Dowans: Another Richmond in making?

Dowans: Another Richmond in making?

Nimebahatika kuzungumza na wajumbe wengi wa kamati ya Zitto, nimebahatika pia kuzungumza na wajumbe wengi wa kamati ya kina Mwakyembe, nimebahatika pia kuzungumza na watu wa ofisi ya Bunge, nimebahatika pia kusoma nyaraka za kamati ya Zitto na ile ya Mwakyembe, nimebahatika pia kusoma nyaraka za Waziri Ngeleja na mawasiliano yake na....... (nitaweka wazi siku mwafaka)... Nimebahatika pia kupata nyaraka zote muhimu na ambazo nadhani zitaanikwa JF soon.

Kwa maelezo hayo hapo juu, hakuna ambaye haiungi mkono Tanesco (si Dk. Rashidi) kupata mitambo mipya, hiyo iko katika mipango yao ya muda mrefu na mfupi. Hata wewe utapenda Tanesco wapate mitambo. Zitto anakosea kutosema asichosema na hivyo kutoa nafasi ya kuwachanganya watu, na kuna mahali alisema anafanya makusudi. Sijui anateka kutuambia nini. Pengine huu mjadala umesaidia sana kuwabana Tanesco mpaka wamekwama. Zitto amefanikiwa lakini amekuwa KAFARA wetu. Kama si Zitto suala hili lisingekuwa HOT kama ilivyo sasa na ndio maana limekuwa na wasemaji wengi na limesaidia mjadala kupaaa na kuwatisha kina Dk Rashidi am baya akageuka kuwatisha Watanzania.

Soma maandiko yake. Sikiliza matamshi yake ya SAUTI si ya kunukuliwa, utaona hakusema anaunga mkono kwamba lazima kunuliwa kwa DOwans. Kuna mahala amesema (narudia) kwamba kaama kuna ulazima wa kununua Dowans basi sheria zizingatiwe. na Kuwepo mjadala ili uamuzi ufanyike kwa HOJA si kwa JAZBA. Hapo sioni kosa la kimantiki ila kuna kosa la KISIASA kwam ba Dowans/Richmond ni alama ya mafanikio ya vita ya UFISADI kwa hiyo hatuwezi kukubali kwa gharama yoyote mtu yeyote (hata Zitto) kuuvunja huu MNARA wa vita ya UFISADI

Halisi,
Zitto nimemsoma kw amakini sana kauli zake hapa JF

1. Zitto alizungumza kwa niaba ya Kamati

2. Ni kweli Zitto alisema kama kuna ulazima wa kununua Mitambo ya Dowans basi sheria zifuatwe..............wat wakamuwekea sheria.........yeye akasema sheria mama haisemi hivyo....watu wakamwambia unaposoma sheria mama unatakiwa usome na regulations zake.....sikumsikia akijibu......Zitto anasahau kuwa sheria mama haiwezi kuainisha kila kitu

sasa basi narudia

1. Msimamo wa TANESCO ulikuwa nikununua mitambo ya Dowans....eti wakidai ni "Opportunity" iliyojitokeza

2.Zitto akaja boldly kuweka msimamo wake hapa JF kuwa he stands with TANESCO......nafikrir hili kosa la KIMANTIKI na wala si kisiasa au

3.Kosa lake kisiasa ni kukubali kuburuzwa na msimamo wa kamati yake.......kama alivyotuonyesha awali kuwa anasimama na kamati yake

4.Nia yake ya kukutana na Kamati ya Shelukindo...naweza kuelewa ilikuwa ni opportunity nzuri kwake kupata support kama yeye KWELI alikuwa anapinga ununuzi wa Mitambo ambayo TANESCO wanaitaka i.e. DOWANS....unfortunately hiyo nafasi haikutokea......na akaja akaharibu zaidi kuja kuweka msimamo wake hapa JF........

Well Halisi.....Mkuu wewe nakuaminia sana tu........labda hapo baadaye utakapokuja na facts zingine pengine nitakuelewa..........
 
Halisi: nimerudia mara mbili kuisoma thread yako ya awali na ninakiri kusema kwamba nashindwa kuelewa unasimama wapi katika sakata hili la Zitto na Dowans! Kuna mmoja umemjibu kuwa tatizo si Zitto, ni Dowans. Nadhani ungekuwa sahihi zaidi iwapo ungesema "chanzo ni Dowans, na si Zitto". Zitto kawahuzunisha mamilioni ya mashabiki wake kwa kuchukuwa msimamo ambao waliona asingeuchukuwa -- ni msimamo wa upande wa pili.

Hao wa upande wa pili waliona hawana mtu credible upande wao (maana wote wanatajwa kuwa mafisadi) kuwapigia debe kuhusu ununuzi wa mitambo hiyo, na hivyo wakamsajili Zitto, naye akakubali. Waliamua kuwakaanga 'wapinga ufisadi' kwa mafuta yao wenyewe!

