Dowans: Another Richmond in making?

Dowans: Another Richmond in making?

Kikwete alipomchagua Zitto ktk kamati hizi, viongozi wengi wa Chadema walipinga uchaguzi huo na kumkanya Zitto asijiunge, lakini yeye alichukua msimamo wake ambao wengine tulimuunga mkono.. !

Kaka Kikwete hahusiki katika kuchagua wenyeviti wa kamati za bunge. Zitto amechaguliwa na wabunge wenziwe na kutokana na kuwa taratibu mpya za bunge zinasema kuwa nafasi ya uenyekiti katikaKAMATI YA KUDUMU YA MAHESABU YA MASHIRIKA YA UMMA kama ilivyo katika kamati zingine mbili za mahesabu ni LAZIMA iwe kwa vyama tofauti na chama tawala basi Zitto pamoja na mgombea mmoja wa CUF ndio walisimama na Zitto akafanikiwa kuchaguliwa kama mwenyekiti. Huu ni mtindo unaofuatwa na mabunge mengi ya jumuiya ya madola, natumai hata huko Canada ndivyo ilivyo.

Otherwise kaka tupo pamoja...hongera kwa msimamo wako ambao ulikuwa very consructive..

omarilyas
 
I want to state here in explicit terms that, I, Kabwe Zuberi Zitto (MP), Chairman Public Investments Committee of Parliament of Tanzania, stand with TANESCO on their desire to acquire gas fired turbines to improve electricity generation to the country. I stand firm to my decision and ready to be held accountable to that. I do this in good faith. I am genuine and honest. People can say all what they want to say, so long as this decision is mine based on the information i have, technical information. So long as i reached to this decision without any influence whatsover, i stand by it.

mdogo wangu muhashimiwa zitto..you have our support....!!

usikate tamaaa,watu wameshazoea kufanya siasa kwenye kila jambo....mara ooh ...kanunuliwa ,mara operation sangara..mara mbona tuliambiwa tule majani na hatukufa...!!

kauli za wasomi wenye phd hizo...opph bora giza....

ugomvi wao wa ndani kwa ndani wa kikwete na genge lake na sitta na genge lake ...utatukosesha umeme .....!!

pole sana ..usikate tamaaaaaaa...safari ni ndefu titafika!!!

wala usiyumbishwe na wanaotukana wataendelea ..na wengi walikuwa wanatafuta nafasi wakutukane ..hata kama hawajui kwa nini wanatukana ....!
 
Ameshaota mapembe huyo.......

wanaJF hatuna mchezo tutampotezee muda si mwingi......

Hizo kauli namkumbuka Edward Lowassa akijiuzulu kwa hasira bungeni.....

Bua ha ha..

Ukiona mtu anaanza kuwa apologetic & defensive na kuanza ad hominem ujue kuna ka-kitu hapo. Ukichokonoa zaidi kidogo tu wataanza kutajana.(Just a joke)
 
I want to state here in explicit terms that, I, Kabwe Zuberi Zitto (MP), Chairman Public Investments Committee of Parliament of Tanzania, stand with TANESCO on their desire to acquire gas fired turbines to improve electricity generation to the country. I stand firm to my decision and ready to be held accountable to that. I do this in good faith. I am genuine and honest. People can say all what they want to say, so long as this decision is mine based on the information i have, technical information. So long as i reached to this decision without any influence whatsover, i stand by it.

Nimetukanwa sana humu. Nimesimangwa sana humu na kuzushiwa kila aina ya tuhuma. Ninajijua kuwa sina bei. Siwezi kununuliwa na yeyote. Ninajijua na nimekuzwa kusimamia yale ninayoamini hata nikibaki peke yangu. Siyumbi. Siyumbishwi. Niliokuwa nao Chuo Kikuu wanajua nilivyo.

Nimefuatilia sana mjadala huu na kuona umejaa hisia kali sana. Ninajua ni hisia za watu wanaopenda nchi yao. Ninajua ni hisia za kizalendo. Sina mashaka na hili hata kidogo. Hata hivyo uongozi hauendeshwi kwa hisia tu. Uongozi wa nchi ni zaidi ya hisia na maneno matupu (hot air).
Nimesema hapo awali kuwa kwa kuwa Watanzania wamezoea kuwa na viongozi wala rushwa na waongo, itawachukua muda kukubali viongozi honest. Hata hivyo, muda huo utafika tu.

Hata hivyo, ni vema sana tujifunze kuheshimu maamuzi ya watu wengine. Kwamba leo mtu akiamua usivyotaka kanunuliwa? Je hayo maamuzi mengine hayawezi pia ya kununuliwa? Hapana, nadhani pale ambapo mwingine ana maamuzi tofauti ni vema kuheshimu maamuzi hayo bila kumwita kila aina ya majina mabaya.

Mimi binafsi, ninaamini kabisa kuwa hoja za TANESCO kuhusiana na suala la equipments hizi ni hoja zenye mshiko. Hoja za Kamati ya Nishati na Madini ni hisia za kisiasa.

Sio kweli kuwa TANESCO hawakuja katika kamati na alternatives. Walikuja na alternatives kadhaa na zote tulizijadili.

