Dowans: Another Richmond in making?

Dowans: Another Richmond in making?

Mzee Mwanakijiji na MtindiowaUbungo: nadhani mmezungumzia ishu moja ambayo mi naomba tulizungumzie kwa kirefu bila jazba: - tatizo la umeme halijaanza leo Tanzania. Mimi kinachonifanya nisikie hasira kabisa (najitahidi kutoa jazba) ni hii ya Idrisa kututishia eti tukikaa kizani tusimlaumu. No! Naomba ajiuzulu mara moja, kwani ameshindwa kazi.

Mheshimiwa Zitto, naamini kwamba umetetea dili hili kwa good faith na kwa uzalendo lakini naomba nikuulize, mlikuwa wapi muda wote huu ,mlipokuwa mna-debate kununua mitambo ya Dowans? Kwa nini mitambo mipya haikuagizwa mwaka moja uliopita wakati hili ishu liliibuka? Ina maana hata kamati pia haikuwa na foresight, na itabidi na nyie mkubali responsibility. Je kamati yako itakuwa tayari kuwajibika bila ya kusema eti tunawasukumizia lawama so and so. Kama mzalendo wa kweli, step up and take responsibility. Alternatives zote ulizotaja zinaonekana they were dressed to appear as failure, and you should have known better. Did the committee contact independent specialists to counter opinion by Tanesco? Je ni kweli kwamba ni miaka 2 kupata mitambo na haiwezi kupatikana kwa wepesi zaidi?
Mimi ni mtu ambaye nimeku-hold in very high esteem, but you have failed in this, kwa kukubali to be led by your nose by people with their own interest. Naomba usiwe kama wanasiasa tuliowazoea who take it personally, bali ulete mjadala utakaosogeza nchi mbele.
BTW naomba ni -point out that all the odds and alternatives zilikuwa against ushindi wa Obama but he said YES WE CAN. Where there is a will there is a way!
 
Naungana na wote wanaomshangaa Mh. Zitto kwa majibu yake! Kweli Mh anashangaza sana! Inaonyesha anajiona kuwa anajua ukweli wa TANESCO na DOWANS kuliko mtu yeyote hapa JF as if watu wote wa hapa JF anawafahamu kwa sura na majina yao halisi! Zitto amejisahau kuwa yeye ni mwanasiasa na amesahau kuwa anapingana na kura za maoni kwa sababu tu zinaonyesha approval rating yake imeplunge! (JF ni reflection ya opinion ya umma)!

Sitaki ajisafishe kwa kuwapaka matope watu wengine! Aache kuwasingizia watu wanaoonyesha uzalendo eti kwa kusema wana vita ya kisiasa! Mbona yeye muda wote alipotoa hoja za msingi bungeni tumekuwa tunamuunga mkono! Wana JF wengi hawakumchukulia Zitto kuwa anajitafutia umaarufu wa kisiasa. Tukikuunga mkono hatukutazami kama mwanasiasa tunakutazama kama mzalendo ndio maana hata wana CCM huwa wanakufagilia. Kwa hiyo leo Mwakyembe, Sitta nk nao hatuwatazami kama wana CCM tunawatazama kama wapambanaji katika vita dhidi ya ufisadi, vita ambayo wana JF ni wadau wakubwa sana.

Katika hili la DOWANS Zitto umejitenga kabisa hata usitafute visingizio - Hapa kilichobaki ni wewe kuchuchumaa tu. Ngoja tuendelee kukutafiki kama kweli ulighafirika au siku zote hizi ulivaa ngozi ya kondoo. Lakini umenasa tundu bovu kweli kweli. Ushauri wa Bure: Zitto usipigane na ukuta (JF). Kama ulighafirika jirudi na hili liwe fundisho. Kubali kujifunza na kwa rekodi yako watu bado watakuelewa! Kama umepewa kitu kidogo ndio basi tena, tupishe na wewe nenda uka mjoin Rev. Mtikila!

Ndugu kama utamuelewa ni wewe, au hujamsoma vizuri nini?, Maandishi yake yote yamejaa damu ya UFISADI humu ndani. Kwa kujifanya kujua sasa, yaani yeye ndio mwisho wa mambo yote. Kiburi kimemjaa ni hakuna. Au kalogwa? Yaani badala ya kuja kuomba msamaha humu ndani, anakuja na vitisho kama FISADI mwenzie RASHID. Maisha ya KEKO yanakutafuta ZITO huna ujanja wa kuwepa JELA kama RA. Maana jaribio lako la kwanza watu tumepiga bao. Huna chako tena.
 
I want to state here in explicit terms that, I, Kabwe Zuberi Zitto (MP), Chairman Public Investments Committee of Parliament of Tanzania, stand with TANESCO on their desire to acquire gas fired turbines to improve electricity generation to the country. I stand firm to my decision and ready to be held accountable to that. I do this in good faith. I am genuine and honest. People can say all what they want to say, so long as this decision is mine based on the information i have, technical information. So long as i reached to this decision without any influence whatsover, i stand by it.