Ni kama vile tunaweza kusema 'wapinga ufisadi' wanawatumia wabunge wa CCM kuikaanga CCM kwa mafuta yake. Lakini alijikuta katika awkward situation, kutumikia mabwana wawili wenye msimamo tofauti na hivyo kwa vyovyote vile aijikuta anaicheza karata yake vibaya.
 
Halisi,
Zitto nimemsoma kw amakini sana kauli zake hapa JF

1. Zitto alizungumza kwa niaba ya Kamati

2. Ni kweli Zitto alisema kama kuna ulazima wa kununua Mitambo ya Dowans basi sheria zifuatwe..............wat wakamuwekea sheria.........yeye akasema sheria mama haisemi hivyo....watu wakamwambia unaposoma sheria mama unatakiwa usome na regulations zake.....sikumsikia akijibu......Zitto anasahau kuwa sheria mama haiwezi kuainisha kila kitu

...

Mkuu Ogah, Tuko pamoja. Tena umenikumbusha. Zitto tabia yake ya ubishi na kutaka faida hapo ilimponza na narudia makosa ya kisiasa hakupima upepo wa kisiasa na kwa bahati mbaya nadhani ni sababu alikuwa nje ya nchi hakuwa anaona joto la Tanzania kwa vizuri zaidi, akaanza kutaka watu wamuonyeshe kipengele cha sheria ili aelewe. Lakn tatizo halikuwa sheria tu, kuna mambo mengi yamejificha nyuma ya DOwans na mengine Zitto atayajua baadaye, hakupaswa kwenda mbio.

Halisi,
1. Msimamo wa TANESCO ulikuwa nikununua mitambo ya Dowans....eti wakidai ni "Opportunity" iliyojitokeza

2.Zitto akaja boldly kuweka msimamo wake hapa JF kuwa he stands with TANESCO......nafikrir hili kosa la KIMANTIKI na wala si kisiasa au
.

Tanesco walikuwa na nia thabiti ya kununua Dowans na walishaandaa kila kitu, kuna watu wandai wamelipa hata advance (hakuna hakika), lakini kitendo cha kuietetea mitambo kuwa ndio opportunity ni wenda wazimu wao kutaka kutufanya MABWEGE. Tanesco waliapa nafasi ya kwanza Dowans na kwamba ikishindikana ndio wanunue mipya. Wamekwama na bado wataumbuka. Zitto alikosea, angeweka wazi anaungana na Tanesco kwamba wanahitaji mitambo na suala la mitambo gani liwe mjadala wa baada ya kuamua sasa ni lazima wanunue. Si kutoa statementa kavu kavu.

3.Kosa lake kisiasa ni kukubali kuburuzwa na msimamo wa kamati yake.......kama alivyotuonyesha awali kuwa anasimama na kamati yake

4.Nia yake ya kukutana na Kamati ya Shelukindo...naweza kuelewa ilikuwa ni opportunity nzuri kwake kupata support kama yeye KWELI alikuwa anapinga ununuzi wa Mitambo ambayo TANESCO wanaitaka i.e. DOWANS....unfortunately hiyo nafasi haikutokea......na akaja akaharibu zaidi kuja kuweka msimamo wake hapa JF........
....

KWa kweli Kamati yake haikumburuza, kamati yake ilikuwa wazi kwamba haibariki ununuzi wa Dowans bali inapenda mjadala wa pamoja na kamati ya Shellukindo ili waliyoyasema tanesco wayaseme kwa magwiji wa sekta hiyo ambao baadhi walisafiri nje ya nchi kufuatilia. Kwa hili Kamati ya ZItto ilikuwa tayari kwa uamuzi wowote wa pamoja, kwa bahati mbaya kama ulivyosema mkuu hakupata hiyo nafasi na sasa wanamshughulikia kisiasa.
 
Halisi: nimerudia mara mbili kuisoma thread yako ya awali na ninakiri kusema kwamba nashindwa kuelewa unasimama wapi katika sakata hili la Zitto na Dowans! Kuna mmoja umemjibu kuwa tatizo si Zitto, ni Dowans. Nadhani ungekuwa sahihi zaidi iwapo ungesema "chanzo ni Dowans, na si Zitto". Zitto kawahuzunisha mamilioni ya mashabiki wake kwa kuchukuwa msimamo ambao waliona asingeuchukuwa -- ni msimamo wa upande wa pili.
.

Niliposema tatizo ni Dowans nilikuwa na maana hiyo hiyo kwamba chanzo ni Dowans lakini, nilikuwa na maana pana zaidi kwamba, mjadala tunaopaswa kuelekeza nguvu zetu sasa si Zitto tena ni Dowans na jinsi ya kuhakikisha tunarudisha fedha zetu. Hata Zitto naamini alitamani hata mitambo ya Dowans itaifishwe ili tuweze kuokoa fedha ambazo tunawadai
 
Nasikitika kusema kwamba nalazimika kuzima PC ili niweze kwenda kupata pilau ya Maulidi. Maulidi njema
 
Mkuu Halisi, nakusoma na ninasoma kama ilivyo hapo juu, sio kama ulivyoandika.

Zitto kachemsha, aombe radhi.