  1. Walieleza kushindwa kwa Kiwira kuzalisha 50MW mwezi huu na pia 150MW mwezi wa Septemba.
    1. Walieleza mradi wa Kinyerezi wa 240MW kushindwa kuanza kupitia PPP kufuatia wawekezaji kukosekana
      1. Walieleza mradi wa umeme wa upepo Singida kukwama
        1. Walieleza kuhusu mradi wa 300MW wa Mtwara.

          Katika hili mnawalaumu TANESCO bure tu. walitoa altrnative ya Dowans. walisema mbadala ni kununua mtambo mpya lakini walitahadharisha muda kwani mitambo mipya haipo tayari imetengenezwa na kuwekwa katika show room. Huwa inakuwa ordered kwa mtengenezaji na kuundiwa, kisha kufungwa na baadae kuwa commissioned ndio uanze kazi.

          Mwanakijiji alizungumzia umeme wa Zambia. Tunanunua umeme wa Zambia na ndio unatumika Sumbawanga. Umeme huu ni mdogo sana na ubora wake pia ni mdogo. Kimsingi nchi zote za SADC zina tatizo kubwa sana la Umeme isipokuwa (potentialities) Msumbiji, Tanzania na Congo DR.

          Mwanakijiji alizungumzia Stigler's gorge. Huu ni mkakati wa muda mrefu. It takes time kujenga hydro plant. Kule Kigoma wanajenga Malagarasi mini hydro, itachukua miaka 2 (8MW).

          Ni rahisi sana kuzungumza masuala haya lakini realities are different. Ninashauri baada ya mjadala huu wa TANESCO na DOWANS kuwa umekwisha (TANESCO wameumaliza) tuanze mjadala sober kuhusu 'energy sector' in Tanzania. Tuwe proactive na sio reactioneries.

          Power masterplan ipo. Haitekelezeki. Energy policy ipo. Tujadiliane baada ya kadhia hii ili tuone nchi yetu iendaje katika sekta ya Nishati.
    2. 2

Zitto bribed or not (and i personally think you are clean) you have shown extremely poor judgement in this case. It cannot be a surprise to you that you have lost a lot of respect and will continue to do so by supporting this completely ridiculous idea.

Buying used, overpriced equipment from a company that is linked to one of the worst corruption cases in Tanzanian history is just not going to fly. There are so many things that do not add up here, so many red flags (which i'm not going to list because i'm pretty sure you are aware of them) that it boggles the mind that anyone would even consider this.
 
Kama kikampuni tu cha kitapeli DOWANS ambacho hakina shughuli ya umeme popote dunia hii kiliweza kuinstall new generator kama mashabiki wake wanavyosema in less than 6 months baada ya kuinherit mkataba wa Richmond, leo hii TANESCO WITH A FULL GUARANTEE OF THE TANZANIA GOVT, inasema ooh itachukua almost miaka 2 kuinstall new generators???


No wonder Rostam anawacontrol haya maboga yanayoact kama viongozi wetu.
 
mdogo wangu muhashimiwa zitto..you have our support....!!

usikate tamaaa,watu wameshazoea kufanya siasa kwenye kila jambo....mara ooh ...kanunuliwa ,mara operation sangara..mara mbona tuliambiwa tule majani na hatukufa...!!

kauli za wasomi wenye phd hizo...opph bora giza....

ugomvi wao wa ndani kwa ndani wa kikwete na genge lake na sitta na genge lake ...utatukosesha umeme .....!!

pole sana ..usikate tamaaaaaaa...safari ni ndefu titafika!!!

wala usiyumbishwe na wanaotukana wataendelea ..na wengi walikuwa wanatafuta nafasi wakutukane ..hata kama hawajui kwa nini wanatukana ....![/SIZE]
Kwea hiyo unasapoti ununuzi wa mtambo chaklavu toka kwa kampuni ya mfukoni na kifisadi...umeshasahau Richmond?
 
Zitto, mimi ninakusikia vizuri sana na ninashare sentiments zako. Lakini tukumbuke:

HALI HALISI
a. Tatizo la Nishati siyo geni.

Wewe kama mimi na Watanzania wengine wengi tunajua kuwa tanzania ina tatizo la nishati ya umeme. Tunajua pia kuwa tatizo la nishati ya umeme ya Tanzania siyo kutokana na kukosekana kwa 'vyanzo' vya umeme. Tunavyo vyanzo vya kutosha kabisa. Tunajua kabisa kuwa umeme wa kutumia maji unategemea majira na hali ya hewa. Hili tunalifahamu. Tunafahamu pia kuwa uchumi wetu unakua na matumizi ya umeme yameongezeka. Haya yote tunayafahamu.

Serikali ya CCM inafahamu juu ya hali hii kwa miaka 45!

b. Kwamba licha ya kujua ukweli wa hali halisi ya umeme nchini tumeishia kufanya vitu hivi: (1) kujenga vibwawa hapa na pale (natumia neno vibaya kumaanisha vimiradi vidogovidogo vya umeme wa maji) na (2) kukodisha au kuingiza hawa IPPs ili tuweze kuongeza umeme nchini. Haya ndiyo masuluhisho pekee ambayo tunayo na tunayoyatekeleza.

