Zitto
Former MP Kigoma Urban
- Mar 2, 2007
- 1,562
- 10,890
Yule mbunge wetu kijana anasemaje sasa!.Kwa kweli ameacha picha mbaya hasa kwenye kambi ya upinzani.
Itakuwa jambo jema kama ataacha siasa kwasababu kuna kila dalili amenaswa katika mtego wa mafisadi pengine kwa kujua au kwa kutokujua.inafaa aelezwe aache kudandia mambo bila kufanya utafiti wa kutosha.Sijui atawaambia nini watanzania waliokuwa wakimwamini kwa kiasi kikubwa kwamba ni mpiganaji mwenzao kumbe ni mganga njaa.
I want to state here in explicit terms that, I, Kabwe Zuberi Zitto (MP), Chairman Public Investments Committee of Parliament of Tanzania, stand with TANESCO on their desire to acquire gas fired turbines to improve electricity generation to the country. I stand firm to my decision and ready to be held accountable to that. I do this in good faith. I am genuine and honest. People can say all what they want to say, so long as this decision is mine based on the information i have, technical information. So long as i reached to this decision without any influence whatsover, i stand by it.
Nimetukanwa sana humu. Nimesimangwa sana humu na kuzushiwa kila aina ya tuhuma. Ninajijua kuwa sina bei. Siwezi kununuliwa na yeyote. Ninajijua na nimekuzwa kusimamia yale ninayoamini hata nikibaki peke yangu. Siyumbi. Siyumbishwi. Niliokuwa nao Chuo Kikuu wanajua nilivyo.
Nimefuatilia sana mjadala huu na kuona umejaa hisia kali sana. Ninajua ni hisia za watu wanaopenda nchi yao. Ninajua ni hisia za kizalendo. Sina mashaka na hili hata kidogo. Hata hivyo uongozi hauendeshwi kwa hisia tu. Uongozi wa nchi ni zaidi ya hisia na maneno matupu (hot air).
Nimesema hapo awali kuwa kwa kuwa Watanzania wamezoea kuwa na viongozi wala rushwa na waongo, itawachukua muda kukubali viongozi honest. Hata hivyo, muda huo utafika tu.
Hata hivyo, ni vema sana tujifunze kuheshimu maamuzi ya watu wengine. Kwamba leo mtu akiamua usivyotaka kanunuliwa? Je hayo maamuzi mengine hayawezi pia ya kununuliwa? Hapana, nadhani pale ambapo mwingine ana maamuzi tofauti ni vema kuheshimu maamuzi hayo bila kumwita kila aina ya majina mabaya.
Mimi binafsi, ninaamini kabisa kuwa hoja za TANESCO kuhusiana na suala la equipments hizi ni hoja zenye mshiko. Hoja za Kamati ya Nishati na Madini ni hisia za kisiasa.
Sio kweli kuwa TANESCO hawakuja katika kamati na alternatives. Walikuja na alternatives kadhaa na zote tulizijadili.
- Walieleza kushindwa kwa Kiwira kuzalisha 50MW mwezi huu na pia 150MW mwezi wa Septemba.
- Walieleza mradi wa Kinyerezi wa 240MW kushindwa kuanza kupitia PPP kufuatia wawekezaji kukosekana
- Walieleza mradi wa umeme wa upepo Singida kukwama
- Walieleza kuhusu mradi wa 300MW wa Mtwara.
Katika hili mnawalaumu TANESCO bure tu. walitoa altrnative ya Dowans. walisema mbadala ni kununua mtambo mpya lakini walitahadharisha muda kwani mitambo mipya haipo tayari imetengenezwa na kuwekwa katika show room. Huwa inakuwa ordered kwa mtengenezaji na kuundiwa, kisha kufungwa na baadae kuwa commissioned ndio uanze kazi.
Mwanakijiji alizungumzia umeme wa Zambia. Tunanunua umeme wa Zambia na ndio unatumika Sumbawanga. Umeme huu ni mdogo sana na ubora wake pia ni mdogo. Kimsingi nchi zote za SADC zina tatizo kubwa sana la Umeme isipokuwa (potentialities) Msumbiji, Tanzania na Congo DR.
Mwanakijiji alizungumzia Stigler's gorge. Huu ni mkakati wa muda mrefu. It takes time kujenga hydro plant. Kule Kigoma wanajenga Malagarasi mini hydro, itachukua miaka 2 (8MW).
Ni rahisi sana kuzungumza masuala haya lakini realities are different. Ninashauri baada ya mjadala huu wa TANESCO na DOWANS kuwa umekwisha (TANESCO wameumaliza) tuanze mjadala sober kuhusu 'energy sector' in Tanzania. Tuwe proactive na sio reactioneries.
Power masterplan ipo. Haitekelezeki. Energy policy ipo. Tujadiliane baada ya kadhia hii ili tuone nchi yetu iendaje katika sekta ya Nishati.
- Walieleza kuhusu mradi wa 300MW wa Mtwara.
- Walieleza mradi wa umeme wa upepo Singida kukwama
- 2
- Walieleza mradi wa Kinyerezi wa 240MW kushindwa kuanza kupitia PPP kufuatia wawekezaji kukosekana