Nimetukanwa sana humu. Nimesimangwa sana humu na kuzushiwa kila aina ya tuhuma. Ninajijua kuwa sina bei. Siwezi kununuliwa na yeyote. Ninajijua na nimekuzwa kusimamia yale ninayoamini hata nikibaki peke yangu. Siyumbi. Siyumbishwi. Niliokuwa nao Chuo Kikuu wanajua nilivyo.

Nimefuatilia sana mjadala huu na kuona umejaa hisia kali sana. Ninajua ni hisia za watu wanaopenda nchi yao. Ninajua ni hisia za kizalendo. Sina mashaka na hili hata kidogo. Hata hivyo uongozi hauendeshwi kwa hisia tu. Uongozi wa nchi ni zaidi ya hisia na maneno matupu (hot air).
Nimesema hapo awali kuwa kwa kuwa Watanzania wamezoea kuwa na viongozi wala rushwa na waongo, itawachukua muda kukubali viongozi honest. Hata hivyo, muda huo utafika tu.

Hata hivyo, ni vema sana tujifunze kuheshimu maamuzi ya watu wengine. Kwamba leo mtu akiamua usivyotaka kanunuliwa? Je hayo maamuzi mengine hayawezi pia ya kununuliwa? Hapana, nadhani pale ambapo mwingine ana maamuzi tofauti ni vema kuheshimu maamuzi hayo bila kumwita kila aina ya majina mabaya.

Mimi binafsi, ninaamini kabisa kuwa hoja za TANESCO kuhusiana na suala la equipments hizi ni hoja zenye mshiko. Hoja za Kamati ya Nishati na Madini ni hisia za kisiasa.

Sio kweli kuwa TANESCO hawakuja katika kamati na alternatives. Walikuja na alternatives kadhaa na zote tulizijadili.

Mh. Zitto, maneno mazito kweli hapo juu. Pole kwa majukumu magumu.
Msimamo wako katika hili sakata zima unanikumbusha yafuatayo yaliyomkumba mwenzetu Powell, "the once upon time, only pentagon dove!" :

steved-albums-international-picture366-powell-un.jpg

Alipokuwa akionesha msimamamo wake dhidi ya Sadam na WMD.

steved-albums-international-picture362-colin-powell-united-nations-chemical-wmd-lie-anthrax-vial.jpg

Alisisitiza na kusisitiza.

steved-albums-international-picture363-collin-powel-wmd.jpg

Kwa vielelezo mbalimbali...

steved-albums-international-picture371-iraq-030205-powell-un-17300pf-20.jpg

Na zaidi na zaidi....

steved-albums-international-picture364-iraq-030205-powell-un-17300pf-14.jpg

Na zaidi....

steved-albums-international-picture369-iraq-030205-powell-un-17300pf-21.jpg

Kwa maelezo mbalimbali...

...My second purpose today is to provide you with additional information, to share with you what the United States knows about Iraq's weapons of mass destruction, as well as Iraq's involvement in terrorism, which is also the subject of Resolution 1441 and other earlier resolutions...
Zaidi na zaidi...
.....The material I will present to you comes from a variety of sources. Some are U.S. sources and some are those of other countries. Some are the sources are technical, such as intercepted telephone conversations and
photos taken by satellites. Other sources are people who have risked their lives to let the world know what Saddam Hussein is really up to.

......I cannot tell you everything that we know, but what I can share with you, when combined with what all of us have learned over the years, is deeply troubling.

With all the effort to present the evidence, sadly, much of it turned out to be a load of hoaxes!

Mh. Zitto, once the waters in this ever turbulent pond have settled, I really hope that you come out of the ordeal with your integrity intact.

Kazi njema kaka!

SteveD.
 
....kwa hiyo point ya ZITTO anaunga mkono ununuzi wa mitambo michafu iliyotumika ya kampuni tapeli kwa sababu anafikiri kununua mtambo mipya na ya hali ya juu yenye warrant na good price ni process ndefu sana na itachukua muda mrefu,wewe Zitto hatutaki njia za mikato na unaonekana huna idea kabisa na nani alikuambia kununua mitambo ya Gas inachukua muda mrefu,sio meli au ndege hiyo ni mitambo tuu ya gas ambayo mingi iko ready made for delivery,seems nyie na politics zenu ambazo mnaongea bila data ndio mnapoteza muda...nyanyua simu mwenyewe upige simu kampuni yeyote kama GE na nyingine nyingi tuu za maana all over the internet nina uhakika wengi wao wakipokea $$$ ni next day delivery,nyanyua simu nakushauri au andika email sio kusikiliza porojo utafikiri mnataka kununua meli mpya!
 
I want to state here in explicit terms that, I, Kabwe Zuberi Zitto (MP), Chairman Public Investments Committee of Parliament of Tanzania, stand with TANESCO on their desire to acquire gas fired turbines to improve electricity generation to the country. I stand firm to my decision and ready to be held accountable to that. I do this in good faith. I am genuine and honest. People can say all what they want to say, so long as this decision is mine based on the information i have, technical information. So long as i reached to this decision without any influence whatsover, i stand by it.