c. Umeme wa Jua na wa Upepo
Licha ya (b) tunatumia umeme wa upepo na umeme wa jua sehemu mbalimbali (nilikosooma sekondari tulikuwa tunatumia umeme wa jua). Kwa nchi iliyoko kwenye eneo la Ikweta jua siyo tatizo. Kuna maeneo yana upepo sana wa kutosha kuweka majenereta ya umeme wa upepo. Kati ya hivyo viwili (jua na upepo) Upepo ndiyo wenye gharama ya chini kidogo, ni rahisi kukusanya uwezo wake. Hadi hivi sasa hatujathubutu kufanya mradi mkubwa wa umeme wa upepo ukizingatia kuwa (a) hapo juu ni kweli.

d. Vyanzo vinazalisha chini ya kiwango chao.
Pia inafahamika kuwa vyanzo mbalimbali hasa vya maji vinazalisha chini ya uwezo wake. Mara nyingi tunaambiwa vinazalisha chini ya uwezo wake kwa sababu ya maji kupungua lakini hata maji yakiwa yamejaa bado vinazalisha chini ya uwezo wake. Sababu tuliambiwa na Karamagi kuwa ni kwa sababu mitambo mingi imechakaa na kuikarabati yote kuirudisha katika kiwango chake cha juu kutaligharimu taifa dola bilioni 1.3

Katika hotuba yake ya bajeti ya 2007/2008 alisema hivi: Hata hivyo, tatizo la kukatika umeme mara kwa mara kwenye gridi ya Taifa limeendelea kutokana na
uchakavu wa miundombinu ya usafirishaji na usambazaji wa umeme. Gharama za kukarabati mfumo mzima wa umeme kwa kipindi cha miaka mitano ijayo zinakadiriwa kuwa Dola za Marekani bilioni 1.3."

Hiyo namba ni muhimu nitaonesha hapa chini. Kwa maneno mengine ni kuwa kuanzia 2007 hadi 2012 tukiamua kukarabati mitambo yote hiyo tutatumia kiasi hicho cha fedha. Lakini tukikamilisha tutakuwa tumerudisha uwezo wa mabwawa yote kuzalisha to their maximum capacity ambayo ni 560MW na yale ya mafuta n.k vyote vitafikia karibu MW900 hivi.

Sasa hayo yote hapo juu ni mambo ambayo yanafahamika; yanafahamika na Tanesco, yanafahamika serikalini, yanafahamika na wataalamu n.k Hakuna geni hata moja. Hayo niliyoyasema Mheshimiwa ni mambo ambayo tunayajua, hayana hisia, ni halisia.

Matatizo ya sasa:
Mheshimiwa matatizo ya sasa pia siyo mageni. Kuanzia mwaka 2006 tumeandika kuhusu suala la nishati na ninyi wawakilishi wetu mmelijadiri hili Bungeni kwa kina wakati mwingine kwa jazba na pia kwa utamu wote wa kushawishi akili. Miaka mitatu sasa tunajua kuwa tuna mapungufu ya nishati ya umeme.

a. Richmond
Tatizo la mgogoro wa Richmond lilikuwa ni hilo hilo. Kwamba licha ya nchi kuingizwa kwenye mkataba huu kwa sababu ya "dharura" majenereta hayakufanya kazi na hawakuingia kwa muda kwa karibu mwaka mzima. Na walipoingia (chini ya Dowans) na kuanza kuzalisha tatizo la nishati ya umeme iliyolazimisha mkataba huo halikuwepo tena.

Hii ina maana dharura iliyokuwapo 2006 na kusababisha blackouts na usumbufu mkubwa haikulipigisha magoti taifa! Hatukuona mamilioni ya watu wetu wakifa mahospitalini, au wanafunzi kushindwa kabisa kusoma; na hatukuona mamia ya viwanda yakifungwa kwa kushindwa kuzalisha. Tulihimili na tukasalimika. Gharama yake kwenye uchumi ikiwa bado ni kubwa mno.

b.Richmond/Dowans
WAliporithisha mkataba wao kinyemela kwa Dowans kampuni ambayo ni ya kitapeli (and I can say with authority ni kampuni ya kitapeli kama ilivyo Richmond) wabunge wetu mling'aka na kukataa. Mlipinga kwa nguvu zote na matokeo yake Waziri Mkuu akajiuzulu na baraza la mawaziri kuvunjika. Tukaamini kuwa Serikali imejifunza, na Tanesco imejifunza kitu.

Sasa mazingira ya kupewa richmond mkataba ndiyo yale yale ambayo yanakuja tena leo.

-. Richmond iliiingia kwa sababu kuna dharura; Dowans imeingia kwa sababu kuna dharura
-. Richmond haikujulikana wamiliki wake; Dowans haijulikani wamiliki wake
-. Richmond ilipigiwa debe na viongozi serikalini; Dowans inapigiwa debe na viongozi serikalini
-. Richmond ilitangazwa ndiyo mkombozi; Dowans inatangazwa kuwa ni mkombozi
- Richmond ikaingia mkataba mbovu kabisa; Dowans ilirithi mkataba mbovu vile vile na kuingia mkataba mbovu na Tanesco


Tofauti iliyopo katika sakata hili na lile la Richmond ni kile ambacho umekirudia hapa na Kasheshe naye amekirudia nacho ni kuwa wakati kwenye Richmond Tanesco walionekana kupinga, katika hili la Dowans Tanesco wako tayari kulikumbatia. Hii ndiyo tofauti pekee. Kwamba kwa vile Tanesco sasa hivi wanakubali na kutaka kununua basi tukubali nia yao nzuri bila kuihojia au kuangalia motivations nyuma yake.