Uwiano...Sidhani kama Zitto ataomba radhi, kwanza issue ilipofikia sasa akifanya hivyo ndiyo itakuwa kama amezidi kuchemsha, na pia ile dhana yake ya misimamo isiyoyumba itakosa mantiki.
Kwa upande wa pili naona Mwanahalisi ameamua kumpigia kifua, nadhani ameamua kubaki na msimamo wake.
 
Should Zitto issue a statement that, "I screwed up and I am very sorry"?

ANALYSIS: Zitto is now the opposition’s biggest liability

RUTASHUBANYUMA NESTORY
THIS DAY
Arusha

THE perfidious goofs and gaffes from a once promising opposition luminary Zitto Kabwe can be likened to a political comet hastily flickering out into obscurity.

Lately, Zitto Kabwe had straddled the political terrain like a colossus when he took the Buzwagi mining scam by its horns.

During that time it was risky and unpopular to stand against state sponsored graft where the CCM dominated House had an infamous reputation muffling executive dissent.

But whether Zitto’s Buzwagi touch was inspired by our collective good or he was simply a political homo sapien capable of seizing the moment to advance by then his political career is something we now have the evidence to scour through.

If through Zitto’s acts of commission or omission our collective wellbeing was served by his teeters, it was just a mere coincidence but nothing more.

Where we had empathized on his poor soul when CCM temporarily booted him out of the then House of Adulators; the executive stealthily approached him to be part of another junketing commission to snoop over mining conundrums.

Common sense should have informed the fledgling politician to thwart CCM advances since it was a ploy to slime the opposition with CCM’s own mess. But a self-serving Zitto had other ideas.

The House indictment had left Zitto with a half pay and a fourth mining commission presented him with a rare opportunity to bury a gaping fiscal hole the House had inflicted upon him.

In this case, Zitto chose personal agenda at the expense of principled leadership when he succumbed and reciprocated to CCM’s devious plot.

Though Zitto may say he is well drilled in trade economics and was lavished with the privilege of brushing his career teeth at the treasury, mining quagmires were by far way up his league.

He lacked the necessary vitae to fiddle with the complex subject of mining discipline.

Besides, his lone ranger antics in that commission were least effective as they were embellished by the poor quality of the report. The report was a distant cry at challenging the iron grip of a perverse status quo in the mining schemes.

Zitto's political stature was exalted within the opposition ranks and like an old African saying: ’’Mgema ukimsifia tembo huliweka maji.’’

The rise of Zitto into political stardom had falsely emboldened him to the extent that he had won our national confidence.

He could therefore wag his tongue in a manner he likes while a gullible public will marvel at his messianic deliverance!

It is in the rippling Tanesco- Dowans entanglement where his true colours have come to the fore. While we have procurement laws against Tanesco, Zitto sees no evil and in fact he feels the laws can just go to hell!

What Tanesco is manoeuvring is to co-opt the House into a collusive partnership of offending the law as if the House is above the law!

Tanesco’s inopportune tactics of instilling fear of perennial blackouts must be exposed for what they are: With the rainfall season around the corner is there a real grain of truth there?

Dowans’ offer is devoid of sale guarantees and what will happen if the loudly claimed tested generators fail the real test of generating power a few months after Dowans had laughed all the way to the Bank

Can Zitto think along these lines before he misleads us Is his weird position above political partisanship.

If I have to pen down Zitto's unauthorized biography, the epigraph will read something like: ’’Here is a narration of a political upstart who licked his gruel before catering my tureen!’’

Rutashubanyuma Nestory is a public policy analyst based in Arusha
 
Zitto hana sababu ya kuomba radhi kwa kuchukua msimamo alioamini kufuatana na taarifa zote alizokuwa nazo na dhamira yake kuwa alikuwa sahihi.

Kuna watu hapa naamini wanataka kutumia nafasi hii ya tofauti na Zitto kumsambaratisha na kumdunisha kijana huyu na ikiwezekana kumkatisha tamaa. Zitto kama mwanasiasa yeyote au Mtanzania yeyote mwingine ana haki ya kuwa na msimamo wake tofauti na wa watu wengine.

Mambo ya siasa za "fuata upepo" yamepitwa na wakati. Ati kwa vile watu wengi JF wamepinga ununuzi wa majenereta ya Dowans basi Zitto alitakiwa naye awe upande huo kwa sababu moja tu nayo ni kufanana (uniformity). Kwamba ili kweli tujue yuko upande wetu basi ni lazima awe na msimamo kama wa kwetu.

Matokeo yake ni kuanza kuwa na wanasiasa wa kuturidhisha kujisikia vizuri. Wanasiasa wasio na mawazo yao bali yale ya mkumbo.

Imesemwa vizuri tangu mwanzo kuwa Zitto alichukua msimamo ambao kisiasa ulikuwa na makosa makubwa. Hili wala halina ubishi. Tatizo ni kuwa makosa hayo tunayaona sisi na yeye hajayaona au hajashawishika kuyaona. Kilichonisikitisha sana katika mjadala huu ni kuwa mara nyingi watu wanaposhindwa kujenga hoja wao huleta vioja.

