmiliki/wamiliki wa Richmond/Dowans anang'aka haraka sana kwamba yeye hajui wamiliki. Bado hili sakata la Richmond/Dowans lina safari ndefu sana na litaondoka na wengi tu.
 
Hivi ni wapi ambako maisha ya mtanzania yemeboreka tulipobinafsisha mashirika/sekta ya HUDUMA? Kama mtoto anakuwa mtukutu hivi dawa ni kumtupa ama kumgawia jirani? Hivi tutakapo binafisisha TANESCO na kuanza kuendeshwa kwa ajili ya kutengeneza faida kwa wenye hisa ni watanzania wangapi wataweza kupata huduma hiyo nyeti na ni mnunuzi gani binafsi ataakubali kumpelekea umeme mlalahoi na kuacha kutumia capital kiduchu aliyo nayo kuwapelekea umeme WACHUKUAJI (Wawekezaji) walio tayari kuwalipa kwa faida nono?

omarilyas

Omarilyas,

Watu kama wewe walikuwa wanasema hivyo hivyo kwenye kutaifisha TTCL. Kwamba nani atapeleka simu mpaka vijijini, leo tumeona simu zimefika mpaka kule ambako ingewachukua TTCL miaka 100 kufikisha mawasiliano.

Hata sasa na monopoly plus pesa za serikali bado umeme haujafika vijijini na hata huko mjini ulikofika ni ubabaishaji mtupu.

Mashirika yakiwa ya umma yanaingiliwa na wanasiasa na kuishia kufanya maamuzi ya kisiasa ambayo kila mara yanaishia kushindwa. Kwanini wananchi waendelee kuchangia huduma mbovu?
 
Ogah,

Usiwe unaandika mambo ambayo huna uhakika nayo kabisa. Shemeji zako gani hao muda wote walikuwa wanapata joto ya jiwe?

Kwa muda mrefu kulikuwa na mkataba kati ya Tanesco na Kiwira na hata wakati wa migawo ya umeme Dar, Kyela ilikuwa inapata umeme muda wote.

Ni kuanzia mwaka jana tu Kyela imeanza kukumbwa na mambo ya mgawo wa umeme.

Kama huna uhakika uliza hata hapa watu watakuambia.

Hiyo Kanjunjumele unayoiongelea siku zote haina umeme kabisa wakati mimi naongelei sehemu ambazo tayari zimeunganishwa na umeme.

Tusifanye mizaha hata kwenye mijadala ambayo kuna watu wengi wanaathirika. Suala la umeme ni muhimu mno kwenye uchumi, mimi Mtanzania nikiwa hapa London naweza kufanya utani wowote lakini kumbuka Tanzania kuna real people and real businesses wako affected sana na hili suala la kukosekana kwa umeme wa uhakika. Tusichukulie kila jambo ni mzaha au ni siasa.

Mtanzania im sorry kama umekuwa offended, sikupenda/sikupanga kuwa na mashemeji kutoka huko Kajunjumele (imetokea baada ya "kaka" yako mmoja kuoa dada yangu) na ndio hasa sababu ya kufika kwangu huko, nisingeweza kusema kitu ambacho sina uhakika nacho.......nimeishuhudia hiyo hali Kajunjumele na hata wewe umethibitisha hilo kuhusu kajunjumele.......kwa hiyo sikuwa na mzaha.......nimesema nilichokiona...atleast

Kuna sehemu kubwa ndani ya Wilaya ya Kyela haina umeme....sasa nilipoona umetumia neneo wana Kyela walikuwa WANATAMBA kwa kuw ana umeme....ndio maana nikaandika vile....kwa nimeshuhudia sehemu nyingi tu za kyela bila umeme......ningekuwa mwenyeji huko ningekuapatia majina zaidi ya sehemu kubwa tu ambazo hazina umeme........Pengine utofauti huo i.e. comparison umetokana na sehemu ninayotoka mimi......yote hiyo ni katika kujaribu kuonyesha kuwa bado sehemu kubwa ya nchi yetu inakabiliwa na shida ya umeme...........im sorry kama mradi wako umeathirika.........ila mimi naagalia in a bigger picture....than few places za Kyela ambazo zina umeme.......

again im sorry
 
Hakuna tatizo. Naona tulikuwa tunaongelea vitu viwili tofauti.

Najua karibu asilimia 90 ya Kyela haijaunganishwa na umeme wa Tanesco. Mimi nilikuwa naongelea mgao wa umeme kwa sehemu ambazo zina umeme wakati statement yako kwa mtu ambaye haijui Kyela angefikiri Kanjunjumele imeunganishwa na umeme na imekuwa ikikabiliwa na mgao wa umeme kwa muda mrefu.

Laiti Kiwira ingeendelezwa, ingeweza kuhudumia mkoa mzima wa Mbeya. Pia ni muhimu kuelewa big picture inaanzia na small picture. Huwezi kuwa na umeme wa kuaminika kwa nchi nzima wakati hata unashindwa kuwa na umeme wa kuamini kwa sehemu chache. Kabla ya kufikiria umeme wa nchi nzima lazima kwanza tuhakikishe sehemu zilizounganishwa kwasasa zina umeme wa kuaminika kukidhi mahitaji ya wananchi wake. Vionginevyo hiyo big picture inabaki kuwa usanii tu kama ule wa JK wa 2-million jobs. Mimi sio mwumini wa big is good, ni muumini wa quality. Jambo lolote unalolifanya hata kama ni dogo lakini lifanye kwa umahili. Huwezi kusema unaweza kujenga nchi wakati hata unashindwa kujenga wilaya. Mfano wa JK na wilaya yake ya Chalinze ni somo tosha.
 
