Dark City
JF-Expert Member
- Oct 18, 2008
- 16,252
- 11,648
Napenda uelewe kuwa, mitambo yote mikubwa ni bora zaidi iliyokwisha tumika kwa muda mfupi na kurekebishwa faults zote zilizojitokeza kuliko kuinunuwa brand new, ambayo hakuna company yoyote duniani itayoweza kukupa guarantee kuwa ni ''plug and play''. commissioning ya mitambo kama hii inachukuwa at least mwaka mmoja. Jee unafahamu hilo?
Nafahamu ila inategemea na mtazamo pamoja na mambo mengine.
Sheria inasemaje?
Na hiyo iliyokwishatumika ilitoka wapi? Ilishuka toka mbinguni au nayo ilinunuliwa brand new then ikarekebishwa hadi ikawa kwenye hali hii tunayoiona?
Mwenye mali ni nani? Mwizi au mtu muungwana ambaye nikipata tatizo na mali aliyoniuzia tutaonge tuelewane jinsi ya kufanya?
Je ni bora kununua kwa machinga kuliko kwa mwenye mali (dukani) hata kama utapoteza muda na gharama kidogo?
Je mke alieyezaa ni bora kuliko binti kwa sababu huna hakika kama atazaa?
Je makuwadi wako wanakusaidia kumpata huyo ni akina na nani na wana sifa zipi kuhusiana na dili yenyewe? Ni watu wa kuwaamini na wana aminika?
Samahani mkuu, mimi siko tayari kununua kanyaboya kwa ajili ya kukwepa gharama!