Badala ya kumuita Zitto kila aina ya majina kwa sababu hana msimamo kama wa mtu mwingine lilikuwa ni jukumu la watu kumshawishi kwa hoja. Sehemu moja ambapo nilipenda mjadala huu ni pale lilipokuja suala la Kisheria na Kanuni za Manunuzi ya serikali. Pale palikuwa na hoja na ushahidi wa hoja. Lakini wengine hawawezi hayo na wao kwao kwa vile "wameumizwa" basi wanachukulia tu kawasaliti.

I'll tell you what, Nitawachukua watu wenye ujasiri wa kina Zitto anyday kuliko viongozi ambao wanafuata upepo wa wafadhili wao au mabwana zao.

Lakini kubwa zaidi ni kuwa ni kutofanya maamuzi ya kisiasa kweli kwa mtu kuweka imani, hisia na vionjo juu ya mtu mmoja kuwa huyo mtu hatakiwi kukuudhi, kuchukua msimamo kinyume na wewe au hata kupingana na wewe! Kwamba akienda nje ya mstari uliojichorea basi mtu huyo ni msaliti, fisadi na katugeuka, ati hatumwelewi. Huwezi kuweka imani yako juu ya mtu mmoja namna hiyoo hiyo.

Katika maisha haya nimejifunza kuwa marafiki watakusaliti, ndugu watakukana, adui atakuwa mwokozi na wale uliowadharau watasimama kama mashujaa! Yote ni sehemu ya hili drama tunaloliita maisha. Hivyo, kweli Zitto kachukua msimamo tofauti ambao kisiasa haukuwa na hekima (kama alivyosema Halisi na wengine) lakini kufikia mahali pa kumshusha na kumfanya duni na kujaribu kumuangamiza na ati kumtaka ajiuzulu na kuomba radhi ni jazba isiyo na sababu!

Ninafahamu bado kuna watu ambao wana kisasi na kijana huyu na umaarufu wake na mvuto wake na sasa wanataka kutumia nafasi hii kumuangamiza hasa kuelekea 2010. Nakumbuka jinsi walivyojaribu baada ya mambo ya Buzwagi na kifo cha Mhe. Wangwe, nguvu zile zile zipo leo tena. Ninafahamu wapo wale ambapo kweli walikwazika kwa sababu ya jinsi walivyo/wanavyomheshimu Zitto, lakini ninafahamu pia kuwa na wale ambao sasa wanachekelea kwamba "wamempata". Hawa wote wanataka kuona Zitto anakuwa duni, anaondolewa na kufanywa kuwa irrelevant.

Hii yote ni sehemu ya siasa, ni matumaini yangu kuwa hili halitamrudisha nyuma, atatambua political misstep that he took, he'll learn to be calculating, and he will always look into political ramification of whatever position he might take in the future. Naamini Zitto is not a typical politician, he is a technocrat who got into politics. Nadhani pole pole ataielewa siasa kuwa it is more than simple right and wrong, maslahi ya taifa au la..

So, I heard ya'll but cut the guy some slack! vinginevyo, bado tutakwazika na kina Mwakyembe, Selelii, mama Kilango, na wengine siku wakichukua maamuzi au misimamo ambayo itafutanya tukune vichwa.
 
Zitto hawezi omba msamaha, hilo litamwaribia zaidi..Ni matamanio ya walio wengi kwa nia tofauti kuona Mh Zitto anaomba msamaha...Kama ilivyokuwa kwenye issue ya mitambo michakavu....Sasa issue ya kuomba msamaha ni mgogoro mwingine unaomkabili mbunge wetu kijana.
Paugumu sana hapo...Tunamtakia kila la kheri.
Isipokuwa hao wanaotaka aombe msamaha wamesahau kuwa hagombei tena ubunge? Ama wanataka waje kumtisha tena atakapogombea urahisi kama alivyoweka wazi huko nyuma? Je kuomba ama kutokuomba msamaha lipi ni bora?
 
Halisi,

Mkuu nadhani mada hii haihitaji mwanasiasa au mtaalam kuweza kutafsiri alichosema Zitto ndani ya kijiwe hiki... Ya JF yabakie JF lakini bob....mmmmnnnnh!

Tunaposema Zitto kachemsha tuna maana ni ile KAULI yake tata kuhusiana na manunuzi ya mitambo hii sio swala la umuhimu wa mitambo ya dharura kwa upenyo mdogo sana wa muda unaohitajika..

Kama Zitto hakuchemsha basi bila shaka sisi hapa JF ndio tumechemsha!..hatukumwelewa au sijui tumezusha..No mkuu wangu, Zitto shikaji tena la nguvu lakini alichemsha tena bigtime..
Mkuu, sote tunafahamu kwamba tunahitaji mitambo ku replace ile ya Dowans, na ajabu haikuwa issue siku zote hadi siku Dowans walipotangaza Tender ndipo uharaka na dharura ilipokomaa..