Mheshimiwa Zitto, wengi wetu tumesikitishwa na nia ya TANESCO kukusudia kununua mitambo yenye utata kwa matumizi ya kuzalisha umeme, kutoka kwenye kampuni isiyotengeneza mitambo hiyo. Tunaamini kuwa nchi yetu inastahili kupata best deal kutoka kwenye kampuni zinazotengeneza mitambo kama hiyo kwa manufaa ya nchi yetu. Hasa kama tuna mahitaji ya kweli.

Tunaamini kuwa kununua mitambo hiyo kutoka kwenye Kampuni ambayo imedhihirika kuwa na matatizo kimkataba, yenye kesi na serikali, na isiyofahamika vizuri na yenye nia ya kuuza mitambo isiyo mipya ni hatari kwa Taifa na uvunjaji wa sheria za manunuzi ya mashirika ya umma.

Mheshimiwa, kauli yako inayofahamika hapa JF ni kuwa, wewe na Kamati yako mmekuwa mkitaka mitambo ya DOWANS inunuliwe na TANESCO baada ya kuridhishwa na nia yao kufanya hivyo. Kama ingefahamika kuwa, msimamo wako ni kununua mitambo mipya ya umeme kutoka kwenye kampuni zinazotengeneza mitambo hiyo (kwa kufuata sheria), nadhani mjadala huu ungekuwa umeshakwisha siku nyingi.

Nimetukanwa sana humu. Nimesimangwa sana humu na kuzushiwa kila aina ya tuhuma. Ninajijua kuwa sina bei. Siwezi kununuliwa na yeyote. Ninajijua na nimekuzwa kusimamia yale ninayoamini hata nikibaki peke yangu. Siyumbi. Siyumbishwi. Niliokuwa nao Chuo Kikuu wanajua nilivyo.

Mheshimiwa, sisi wote tunafahamu (japo kwa muda mfupi) jitihada zako katika mambo mbalimbali yenye maslahi ya Taifa. Tumekuwa tukisikia kwa matumaini makubwa misimamo yako thabiti kwenye mambo unayoyaamini. Na ndio maana hili lilipotokea na wewe kulisimamia katika upande ambao hatukutegemea, ilitushangaza wote, na zaidi ilitusikitisha sana.

Naamini kuwa, hakuna lolote linalohusiana na rushwa katika sakata hili. Ila naamini pia kuwa uamuzi uliouchukua ulikuwa wa hatari sana kwako na kwa kamati yako kisiasa, kwasababu haukuwa rahisi kueleweka kwa wananchi.

Nimefuatilia sana mjadala huu na kuona umejaa hisia kali sana. Ninajua ni hisia za watu wanaopenda nchi yao. Ninajua ni hisia za kizalendo. Sina mashaka na hili hata kidogo. Hata hivyo uongozi hauendeshwi kwa hisia tu. Uongozi wa nchi ni zaidi ya hisia na maneno matupu (hot air).
Nimesema hapo awali kuwa kwa kuwa Watanzania wamezoea kuwa na viongozi wala rushwa na waongo, itawachukua muda kukubali viongozi honest. Hata hivyo, muda huo utafika tu.

Hata hivyo, ni vema sana tujifunze kuheshimu maamuzi ya watu wengine. Kwamba leo mtu akiamua usivyotaka kanunuliwa? Je hayo maamuzi mengine hayawezi pia ya kununuliwa? Hapana, nadhani pale ambapo mwingine ana maamuzi tofauti ni vema kuheshimu maamuzi hayo bila kumwita kila aina ya majina mabaya.

Mheshimiwa, naamini kuwa kutukana ni kosa la jinai. Naamini kama kuna mtu alietumia kauli mbaya dhidi yako, amekosea sana. Nakuunga mkono kabisa katika hilo, na nakusihi usijali kauli hizo kwasababu hazijengi.

Mkuu, kutofautiana kimawazo ni jambo la kawaida. Kuheshimu mawazo ya mtu mwingine pia ni wajibu wa kila mtu mwenye ustaarabu.

Ninachoona kina matatizo, ni kuheshimu mawazo ya kiongozi mwenye mamlaka ya kulinda na kutetea maslahi ya nchi yake ambae ameamua kutumia uwezo wake huo kutoa kauli zinazoweza kuleta madhara kwa Taifa. Hili hata Katiba ya nchi hailikubali. Suala linalojadiliwa kuhusu TANESCO na manunuzi ya mitambo ya DOWANS, ni suala la maslahi ya Taifa na ni suala la kila mwenye nia njema na nchi hii. Kuacha kauli potofu kuendelea na hatimaye kutekelezwa ni kosa. Ndio maana wengi walilipinga na wamefanya hivyo kwa nguvu nyingi.

Nchi hii italindwa na wananchi wenyewe.

Mimi binafsi, ninaamini kabisa kuwa hoja za TANESCO kuhusiana na suala la equipments hizi ni hoja zenye mshiko. Hoja za Kamati ya Nishati na Madini ni hisia za kisiasa.