1. Tanesco kutafuta suluhishi la tatizo la nishati.
Tutakuwa hatuwatendei haki Tanesco na serikali kama hatutatambua uzito wa hali iliyopo mbele yetu. Tutakuwa hatukiri ukweli uliopo. Hata hivyo binafsi naamini kinacholetwa mbele yetu ni suluhisho la kukwepa kushughulikia tatizo halisi la umeme nchini. NI suluhisho la kufunika kidonda kwa kitambaa bila kuweka dawa ya kuzuia vijidudu zaidi. Ni suluhisho jepesi la tatizo gumu.

Sikubaliani na wazo la wabunge kwenda kutafuta majenereta ya umeme kwani kwa kufanya hivyo wanavuka mpaka wa watunga sheria na wasimamizi wa serikali na kuwa watendaji. Hili nalo ni "no no".

2. Kuzungumza na Watengenezaji
Makampuni mbalimbali ya majenereta ikiwemo GE yana in stock majenereta ambayo yako tayari kupelekwa sehemu yoyote duniani. GE hali yake kiuchumi siyo nzuri sana kwa siku za hivi karibuni na kutokana na kumomonyoka kwa uchumi duniani. Endapo serikali yetu ikizungumza na GE moja kwa moja kutokana na dharura n.k nina uhakika GE watafurahi sana kuhakikisha tunapata majenereta mapya kabisa wakijua kuwa within hours watakuwa na dola karibu milioni 30! Basically we will give them some kind of a bailout while they are bailing out our energy sector!

WAbunge wetu tunaomba muishawishi serikali na watendaji kuzungumza moja kwa moja na watengenezaji na kuona nini kinaweza kufanyika sasa hivi kuondoa tatizo linalokuja. Kama Watanzania waliweza kusubiri kwa mwaka mzima suala la Dowans nina uhakika watawala wakiwaambia wananchi wasubiri miezi mitatu au sita kwa majenereta mapya kabisa kwa bei nzuri na kutoka kwa watengenezaji wenyewe wananchi wataelewa. Tatizo hakuna aliyejaribu njia hiyo wamebakia leo kulitisha taifa na kama kutuchukua mateka wanatuambia viwanda vyetu vitafungwa, na mahospitali kusitisha huduma. That is unacceptable!

Hivyo tatizo la nishati ya sasa hivi linaweza kabisa kutatuliwa bila kusababisha athari kama ile ya Richmond. Nakuomba usimamie pendekezo hilo kwani hili la Dowans ni No no. Ihamasisheni serikali na Wizara au tanesco kuzungumza na GE au makampuni mengine.

3. Wanachoogopa kuprocure moja kwa moja toka Marekani ni nini?
Kwa mara kadhaa sasa tumeona watawala wanakwepa kuzungumza na Wamarekani moja kwa moja na matokeo yake wanazunguka kwa madalali. Walilifanya hili pia kwenye suala la Rada na hata ndege ya Rais. Matokeo yake ni kuzunguka sheria za Marekani.

Wamarekani wanasheria inayokataza makampuni ya Marekani kujihusisha vitendo vya kifisadi kwenye nchi za kigeni. Sheria hiyo ya Forein Corrupt Practices ni tishio kwa wanasiasa na watendaji wetu. Leo hii tunavyozungumza kuna jamaa wa Nigeria amefikishwa mahakamani kwa kuwa dalali wa kifisadi alipojaribu kujihusisha na ufisadi kwa niaba ya kampuni za Kimarekani. Sheria hiyo ni mwiba mkubwa na ni tishio. Ndiyo maana ni rahisi kwa watawala wetu kwenda UAE na Costa Rica kutuletea Dowans.

Hata ile Richmond wengine tulipendekeza karibu miaka miwili iliyopita kwa serikali yetu kuiomba serikali ya Marekani kuishughulikia Richmond Printing ya Houston under that ACT kwani ingefumua mengi. Of course hawakusikiliza.

Kama tunataka uwazi na ukweli twendeni tuzungumze na watengenezaji moja kwa moja.

Baadhi ya taarifa tayari zimepitishwa kwa watendaji kadhaa huko nyumbani juu ya hili na kuwahakikishia kuwa watu kama wa GE wako tayari kuzungumza nao.

4. Kiza kijacho kitatokana na uzembe na siyo sababu tumepinga Dowans.
Mheshimiwa Zitto kama kutatokea kiza nchini si kwa sababu hatukununua majenereta ya umeme toka Dowans. Itakuwa ni makosa makubwa kusema kuwa ati nchi kuwa giza ni kwa sababu hatukuwasikiliza Tanesco, Kamati yako au Waziri. Hapana.

Nchi ikiingia gizani ni kwa sababu viongozi wetu wameshindwa. Kwa sababu wamejaribu kutafuta suluhisho la kiraka.

5. Mradi wa Stiglers
Mwaka jana Rais Kikwete mwenyewe akizungumza kwenye hafla ya kuzawadia tuzo ya Rais kwa Wazalishaji wa mwaka inayoandaliwa na CTI alisema wazi kuwa mradi huo ndiyo utaondoa tatizo la upungufu wa nishati nchini. Mradi huo una uwezo wa kuzalisha hadi MW2100.