Binafsi nadhani maamuzi ya kamati yake hayakuwa source ya mfarakano mkubwa uliotokea kati ya wana JF (nikiwamo mimi) na Mh. Zitto isipokuwa ni ile kauli yake ama lugha aliyotumia ku justify umuhimu wa kununuzi wa mitambo chakavu ya Dowans..Na hata kushauri sheria ivunjwe kama ikiwezekana kwa sababu huko nyuma tumewahi kuvunja!...ati sio kitu kigeni.. jamani hivi kweli wangefikia ku propose kuvunja sheria ikiwa Dowans haikuwa mazungumzo..

Mkuu, kauli ya Zitto ilikuwa heavy, nzito sana kutetea manunuzi ya mitambo ya Dowans, binafsi sikuona mahala akisisitiza ununuzi wa mitambo chakavu toka shirika jingine, mitambo mipya toka shirika fulani yaani mazungumzo yote ya kamati ya Zitto na Tanesco yalihusiana na mitambo ya Dowans kufuatia maamuzi ya kamati ya Mwakyembe - as if somethin wasn't right!...na ndio maana nikasema Zitto anakuwa kama waziri Kijana..na ndiyo iliyo nukuliwa ktk baadhi ya magazeti lakini source yake imetoka hapa JF... Na ndicho kilichomponza Zitto..

Pili, Siku zote mwanasiasa unapoingia ushirika kama huu hukatazwi kuwa by Partisan, lakini muhimu sana uwe makini na kile kilichokusudiwa toka upande wa pili kwani sio mara zote sera inayosomeka kama inajenga ikatumiwa ipaswavyo..Mfano sera ya kusamehe kodi wawekeshaji Tanzania inasomeka vizuri sana kama kivutio cha wageni nchini lakini in reality ni sera iliyo tu cost miaka 10 ya Maendeleo..haihitaji mchumi kuwaelezea wananchi uzito wa maumivu walikwisha yabeba..Kisha kibaya zaidi ni pale utakapo unga mkono kutofautiana na wanachama/wananchi unaowawakilisha..

Mkuu Halisi, Zitto alichemsha... na tutamsamehe au tunamsamehe lakini sidhani kama wananchi wataweza kusahau kwa urahisi sinema hii kutoipa Oscar nominee mwisho wa mwaka!. Hasa ukizingatia kwamba kauli yake ilikuwa ikijibu hukumu ya kamati ya Mwakyembe iliyotangulia kupinga ununuzi wa mitambo ya Dowans!...

Straight to the point, kamati ya Mwakyembe waliztoa maamuzi kuhusiana na mitambo ya Dowans, hawakupindisha ukweli wala kusema hatuhitaji mitambo mipya haraka iwezekanavyo..Na Zitto na kamati yake hawakukaa kitako na Tanesco kutafuta another solution nje ya Dowans, hakuna mapendekezo yoyote ya haraka toka shirika hata MOJA! zaidi ya Dowans.. na hata ukisoma taarifa zote toka huyo Ngereja, Idrissa na wapambe wote hawa walikuwa wakipingana na maamuzi ya kamati ya Mwakyembe kuhusiana na Dowans..Hakuna hata sehemu moja wametaja au kupendekeza shirika jingine zaidi ya Diowans.. iwe kwa mitambo mipya au chakavu.

Sasa wana JF wanamlaumu kwasababu:-
1. Zitto alafahamu fika Utata wa Dowans na nini chimbuko lake na who're the player..
2. Zitto anafahamu vita iliyomo ndani ya CCM na makundi yake yalivyojipanga, na kwa nini mtu kama Mwakyembe na kamati yake walipiga vita ununuzi wa mitambo hiyo ya Dowans..Mwakyembe alikwisha chimba undani wa Richmond/ Dowans..he knows better.
3. Zitto alifahamu sheria yetu inasema nini dhidi ya ununuzi wa mitambo chakavu...Ni imani ambayo sio tu inapongezwa na wataalam, bali pia wananchi na wanachama wa Chama chake ktk utekelezaji wa uongozi bora..
4. Zitto pia alifahamu Tanesco (hasa mtu kama Idrissa) wangempa sura ya upande mmoja wa shilingi..

Kwa hiyo mkuu mmlolongo wa haya yote ndiyo chimbuko la wananchi hasa hapa JF kuanza kuhoji maamuzi ya kamati ya Zitto na hasa ile taarifa kali aliyoitoa humu kuhusiana na MSIMAMO WAKE na hasa pale aliposema HATAJALI mawazo ya wananchi maadam yeye anafahamu he is RIGHT!..
 
Zitto hana sababu ya kuomba radhi kwa kuchukua msimamo alioamini kufuatana na taarifa zote alizokuwa nazo na dhamira yake kuwa alikuwa sahihi.

Kuna watu hapa naamini wanataka kutumia nafasi hii ya tofauti na Zitto kumsambaratisha na kumdunisha kijana huyu na ikiwezekana kumkatisha tamaa. Zitto kama mwanasiasa yeyote au Mtanzania yeyote mwingine ana haki ya kuwa na msimamo wake tofauti na wa watu wengine.