Mkuu, sidhani kama kuna hoja yenye mshiko katika kuvunja sheria. Kila kitu kinaweza kuonekana kadiri mtazamaji anavyotaka kukitazama. Katika suala la mitambo hii, sidhani kama kuna lolote zaidi ya utata na uvunjaji wa sheria za nchi.

Mkuu, sijaona popote katika maelezo yoyote panapoonyesha kuwa kuna tathmini au jitihada zozote ziliyofanyika kuangalia uwezekano wa kupata mitambo bora kutoka kwa manufacturer wa mitambo hiyo (sio suppliers) zaidi ya kuelezwa tu kuwa kuiagiza mipya inachukua muda mrefu na bei kubwa. Inabidi wahusika wafanye kazi zaidi kutafuta mitambo bora zaidi, yenye uhakika wa technical support nzuri, itakayodumu zaidi na ambayo ni mipya.

Mkuu nakutakia kila la kheri katika ujenzi wa Taifa. Naomba uelewe nia njema ya wachangiaji wote katika mada hii kwa maslahi ya Taifa. Hakuna hata mmoja mwenye nia ya kukudhalilisha wewe wala Kamati yako tukufu. Tunachoomba ni uadilifu, uwajibikaji na utetezi bora zaidi wa maslahi ya Taifa.
 
I want to state here in explicit terms that, I, Kabwe Zuberi Zitto (MP), Chairman Public Investments Committee of Parliament of Tanzania, stand with TANESCO on their desire to acquire gas fired turbines to improve electricity generation to the country. I stand firm to my decision and ready to be held accountable to that. I do this in good faith. I am genuine and honest. People can say all what they want to say, so long as this decision is mine based on the information i have, technical information. So long as i reached to this decision without any influence whatsover, i stand by it.

Nimetukanwa sana humu. Nimesimangwa sana humu na kuzushiwa kila aina ya tuhuma. Ninajijua kuwa sina bei. Siwezi kununuliwa na yeyote. Ninajijua na nimekuzwa kusimamia yale ninayoamini hata nikibaki peke yangu. Siyumbi. Siyumbishwi. Niliokuwa nao Chuo Kikuu wanajua nilivyo.

[/LIST]

...na utatukanwa sana maana unafanya mambo kama fisadi tuu na bila kutumia akili,haiingii akilini kutetea ununuzi wa mitambo mibovu from corrupt company...na inawezekana huna bei lakini hili la mitambo huna akili kabisa!
 
SteveD your analogy is very correct. Sasa Powell anajuta na analalama lakini hii inabaki doa katika career yake nzuri sana!
Mi nadhani mheshimiwa Zitto angechukua time off akasome vizuri maoni yetu na pia atafakari akijua kuna watu katika kamati hii wenye maslahi including huyo Idrisa anayetutishia!
 
The trust is breached, the bridge is burnt its now time to cry a river. Kweli nimekubali kumshabikia mwanasiasa is suicidal.

Mi nadhani mzizi wa fitnah mwingine ni hawa ma-executive wa TANESCO. Mi nadhani ni vyema wakapewa kwaheri ya kuonana, maana naona hawana jipya kwa kweli, wao na wanasiasa uchwara ngoma droo, hamna wa kumshauri mwenzake.
 
Kampuni ya Tanesco imejitoa rasmi katika mchakato wa kununua mitambo ya Dowans kwa kudai kuwa suala hili limeingiza malumbano makali ya wanasiasa. Katika kujitoa kwake kampuni hiyo imesema kuwa siku nchi ikiingia kizani wasilaumiwe wao kwa sababu watu walishindwa kufanya maamuzi magumu.

Habari ndiyo hiyo, nyamanyama na mafuta mengine baadaye!

Statement yake Idrisa inaonyesha kichwani ubongo wake haufanyi kazi.Anaposema anaingiliwa na wanasiasa ana maana gani kwani yeye sio mwanasiasa? Kwani hiyo nafasi ya ukurugenzi aliipataje? Je alipita kwenye mchujo vizuri au siasa zilitumika kumuweka hiyo nafasi ya ukurugenzi mkuu? Wanasiasa wakiingilia mchakato wa kumweka katika nafasi hapo halalamiki!!!

kuna vitu nimeviona kwenye huu mgogoro.
Part I Kwa ufupi kuna kitu kinaitwa Arusha Connection.Arusha kuna mtu anaitwa Lowasa ambaye ni ARCHITECT wa richmond na Dowans,Tanesco Akawekwa muarusha mwingine Mwenye kesi ya ufisadi na Chenge ambaye ni Idrisa Rashid kisiasa akalie pale kusimamia maslahi ya muarusha Lowasa,Upande wa Serikali kuna waziri mwingine anayeshughulikia mambo ya serikali bungeni toka Arusha ANAITWA MARMO huyu ndiye kamkemea Spika Sitta na kufoka Kuwa anaingilia mchakato wa mitambo ya Dowans akome kwani si kazi ya bunge.Ukiangalia unapata Crime arena kuwa iko connected na Arusha.

