Dowans: Another Richmond in making?

Dowans: Another Richmond in making?

Siasa zinaipeleka nchi bapaya!!!!

Niko upande wa TANESCO 110% shabikieni siasa lakini nchi iko kwenye hati hati... siku yoyote kukiwa na mtambo wa MW hata 45 unatatizo tunaenda kwenye mgao...

It takes time kununua, kuagiza, kufunga na ku-komisheni mtambo... tutakuwa pamoja kwenye vibari au sio...

Heri yenu mlioko US... mtatucheka tu.

Hii ndo master plan ya TANESCO? Ooops. Tamaa mbele mauti nyuma. Kuuziwa mbuzi kwenye gunia ni mbaya zaidi. Today we are paying to our ass because someone brought IPTL without scrutiny. It ended to be a rotten deal. Na hapa kuna every hallmark of a rotten deal. The contract with Dowans was terminated by TANESCO last year (July 2008). After terminating the contract what did they do???

WE WILL FRY THE TANESCO BOSS AND HIS MINISTER FOR THIS. THE DOWANS DEAL WAS ALREADY IN THE MAKING, THAT'S WHY TANESCO CLOSED THEIR HANDS AND WAITED.
 
Yule mbunge wetu kijana anasemaje sasa!.Kwa kweli ameacha picha mbaya hasa kwenye kambi ya upinzani.
Itakuwa jambo jema kama ataacha siasa kwasababu kuna kila dalili amenaswa katika mtego wa mafisadi pengine kwa kujua au kwa kutokujua.inafaa aelezwe aache kudandia mambo bila kufanya utafiti wa kutosha.Sijui atawaambia nini watanzania waliokuwa wakimwamini kwa kiasi kikubwa kwamba ni mpiganaji mwenzao kumbe ni mganga njaa.
 
Anayefikiri Dr. Idrisa alikaa board room mwenyewe kusema mitambo ya DOWANS inunuliwe ana miwani ya mbao na masikio yenye vigingi...

Kauli ya Dr. Idrisa ni ya TANESCO.... na ni vyema muwe na kawaida ya kuheshimu proffesional za watu....

Historia ya TANESCO kuto-invest kwa muda mrefu inafahamika... sasa sijui mwataka nini
 
Hivi tuna rais mtendaji au rais ceremonial?.... Can somebody please help me. Im lost.

kwi kwi kwi kwi kwi.......................................Sober unamichekesha sana..doh!! thank you for making my day doh!! asante sana Sober
 
Mimi naamini hapa hakuna cha kutishia nyau hapa. Kitendo cha kusema kuwa nchi itakapoingia gizani wasilaumiwe, ni kosa la pili baada ya lile la kwanza la kutaka kuisababishi serikali hasara kwa kununua mitambo chakavu ya binamu yake na Richmonduli. Hapa ni kusema kuwa wamezira na hawako tayari kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

Kwa haya pamoja na hayo yaliotokea sioni ni kwanini mteuzi wao asiwaondoe madarakani mara moja (kwani hawako tayari kuwajibika wenyewe) kwa kuwa wameonyesha kuwa hawawezi kutekeza wajibu wao kwa mujibu wa sheria.

Tanzania na serikali yake lazima tubadilike, wakati wa ndio mzee sio sasa tena


----------------------------------------------------------------------------
Together, let us build tomorrow's Tanzania today!
 

CHARLES RUMISHA
THIS DAY
Dar es Salaam

Reports emanating from State House yesterday said the president has not intervened in the Dowans gas turbine wrangle. In other words, the matter has not attracted State House.

Hapa ndio huwa sielewi. State House wanakwepa lawama?
 
- TANESCO/Ngeleja walikuwa wanatishis nyau au ndiyo staili mpya ya maisha ya TZ? kwa maana kila kukicha kunakuwa na "Headlines" zinazosahulisha jamii matatizo ya msingi waliyonanyo. SAWA umeme ni mojawapo ya hayo matatizo lakini hili swala lilivyopenyezwa limewafanya watu wasahau hata TATIZO la umeme.

- Richmond, EPA-Jeetu, Mramba&Co, Twin Towers, Warioba-Ataka-Kusema, Mengi v/s Masha,& Others, Albino Killings,Pinda-Crying, (Kitine), EPA-Liumba, DOWANS ... What next? or it might be Richimond and we start all over again?

- This makes me sick!!!!!!!!!!
 