Mambo ya siasa za "fuata upepo" yamepitwa na wakati. Ati kwa vile watu wengi JF wamepinga ununuzi wa majenereta ya Dowans basi Zitto alitakiwa naye awe upande huo kwa sababu moja tu nayo ni kufanana (uniformity). Kwamba ili kweli tujue yuko upande wetu basi ni lazima awe na msimamo kama wa kwetu.

Matokeo yake ni kuanza kuwa na wanasiasa wa kuturidhisha kujisikia vizuri. Wanasiasa wasio na mawazo yao bali yale ya mkumbo.

Imesemwa vizuri tangu mwanzo kuwa Zitto alichukua msimamo ambao kisiasa ulikuwa na makosa makubwa. Hili wala halina ubishi. Tatizo ni kuwa makosa hayo tunayaona sisi na yeye hajayaona au hajashawishika kuyaona. Kilichonisikitisha sana katika mjadala huu ni kuwa mara nyingi watu wanaposhindwa kujenga hoja wao huleta vioja.

Badala ya kumuita Zitto kila aina ya majina kwa sababu hana msimamo kama wa mtu mwingine lilikuwa ni jukumu la watu kumshawishi kwa hoja. Sehemu moja ambapo nilipenda mjadala huu ni pale lilipokuja suala la Kisheria na Kanuni za Manunuzi ya serikali. Pale palikuwa na hoja na ushahidi wa hoja. Lakini wengine hawawezi hayo na wao kwao kwa vile "wameumizwa" basi wanachukulia tu kawasaliti.

I'll tell you what, Nitawachukua watu wenye ujasiri wa kina Zitto anyday kuliko viongozi ambao wanafuata upepo wa wafadhili wao au mabwana zao.

Lakini kubwa zaidi ni kuwa ni kutofanya maamuzi ya kisiasa kweli kwa mtu kuweka imani, hisia na vionjo juu ya mtu mmoja kuwa huyo mtu hatakiwi kukuudhi, kuchukua msimamo kinyume na wewe au hata kupingana na wewe! Kwamba akienda nje ya mstari uliojichorea basi mtu huyo ni msaliti, fisadi na katugeuka, ati hatumwelewi. Huwezi kuweka imani yako juu ya mtu mmoja namna hiyoo hiyo.

Katika maisha haya nimejifunza kuwa marafiki watakusaliti, ndugu watakukana, adui atakuwa mwokozi na wale uliowadharau watasimama kama mashujaa! Yote ni sehemu ya hili drama tunaloliita maisha. Hivyo, kweli Zitto kachukua msimamo tofauti ambao kisiasa haukuwa na hekima (kama alivyosema Halisi na wengine) lakini kufikia mahali pa kumshusha na kumfanya duni na kujaribu kumuangamiza na ati kumtaka ajiuzulu na kuomba radhi ni jazba isiyo na sababu!

Ninafahamu bado kuna watu ambao wana kisasi na kijana huyu na umaarufu wake na mvuto wake na sasa wanataka kutumia nafasi hii kumuangamiza hasa kuelekea 2010. Nakumbuka jinsi walivyojaribu baada ya mambo ya Buzwagi na kifo cha Mhe. Wangwe, nguvu zile zile zipo leo tena. Ninafahamu wapo wale ambapo kweli walikwazika kwa sababu ya jinsi walivyo/wanavyomheshimu Zitto, lakini ninafahamu pia kuwa na wale ambao sasa wanachekelea kwamba "wamempata". Hawa wote wanataka kuona Zitto anakuwa duni, anaondolewa na kufanywa kuwa irrelevant.

Hii yote ni sehemu ya siasa, ni matumaini yangu kuwa hili halitamrudisha nyuma, atatambua political misstep that he took, he'll learn to be calculating, and he will always look into political ramification of whatever position he might take in the future. Naamini Zitto is not a typical politician, he is a technocrat who got into politics. Nadhani pole pole ataielewa siasa kuwa it is more than simple right and wrong, maslahi ya taifa au la..

So, I heard ya'll but cut the guy some slack! vinginevyo, bado tutakwazika na kina Mwakyembe, Selelii, mama Kilango, na wengine siku wakichukua maamuzi au misimamo ambayo itafutanya tukune vichwa.

NBC, msnbc.com and news services
updated 10:21 p.m. ET, Tues., Feb. 3, 2009

WASHINGTON - President Barack Obama on Tuesday abruptly abandoned his nomination fight for Tom Daschle and a second major appointee who failed to pay all their taxes, telling NBC News: "I screwed up."

"I've got to own up to my mistake.
Ultimately, it's important for this administration to send a message that there aren't two sets of rules - you know, one for prominent people and one for ordinary folks who have to pay their taxes," Obama said on NBC's "Nightly News with Brian Williams."

