Wakuu naomba kuklarify hili suala.... Kuna alot of confusion kutokana na either misunderstandings or personal opinions.
...kukitokea mafuriko, au uharibifu mkubwa wa ghafla wa mitambo iliyokuwa ikitumika....In less than three months you can get them from any corner in the world.
...Tulinunnua portable power plant from Caterpillar (KQ2000) ambazo ni containerized zinalingana lingana kama zile ze dowans (Fuel inaweza kuwa natural gas, diesel au HFO). Capacity yake ilikuwa ni 1.6MW per container ss tulinunua tano and therefore totaling 8MW. Bei ilikuwa ni USD 252,000.00per container kwa hiyo kwa tano = USD 1,260,000.00.
Sasa basi kutokana na mfano huo hapo juu. That means mara kumi yake kwa bei na capacity ni 80MW for 12,600,000.00. Na kwa 100MW = USD 15,750,000.00. Ukichukulia bei ya controls na transformers say USD 5,000,000.00 which is a very high estimate unapata total ya USD 20,750,000.00. Assume kodi ni 100% which is also very high estimate unapata ni USD41,500,000.00. Hii ni kwa mitambo mipya kabisaaaaaaa.... enzi zile tulikuwa tunasema unachana karatasi.... Kwa nini Tanesco isitafute mitambo mipya kama ni ya aina hiyo
...Hivi kwenye hiyo sheria ya manunuzi ya umma hakuna kipengele cha dharura. Kwa nini Tanesco isitumie hicho?
...Ni kwa Nini Dr. Idris atutishe watanzania woote...Jeuri hii anaitoa wapi Dr. Idris? wakati kukosekana kwa umeme ni kuonyesha kwamba ameshindwa kazi?
Wakuu suala la mitambo ya Dowans limejadiliwa mna na ktk threads mbali mbali humu jamvini. Personally nimeona ni vema tukawa na thread maalum kama mada isemavyo hapo juu. Hii ni kutokana kwamba Tanesco, Zito na kamat yake, na wale wote wanaotaka kutuaminisha kwamba ununuzi huo ni jambo la busara wanaegemea hapo.
1. Eti kuna mkaguzi kutoka ujerumani amekagua mitambo hiyo na kuiona ni ok na mingine ni mipya ikiwa imetembea for only 400 hrs.
2. Eti mitambo hii itaweza kutembea kwa miaka 13 bila kufanyiwa overhaul.
Ningependa kuanza na huyu the so called mkaguzi:
1. Anatoka kampuni gani?
2. Ana qualifications gani?
3. Ana uzoefu gani na kazi kama hii na amewahi kutumika wapi na kampuni zipi?
4. Ana bima yeyote inayotulinda iwapo ikigundulika alituingiza mkenge?
5. Anatambuliwa na Pratt and Whitney kama mkaguzi wa mitambo yao i.e is he a certified inspector?
6. Mtaalamu huyu aliletwa na Dowans au Tanesco na ni lini alianza kuwa contacted?
7. Kama ni Tanesco nini kilipelekea Tanesco kumuita mtaalamu huyu? Ina maana walikuwa na nia ya kununua mitambo hiyo kabla hata ya kuangalia taratibu zingine?
8. Alifanya kazi hiyo ya ukaguzi kwa muda gani?
9. Alitumia method gani kufanya uhakiki?
10. Tanesco ilimpataje mkaguzi huyu? Wangapi waliapply?
11. Je Tanesco ipo tayari kutoa ripoti ya mkaguzi huo?
12. Wakati wa ukaguzi Tanesco iliwakilishwa na nani? Na Dowans pia na nani?
13. Je mtaalamu huyo amewahi kuifanyia kazi yeyote Tanesco au Dowans before?
Well I know some of you might think we are now going in circles on this SAGA.