Inaonyesha na wewe umesoma hesabu kama mimi!!! tupo pamoja

Ha ha ha wengine wote ambao tunapinga kununuliwa kwa mitambo chakavu ya Dowans hatukusoma hesabu...😉 Sijui kusoma hesabu na hili swala la kupinga kununuliwa mitambo chakavu iliyoingia nchini kwa njia za kifisadi vina uhusiano gani!!!!
 
Kasheshe na DSM the premise of your argument is false:
1. Dowans na Richmond are not clean legal entitites as they do not even have a country of origin where they have been legally registered. Ni makampuni hewa. So we cannot negotiate with makampuni hewa. Mwakilishi wa Dowans na mawasiliano ya kimaandishi ya Dowans hufanyika baina ya nani na nani?
2. There is no immediate emrgency ya umeme kama inavyodaiwa. MTera dam imejaa etc (soma magazeti). So where is the emergency?

Once we agree on this basi, utagundua hakuna maana yoyote ya kununua mitambo ya Dowans.
 
Nilishapendekeza Dr. Rashid afukuzwe kazi tangu mwaka 2007. Lakini nashangaa JK anaendelea kumbaby sit. Huyu jamaa ameshindwa kuendeleza Tanesco katika mwendo wa karne ya 21. Just fire the guy.
 
Nilishapendekeza Dr. Rashid afukuzwe kazi tangu mwaka 2007. Lakini nashangaa JK anaendelea kumbaby sit. Huyu jamaa ameshindwa kuendeleza Tanesco katika mwendo wa karne ya 21. Just fire the guy.

Kweli Mkuu, labda ndiye mbia mkuu wa urais wake!

Yeye JK anashughulikia vinali vidogo (akina Mnali) lakini haya Manali makubwa inaonekana hayawezi!! Kwani akina Hosea, Mwanyika n.k wamefanywa nini?🙄
 
MEMBERS of parliament from the ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM) have joined the growing public condemnation of Energy and Minerals Minister William Ngeleja and Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) Managing Director Dr Idris Rashidi over the roundly rejected Dowans deal.

A number of influential CCM legislators yesterday offered a variety of indignant responses to the TANESCO chief’s threatening statement last Friday that the country will inevitably be plunged into a crippling power crisis, simply because a dubious plan to buy the used Dowans power turbines had been effectively nipped in the bud.

The ruling party MPs turned on both Rashidi and minister Ngeleja, the general consensus being that the duo is now left with little option but to step down in the aftermath of their failed bid to convince the government to purchase the Dowans turbines.

Responding specifically to Rashidi’s assertion that the nation was on the brink of being engulfed in darkness, hospitals without services, factories shut-downs, and unlearning students as a result of the Dowans deal fallout, Nzega MP Lucas Selelii (CCM) told THISDAY:

’’Tanzanians are not stupid...Such threats cannot be used to justify an obviously flawed deal.’’

According to Selelii, both the TANESCO board of directors and the parliamentary energy and minerals committee had rejected the proposal to buy the second-hand power turbines for valid reasons.

He said he was consequently bewildered as to why Ngeleja and Rashidi continued to pursue the deal so vigorously, to the point of the latter resorting to uttering public threats of the inevitability of national blackouts in the not-too-distant future.

The Nzega legislator pointed out that if the proposed deal to purchase the Dowans turbines was genuine, TANESCO’s board of directors for one would have had no reason to reject it.

’’There must be a hidden agenda here...There’s a possibility of sabotaging the power company (TANESCO),’’ Selelii said.

He added that both Ngeleja and Rashidi would find themselves in untenable positions if it emerges that they were not upfront in all matters regarding the Dowans deal.

’’They would have to weigh the public sentiments against them - and decide accordingly,’’ he remarked.

Selelii, who was a member of the Richmond parliamentary probe team chaired by Dr Harrison Mwakyembe, dismissed claims by the minister and the TANESCO boss that it would take too long for the government to order brand new turbines directly from manufacturers abroad.

’’There are ready-made power turbines available out there...brand-new, 100MW, and at reasonable prices (between 40bn/- and 50bn/-). All that TANESCO needs to do is to start negotiations for purchase with the manufacturers,’’ he said.

Likewise, Ms Stella Manyanya (CCM-Special Seats, and also a member of the Richmond probe team) rejected suggestions that Dowans was the only solution to the nation’s energy problems.

Ms Manyanya, herself an electrical engineer by profession and who was once employed by TANESCO, supported assertions by Selelii that it would be ludicrous for TANESCO to spend $60m (approx. 90bn/-) to buy the used Dowans turbines on offer at that price, instead of opting for brand-new power generators at much cheaper price tags.

She accused the public utility and its parent ministry of deliberately trying to confuse members of the public with ’false alarms’ of an impending power blackout, noting that during the 2006 national power crisis, TANESCO came up with both short and long-term plans to ensure the situation did not repeat itself in the future.

’’What has TANESCO done to implement those plans, so that the nation may not be plunged into darkness?’’ the MP queried.

Ms Manyanya also noted with much concern that although parliament has already passed new power sector legislation that allows private companies to generate electricity, there has been much delay in enforcing the new legislation.