The admission came little more than 24 hours after Obama had said he was "absolutely" committed to Daschle's confirmation as secretary of health and human services, a job in which he would taken the lead in the president's ambitious plans for the nation's health care system.
/
 
Mzee Mwakijiji,
Katika maisha haya nimejifunza kuwa marafiki watakusaliti, ndugu watakukana, adui atakuwa mwokozi na wale uliowadharau watasimama kama mashujaa! Yote ni sehemu ya hili drama tunaloliita maisha. Hivyo, kweli Zitto kachukua msimamo tofauti ambao kisiasa haukuwa na hekima (kama alivyosema Halisi na wengine) lakini kufikia mahali pa kumshusha na kumfanya duni na kujaribu kumuangamiza na ati kumtaka ajiuzulu na kuomba radhi ni jazba isiyo na sababu!
..
Mkuu hapa wala sikubaliani na wewe kabisa.. Ni mawili Aidha hao marafiki wako ni Wanafiki au wewe mwenyewe una matatizo!..
Nikirudi kwa issue ya Zitto kulingana na maneno haya - naogopa hata kufikiria ulichoandika!...
 
Mzee Mwakijiji,
..
Mkuu hapa wala sikubaliani na wewe kabisa.. Ni mawili Aidha hao marafiki wako ni Wanafiki au wewe mwenyewe una matatizo!..

Hapana.. duniani hakuna machaguzi mawili tu (fallacy of false dilemma) Yawezekana yote mawili! marafiki ni wanafiki na mimi nina matatizo au manne, kwamba wao siyo wanafiki na mimi sina tatizo!

Nikirudi kwa issue ya Zitto kulingana na maneno haya - naogopa hata kufikiria ulichoandika!...

Its ok, wakati mwingine hata mimi mwenyewe sipendi ninachoandika, hivyo sirudii kukisoma.
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu, kufuatia maelezo yako hapo juu...nilichosema mimi sio swala la uchaguzi..Kama ume experience mambo hayo toka kwa marafiki zako basi kuna tafsiri mbili tu..
1. Marafiki zako wanafiki au 2. Wewe mwenyewe una matatizo..

In real life marafiki wanatakiwa kinyume kabisa cha yaliyokutokea..haikutokea hivyo basi jibu umelipata..Na nikitazama upande wa issue hii naogopa sana kuwepo Uwezekano kuwa Zitto kapitia yaliyokukuta wewe..
 
Nilijuwa Zitto ataleta mgawanyiko mkubwa sana hapa JF...Zitto ni kweli amewaweka mashabiki wake kwenye hard times sana...Well lets wait and see, nina imani Zitto anaweza kuja na maelezo ya kina ambayo at least watu wataweza ku level na uamuzi wake ambao ulikuwa so un popular.
 
Mzee Mkandara nimesema "katika maisha haya nimejifunza" sikusema mambo hayo yote yamenitokea mimi. Nadhani hapo umenikosa kidogo.
 
Nilijuwa Zitto ataleta mgawanyiko mkubwa sana hapa JF...Zitto ni kweli amewaweka mashabiki wake kwenye hard times sana...Well lets wait and see, nina imani Zitto anaweza kuja na maelezo ya kina ambayo at least watu wataweza ku level na uamuzi wake ambao ulikuwa so un popular.

My point ni kuwa Zitto haitaji kutoa maelezo zaidi ya aliyoyatoa. Wote tunajua alichosema. Wapo ambao hawakubaliani naye na wapo wanaokubaliana naye. Mimi sijakubaliana naye, lakini kutokubaliana naye haina maana namuona fisadi, kanunuliwa au kanisaliti! Ninachukulia tu kuwa tumetofautiana kimtazamo na hasa kisiasa. Naamini position yangu ina nguvu kuliko ya kwake (bila ya shaka na yeye anaona kinyume chake). Lakini tofauti hiyo haisemi lolote kuhusu ninavyomfikiria au kumdhania kwa sababu ya kutofautiana naye.
 
NBC, msnbc.com and news services
updated 10:21 p.m. ET, Tues., Feb. 3, 2009

WASHINGTON - President Barack Obama on Tuesday abruptly abandoned his nomination fight for Tom Daschle and a second major appointee who failed to pay all their taxes, telling NBC News: "I screwed up."

"I've got to own up to my mistake. Ultimately, it's important for this administration to send a message that there aren't two sets of rules - you know, one for prominent people and one for ordinary folks who have to pay their taxes," Obama said on NBC's "Nightly News with Brian Williams."

The admission came little more than 24 hours after Obama had said he was "absolutely" committed to Daschle's confirmation as secretary of health and human services, a job in which he would taken the lead in the president's ambitious plans for the nation's health care system.
/

BAK...Pointi yako nimeipata, lakini kwanza tujiulize; Je aombe msamaha kwa lipi?

Tukiangalia kwa undani....Ni kweli kuna hoja kuwa inaweza kulazimu mbunge Zitto aombe radhi...Aombe radhi kwamba licha ya kwamba nia yake ni nzuri, bado uamuzi aliouchukuwa haukuwa maarufu miongoni mwa wananchi walio wengi kutokana na mazingira mpango mzima wa ununuzi wa mitambo hiyo chakavu.