Lakini vijiswali hivi ni rahisi na vinaweza kujibiwa na Idris au mtaalam yeyote wa Tanesco aliyehusika na mchakato huu in just 10 mins tena bila hata kusoma mahali for any smart kiongozi. Cha msingi hapa na nia ya maswali haya ni kujiridhisha na kamchakatohaka kanakoonekana kujustfy ununuzi wa mitambo hii.
Pia kuna hili la mitambokuwa mipya na eti mingine imetembea masaa 400 tu. Ikumbukwe kuwa mitambo in this new tecnlogical era hauijaji kwa time based bali condition based. That applies kwenye hili la kwamba mitambo hii haitakuwa overhualed in 13 yrs. Nikiwa kama muhandisi hii sentensi naona imekaa kisiasa zaidi kwani overhauling pia ni condition based and not time based. How do you sell me an equipment and tell me it won't be overhauled in so many yrs? Nchofahamu hapa huyu jamaa atakuwa alikuwa nazungumzia PM (Preventive maintenance) ambayo inaweza kuwa say kuna za daily, monthly, yearly na labda hiyo ya say after every 5 or 10 or even 20 yrs fungua hiki au kile angalia pale na hapa. Hii ni staili ya zamani ya maintenance. You don't have to just overhaul a machine et kwa sababu imetembea masaa 100, 000. (Anyways anayehitaji ziada ya hii I am ready to debate ). Ninachoshangazwa hapa ni how huyu mkaguzi ali come up na hiyo miaka 13 -tena kwa mtambo iliyotumika?
Haya yote yanakuja just because historia ya kampuni hii formely known as Richmond ina utata. Tanesco pia ni watata, serikali ni watata. Hivyo basi kuna kila haja Tanesco itoe press release ya kuelezea mtaalam huyu namaswali hapo juu. Si mnakumbuka hata Richmond waliatuambia wamekubaliana na Pratt and Whitney kushirikiana kuzaisha zile 100 MW? of which they any written doc to support that. Sasa hili la mtaalamu mjerumani tunaaminije kirahisi rahisi? Tunamuaminije kirahisi rahisi Dr. Idris wakati ana questionable credibility? Tunaiaminije Tanesco kirahisi rahisi wakati imekuwa ikitudisapoint thousands of times?
Infact hata power rationing ikifanyika vizuri na kwa mipango sahihi, tunaweza kudunda vilevile bila karaha mpaka pale tutakapokuja na suluhisho la kudumu na si kila siku kuweka plasta mpya!
Politicized mathematics!
Nyambala, unasema mitambo yenu ilikuwa "inalingana lingana na ile ya dowans." Mitambo yenu ilikuwa ni ya 1.6MW kila mmoja. Ilibidi muunge unge mitambo mitano ili kupata 8MW. Dowans wanaweza kuzalisha 100MW. Kupata 100MW kama Dowans inabidi ku string along vimitambo vyenu 63 (100MW divide by 1.6MW = 62.5). Uwezo wa Dowans ni sawa na vimitambo venyu 63!! Sasa hiyo "inalingana lingana"?
Politicized mathematics!
Nyambala, unasema mitambo yenu ilikuwa "inalingana lingana na ile ya dowans." Mitambo yenu ilikuwa ni ya 1.6MW kila mmoja. Ilibidi muunge unge mitambo mitano ili kupata 8MW. Dowans wanaweza kuzalisha 100MW. Kupata 100MW kama Dowans inabidi ku string along vimitambo vyenu 63 (100MW divide by 1.6MW = 62.5). Uwezo wa Dowans ni sawa na vimitambo venyu 63!! Sasa hiyo "inalingana lingana"?
Kuhani,
Mkuu swala sio kuunga unga isipokuwa ni uwezo wa kupatikana kiwango cha umeme kinachotakiwa... Mara nyingi ktk maswala ya mitambo kama hii inategemea na maamuzi ya wahusika.. unaweza kuwa na mtambo mmoja lakini ukiharibika ndio kila kitu kinasimamma pia unaweza kuwa na vipande kikiharibika kimoja vingine bado vinafanya kazi... zipo faida hasara kwa kila design ya mmitambo kama hii..Na zaidi ya hapo kila mtambo unaweza kuwa na kiwango tofauti ya turbines.. inategemea na muundo. au sio!