Siasa zinaipeleka nchi bapaya!!!!

Niko upande wa TANESCO 110% shabikieni siasa lakini nchi iko kwenye hati hati... siku yoyote kukiwa na mtambo wa MW hata 45 unatatizo tunaenda kwenye mgao...

It takes time kununua, kuagiza, kufunga na ku-komisheni mtambo... tutakuwa pamoja kwenye vibari au sio...

Heri yenu mlioko US... mtatucheka tu.

TANESCO wana facts,,, ninyi mnaongelea HISIA.


Kasheshe, niruhusu nizungumze kama kwa niaba ya watanzania walioko nje ya nchi na ambao wamechukua msimamo wa kuipinga Dowans!

1. Ninakuelewa unachosema na usifikiri ya kwamba tunapopinga hivi sisi familia zetu zote ziko marekani au ulaya. Tuna mama, kaka, dada, watoto na wengine tumeacha wenzi wetu huko. Tunapopinga miradi hii ya kifisadi siyo kwamba hatujui gharama yake. Kwa hiyo kutufikiria kwamba tunaandika kwa sababu hatuguswi na tatizo la umeme moja kwa moja ni kutokututendea haki. Hali ya umeme inagusa vimiradi vyetu, inagusa mipango yetu, na inagusa maisha ya ndugu zetu na wale tunaowapenda. Hivyo hatupingi kama watu tusio na maslahi katika matokeo ya upingaji wetu.

2. Kusema kuwa uko upande wa Tanesco unataka tuonekane kuwa sisi tunaipinga Tanesco. Hii ni kutubebesha mzigo ambao wenyewe hatukuchutama kuubeba. Tulichokipinga ni Tanesco kununua mitambo toka kampuni ya kifisadi ya Dowans. Period. Hakuna mtu aliyeipinga Tanesco kama miezi sita iliyopita ingeanza mchakato wa kununua majenereta toka GE au watengenezaji wengine. Kama Tanesco wangetangaza tenda mwezi ule ule wa nane walipovunja mkataba na Dowans nina uhakika makampuni mbalimbali yangejitokeza kushindania na hasa katika hali hii mbaya ya kiuchumi.

Hadi hivi sasa ninajua for a fact kuna majenereta ambayo yako tayari GE (gas turbines ya uwezo mbalimbali) ambayo waliotaka kuyanunua wameahirisha kutokana na hali mbaya ya kiuchumi. Taarifa hizi tayari zimefikishwa nyumbani na kinachohitajika ni uongozi makini tu. Kama kweli tunataka majenereta hayo yatakuwa nchini ndani ya miezi mitatu na yakaanza kazi. Watanzania wanaweza kuvumilia kwa miezi mitatu!

Hivyo hatuko kinyume na Tanesco bali tunaungana na bodi ya tanesco, wanasheria, na wadau mbalimbali ambao katika suala la Dowans waliona mwelekeo wa kifisadi wa Watanzania kulishwa kwa nguvu chakula kilichooza ati kwa vile nyama imeisha jikoni. Wakati kuna kuku wako bandani, na msitu umejaa paa na visungura!

3. Katika hili hakuna cha kuchekesha. Hili ni suala nyeti na zito. Ni suala ambalo maamuzi yake ni lazima yaume. Hata hivyo katika kuumiza huko tusikubali hata kidogo kuvunja sheria zetu au kuwanufaisha watu wachache ati kwa kuwa!

Tuungane tulilie utawala bora, uwajibikaji, uwazi, na matumizi bora ya madaraka. Inashangaza kuona kuwa wewe hutatizwi na tishio/mkwara wa Dr. Idris kwa vile unajua kuwa ni kweli anachosema kwamba kwa vile hatujanunua mitambo ya Dowans basi nchi itakuwa gizani, wagonjwa watakufa mahospitalini, wanafunzi hawatasoma vizuri na viwanda vitafungwa! Yote haya nii kwa sababu ya Dowans!
 
Anayefikiri Dr. Idrisa alikaa board room mwenyewe kusema mitambo ya DOWANS inunuliwe ana miwani ya mbao na masikio yenye vigingi...
Kauli ya Dr. Idrisa ni ya TANESCO.... na ni vyema muwe na kawaida ya kuheshimu proffesional za watu....

Historia ya TANESCO kuto-invest kwa muda mrefu inafahamika... sasa sijui mwataka nini

Kwani ni mara ya kwanza Dr. Rashid kupingana na maamuzi ya Bodi ya TANESCO?

