Dowans: Another Richmond in making?

Dowans: Another Richmond in making?

One step. Good.

Id / Bill , je mnaweza kuongelea lolote kuhusu uwezekano kuitaifisha hiyo mitambo ya Dowans?

Naam Mama. hili linawezekana maana hao Dowans wanadaiwa na TANESCO/Serikali shilingi bilioni 23 na sidhani kama wana uwezo wa kuzilipa leo au kesho. Kama hawana uwezo wa kulipa basi Serikali itaifishe mitambo hiyo ili kufidia deni hilo.
 
Eti nchi itaingia gizani........watu wakitaka kula pesa yetu wana kuwa na lugha tamu.....

wanaJF napena kuuliza hii mitambo ya kutuokoa na giza ina warranty??

....kama ni ya Dowans - jibu ni: haina na haitakuwa na hiyo warranty! Ni IMANI tu kutokana na report ya assessor mmoja ya kwamba mitambo yao hiyo itaweza kupiga miaka mingine kenda mpaka 10 bila matengenezo makubwa.

....Je, unaswali jingine rahisi rahisi Yoyo (ambalo hata mimi naweza kulijibu 🙂) kabla hujaenda kwenye blog yako pendwa?!
 
Chinga huwa wanatoa warranty/guarantee ?
aisee mkuu umenimaliza nguvu.......mie leo hii sinunui hata spoku ya baiskeli ambayo haina warranty.......

.....watz tusikubali hili jambo yaani mpaka natetemeka kwa hasira siamini kama maamuzi ya watu tuliowaamini na kuwakabidhi dhamana ya nchi wanaamua namna hii......siamini......
 
....sasa tunaomba mwakyembe na wenzake waje na action plan itakayowezesha kupata majenereta haraka ....kama unavyonunua jeans kwa fundi....kuna mtu amechambua hapa kununua eqp kunachukua mwaka mmoja na nusu..sio kama kununua gari dubai...au japan...!!

Kwanini Mwakyembe ahusike na kutafuta mitambo mipya ya kuzalisha umeme na siyo Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Idrissa Rashid!? Kama kazi imemshinda basi ni bora aachie ngazi haraka sana.Hata kama kununua mtambo mpya kunahitaji miaka miwili, hili lilipaswa kufahamika na Wataalamu wa TANESCO akiwemo Mkurugenzi Idrisa Rashid na hivyo kuanza kulifanyia kazi mapema na siyo kusubiri miezi michache kabla ya nchi kuingia kizani ndiyo kutaka kuishinikiza nchi kununua mitambo michakavu iliyojaa ufisadi.
 
Inawezekana jeuri ya Idris inatoka kwa JK? Tetesi zinasema kuwa siku ya Alhamisi hakuweza kuzungumza na waandishi wa habari kwa sababu alizuiwa na Ikulu, na akamriwa kuipeleka statement yake Ikulu iangaliwe kwanza. Ikapelekwa na kukutwa ilikuwa kali zaidi kuliko hii ya leo, maana ilirekebishwa na kurudishwa na hatimaye kusomwa leo (ijumaa).

Kama kweli hii, basi inatisha -- maana hatuna serikali!. Ikumbukwe kwamba mwaka jana Idris alijiuzulu kwa suala dogo sana kuliko hili (kuhusu kukatiwa umeme Tanga Cement) lakini akaombwa na swahiba wake afute kujiuzulu kwake. Alikuwa anatikisa kiberiti? Kwanini hili la Dowans, ambayo ni issue mkubwa mno -- maana anapingwa wazi wazi na karibu umma mzima kutonunua mitumba -- hataki kujiuzulu?

Zak, mi naendelea kusema tuanzishe petition, Idrisa ajiuzulu, hili halina mjadala! Maana amekiri hana la kufanya zaidi ya akusubiri tukae gizani! Sijui Mh Zitto naye anasapoti tukubali kukaa gizani?
 
Nishati ni suala Nyeti sana, pia ni suala linalochukua umakini mkubwa kulifanyia kazi.

Kikubwa kinachotusumbua sisi watu wa Dunia ya 3 ni kuwa na mipango ya muda mfupi na kuipa kisogo mipango ya muda mrefu.

Pamoja na kuipa kisogo mipango ya muda mrefu, sisi watu wa dunia ya 3 ni hodari katika kuoa wake wengi na kuwa na watoto wengi ambao watahitaji nishati miaka mingi ijayo, nishati ambayo hatuna mikakati au mipango inayoeleweka ya kuitatua leo au kesho.

Bado tuna safari ndefu sana katika suala zima la nishati, kwa sababu suala hili linajadiliwa kisiasa zaidi kuliko kiuhandisi au limekuwa likiingiliwa na watu wasio kuwa na ABC ya nishati kwa sababu za kifisadi.

Lilitakiwa liwepo jopo la Wahandisi wa serikali na wa kujitegemea nje na ndani ya nchi watakao weka kila kitu hadharani kuhusu sekata hii nyeti, kuwafanya Watanzania wote wajua alternatives tulizo nazo.