Mkuu nitaendelea kuuliza ikiwa Dowans wanatoa MW100 na leo hii bado...
Kuhani,
Maelezo ya Nyambala yako sahihi kabisa. Kama mgodi wanaunganisha unganisha hizo 1.6 MW, kama nchi tunatakiwa tuunganishe unganishe 20-50MW. Hizi zisambazwe nchi nzima. Kwenye maji, upepo, makaa ya mawe, solar panel etc. Ili mradi hizi mashine kubwa za 50MW kwenda juu zisiwe za kutegemewa sana au ziwepo kwa tahadhali kuwa ikikwama basi kuna nyingine 5 za 50MW zinafanya au zinasubiri kufanya kazi. Ikibidi hata muda kwa muda zinapumzishwa na kufanyiwa ukaguzi.
Hii inafaida kubwa kuwa ukiharibika moja ya mtambo mdogo nchini, nchi haiteteleki. Ila sasa mkiwa na mtambo kama huu wanasema ujengwe Rufiji, na unaanza kutoa 300MW, loo ni poa sana. Ila siku ukisimama basi nusu ya nchi ni mgao.
Nafikiri swala sio Rais wetu yuko upande upi,
Tazama aliwahi kuulizwa na mwandishi mmoja kule Paris juu ya umasikini wa afrika, akajibu namnukuu " hata mimi sijui kwanini mpaka leo sisi ni masikini" Hili ni jibu la mpumbavu haswa akiwa kiongozi wa nchi Aliye ingia madarakani na kukuta Gari mpya za aina ya benz mpya kwa ajili ya msafara wake zimenunuliwa punde tu kwa mapesa mengi lakini baada ya miaka mitatu ananunua gari nyingine aina ya BMW kwa mapesa mengi tu, bila hata ya kutueleza wananchi zile nyingine zina matatizo gani????? kwenye nchi maskini kama hii, inashangaza, tazama kama ukinunua gari mpya inaweza kutumika hata miaka ishirini kama inatunzwa vizuri, Haya kuna mradi wa vitambulisho vya Taifa utakaogharimu bilioni 200, hiki ni kichekesho kwenye nchi ambayo watu hufa kwa malaria na mama wajawazito kwa kujifungua, na albino na vikongwe kwa baadhi ya watu kukosa elimu kwa sababu tu eti hakuna pesa za kutosha kuweka zahanati na shule ili watu waondokane na ujinga, inashangaza priorities zetu ni zipi????? hivyo vitambulisho ni muhimu kuliko elimu na uhai wetu?????????, Tazama ziara yake ya bandarini ndio iliyo nitia kishefushefu kabisaaaaa, aliwauliza kuhusu idadi ya container ( makasha ) yaliyopo na yaliyokwishatolewa akajibiwa bado wanafanyia kazi eti kwa sababu bado wanatumia manual hawana computer, jibu lili tolewa na waziri mwenye dhamana yeye akacheka tu, huu ni upuuzi kwanini hatimui waziri na watendaji wa bandari kama bandari inanunua vogue ya mamilioni kila baada ya miaka miwili kwa ajilia ya mkurugenzi mkuu kutembelea hivi hawaoni kwamba wakiacha kununua mwaka mmoja tu hiyo pesa inatosha kuweka mtandao wa computer ili kazi ifanyike kwa ufanisi faida ikue mara dufu hapo wataweza kununua hata gari kama analotembelea obama?????, yapo mengi siwezi kuandika yote yanatia hasira sana,
Dowans wanauwezo wa kuzalisha hiyo 100MW kwa namna gani?