Una uhakika kwamba Bodi ya Tanesco ilibariki ununuzi wa Dowans?
 
Ha ha ha wamekaa pembeni wamekunja mikono yao na hawafanyi lolote ili kuhakikisha nchi haiendi kizani. Wanangoja nchi iingie kizani kwa sababu kuna kampuni moja tu duniani inayouza mitambo ya kuzalisha umeme tena mitambo yenyewe ni michakavu. Huyu Idrissa Rashid ni wa kufukuza kazi haraka sana sijui ni kwanini bado yuko kazini.

BAK hapo umesema kweli. Ni tabia mbaya kwa kiongozi kuwa na tabia za kususa eti kisa hakupata alichokitaka. Sijui ni meneja wa aina gani huyo? Maana hata kwenye private unaweza kuanzisha product wateja wasiikubali lakini hususi kuzalisha bali unaibadilisha ili iendane na matakwa ya wateja. Sasa hapa unataka kutumia pesa za walipa kodi vibaya, wao wanakwambia hii haiwezekani wewe unasema sasa mtanikoma sifanyi kitu. Ni utovu wa nidhamu na ni very unprofessional at its best level. Ilichotakiwa wao waje na alternative kama wanaona kuwa hawawezi basi walitakiwa wakae pembeni. Na kwa sababu hawataki kukaa pembeni basi inabidi tuwaweke kando.
 
Kasheshe:

kama bodi yake mwenyewe imekataa, hiyo ni professionalism gani unayoongelea?
 
Kututishia nyau kajitahidi lakini kasahau siye watu wazima. Kwamba watachekelea nchi kukumbwa na giza na bado wanastahili nafasi walizo nazo? Nani mwenye uhakika na utendaji tarajiwa wa hiyo mitambo chakavu ex Richmond kutuepusha na giza? Pendekezo halikuwa namana ya kupata pesa bali ruhusa ya kununua mitambo chakavu. Mapendekezo ya kupata mitambo mipya tena yenye bima kwa bei karibu nusu ya ile chakavu bado yasubiri utekelezaji wao. Wamekwama wapi katika hilo? Kuliko kututishia nyau wasema ofisi yenu hiyo tafuteni wa kutekeleza hayo mapendekezo yenu halafu wasubiri muda ubainishe alokuwa sahihi.

Pamoja na yote je? hawa DAWNS tuna mikakati ya kuwataka waondoe mapema mitambo yao kwenye site ili isikwamishe ufungaji wa mitambo yetu mipya?. Mafisadi hawana dogo! Wakipata mwanya hawana aibu hawa watatuhujumu kinyama.
 
Dr. Idriss hakuwa peke yake, poa. Hata waziri Ngeleja alikuwemo vile vile vile. Na kamati ya hesabu za mashirika ya umma iliwaunga mkono pia. Ikiwa wanaamini kuwa walichokuwa wanataka kukifanya ni kitu halali, kina fuata sheria na ni kwa maslahi ya nchi, sasa wameshindwa kutokana na kuzuiwa na kelele, kuna mambo mawili wanaweza kufnya moja wapo.

1. Kuendelea na mradi wao - Maslahi yataonekana mbele ya safari kwani mgawo itakuwa historia. Vile vile wanaowapigia kelele hawana nguvu ya kisheria kuwazuia kufanya hicho wanachotaka kukifanya - ikiwa wanaamini ni kwa maslahi ya umma. Mafanikio yatakuwa obvious!

2. Kuachana na mradi na kujiuzulu. Ikiwa wameshindwa kutekeleza mradi wenye maslahi kwa umma, na hawana njia nyingine yoyote, kujiuzulu ni njia pekee ya kutoa ujumbe kuwa leteni watu wengine. Sisi kazi mliyotutuma tumeifanya lakini mmetuzuia kutekeleza mipango yetu. Hatuna lingine tunalojuaaaaa. Na ninyi mliotuteua hamtuamini.

Wakiuacha mradi (Dowans project), wakaendelea kukaa bila kufanya kingine, na mgawo ukaja, basi wafukuzwe maana hawafanyi kazi waliyotumwa.