Nimesema hapo nyuma juu ya gharama ya kukarabati vyanzo vya sasa kuwa ni dola bilioni 1.3 za Kimarekani. Hayo ni kwa mujibu wa Karamagi. Mradi wa Stiglers jinsi unavyokadiriwa sasa utagharimu dola bilioni 2! Yaani, ni lazima tuchague aidha kutumia dola bilioni 1.3 kupata MW1000 hivi au kutumia bilioni 2 kupata MW2100!

Kwenye taifa lenye viongozi wenye kuthubutu uchaguzi hapo wala si mgumu. Kwanini basi hakuna mkazo wa mradi mkubwa kama huu? Yawezekana kuna siasa na matatizo yake, lakini huu ni mradi pekee ambao tunaweza kuutekeleza hata kwa fedha zetu wenyewe! Kwanini hatujauchangamkia? Sijui kama Chadema mna sera ya kuendelea mradi huo mkipata madaraka, CCM wao wana sera ya nishati lakini hawajathubutu kuuweka mradi huu kwenye vipaumbele!

Kwanini?

Sababu ni kuwa kujengwa kwa Stiglers kutaondoa kabisa masuala ya vimiradi hivi vidogo vidogo vya ulaji! Vitaondoa kina Richmond na Dowans, na miradi mingine yenye sura ya kifisadi. It is not in the interest of a small group of people kuwa na Stiglers Dam! Kwanini wahangaikie mradi ambao utakuwa ni mwisho wa kula kwao?

Tatizo basi hapa ni kuwa hatuna viongozi wenye kuthubutu kufanya "maamuzi magumu" kama alivyosema Dr. Idris. Tuna viongozi (baadhi yao anyway) ambao kufanya mradi mkubwa itaonekana ni "hatuna fedha" lakini vimiradi hivi vya kuchezea akili fedha ipo! Tuna tayari dola milioni 260 (vitambulisho na hizi za Dowans), tuna milioni 40 za Dowans, tuna zile zilizoenda Deep Green, Mwananchi, Meremeta na Tangold..!! Hatuna viongozi wenye kuthubutu kukomalia hayo yote tupate fedha za kukomboa sekta yetu ya nishati!

Sasa, nakubaliana na wewe kuwa ipo haya ya kuziba pengo la nishati. Tatizo ni kuwa Dowans isiwe sehemu ya suluhisho hilo. Inasikitisha kuwa Tanesco katika kugonganisha vichwa vyao wameshindwa kupata suluhisho jingine isipokuwa Dowans! Kwamba Watanzania na wataalamu wote walioko Tanzania wote wameshindwa kufikiria njia nyingine mbadala isipokuwa Dowans.

Nakubaliana na kauli yako:

I want to state here in explicit terms that, I, Kabwe Zuberi Zitto (MP), Chairman Public Investments Committee of Parliament of Tanzania, stand with TANESCO on their desire to acquire gas fired turbines to improve electricity generation to the country.

Hii haina utata. Tatizo langu liko kwenye njia ya pekee na moja tu nayo ni Dowans! Sidhani kama kuna mtanzania mwenye akili timamu ambaye anapinga Tanesco kuongeza uwezo wa nishati. Hoja zao tumezisikia lakini wakati umefika wa hatua za makusudi kuchukuliwa.

a. Kuepusha tishio la kiza kwa sasa hivi, na suluhisho hilo liwe nje ya Dowans, watoto wake au shemeji zake.

b. Kuandaa mkakati na kuanza kuutekeleza ili ndani ya miaka kati ya 5-7 ijayo Tanzania isiwe kabisa na tatizo la nishati.

Nje ya hapo tutazungushana kwenye mambo haya kila mwaka hadi tuchoke.

Mwisho swali kwako:

Unachukuliaje kauli ya Dr. Rashid ambayo wananchi (mimi mmojawapo) tumeichukulia kuwa ni tishio kwa nchi, kwamba bila Dowans giza laja, viwanda kufungwa, mahospitali kukosa huduma na wanafunzi kutosoma?

NB: Don't mind my numbering system kwani hadi nimefika mwisho sijui where is "a"~!
 
Kaka Kikwete hahusiki katika kuchagua wenyeviti wa kamati za bunge. Zitto amechaguliwa na wabunge wenziwe na kutokana na kuwa taratibu mpya za bunge zinasema kuwa nafasi ya uenyekiti katikaKAMATI YA KUDUMU YA MAHESABU YA MASHIRIKA YA UMMA kama ilivyo katika kamati zingine mbili za mahesabu ni LAZIMA iwe kwa vyama tofauti na chama tawala basi Zitto pamoja na mgombea mmoja wa CUF ndio walisimama na Zitto akafanikiwa kuchaguliwa kama mwenyekiti. Huu ni mtindo unaofuatwa na mabunge mengi ya jumuiya ya madola, natumai hata huko Canada ndivyo ilivyo.

Otherwise kaka tupo pamoja...hongera kwa msimamo wako ambao ulikuwa very consructive..

omarilyas


Mkuu Mkandara ni mtu makini sana. Anazungumzia kamati ya madini ambayo rais alimweka Zitto, nitabet 100% ndio ivyo.

Wewe naona uko very busy kuspin mambo bahati mbaya magwiji humu ndani hutawaweza.
 