Part II kuna kitu kinaitwa VODACOM CONNECTION ni kuwa Idirisa Rashid ana connection na Rostam Aziz kwa kuwa wote wana hisa kwenye Vodacom kupitia kampuni zao ambako Idrisa alishashika wadhifa mkubwa . Na Idrisa na Rostam Azizi wana connection na Ngeleja waziri wa madini sababu Ngereja alikuwa mwanasheria wa Kampuni ya Vodacom na ndio maana kununua majenereta alikuwa mkali yanunuliwa ili alinde hiyo connection.

Kinachotakiwa tunaomba watu wa usalama wa taifa wafanye vetting ya watu kabla hawajapewa vyeo.Mnatuangusha hadi wahuni mafisadi wanashika nyadhifa na kuyumbisha nchi .Kikwete hayuko stable sana naona kama bado yuko kipindi cha probation period ya uraisi msaidieni jamani.Hili genge la wahalifu ni vizuri likatimuliwa lote kabla halija sabotage nchi kupitia eneo la umeme na kulipiza visasi vya mitambo yao kutonunuliwa kwa kuwakomesha wananchi.Usalama wa Taifa au jeshi shinikizeni Ngereja,Idrisa na Marmo waondolewe.Nchi haiwezi kuendeshwa kijinga namna hiyo.

Kuhusu tishio lake la kuwa nchi itaingia gizani ni kuwa hakujua kuwa nchi itaingia gizani mbele muda wa mitambo ya Dowans ukiisha akaweka mipango mbadala endelevu? Hakuwekwa pale afanye daily routine kama msoma mita wa Tanesco amewekwa pale awe think Tank na planner.Sasa kama hawezi kuhakikisha mwanga wa umeme unakuwako inabidi aondoke aende zake.Hakuwekwa kuleta giza bali mwanga.Sasa kama kutakuwa na giza Tanesco anafanya nini inabidi aondoke.Nilitarajia katika tamko lake angesema kwa kuwa Sitaweza kuleta umeme kwa kipindi kijacho naondoka maana sitakuwa na kazi ninayotakiwa kufanya kama mkurugenzi wa Tanesco.

Anasema asilaumiwe atalaumiwa tu mambo yasipoenda vizuri Tanesco.Hatutalala.Kama kuendesha shirika hakuwezi ajiendee tu salama.Bodi ya wakurugenzi ya Tanesco kuweni wakali kwa menejimenti ya Tanesco wasiwatishe kwa lolote na ichukulieni hatua mkiona hai-deliver watimueni waende wakaanzishe viduka vya kuuza socket za umeme kama akili zao zimefikia upeo wa kuendesha shirika.
 
One step. Good.

Id / Bill , je mnaweza kuongelea lolote kuhusu uwezekano kuitaifisha hiyo mitambo ya Dowans?
 
Muzee Netanyahu,

Ulivyozipanga hoja zako, zinaleta habari kamili. Inasikitisha lakini ndo ukweli.
 
Kwa miaka kadhaa sasa TANESCO imekuwa ikipata recycled managers. Kweli ni mameneja lakini sio mameneja wa sekta ya nishati na hususan umeme. Ninapenda kuiuliza serikali hivi hatuwezi kupata meneja awe Mtanzania, Mzungu au Mchina au toka popote pale mwenye ujuzi wa uzalishaji na uuzaji umeme kuja kufanya kazi hii.

Hawa mameneja wa TANESCO hadi wa leo ni mameneja wa visingizio na matatizo mtupu. Na sasa upo uwezekano wa wizi mtupu. Hivi kweli Watanzania kwa wingi wetu na akili zetu na rasilimali zetu tukiamua tunashindwa kuifanya nchi hii mchana katika miaka miwili mitatu ijayo hasa kwa kuzingatia kuna mitambo ya umeme sehemu mbalimbali ambayo sasa haina kazi na watengenezaji vifaa hivyo wanaachisha watu wao kazi kwa sababu vifaa hivyo havina masoko?

Ninadhani sisi Watanzania hatuna nia ya kweli ya kuiondoa nchi yetu masikini. Malengo yetu ni mafupi kama pua zetu zilivyo. Tunajifikiria sisi wenyewe. Tukishapata mianya ya kujitoa kwenye umasikini, sisi, wenetu na ndugu na jamaa zetu wa karibu basi inakuwa tumefikia hatima ya malengo yetu. HIi si aina ya viongozi wanaoweza kuwaondoa kwenye umasikini Watanzania hata kama ni miaka 60 au zaidi ijayo.

NInawauliza JF hivi hakuna vijana hapo jamani wanaoweza kupewa TANESCO na wakaiongoza vizuri na kwa faida na manufaa makubwa kwa nchi katika kipindi kifupi tu kuliko kuendelea na hawa vikongwe wa toka enzi za Uhuru?

