Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,095
- 43,305
Mimi nafikiri kutokana na mazingira ya ununuzi wa awali wa mitambo hiyo michakavu kutoka kwenye kampuni feki ya Richmond...Kusapoti ununuzi wa mitambo hiyo bila vigezo vitakavyojitosheleza mbele za wananchi kunaweza kupelekea mitizamo kwamba there is some sort of ufisadi....Honestly hata kama ni uamuzi wake wa kisiasa..Kuwapa hao watu mipesa yote hiyo na wakti kuna maswali yanaoyotakiwa kujibiwa ni swala linalohitaji maelezo ya kina.
Naona umezungumzia sana kuhusu "kutofautiana naye kimaelezo" Kumbuka ni tofauti za maamuzi na utekelezaji na si tu "maelezo" Malezo aliyoyatoa bado hayawezi kuhalalisha ununuzi wa mitambo hiyo na hivyo basi atueleze nia yake haswa ilikuwa ni nini na si tu kusema haogopi kuitwa fisadi ama kuonekana ana mtizamo wa tofauti.
Na pia unaposema mmetofautiana kisiasa una maana gani? Yani Zitto a lobby kumsadia Rostam na Lowassa na Karamagi halafu useme ni utofauti wa kisiasa tu, well kama wewe ni CHADEMA kama Zitto then utofauti wenu wa kisiasa unahitaji maelezo zaidi.
Ukishindwa kuwaelesha wana JF utaweza vipi kuwaelewesha wananchi kama si kuwadanganya na wizi mtupu?
Zitto ana uamuzi gani katika suala la ununuzi wa majenereta? akiamua yanunuliwe yatanunuliwa? na akiamua yasinunuliwe je?