....sasa tunaomba mwakyembe na wenzake waje na action plan itakayowezesha kupata majenereta haraka ....kama unavyonunua jeans kwa fundi....kuna mtu amechambua hapa kununua eqp kunachukua mwaka mmoja na nusu..sio kama kununua gari dubai...au japan...

wenye akili wanajuwa ...ukiangalia action plan ya emirates air ya kununua ndege mpya utagundua kuwa ndege inayotegemea kuwa delivered mwaka 2012 .....ipo kiwandani inajengwa leo ...ndivo pia kwa vitu kama meli..,mitambo mikubwa ya viwanda nk.....sasa watu wakipewa facts wanasema ni siasa za sangara ....ndio wasomi wetu hawa....

nchi hii siasa nyingi ..ndo maana hatytaendelea!!
 
Unachosema ni kweli lakini kiongozi mkuu wa Shirika nyeti kama TANESCO anayenawa mikono yake kwamba asiulamiwe pindi nchi itakapoingia gizani kwa sababu Watanzania wamekataa mitambo ya Dowans isinunuliwe maoni yangu hatufai. Baada ya kujitoa katika ununuzi huo wa mitambo ya Dowans, Idrissa alitakiwa aje na solution nyingine ambayo itahakikisha nchi haingii gizani lakini yeye kaamua kukaa pembeni. Hasara kwa nchi kama tutaingia tena gizani ni kubwa mno na uamuzi wake wa kutofanya chochote ni sawa kabisa na uhujumu wa uchumi.

Wasi wasi wangu mkubwa ni kuwa Tayari nchi inahujumiwa - there is more to this than we are being told. Huyu bwana ni kawaida yake - historia yale imejaa vituko na kama si uswahiba wake na mkuu wa kaya angekuwa historia.

The cheek of this man - eti ana jeuri ya kusema, "Mmenikatalia kununua mitambo ya Dowans, sasa subirini muone kitakachofuata kama mtaweza hata kuonana humo gizani !" - na bado yuko kazini !!

Nakumbuka alivyotishia kujiuzulu mara ya kwanza:-
images

Hapa aonekana akimkandia mzee wa watu - matokeo tunayajua - alikumbatiwa. Je atendelea kukumbatiwa baada ya kututishia nyau ?? Huyu ni mtu hatari, period.
 
Siasa zinaipeleka nchi bapaya!!!!

Niko upande wa TANESCO 110% shabikieni siasa lakini nchi iko kwenye hati hati... siku yoyote kukiwa na mtambo wa MW hata 45 unatatizo tunaenda kwenye mgao...

It takes time kununua, kuagiza, kufunga na ku-komisheni mtambo... tutakuwa pamoja kwenye vibari au sio...

Heri yenu mlioko US... mtatucheka tu.

TANESCO wana facts,,, ninyi mnaongelea HISIA.

Kila mtu yuko upande wa TANESCO 100%, na ndio maana inazungumziwa hapa kwa kiasi kikubwa. Nia halisi ni kuiokoa TANESCO kutokana na maamuzi yasiyofaa/yanayoweza kuiingiza nchi kwenye matatizo wakati suluhisho likiwepo.

Suala la kuchukua muda mrefu kununua mitambo ya umeme liko kwenye uwezo wa nchi kuamua. Mamlaka zinazohusika zikitakiwa kufanya mambo yaende kwa haraka, muda mrefu unaozungumziwa unaweza kupungua na kukidhi matakwa ya wakati husika. Sheria ya manunuzi ya umma inaweza kuweka nafasi ya manunuzi kama hayo kufanyika ili mradi manunuzi hayo yafuate taratibu zinazohusika. Mara nyingi taratibu hucheleweshwa na vikao visivyokwisha (ili wahusika wapate posho nyingi kadiri inavyowezekana) badala ya kuangalia umuhimu wa kupata huduma haraka.

Imani yangu ni kuwa, TANESCO inaweza kuanza mchakato wa kupata supplier wa kuiuzia mitambo haraka iwezekanavyo kwa kuzingatia sheria za tender (bila kujali kama itanunuliwa ama lah), na ikishapita katika utaratibu huo na kuidhinishwa na vyombo vinavyohusika (bila bureaucracy), manunuzi yakafuata haraka.

Naamini pia kuwa order inapotolewa ya manunuzi, huwa haichukui muda mrefu sana (kwa manufacturer) kabla mitambo hiyo kuwa tayari kwa kusafirishwa. Kwa maana, manufacturer hao hiyo ndio kazi yao mahususi. Kusafirisha mitambo hiyo inaweza kuchukua muda usiozidi miezi 3. Mitambo mingi ya kisasa inafungwa kwa muda mfupi. Hivyo suala la muda mrefu linaweza lisiwe na maana sana. Litakuwa na maana endapo hakuna lolote linalofanyika kupata mitambo mipya kutoka kwa manufacturers sasa hivi.
 
Unachosema ni kweli lakini kiongozi mkuu wa Shirika nyeti kama TANESCO anayenawa mikono yake kwamba asiulamiwe pindi nchi itakapoingia gizani kwa sababu Watanzania wamekataa mitambo ya Dowans isinunuliwe maoni yangu hatufai. Baada ya kujitoa katika ununuzi huo wa mitambo ya Dowans, Idrissa alitakiwa aje na solution nyingine ambayo itahakikisha nchi haingii gizani lakini yeye kaamua kukaa pembeni. Hasara kwa nchi kama tutaingia tena gizani ni kubwa mno na uamuzi wake wa kutofanya chochote ni sawa kabisa na uhujumu wa uchumi.


well anaweza kuja na solution nyingine ..lakini process ya kuagiza hadi kufunga na kuanza ..itachukua mwaka mmoja na zaidi..je wakati huo tutakuwa tunafanya nini..kwenye plan za kiuchumi lazima kuwa na mikakati ya dharura,muda mfupi ,muda wa kati na muda mrefu[normally miaka 25 mbele]...upo hapo???
 