She said the government should address this issue also as another option to solving the problem, but made it clear that should the country eventually have to face renewed power rationing, it would mean the higher-ups in both TANESCO and the energy and minerals ministry ’’will have failed to do their jobs.’’

Another CCM lawmaker, Aloyce Kimaro (Marangu), said Rashidi as TANESCO boss appeared to have lost the qualities of good managership, and advised that he be replaced expeditiously, if only to ensure the nation does not have to deal with artificial power-shedding.

’’He (Rashidi) should resign and give other better managers the chance to try their hand at the problem before the nation enters into darkness - otherwise they (the new managers) might be held accountable,’’ Kimaro said.

A member of the parliamentary energy and minerals committee chaired by William Shellukindo, Christopher Ole Sendeka, also added his voice to the call for Ngeleja and Rashidi to resign or be removed.

The Simanjiro MP, also on a CCM ticket, accused the energy and minerals ministry and TANESCO of resorting to threats and intimidations to try to justify the Dowans deal.

The chairman of the parliamentary Public Organizations Accounts Committee (POAC), Zitto Kabwe, has also come under heavy criticism from members of the public and even senior leaders within his own opposition CHADEMA party for his controversial decision to back the Dowans deal.

Observers say Kabwe, who has already made several public statements in support of the dubious deal, could find himself isolated from the leadership hierarchy of the opposition party, and his entire public credibility and even popularity as a refreshingly maverick and strong-minded politician called into question.

Source:This day
 
Siku za Mkurugenzi Tanesco zahesabika

Siku za Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), Dk Idris Rashid kuendelea kushika wadhifa huo sasa zinahesabika baada ya baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika hilo kuanza mikakati ya chini chini kuhakikisha mkataba wake unaomalizika Septemba mwaka huu, hauongezwi.

Wajumbe hao waliliambia Nipashe kuwa kitendo cha Dk Rashid (pichani), kukaidi maagizo yao na kutangaza katika magazeti mpango wa kununua mitambo ya Dowans, ni kosa ambalo Bodi yao haiwezi kulivumilia.

``Tumedhamiria kwamba mara baada ya kumaliza muda wake wa miaka mitatu, kamwe sisi wajumbe wa Bodi hatutakubali kumpa kipindi kingine ili aiongeze tena Tanesco,`` alisema mmoja wa wajumbe wa bodi hiyo.

Alisema Dk Rashid alikaidi maagizo ya Bodi hiyo na kuamua kwenda kwenye Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma ya Bunge kinyume na maagizo waliyompa.

Uteuzi wa Dk Rashid kushika wadhifa huo wa Ukurugenzi wa shirika hilo ulitangazwa na Bodi hiyo mwishoni mwa mwaka 2006.

Dk Rashidi alichukua nafasi ya kuongoza shirika hilo kufuatia Serikali kuamua kuachana na Kampuni ya Net Group Solutions ya nchini Afrika Kusini ambayo nayo ilimaliza mkataba huku ikiliacha Tanesco likiwa taabani.

Kampuni hiyo ilihitimisha mkataba wake Desemba 31, mwaka 2006 baada ya kuliongoza Tanesco kwa takriban miaka minne mfululizo kuanzia Mei, mwaka 2002.

Mkataba wa kwanza wa miaka miwili kati ya kampuni hiyo na Serikali, ulisainiwa Mei, mwaka 2002 na kumalizika Agosti, mwaka 2004.

Hata hivyo, mkataba huo uliongezwa tena kuanzia Agosti mwaka 2004 na kumalizika Desemba 31, mwaka 2006 ambapo Serikali iliamua kutoendelea na kampuni hiyo hivyo shirika hilo nyeti kuwa chini ya uongozi wa wazalendo.

Wakati hayo yakijiri, Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, inatarajia kumhoji Mkurugenzi huyo wa Tanesco na Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, William Ngeleja kutokana na madai ya Mkurugenzi huyo kukosa nidhamu.

Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu jana Mwenyekiti wa Kamati hiyo, William Shelukindo alisema wanataka Dk Rashid ajieleze kwanini aendelee na wadhifa wake, ili hali ameonyesha dharau kwa vyombo vilivyomuweka madarakani yaani serikali na Bodi ya Shirika hilo.

Shelukindo alisema kauli ya vitisho kwa Watanzania iliyotolewa na Dk Rashid aliyekaririwa akisema “Nchi itaingia gizani na Tanesco tusilaumiwe`` ni yakibabe na ukosefu wa nidhamu wa hali ya juu.

Alisema inaonekana wazi Mkurugenzi huyo ana kiburi ambacho haijulikani kinatoka wapi.

Akifafanua, Shelukindo alisema kama Mkurugenzi aliona hatari iliyo mbele, alipaswa kupeleka taarifa kwa Serikali au Bodi ya Wakurugenzi ya Tanesco.

``Lakini cha kushangaza inaonekana Dk. Rashid amekuwa ndiye Waziri na pia anajifanya yupo juu ya bodi, hali hii hatuikubali,``alisema.

Alipoulizwa wanapendekeza adhabu gani dhidi ya Mkurugenzi huyo, Shelukindo alisema hawezi kutamka kwa sasa kwa vile wanaamini kabla ya kuwekwa `kiti moto` tayari mamlaka zitakuwa zimechukua hatua.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Estherina Kilasi ambaye pia ni Mbunge wa Mbarali (CCM), alisema pia hakubaliani na jinsi Dk Rashidi alivyotangaza mpango wa kujitoa katika sakata la kununua mitambo hiyo ya Dowans.