DAMN IF YOU DO, DAMN IF YOU DON'T
 
Kuna wakati Mkapa alisema sisi wabongo ni wavivu wa kufikiri tukabwata sana,lakini sasa naona alikuwa sahihi.Mbona tu wagumu kuelewa na wepesi wa kusahau kiasi hiki? Hivi ile ripoti ya Mwakyembe ndo tulishaisahau?
 
kwani ni mara ya kwanza dr. Rashid kupingana na maamuzi ya bodi ya tanesco?

Una uhakika kwamba bodi ya tanesco ilibariki ununuzi wa dowans?

hahahaha
kopi ya amatus liyumba. Im wondering at tanzanians 'how can u even think of leaving the guy in the office by this moment??" the way i know him,angekuwa kweli ana sababu muhim na zenye manufaa kwa taifa idrisa ninayemjua mimi angeshawaonyesha waandishi barua ya kujiuzulu.....huwa hana uvumilivu kabisa. Kaka idrisa sijui hujajifunza tu kutokana na rada. Square yako iko keko
 
Mkandara;

Kimantiki tupo pamoja.

Keil;

Analysis nzuri, ukirudia tena posting yangu mojawapo hapo juu. Utaona nimeshindwa kuelewa kwanini Dr Idrissa amekuja na idea moja tu ya kununua mitambo ya Dowans. Nilitegemea angekuja na ni nini thamani ya kuagiza mitambo toka nje na timeframe itakayochukua.

Mie sipo upande wowote najaribu tu kucheck hali halisi.

Hii issue ipo kisiasa zaidi ndugu zangu!

Wasalaam

FP
Vitu vingi vya kiuchumi kama si vyote vinaingiliana na Siasa. Sasa hapa tukiacha siasa pembeni, kuna facts kadha ambazo zitasababisha mtu yoyote makini asiingie kwenye kununua hiyo mitambo.
1 The owners wa Hiyo richmond waliowapa Dowans Mitambo legal status yao ipoje?
2. Cost
3. Warranty and Guarantee
4. Bado zipo issue unresolved kuhusiana na Richmond/Downs Mahakamani na kwenye Report ya Mwakyembe.
5. Solution madhubuti ya umeme wa tanzania ni Nini? Umeme wa dharura or Permanent solution? na Hizo Permanent solution zinafuatiliwa namna gani.
Na mengine mengi watu wanaweza kuongezea, na mengine tukajikita sana kwenye siasa than Economical.
Na Idrissa ni Dr wa Uchumi, sasa hapa sijui anazungumzia uchumi wa ke au wa Nchi
 
(1) Kununua mitambo yenye utata kama ya Dowans ni ufisadi mwingine
(2) Nasikitika kusema kuwa hatimaye Zitto Kabwe amepata dau lake (bei yake imefikia) maana magazeti ya leo yameandika kuwa kwenye kikao na Tanesco alipata kitu kidogo
(3) Nakubaliana na hoja za kamati ya nishati na madini
(4) Dr Rashid hayupo kwa maslahi ya taifa, naye ni fisadi tuu
 
Kemeo la Marmo kwa Sitta juu ya kuitahadharisha Serikali kwenye Mtanzania(06/03/2009) gazeti la mafisadi,ni kauli ya kifisadi kwani watu wenye nia njema hawawezi kunyamaza wakati manyang'au wanaiteketeza nchi kwa tamaa zao za utajiri.
 
Anayefikiri Dr. Idrisa alikaa board room mwenyewe kusema mitambo ya DOWANS inunuliwe ana miwani ya mbao na masikio yenye vigingi...

Kauli ya Dr. Idrisa ni ya TANESCO.... na ni vyema muwe na kawaida ya kuheshimu proffesional za watu....

Historia ya TANESCO kuto-invest kwa muda mrefu inafahamika... sasa sijui mwataka nini

Kauli ya Rashid ni ya TANESCO una hakika? TANESCO wakati uwizi wa mwanzo wa akina EL & RA unafanyika, walifanya nini cha maana? Iweje leo wawe wakali na kujishaua kwiiiingi.

Mimi naona hata kukiwa na kiza haina mbaya. Bora tukose wote, haiwezekani wananchi wanapigika halafu waizi wachache wananeemeka.
 
Yote haya sababu ya kupewa cheo na wanasiasa na kukubali. Aibu imekukuta Idrissa. Watoa maelezo kama hujasoma? Nikionacho umelazimika kutoa hayo matapishi ili uonekane na waliokupa kazi kwamba umepigania deal mpaka mwisho! Utajiju.

Guys, let politics has own play ground and laeve us professionals to deliver delivarables.
 
Back
Top Bottom