Chukulia jambo dogo tu kama vile kuruhusu kampuni za simu au zilizofanana nao kuuza LUKU kupitia kwenye mtandao na kuondosha kuwaabebesha wananchi mzigo wa gharama usio wa lazima unaotokana na kuwa na maofisi ya LUKU mijini sio kwa ajili ya kwamba zinahitajika bali kwa sababu ya kuwapatia mabinti na mashemeji zetu kazi. Hatuhitaji ofisi za LUKU tunataka tupatiwe huduma hiyo kupitia mitandao mbalimbali ya simu kwa gharama nafuu zaidi kwetu sisi watumiaji wa umeme lakini TANESCO imeshupalia lazima ofisi za LUKU ziwepo ili waendelee na ulaji wa kifisadi mdogo mdogo.

Hivi hawa ndio watu wa kukubali ushauri wao kweli..eti tununue mitambo mibovu ya RICHMOND kulipa madeni ya wafadhili wa kina nanihino? Kwendeni huko. Kama TANESCO inashindwa kuona URAHISI wa kutoa huduma kwa kutumia mitandao ya simu inaweza kweli kutushauri nini la maana? Hawa si watumiwaji tu hawa? Halafu mnatutisha kukaa gizani. Tutakaa gizani kwa kuwa mmeshindwa kazi zenu na hapo mnawekwa na wakubwa tu kwa sababu wanazozijua wao. Nani mliona kafa kwa giza? Lakini watu wanakufa kwa nyie kuzodoa na kuzobodoa fedha za umma na kuendelea kulishwa kwa kijiko cha dhahabu na serikali kwa mantiki isiyo eleweka hata kidogo. Ingelikuwa mimi ninalivunjilia mbali shirika hili na kuipa kila kanda kampuni yake binafsi ya umeme hata kama ni kuwaita watu toka nje waje wafanye kazi hiyo eti!
 
Mwaka 2006, iligundulika kuna deficit ya 200MW. Richmond, Aggreko na mwingine wakapewa mikataba ya muda ya miaka miwili ili kufidia hiyo gap ya 200MW @ a very high cost to the people of Tanzania.

MD wa Tanesco yeye kakaa tu anapiga kelele badala ya kuagiza mitambo mipya toka 2006, halafu ghafla 2009 anataka kununua mitambo mibovu ya Dowans, mbona kawaacha Aggreko wenye hiyo biashara dunia nzima waondoe mitambo yao?? Mbona hakusema tununue hiyo mitambo ya Aggreko, ambao hata kama tunapindisha sheria ya PPRA kama Zitto anavyotaka, at least mitambo ikiharibika tungeweza pamoja na kuvunja sheria zetu kwenda Aggreko kuwaambia vipi, tupeni mingine.

Lakini magenius wetu wakiongozwa na Mh. Zitto wao wanangangania Dowans tu, wakati inajulikana ukishawalipa DOWANS baada ya kuvunja sheria za nchi PPRA, wanayeyuka na huko mbele mitambo ikiharibika dowans watakuwa ghost!!!!

Mtu hata ukienda walmart kununua tshirt ya $5, unapewa guarantee ya 30 days, lakini Dowans tuwalipe $80million with no guarantee hata ya siku moja (Since kampuni ni fake na haipo popote dunia hii)??
 
Last edited:
Netanyahu, umeweza kuonyesha na kuunganisha nukta (connecting the dots) na mi nadhani mh Zitto atafanya vizuri kusoma hoja kama hizi za kwako aelewe kwamba analeta ubishi na kupotoshwa...
 
Statement yake Idrisa inaonyesha kichwani ubongo wake haufanyi kazi.Anaposema anaingiliwa na wanasiasa ana maana gani kwani yeye sio mwanasiasa? Kwani hiyo nafasi ya ukurugenzi aliipataje? Je alipita kwenye mchujo vizuri au siasa zilitumika kumuweka hiyo nafasi ya ukurugenzi mkuu? Wanasiasa wakiingilia mchakato wa kumweka katika nafasi hapo halalamiki!!!

kuna vitu nimeviona kwenye huu mgogoro.
Part I Kwa ufupi kuna kitu kinaitwa Arusha Connection.Arusha kuna mtu anaitwa Lowasa ambaye ni ARCHITECT wa richmond na Dowans,Tanesco Akawekwa muarusha mwingine Mwenye kesi ya ufisadi na Chenge ambaye ni Idrisa Rashid kisiasa akalie pale kusimamia maslahi ya muarusha Lowasa,Upande wa Serikali kuna waziri mwingine anayeshughulikia mambo ya serikali bungeni toka Arusha ANAITWA MARMO huyu ndiye kamkemea Spika Sitta na kufoka Kuwa anaingilia mchakato wa mitambo ya Dowans akome kwani si kazi ya bunge.Ukiangalia unapata Crime arena kuwa iko connected na Arusha.

Part II kuna kitu kinaitwa VODACOM CONNECTION ni kuwa Idirisa Rashid ana connection na Rostam Aziz kwa kuwa wote wana hisa kwenye Vodacom kupitia kampuni zao ambako Idrisa alishashika wadhifa mkubwa . Na Idrisa na Rostam Azizi wana connection na Ngeleja waziri wa madini sababu Ngereja alikuwa mwanasheria wa Kampuni ya Vodacom na ndio maana kununua majenereta alikuwa mkali yanunuliwa ili alinde hiyo connection.