....sasa tunaomba mwakyembe na wenzake waje na action plan itakayowezesha kupata majenereta haraka ....kama unavyonunua jeans kwa fundi....kuna mtu amechambua hapa kununua eqp kunachukua mwaka mmoja na nusu..sio kama kununua gari dubai...au japan...

wenye akili wanajuwa ...ukiangalia action plan ya emirates air ya kununua ndege mpya utagundua kuwa ndege inayotegemea kuwa delivered mwaka 2012 .....ipo kiwandani inajengwa leo ...ndivo pia kwa vitu kama meli..,mitambo mikubwa ya viwanda nk.....sasa watu wakipewa facts wanasema ni siasa za sangara ....ndio wasomi wetu hawa....

nchi hii siasa nyingi ..ndo maana hatytaendelea!!

Walikuwa wanasubiria muda uishe ili wanunue mitambo ya DOWANS, si ndio. Muda wote huo walikuwa wapi? Msitake kujifanya wajuaji wakuu, hata sisi wanyonge tunajua mnachofanya mnapojificha kwenye vikao vyenu vya kubomoa nchi, eti kamati, ebo! Hata mtoto mdogo haingii kwenye bongo yake.

Na nani amesema kutakuwa na kiza, kiza nikionacho mimi kipo jikoni kinapikwa.
 
....sasa tunaomba mwakyembe na wenzake waje na action plan itakayowezesha kupata majenereta haraka ....kama unavyonunua jeans kwa fundi....kuna mtu amechambua hapa kununua eqp kunachukua mwaka mmoja na nusu..sio kama kununua gari dubai...au japan...

wenye akili wanajuwa ...ukiangalia action plan ya emirates air ya kununua ndege mpya utagundua kuwa ndege inayotegemea kuwa delivered mwaka 2012 .....ipo kiwandani inajengwa leo ...ndivo pia kwa vitu kama meli..,mitambo mikubwa ya viwanda nk.....sasa watu wakipewa facts wanasema ni siasa za sangara ....ndio wasomi wetu hawa....

nchi hii siasa nyingi ..ndo maana hatytaendelea!!

Yep, lakini baba lao Rostam through Dowans alifanya hayo yote chini ya miezi sita. Rostam Juu!! Rostam bwana kiboko!! Rostam bwana anatisha!!!
 

well anaweza kuja na solution nyingine ..lakini process ya kuagiza hadi kufunga na kuanza ..itachukua mwaka mmoja na zaidi..je wakati huo tutakuwa tunafanya nini..kwenye plan za kiuchumi lazima kuwa na mikakati ya dharura,muda mfupi ,muda wa kati na muda mrefu[normally miaka 25 mbele]...upo hapo???

Hii dharura imeanza leo, wiki jana, mwezi uliopita, mwaka au miaka mingapi iliyopita ? Je, mipango yote ya dharura ilitegemea mitambo ya Dowans tu ? Baada ya mkataba na Dowans kuvunjwa, hakujua kuwa tutahitaji umeme tena ama kashtukizwa na kukataliwa kwa mpango wake wa kununua mitambo chakavu ya Dowans ? Ana hisa gani ama uswahiba gani na Dowans mpaka ndiyo iwe kimbilio pekee la taifa kwenye dharura ?....upo hapo ????
 
Hili c kwamba wametumia busara, walishapindisha sheria,sasa kwa sababu siku hizi watanzania tunatetea kile tunachokiamini,wameona hamna jinsi. Mheshimiwa spika nampongeza saana kwa hili amekuwa msitari wa mbele kuelewesha mambo pale wale anaowaongoza kule bungeni wanapojisahau.

Waheshimiwa hapa kuna idea moja inaniijia kichwani kama mhandisi mdogo saana, mwaka juzi mvua zilinyesha saana hadi tukaambiwa maji yamejaa kwenye mabwawa yote ya kuzalisha umeme. Kwa fikra zangu,huo ulikuwa muda wetu muafaka wa kuvuna maji ya kutosha kwa ajili ya kufua umeme. Lakini tulifurahi saana na kushangilia kwani tulidhani sasa tatizo la umeme basi.Kumbe tunajidanganya, suala la umeme ktk nchi za wenzetu ndo lina first priority.

Hata mimi naamini kuwa hakuna nchi yoyote ile inaweza kuwa na maendeleo bila umeme.Kama viongozi wetu wana nia thabiti na nchi yetu,muda woote walioutumia kutuconvince na hii mitambo walau wangeutumia kuandika qutations za mitambo mipya. Kama ni sayansi na technologia-tutaenda nayo vipi bila umeme wa kutosha? Suala kuwa gizani ngeleja na Idrisa ilibidi walione mapema c baada ya kuwepo mitambo ya dowans na ndo maana wakapewa dhamana kuongoza kitengo hicho ambacho kimeshikilia uchumi wa nchi. Viongozi wasio jua wajibu wao ndo kama hawa wawili,natolea mfano lakini wapo wengi saana serikalini ambao hawana mtazamo wa kazi zao za baadae kama viongozi.