Msimamo wake ni kwamba hakutaka wananchi wakae gizani pamoja na kuhatarisha hali ya kiuchumi kwa kuiokosesha serikali mapato na shughuli za kiuchumi kuzorota.

Ila mgogoro ni mpana zaidi ya hapo kutokana na fact kwamba Zitto alikuwa akiongea kama vile ni maamuzi ya kamati yake,na mara baada ya hapo kama kuna atakaebisha,naomba arejee malumbano kati ya wanakamati mbili,ile ya nishati na madini vs ile ya mahesabu ya mashirika ya umma ambayo Zitto ni mwenyekiti.

Hivyo basi tunamtaka Zitto aombe radhi kwasababu mitambo ni ya Dowans ama kwasababu mitambo ya Dowans ingenunuliwa basi tungepata hasara?

Tuangalie objectives,halafu tuone kama uamuzi wa kunuwa ama kutonunuwa mitambo hiyo itakuwa na impact gani kwenye Taifa kiuchumi na kijamii.

Kuna walioleta hoja kuwa ni asilimia ndogo sana ya wananchi wenye umeme na hivyo pointi ya kuwa wananchi walio wengi wata suffer haina nguvu,je kuna ukweli ndani yake?

Zitto ni lazima aseme something ili kuwaweka wananchi sawa...Itabidi aandike makala na hata kama ni ndefu tutaisoma...Makala yenye maelezo ya kina, kwamba ilibidi achukuwe uamuzi wake huo kwasababu anawapenda sana wananchi zaidi ya Dowans, na kwamba kama vile ile methali inayosema ukimchunguza kuku hutamla...Kwamba tusichunguze sana Dowans la sivyo hatutaikubali mitambo yao? Nafikiri ni possible kwa Mh Zitto kustand somewhere bila kubadili msimamo wake at the same time aki regret mazingira ya mpango mzima wa ununuzi wa awali wa Richmond ambao umepelekea uamuzi wake kuwa unpopular.

Sijui kama Zitto cares lakini kama bado ataendelea kuwa kwenye siasa basi he's gonna have to care.
 
Last edited:
My point ni kuwa Zitto haitaji kutoa maelezo zaidi ya aliyoyatoa. Wote tunajua alichosema. Wapo ambao hawakubaliani naye na wapo wanaokubaliana naye. Mimi sijakubaliana naye, lakini kutokubaliana naye haina maana namuona fisadi, kanunuliwa au kanisaliti! Ninachukulia tu kuwa tumetofautiana kimtazamo na hasa kisiasa. Naamini position yangu ina nguvu kuliko ya kwake (bila ya shaka na yeye anaona kinyume chake). Lakini tofauti hiyo haisemi lolote kuhusu ninavyomfikiria au kumdhania kwa sababu ya kutofautiana naye.

Mimi nafikiri kutokana na mazingira ya ununuzi wa awali wa mitambo hiyo michakavu kutoka kwenye kampuni feki ya Richmond...Kusapoti ununuzi wa mitambo hiyo bila vigezo vitakavyojitosheleza mbele za wananchi kunaweza kupelekea mitizamo kwamba there is some sort of ufisadi....Honestly hata kama ni uamuzi wake wa kisiasa..Kuwapa hao watu mipesa yote hiyo na wakti kuna maswali yanaoyotakiwa kujibiwa ni swala linalohitaji maelezo ya kina.
Naona umezungumzia sana kuhusu "kutofautiana naye kimaelezo" Kumbuka ni tofauti za maamuzi na utekelezaji na si tu "maelezo" Malezo aliyoyatoa bado hayawezi kuhalalisha ununuzi wa mitambo hiyo na hivyo basi atueleze nia yake haswa ilikuwa ni nini na si tu kusema haogopi kuitwa fisadi ama kuonekana ana mtizamo wa tofauti.
Na pia unaposema mmetofautiana kisiasa una maana gani? Yani Zitto a lobby kumsadia Rostam na Lowassa na Karamagi halafu useme ni utofauti wa kisiasa tu, well kama wewe ni CHADEMA kama Zitto then utofauti wenu wa kisiasa unahitaji maelezo zaidi.
Ukishindwa kuwaelesha wana JF utaweza vipi kuwaelewesha wananchi kama si kuwadanganya na wizi mtupu?
 
yanayotokea nchi hii yanasikitisha sana. Hivi kweli nchii tumeshidwa kuwa na mipango ya muda mrefu ya kupata umeme wa kutosha. Upungufu wa umeme unaotokana na kukosekana kwa mvua umekuwa ukitokea karibu kila baada ya miaka miwili. Tumeshidwa namna ya kuliondoa taifa katika tatizo hili?. Ebu tujifunze wenzetu wamewezaje pata umeme wa kudumu. Kama kukopa tufanye hivyo tuondokane na tatizo hilo. Inawezekana suala la kutafuta umeme wa dharula imekuwa miradi ya wanasiasa na chama tawala!!!. Naomba JF members tuendelea Kupiga kelele sana juu ya ufisadi uliokidhiri ndani ya serikali hii. Ama sivyo nchi hii hakuna future.
 
Back
Top Bottom