Kinachotakiwa tunaomba watu wa usalama wa taifa wafanye vetting ya watu kabla hawajapewa vyeo.Mnatuangusha hadi wahuni mafisadi wanashika nyadhifa na kuyumbisha nchi .Kikwete hayuko stable sana naona kama bado yuko kipindi cha probation period ya uraisi msaidieni jamani.Hili genge la wahalifu ni vizuri likatimuliwa lote kabla halija sabotage nchi kupitia eneo la umeme na kulipiza visasi vya mitambo yao kutonunuliwa kwa kuwakomesha wananchi.Usalama wa Taifa au jeshi shinikizeni Ngereja,Idrisa na Marmo waondolewe.Nchi haiwezi kuendeshwa kijinga namna hiyo.

Kuhusu tishio lake la kuwa nchi itaingia gizani ni kuwa hakujua kuwa nchi itaingia gizani mbele muda wa mitambo ya Dowans ukiisha akaweka mipango mbadala endelevu? Hakuwekwa pale afanye daily routine kama msoma mita wa Tanesco amewekwa pale awe think Tank na planner.Sasa kama hawezi kuhakikisha mwanga wa umeme unakuwako inabidi aondoke aende zake.Hakuwekwa kuleta giza bali mwanga.Sasa kama kutakuwa na giza Tanesco anafanya nini inabidi aondoke.Nilitarajia katika tamko lake angesema kwa kuwa Sitaweza kuleta umeme kwa kipindi kijacho naondoka maana sitakuwa na kazi ninayotakiwa kufanya kama mkurugenzi wa Tanesco.

Anasema asilaumiwe atalaumiwa tu mambo yasipoenda vizuri Tanesco.Hatutalala.Kama kuendesha shirika hakuwezi ajiendee tu salama.Bodi ya wakurugenzi ya Tanesco kuweni wakali kwa menejimenti ya Tanesco wasiwatishe kwa lolote na ichukulieni hatua mkiona hai-deliver watimueni waende wakaanzishe viduka vya kuuza socket za umeme kama akili zao zimefikia upeo wa kuendesha shirika.
Ninachoweza ku-comment ni kuwa... Wewe ni kichwa! Umeyanena yote mkuu. I salute
 
kwanza namkubali sana rais wetu, nashindwa kumuelewa mara kwa mara hasa anapokua na team ambayo ina watu kama mkurugenzi wa TANESCO,PCCB,n.k..anyway,TANESCO na mashirika mengine yanatumika kama miradi tu ya wakubwa,siku ipo..
 
I want to state here in explicit terms that, I, Kabwe Zuberi Zitto (MP), Chairman Public Investments Committee of Parliament of Tanzania, stand with TANESCO on their desire to acquire gas fired turbines to improve electricity generation to the country. I stand firm to my decision and ready to be held accountable to that. I do this in good faith. I am genuine and honest. People can say all what they want to say, so long as this decision is mine based on the information i have, technical information. So long as i reached to this decision without any influence whatsover, i stand by it.

Nimetukanwa sana humu. Nimesimangwa sana humu na kuzushiwa kila aina ya tuhuma. Ninajijua kuwa sina bei. Siwezi kununuliwa na yeyote. Ninajijua na nimekuzwa kusimamia yale ninayoamini hata nikibaki peke yangu. Siyumbi. Siyumbishwi. Niliokuwa nao Chuo Kikuu wanajua nilivyo.

Nimefuatilia sana mjadala huu na kuona umejaa hisia kali sana. Ninajua ni hisia za watu wanaopenda nchi yao. Ninajua ni hisia za kizalendo. Sina mashaka na hili hata kidogo. Hata hivyo uongozi hauendeshwi kwa hisia tu. Uongozi wa nchi ni zaidi ya hisia na maneno matupu (hot air).
Nimesema hapo awali kuwa kwa kuwa Watanzania wamezoea kuwa na viongozi wala rushwa na waongo, itawachukua muda kukubali viongozi honest. Hata hivyo, muda huo utafika tu.

Hata hivyo, ni vema sana tujifunze kuheshimu maamuzi ya watu wengine. Kwamba leo mtu akiamua usivyotaka kanunuliwa? Je hayo maamuzi mengine hayawezi pia ya kununuliwa? Hapana, nadhani pale ambapo mwingine ana maamuzi tofauti ni vema kuheshimu maamuzi hayo bila kumwita kila aina ya majina mabaya.

Mimi binafsi, ninaamini kabisa kuwa hoja za TANESCO kuhusiana na suala la equipments hizi ni hoja zenye mshiko. Hoja za Kamati ya Nishati na Madini ni hisia za kisiasa.

Sio kweli kuwa TANESCO hawakuja katika kamati na alternatives. Walikuja na alternatives kadhaa na zote tulizijadili.