Tunahitaji viongozi wenye uchungu na nchi pamoja na wananchi kwa ujumla. Kwa hili nawapongeza viongozi waliosimama imara katika hili na kutetea kile wanachokiamini. Nitakuwa mwizi wa fadhila nisipo wapongeza wadau wa jamii forum kwa mada na kukemea maovu yaliyopo kwenye jamii yetu,hasa serikalini.[/SIZE]
 
Najisikia Vibaya na naogopa,ninapoona kila maamuzi mazito yanafanywa Kisiasa....Ninaogopa zaidi ninapoona hata kundi la wasomi na Wataalam linatekwa na maamuzi ya kisiasa..watu wanashindwa kupambana kwa Hoja..na tumebaki kila siku kumtafuta nani ni "Mchawi" na nani "si Mwenzetu"....Kwa mwendo huu hatuwezi kufika....Tuna miaka 40+ sasa toka tupate Uhuru lakini ni pungufu ya 30% ya watanzania ndio wenye uhakika wa huduma ya Umeme...Tatizo tunalijua siku zote...Kwa nini hatutafuti ufumbuzi wa kudumu? Kwa kweli nipo speechless, lakini naomba Mwenyezi Mungu atupe Nuru ili yule aliyetuloga,atuachilie nasi tupate ahueni ,.....Hakika Historia haitotuachia kizazi hichi!!!Tutakuja kupandishwa kizimbani kushitakiwa kwa Uzembe na kutokuwajibika...."Kila kitu siasa" hata Wataalam sasa wanazungumza siasa,na wote wanakimbilia majimboni ili waihubiri siasa kwa uwazi zaidi.Mungu ibariki Tanzania.
 
Dk. Rashid ametoa kauli ya KITISHO katika hitimisho lake kwa kusema, "Tanesco inatangaza rasmi kujitoa kwenye nia yake ya kununua mitambo hii. Ni imani yetu kwamba tumeishajieleza na kujenga hoja za kutosha, na wananchi wa Tanzania, watafanya maamuzi yao hapo ambapo nchi itakapokuwa imegubikwa na kiza, mahospitali hayatoi huduma, viwanda havizalishi, wanafunzi vyuoni wanashindwa kusoma kwa sababu tulishindwa kufanya maamuzi".

tuelewa
R

Kwa kauli hii ya Idrisa Rashid na wenzake, kama yakitokea haya wanayojitia kututabilia kwamba yatatokea na bila JK kuwawajibisha, JK itabidi atuandalie majibu ya maana yakutupatia 2010 tutakapomuuliza kwanini kura zetu tusimpe mtu mwingine mwenye uchungu na Nchi hii.
 
Naungana na wote wanaomshangaa Mh. Zitto kwa majibu yake! Kweli Mh anashangaza sana! Inaonyesha anajiona kuwa anajua ukweli wa TANESCO na DOWANS kuliko mtu yeyote hapa JF as if watu wote wa hapa JF anawafahamu kwa sura na majina yao halisi! Zitto amejisahau kuwa yeye ni mwanasiasa na amesahau kuwa anapingana na kura za maoni kwa sababu tu zinaonyesha approval rating yake imeplunge! (JF ni reflection ya opinion ya umma)!

Sitaki ajisafishe kwa kuwapaka matope watu wengine! Aache kuwasingizia watu wanaoonyesha uzalendo eti kwa kusema wana vita ya kisiasa! Mbona yeye muda wote alipotoa hoja za msingi bungeni tumekuwa tunamuunga mkono! Wana JF wengi hawakumchukulia Zitto kuwa anajitafutia umaarufu wa kisiasa. Tukikuunga mkono hatukutazami kama mwanasiasa tunakutazama kama mzalendo ndio maana hata wana CCM huwa wanakufagilia. Kwa hiyo leo Mwakyembe, Sitta nk nao hatuwatazami kama wana CCM tunawatazama kama wapambanaji katika vita dhidi ya ufisadi, vita ambayo wana JF ni wadau wakubwa sana.


Katika hili la DOWANS Zitto umejitenga kabisa hata usitafute visingizio - Hapa kilichobaki ni wewe kuchuchumaa tu. Ngoja tuendelee kukutafiki kama kweli ulighafirika au siku zote hizi ulivaa ngozi ya kondoo. Lakini umenasa tundu bovu kweli kweli. Ushauri wa Bure: Zitto usipigane na ukuta (JF). Kama ulighafirika jirudi na hili liwe fundisho. Kubali kujifunza na kwa rekodi yako watu bado watakuelewa! Kama umepewa kitu kidogo ndio basi tena, tupishe na wewe nenda uka mjoin Rev. Mtikila!
 
Zitto,
Unaweza kuwa haununuliki, nakubali, nalifahamu hilo, at least for now. Lakini tahadhari na mafisadi, usije kuwapigia ngoma yao. Facts zinaonyesha kuwa hili deal ni bomu, wamekuingizaje mkenge? Mambo ya kusema tunaingia gizani wameyajua leo jamani? Walikuwa wapi siku zote? I am very disappointed, kweli dont do this again. Ili ufanikiwe katika siasa ni pamoja na kutokuweka misimamo ya ajabuajabu, tumekushangaa!
 
Back
Top Bottom