Alisema kauli yake ya vitisho kwamba nchi itaingia gizani na wao (Tanesco) wasilaumiwe, sio ya kiungwana na haikupaswa kutolewa na mtu anayeongoza Shirika linalowahudumia Watanzania.

Kilasi alisema kauli hiyo inaweza kutafsiriwa kuwa Mkurugenzi huyo alikuwa na usongo wa kununua mitambo hiyo kufa na kupona.

Alisema maneno ambayo yamemkariri Mwenyekiti wao (Zitto Kabwe) yalikuwa maoni yake binafsi na wala sio ya kamati kwa vile hakuna hata kikao kimoja ambako walikubaliana na ombi la kununua mitambo hiyo.

``Wala hatujawahi kutoa ushauri wowote juu ya suala hilo, zaidi ya kuwaelekeza Tanesco walifikishe kwa kamati husika ya Nishati na Madini,``alisema

Akifafanua, alisema kilichotokea siku hiyo ni semina ambayo Tanesco waliiandaa na kuwakaribisha wajumbe wa Kamati hiyo kwa lengo la kuwaelezea mipango ya kununua mitambo ya Dowans kwa kuwa wana kiasi cha Sh. bilioni 60 kwa ajili hiyo.

``Sisi tuliwahoji kama mnazo Sh Bilioni 60 mnashindwajwe kuongezea kidogo ili mnunue mitambo mipya? Vilevile tukawahoji hivi mambo haya mnayotuambia kwenye semina wameyapeleka kwa wahusika ambao ni Kamati ya Niashati inayoongozwa na William Shelukindo?,`` alisema Kilasi na kuongeza:

``Baada ya hapo tuliwashauri suala hilo walifikishe kwa wahusika (Kamati ya Madini) na hakuna hata mahali pamoja tulipolitolea uamuzi suala hilo kwa vile halituhusu.``

Mbunge huyo alisema kufuatia kauli za Zitto ambazo zimezua malumbano, na kuifanya Kamati yao ionekane ina `walakini` wanamsubiri kwa hamu arejee ili wamuweka kiti moto.

``Unajua baada ya semina ile mimi nilienda Zambia, huku nyuma ndo nikasikia malumbano, lakini baada ya kurejea nimewauliza wenzangu na hasa makatibu wanaoandika muhtasari, kama kuna kikao kingine kimeketi na kutoa uamuzi, lakini wakasema hapana. Sasa tunamsubiri Zito arejee safarini ili tumuulize kulikoni? ``Alisema.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema amemtaka Rais Jakaya Kikwete kuingilia kati malumbano yaliyozuka wiki tatu sasa kati ya Kamati mbili za Bunge, Spika Samuel Sitta na Tanesco kuhusu hoja ya kununua mitambo hiyo ya Dowans.

Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya TLP, jijini Dar es Salaam jana, Mrema alisema anatoa rai hiyo kwa vile anaamini kuwa Rais Kikwete amesikia hoja za kila upande kupitia malumbano hayo kuhusu suala hilo.

``Nchi ina uongozi, haiwezekani mambo yakajiendea ovyo, ninachoweza kusema ni kwamba, Rais Jakaya Kikwete asaidie kuondoa utata, asiache watu wakatoana macho,`` alisema Mrema.

Alisema huko nyuma wakati akiwa serikalini, ilikuwa linapotokea jambo, haraka wanalishughulikia kwa vile hawakuona kuwa ni busara kuacha kushughulika na mambo mengine ya kujenga taifa na kusalia kwenye kushughulikia jambo moja pekee kila uchao.

``Haiwezekani kila tukiamka asubuhi ni Tanesco, huyu anakuja na taarifa kwamba, nchi itakumbwa na giza na mwingine anakuja na hili katika jambo moja, halafu Rais wala Waziri Mkuu hawasemi lolote,`` alisema Mrema.

Wengine waliojitosa kwenye malumbano hayo ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Shelukindo, ambaye ni Mbunge wa Kyela (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe na Mbunge wa Karatu (Chadema), Dk. Willibrod Slaa.

Chimbuko la Dowans ni mkataba wa mradi wa ufuaji umeme wa dharura wa megawati 100 kati ya serikali, Tanesco na kampuni ya Richmond uliofikiwa mwaka 2006.

Hatua hiyo ilikuja baada ya Richmond kushindwa kutekeleza mradi huo iliuza mitambo hiyo kwa Dowans.

Mkataba huo ulizua mvutano mkubwa kiasi cha kusababisha Bunge kuunda kamati teule kuchunguza, ikiongozwa na Dk Mwakyembe, na ripoti yake kusababisha Edward Lowassa kujiuzulu wadhifa wa Waziri Mkuu.

Vilevile Nazir Karamagi alijiuzulu Uwaziri wa Nishati na Madini) na Dk Ibrahim Msabaha wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki kutokana na kashfa hiyo.

SOURCE: Nipashe
 
kama hawa wezi kumfukuza , basi wampe likizo mpaka hiyo contract yake iishe, kwani ni very risk kwa taifa kuwa na mtu kama huyo kwa sasa. he have got nothing to loose , bali sisi ndio tunacho cha kupoteza
 
Mi nimeshasema ni lazima tuanze petition ya kumtaka Dr Idris ajiuzulu mara moja, au kama siyo afukuzwe kazi. Mtu ali-abdicate aliposema asilaumiwe... sasa kama ye ndo bosi wa Tanesco akisema asilaumiwe si ina maana ameshindwa kazi. Anataka kutuleta mambo ya nyumbani kusutana? Ebo!
Rais Jk lazima achukue hatua akikaa kimya mimi nitachukulia ya kuwa yeye ndo alimwagiza Dr Idris aseme haya maneno na hata hii ya kununua Dowans ilikuwa ni idea yake JK, maana anaisapoti kichinichini.
 