  1. Walieleza kushindwa kwa Kiwira kuzalisha 50MW mwezi huu na pia 150MW mwezi wa Septemba.
    1. Walieleza mradi wa Kinyerezi wa 240MW kushindwa kuanza kupitia PPP kufuatia wawekezaji kukosekana
      1. Walieleza mradi wa umeme wa upepo Singida kukwama
        1. Walieleza kuhusu mradi wa 300MW wa Mtwara.

          Katika hili mnawalaumu TANESCO bure tu. walitoa altrnative ya Dowans. walisema mbadala ni kununua mtambo mpya lakini walitahadharisha muda kwani mitambo mipya haipo tayari imetengenezwa na kuwekwa katika show room. Huwa inakuwa ordered kwa mtengenezaji na kuundiwa, kisha kufungwa na baadae kuwa commissioned ndio uanze kazi.

          Mwanakijiji alizungumzia umeme wa Zambia. Tunanunua umeme wa Zambia na ndio unatumika Sumbawanga. Umeme huu ni mdogo sana na ubora wake pia ni mdogo. Kimsingi nchi zote za SADC zina tatizo kubwa sana la Umeme isipokuwa (potentialities) Msumbiji, Tanzania na Congo DR.

          Mwanakijiji alizungumzia Stigler's gorge. Huu ni mkakati wa muda mrefu. It takes time kujenga hydro plant. Kule Kigoma wanajenga Malagarasi mini hydro, itachukua miaka 2 (8MW).

          Ni rahisi sana kuzungumza masuala haya lakini realities are different. Ninashauri baada ya mjadala huu wa TANESCO na DOWANS kuwa umekwisha (TANESCO wameumaliza) tuanze mjadala sober kuhusu 'energy sector' in Tanzania. Tuwe proactive na sio reactioneries.

          Power masterplan ipo. Haitekelezeki. Energy policy ipo. Tujadiliane baada ya kadhia hii ili tuone nchi yetu iendaje katika sekta ya Nishati.
    2. 2

Mh Zitto,

Unayosema yaweza kuwa kweli kabisa, uchangiaji wa mawazo hapa JF ni muhimu kuuelewa.....kuna watu wana data kamili (nahisi wew ni mmoja wapo) na kuna watu wana data nusu na kuna watu wantegemea yanayoandikwa hapa JF ndio watoe mawazo yao.

Ndio maana mwanzoni kabisa Dr W. Slaa aliliona hili na kusema kuna "missing information"....inawezekana hilo ndio limetufikisha hapa tulipo kimjadala

Notwithstanding that, kuna fact kuwa RDC/DOWANS ni matapeli fulani waliofanikiwa kutulaghai mapaka tuliwapa LC ili kuweza ku-procure/ku-supply hiyo mitambo.

Umesema kuwa Mitambo kama hiyo haiko SHOW ROOM i.e mtu unakenda na kununua......fine....Je tulipokumbwa na dharula wakati ule.........RDC waliipata ile mitambo Show room? au na yenyewe iliundwa? je ilichukua muda gani........na Je vipi ukitufafanulia (timelines) dharula tuliyokuwa nayo wakati ule na tuliyo nayo sasa hivi.

Umesema tujadili Power Masterplan....nimejaribu kui-search sijafanikiwa kuipata......naomba utuwekee hapa watu tuizamie ili tuibuke kujua kama ni kwa kiwango gani inatekelezeka na kwa kiwango gani haitekelezeki kama ulivyosema.........maana kusema tu haitekelezeki....really it does not make any sense

tuendelee kujadili
 
Eti nchi itaingia gizani........watu wakitaka kula pesa yetu wana kuwa na lugha tamu.....

wanaJF napenda kuuliza hii mitambo ya kutuokoa na giza ina warranty??
 
Inawezekana jeuri ya Idris inatoka kwa JK? Tetesi zinasema kuwa siku ya Alhamisi hakuweza kuzungumza na waandishi wa habari kwa sababu alizuiwa na Ikulu, na akamriwa kuipeleka statement yake Ikulu iangaliwe kwanza. Ikapelekwa na kukutwa ilikuwa kali zaidi kuliko hii ya leo, maana ilirekebishwa na kurudishwa na hatimaye kusomwa leo (ijumaa).

Kama kweli hii, basi inatisha -- maana hatuna serikali!. Ikumbukwe kwamba mwaka jana Idris alijiuzulu kwa suala dogo sana kuliko hili (kuhusu kukatiwa umeme Tanga Cement) lakini akaombwa na swahiba wake afute kujiuzulu kwake. Alikuwa anatikisa kiberiti? Kwanini hili la Dowans, ambayo ni issue mkubwa mno -- maana anapingwa wazi wazi na karibu umma mzima kutonunua mitumba -- hataki kujiuzulu?
 
Last edited:
Eti nchi itaingia gizani........watu wakitaka kula pesa yetu wana kuwa na lugha tamu.....

wanaJF napena kuuliza hii mitambo ya kutuokoa na giza ina warranty??

Chinga huwa wanatoa warranty/guarantee ?
 
Back
Top Bottom