Nyani Ngabu,
Mkuu unajua hawa jamaa wanataka kutufanya sisi wajinga sana..
Ebu jaribu kufikiria tulikotoka..Ule mkataba wa Richmond tulikubaliana nao kuwalipa TShs 172 billion, kisha ndani ya mkataba huo kulikuwa na kipengele kinachotulazimu sisi kuwalipa Usd dollar 137, 000 kwa siku regardless of the amount of electricity provided....mmmhhhhh!
Mkuu hii mitambo ina worth less than Usd 50,000! uliona wapi mtu kaweka mtaji wa dollar 100,000 (mitambo miwili) akaweza kuzalisha gross income ya kiasi hicho..sijawahi kuona wala kusikia maishani mwangu isipokuwa Tanzania..

Pili, wale Richmond walitakiwa kuingiza mitambo na kuanza kazi within six month (from June 2006) kulingana na mkataba lakini hawakufanya hivyo wakati fedha (mtaji) tumewapa sisi kabla hata hawajaingiza kitu, leo hii tunaona viongozi wakisema haiwezekani kuagiza mitambo ktk window ya miezi sita hali ni wao waliosaini mkataba wa kwanza, sijui siku zile kulikuwa na uwezekano gani tofauti na leo hii..
Jamani hizi ni generators tu zenye thamani isiyozidi Usd 50, 000, inakuwaje tunaipa uzito kama vile tunajenga Nuclear power!..Kuna majumba na viwanda hapa yanabeba mtambo kama huo kwa matumizi ya tahadhari tu..iweje leo tunatishiwa nchi kuingiza kizani kwa megawatts 100 wakati generator hizo zipo in stock na zinasubiri wanunuzi sio kitu kinachotengenezwa kulingana na mahitaji ya nchi..Hizi habari wamezipata wapi?..

Tatu, Kama sikosei kabla Richmond hawa pass ile contract kwa Dowans Holdings, Yiule mhindi Gire aliwahi kusema Richmond hawakupokea hata senti moja toka serikali yetu wakati, serikali yetu ilidai kuwa imewalipa hawa jamaa kitu kama Usd 80,000..Habari ipi ni ya kweli?.. hadi leo hii tunabishana hapa hatufahamu ukweli uko wapi na tumeshasahau yote hayo!..
Haya baada ya Dowans Holding kuchukua mkataba kwa mtaji mbuzi walichukua chini ya miezi minne generators ziliingia nchini na wakafunga..ajabu bado ipo pale pale kwamba ikiwa Richmond waliondolea kwa sababu they lacked experience, expertise na kama sikosei financially incapacitated.. ni uchunguzi gani uliopitiwa kwa Dowans kuwhakikisha hawakuwa na makosa kama hayo.. hakuna report hiyo hadi leo hii tunavyozungumza.. kifupi hakuna mtu anayefahamu undani wa Dowans kama tulivyofuatilia kuhusu Richmond zaidi ya kuamini tu kwamba shirika hili linatoka South Afrika.. mitambo wameagiza Marekani wakati South penyewe mitambo kama hiyo ipo!..
Nne zaidi ya matukio yote haya, leo hii tumefikia kutaka kuinunua mitambo chakavu na yenye kila harufu mbaya kisha viongozi wetu wanatishia kuingia kizani.. ile ile hadithi ya 2006 kabla Richmond hawajapewa deal. Na tulikaa kizani sana tu hakuna kiongozi hata mmoja aliyesimama na kusema shauri yenu hali ni wao waliotuweka kizani..Kila siku inavyokwenda ndivyo tunavyozidi kusahau tulikotoka!...

Na kibaya kuliko yote wapo watu wanaoshadidia na kujaribu kujenga hoja mahala ambapo tumekaa uchi wa nyama kama ngedere..Mawili aidha sisi ni wajinga kuliko watu wote duniani ama tumerogwa na mchawi mwenyewe kisha kufa!..Lakini ukiuliza waswahili wenyewe watakwambia YOTE haya ni kazi ya MUNGU!..
Miafrika ndivyo Tulivyo mkuu wangu yaani nimechoka!................

Mkuu Mkandara nakuunga mkono moja kwa moja katika tathimini yako. Ila Mkuu umepunguza sifuri tatu kwenye figure zako (ujumbe wako umefika, loud and clear).

Mimi nadhani kuna jambo kubwa linafichwa. Najaribu kuangalia DOWANS walitokea wapi katika kukabidhiwa Mkataba wa RDC. DOWANS hawakuwepo katika mchakato wa zabuni hii hapo awali. Kwa nini? DOWANS waliwezaje kujipanga na ku-deliver mitambo ya kuzalisha umeme katika kipindi kifupi kiasi hicho? Waliandaliwa kufanya hivyo lini , na nani? DOWANS kwa kuweza kufanya delivery ya mitambo hiyo, inaonyesha wana ujuzi (experience) ya muda mrefu katika sekta ya nishati. Wameitoa wapi (kuna reference zozote?). DOWANS walishindanishwa na nani katika kupewa nafasi ya kuuza mitambo yao kwa TANESCO baada ya RDC kushindwa? Je ilifanyika kihalali?

Mimi nadhani kama TANESCO inataka kweli kuinunua mitambo hii, ijue madhara yake. DOWANS wanawezaje kuihakikishia TANESCO kuwa watapata Technical support ya mitambo hii baada ya wao kuiuza kwao? TANESCO wanajua jinsi wanavyoweza kujihakikishia usalama wao katika Tech Support?

Mitambo ya DOWANS ina uwezo wa kuzalisha 100MW. TANESCO inahitaji more than 220MW by December 2009. Ina maana kuna ki-DOWANS kingine kinakuja baada tu ya mitambo hii kununuliwa. Je, kwa nini TANESCO isinunue mitambo ya 300MW once and for all? Kama uwezo haupo sasa, je kwanini wasinunue walau 250MW? Au kwanini iwe muhimu zaidi kuchapisha vitambulisho vya Taifa kuliko kupata umeme ambao ni muhimu zaidi kwa maisha ya watu wote waishio Tanzania?
 
Waungwana,
Lazima tukiri Rostam aka RA ni kichwa saana, ameiteka system yote ya nchi. Kwanza alianza kwa kununua nyumba karibu na mkurungenzi wa usalama wa Taifa (mstaafu) na kupenyeza na kuwa rafiki yake wa karibu. baada ya hapo sasa ndo akaingie ataratibu na kuimeza system yeto.
Mkurugenzi huyo ndo aliyemshauri BWM kumrudisha kwenye kabinet EL, maana yeye na EL ni marafiki wakubwa saana wa miaka mingi.
Swali, BWM alikuwa wapi? kwa nini asimtimue mkurungenzi kabla jamaa hajanunuliwa na kumfanya RA awe anaongea kama a shadow president?
 
Dowans deal fallout: CCM MPs pour scorn on power blackouts threat

-Insist TANESCO boss, minister responsible should be held accountable

SEBASTIAN MRINDOKO
THIS DAY
Dar es Salaam

MEMBERS of parliament from the ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM) have joined the growing public condemnation of Energy and Minerals Minister William Ngeleja and Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) Managing Director Dr Idris Rashidi over the roundly rejected Dowans deal.

A number of influential CCM legislators yesterday offered a variety of indignant responses to the TANESCO chief's threatening statement last Friday that the country will inevitably be plunged into a crippling power crisis, simply because a dubious plan to buy the used Dowans power turbines had been effectively nipped in the bud.

The ruling party MPs turned on both Rashidi and minister Ngeleja, the general consensus being that the duo is now left with little option but to step down in the aftermath of their failed bid to convince the government to purchase the Dowans turbines.

Responding specifically to Rashidi's assertion that the nation was on the brink of being engulfed in darkness, hospitals without services, factories shut-downs, and unlearning students as a result of the Dowans deal fallout, Nzega MP Lucas Selelii (CCM) told THISDAY:

''Tanzanians are not stupid...Such threats cannot be used to justify an obviously flawed deal.''

According to Selelii, both the TANESCO board of directors and the parliamentary energy and minerals committee had rejected the proposal to buy the second-hand power turbines for valid reasons.

He said he was consequently bewildered as to why Ngeleja and Rashidi continued to pursue the deal so vigorously, to the point of the latter resorting to uttering public threats of the inevitability of national blackouts in the not-too-distant future.

The Nzega legislator pointed out that if the proposed deal to purchase the Dowans turbines was genuine, TANESCO's board of directors for one would have had no reason to reject it.

''There must be a hidden agenda here...There's a possibility of sabotaging the power company (TANESCO),'' Selelii said.

He added that both Ngeleja and Rashidi would find themselves in untenable positions if it emerges that they were not upfront in all matters regarding the Dowans deal.

''They would have to weigh the public sentiments against them - and decide accordingly,'' he remarked.

Selelii, who was a member of the Richmond parliamentary probe team chaired by Dr Harrison Mwakyembe, dismissed claims by the minister and the TANESCO boss that it would take too long for the government to order brand new turbines directly from manufacturers abroad.

''There are ready-made power turbines available out there...brand-new, 100MW, and at reasonable prices (between 40bn/- and 50bn/-). All that TANESCO needs to do is to start negotiations for purchase with the manufacturers,'' he said.

Likewise, Ms Stella Manyanya (CCM-Special Seats, and also a member of the Richmond probe team) rejected suggestions that Dowans was the only solution to the nation's energy problems.

Ms Manyanya, herself an electrical engineer by profession and who was once employed by TANESCO, supported assertions by Selelii that it would be ludicrous for TANESCO to spend $60m (approx. 90bn/-) to buy the used Dowans turbines on offer at that price, instead of opting for brand-new power generators at much cheaper price tags.

She accused the public utility and its parent ministry of deliberately trying to confuse members of the public with 'false alarms' of an impending power blackout, noting that during the 2006 national power crisis, TANESCO came up with both short and long-term plans to ensure the situation did not repeat itself in the future.

''What has TANESCO done to implement those plans, so that the nation may not be plunged into darkness?'' the MP queried.

Ms Manyanya also noted with much concern that although parliament has already passed new power sector legislation that allows private companies to generate electricity, there has been much delay in enforcing the new legislation.

She said the government should address this issue also as another option to solving the problem, but made it clear that should the country eventually have to face renewed power rationing, it would mean the higher-ups in both TANESCO and the energy and minerals ministry ''will have failed to do their jobs.''

Another CCM lawmaker, Aloyce Kimaro (Marangu), said Rashidi as TANESCO boss appeared to have lost the qualities of good managership, and advised that he be replaced expeditiously, if only to ensure the nation does not have to deal with artificial power-shedding.

''He (Rashidi) should resign and give other better managers the chance to try their hand at the problem before the nation enters into darkness - otherwise they (the new managers) might be held accountable,'' Kimaro said.

A member of the parliamentary energy and minerals committee chaired by William Shellukindo, Christopher Ole Sendeka, also added his voice to the call for Ngeleja and Rashidi to resign or be removed.

The Simanjiro MP, also on a CCM ticket, accused the energy and minerals ministry and TANESCO of resorting to threats and intimidations to try to justify the Dowans deal.

The chairman of the parliamentary Public Organizations Accounts Committee (POAC), Zitto Kabwe, has also come under heavy criticism from members of the public and even senior leaders within his own opposition CHADEMA party for his controversial decision to back the Dowans deal.

Observers say Kabwe, who has already made several public statements in support of the dubious deal, could find himself isolated from the leadership hierarchy of the opposition party, and his entire public credibility and even popularity as a refreshingly maverick and strong-minded politician called into question.
 
Nilishapendekeza Dr. Rashid afukuzwe kazi tangu mwaka 2007. Lakini nashangaa JK anaendelea kumbaby sit. Huyu jamaa ameshindwa kuendeleza Tanesco katika mwendo wa karne ya 21. Just fire the guy.

Kundi la wanaostahili kufukuzwa kazi na JK linazidi kuongezeka. Kwa mshangao wa Watanzania wengi jamaa anaacha matatizo dhidi ya serikali yake yakizidi kulundikana kila kukicha. Wanaostahili kufukuzwa hadi sasa ni Mkuu wa PCCB Edwards Hosea, Mwanasheria Mkuu Mwanyika, Waziri wa mambo ya ndani Masha, Waziri wa Nishati Ngeleja, Mkuu wa ATCL Mattaka, Mkuu wa Bandari, Mkuu wa BoT Ndullu, Mkuu wa TANESCO Idrissa Rashid. Katibu Mkuu wa CCM Makamba. Sijui Mkuu anaogopa kitu gani kuwafukuza kazi watu hawa labda kuna siri kubwa inayosababisha JK kushindwa kutumia uwezo alionao kama Rais wa nchi na pia Mwenyekiti wa CCM.
 
Mh. Zitto nimemsamehe lakini alikuwa anakazania sana ooh msimamo wa kamati wakati sisi taarifa tunazopewa zilikuwa zinasema hamna cha kamati wala nini. Nashukuru MwanaCCM ambaye ni high ranking member wa hiyo kamati kaweka mambo wazi::::::

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Estherina Kilasi ambaye pia ni Mbunge wa Mbarali (CCM), alisema pia hakubaliani na jinsi Dk Rashidi alivyotangaza mpango wa kujitoa katika sakata la kununua mitambo hiyo ya Dowans.

Alisema kauli yake ya vitisho kwamba nchi itaingia gizani na wao (Tanesco) wasilaumiwe, sio ya kiungwana na haikupaswa kutolewa na mtu anayeongoza Shirika linalowahudumia Watanzania.

Kilasi alisema kauli hiyo inaweza kutafsiriwa kuwa Mkurugenzi huyo alikuwa na usongo wa kununua mitambo hiyo kufa na kupona.

Alisema maneno ambayo yamemkariri Mwenyekiti wao (Zitto Kabwe) yalikuwa maoni yake binafsi na wala sio ya kamati kwa vile hakuna hata kikao kimoja ambako walikubaliana na ombi la kununua mitambo hiyo.

``Wala hatujawahi kutoa ushauri wowote juu ya suala hilo, zaidi ya kuwaelekeza Tanesco walifikishe kwa kamati husika ya Nishati na Madini,``alisema

Akifafanua, alisema kilichotokea siku hiyo ni semina ambayo Tanesco waliiandaa na kuwakaribisha wajumbe wa Kamati hiyo kwa lengo la kuwaelezea mipango ya kununua mitambo ya Dowans kwa kuwa wana kiasi cha Sh. bilioni 60 kwa ajili hiyo.

``Sisi tuliwahoji kama mnazo Sh Bilioni 60 mnashindwajwe kuongezea kidogo ili mnunue mitambo mipya? Vilevile tukawahoji hivi mambo haya mnayotuambia kwenye semina wameyapeleka kwa wahusika ambao ni Kamati ya Niashati inayoongozwa na William Shelukindo?,`` alisema Kilasi na kuongeza:

``Baada ya hapo tuliwashauri suala hilo walifikishe kwa wahusika (Kamati ya Madini) na hakuna hata mahali pamoja tulipolitolea uamuzi suala hilo kwa vile halituhusu.``

Mbunge huyo alisema kufuatia kauli za Zitto ambazo zimezua malumbano, na kuifanya Kamati yao ionekane ina `walakini` wanamsubiri kwa hamu arejee ili wamuweka kiti moto.

``Unajua baada ya semina ile mimi nilienda Zambia, huku nyuma ndo nikasikia malumbano, lakini baada ya kurejea nimewauliza wenzangu na hasa makatibu wanaoandika muhtasari, kama kuna kikao kingine kimeketi na kutoa uamuzi, lakini wakasema hapana. Sasa tunamsubiri Zito arejee safarini ili tumuulize kulikoni? ``Alisema.
 
Kuna siku tutapata jibu kuhusu lililowasibu Salome Mbatia, Daudi Balali, Chacha Wangwe, Amina Chifupa na msururu wa waliokuwepo na ambao hawakuwepo. Kuna siku tutajuta kwa nini tulitoa kura zetu bila kujua ni shetani gani hasa tunampa uongozi wa nchi. Kuna siku tutajua kwa nini Mh. Zitto kachukua msimamo aliouchukua, yeye mwenyewe keshasema hanunuliki - je alishikiwa bastola ? Kuna siku mambo mengi tu yatafumka - I hope Tanzania bado itaendelea kukalika and we will live to tell the story kwa wajukuu zetu. Ipo siku tutawaelewa wale wote wanaotetea uovu kwa nini wanafanya hivyo na bila woga tutawawajibisha. Siku hiyo tutamjua Richmond, tutamjua Dowans, tutamjua Kagoda, tutamjua Deeo Green, tutamjua Meremeta, Tutamjua EPA, tutamjua Anbem, tutamjua Kiwira na tutamjua shetani wetu na kwa nini anaendelea kutufanya masikini. Siku hiyo kuna watu watalia na kusaga meno, iko siku - inakuja aliye nacho atanyanganywa na kupewa asiyenacho na nchi itawarudi kwa wenyewe - tusubiri.
 
Akifafanua, alisema kilichotokea siku hiyo ni semina ambayo Tanesco waliiandaa na kuwakaribisha wajumbe wa Kamati hiyo kwa lengo la kuwaelezea mipango ya kununua mitambo ya Dowans kwa kuwa wana kiasi cha Sh. bilioni 60 kwa ajili hiyo.

``Sisi tuliwahoji kama mnazo Sh Bilioni 60 mnashindwajwe kuongezea kidogo ili mnunue mitambo mipya? Vilevile tukawahoji hivi mambo haya mnayotuambia kwenye semina wameyapeleka kwa wahusika ambao ni Kamati ya Niashati inayoongozwa na William Shelukindo?,`` alisema Kilasi na kuongeza:

``Baada ya hapo tuliwashauri suala hilo walifikishe kwa wahusika (Kamati ya Madini) na hakuna hata mahali pamoja tulipolitolea uamuzi suala hilo kwa vile halituhusu.``

Mbunge huyo alisema kufuatia kauli za Zitto ambazo zimezua malumbano, na kuifanya Kamati yao ionekane ina `walakini` wanamsubiri kwa hamu arejee ili wamuweka kiti moto.

``Unajua baada ya semina ile mimi nilienda Zambia, huku nyuma ndo nikasikia malumbano, lakini baada ya kurejea nimewauliza wenzangu na hasa makatibu wanaoandika muhtasari, kama kuna kikao kingine kimeketi na kutoa uamuzi, lakini wakasema hapana. Sasa tunamsubiri Zito arejee safarini ili tumuulize kulikoni? ``Alisema.

Zitto,
Ukajieleze sio tu kwenye kamati bali hata na humu JF.
 
Mimi kama mwana chadema ambaye nimejitahidi kuhamasisha vijana wengi walioko nje na ndani ya nchi ujiunga na chadema nimekatishwa tamaa kiasa kikubwa na Zito kabwe na ushabiki wake wa kununua dowans.
Nimepata simu nyingi na email nyingi kutoka ndani na nje ya nchi vijana na watu mbali mbali wakitaka kujua nini kimemsibu Zito.

Wengi wanataka kujua nini msimamo wa Zito zaidi ya rushwa kwenye swala hili. kama si rushwa basi kijana atakuwa amechemsha kisiasa kwa kiasi kikubwa mno.

Kwanini Zito hana washauri kabla hajatoa kauli zake? kwanini chadema haina wataalamu wa maswala ya uchumi na mikataba? kwanini chadema haina wanasheria wanaotoa ushauri kwa wabunge wao kabla ya matamshi yao? kwa nini chadema haifanyi collective maamuzi kabla hawajawafikia waandishi wa habari kwani kama hali ni hii kila mmoja anaropoka anachokijua kwa umaarufu wake au ujuaji wake chama kitatekea.

Zito kachemka big time atulie aanze kurudia wananchi apange sentesi zinazoeleweka. Ila kama kala rushwa mazara ya rushwa ni makubwa sana yanakula ubongo na kumaliza akili yana jenga kiburi na kumwona yeyeto hamnazo. kama umekula mlungula tuachie chadema yetu na uende ccm kwa wala rushwa. nimesoma makala za Tindu Lisu na Mnyika niwazi hamko kundi moja na zito inavyoonekana tumempoteza zito.

Kwa kuonyesha Chadema ni chama makini nashauri Zito ajiuzulu wadhifa wake na kuachia ubunge ili tuweze kuendelea kuheshimika ndani ya nchi na nje kwa wanachama wetu waliojitolea mhanga.

zito ulipofika north amerika tulijitolea mhanga kukusapoti tulijitolea mida yetu na fedha zetu kuandaa midahalo na wewe wana kuja ccm wengi tunawakimbiza tukiamini tunajenga njia mbadala ya kuendesha nchi ila kwa hili umetutisha tulikupa data zote na tukakuonyesha urahisi wa kuwa na nishati ya bei rahisi sijui nini kimekusibu zaidi ya rushwa. tujibu kwa hoja sio kwa hasira au kudata.
 
Back
Top Bottom