Suala la nishati linajadiliwa kwa usiri mkubwa kwa sababu ya walio wengi kuendelea kuikumbatia Rushwa na aina zote za kufaidi zilizo kinyume na maadili na sheria ya nchi.

Kila mtu anataka kula leo kama siyo kula sasa hivi.

Tuna Wahandisi wengi sana nchini Tanzania pia tunawahandisi wengi sana katika nchi mbali mbali za dunia ya kwanza. Kuna Wahandisi wa Kitanzania hapa Marekani ambao wanaheshimiwa sana na vyuo vikuu kama Frolida,Oregon,North Carolina, Ohio, MIT na hata ile idara ya serikali ya National Science Foundation, kuna wengine ambao wamepata Award za kitaifa hapa Marekani kwa michango yao mikubwa katika sekta ya teknolojia.

Tulipaswa kuwatumia Wataalamu wetu wa nje na ndani kuliangalia suala hili kwa undani na kuja na plan kubwa ya kitaifa isiyolemea katika itikadi yeyote.

Wataalamu hawa wangejadili nguvu zote za nishati kuanzia zile za Nuckear mpaka za kinyesi cha ng'ombe.

Kwa vile tunataka wanasheria na mangwini waendelee kujadili suala hili la nishati,huku kila mwaka wakifanya timing za msimu wa uhaba wa nishati na kuanza kuliongelea suala la nishati kama vile ni ermegency, tutaishia kuumiza makalio yetu kwenye vikao, mwisho kitakachoumia zaidi ni sisi wananchi na per DM.
 
MadelawaMadilu: hoja yangu imeniacha hoi hasa ya kukosa uzazi wa mpango! Lakini hii dharura ya umeme ni kama uhaba wa chakula, or what say you?
 
Recurring phenomenon: panapokaribia uchaguzi mkuu nchini, dharura na maidhinisho ya kununua vitu kwa kulazimisha yanaongezeka..!! So unfortunate for them few, kwani Watanzania si mabwege tena!!
 
....Je, unaswali jingine rahisi rahisi Yoyo (ambalo hata mimi naweza kulijibu 🙂) kabla hujaenda kwenye blog yako pendwa?!
Mkuu wee acha tu nasikitika sana hapa.....haya mambo mtu mzima nashindwa kuamini kama yanafanyika.....aisee nahisi Zitto hajajua au anajua anajifanya kutojua.....mkuu kule baadae
 
....kama ni ya Dowans - jibu ni: haina na haitakuwa na hiyo warranty! Ni IMANI tu kutokana na report ya assessor mmoja ya kwamba mitambo yao hiyo itaweza kupiga miaka mingine kenda mpaka 10 bila matengenezo makubwa.

....Je, unaswali jingine rahisi rahisi Yoyo (ambalo hata mimi naweza kulijibu 🙂) kabla hujaenda kwenye blog yako pendwa?!

Pamoja na hasira zote nilizo nazo kwenye hii ishu lakini SteveD umenipa wala muda wa kuvunjika mbavu kidogo
 
We nawe, nimewataja Id na Bill waongelee hilo, wewe ni katika hao wawili au ni kuwadi wao!

that is the point.. kama ungetala waliongelee hilo wewe kimekushinda nini? Vinginevyo kama ulitaka watu hao wawili tu waliongelee, kwanini umeliweka public mngekuwa mnatumiana PM na kuzungumza huko chemba hizo topics ambazo wengine hawatakiwi kuzizungumzia!
 
Unaamini based on what? Unaogopa kusema kwamba umepata fununu ambazo bado hazijathibitika?

Haa ahahahaaaa

"Naamini..." umekuwa Sheikh Yahya?


Ningekuambia nimepata fununu isingekuwa imani! once again it you are reasong borders the same line .. imani ni imani haina msingi katika facts au uthibitisho wa kihalisia. Nachagua maneno yangu vizuri.
 
MadelawaMadilu: hoja yangu imeniacha hoi hasa ya kukosa uzazi wa mpango! Lakini hii dharura ya umeme ni kama uhaba wa chakula, or what say you?

Unaweza ita dharura ya kila siku

Tunaingiza Mashangingi ya nguvu sana ili tuweze kukatiza nyika za Tanzania kiulaini. Wakati huo huo hatuagizi matrekta, hata Used Tractors tu.
Hivi tukiwa na njaa ni dharura?

Jembe la mkono tunalihusudu sana. Yapata zaidi ya miaka 20 ilopita kulikuwa na noti ya shillingi 100 ikiwa na wanafunzi wawili wakilima kwa jembe la mkono bila kuwa na viatu miguuni. Sijui ni mbumbu gani alisagesti picha kama ile iwekwe katika noti. Wakati huo nilikuwa bado sekondari, pamoja na upeo wangu mdogo nilijua wazi kwamba kuna waheshimiwa wengi huko serikali wenye mawazo finyu kama picha yenyewe ilivyokuwa. Tunajivunia sana umasikini wetu, tumefikia mahali tumeamua kuufanya iwe kama tunu ya kitaifa.
HAta tukienda nchi za watu wengine hatukosi kuutaja umasikini wetu kama kionjo cha mazungumzo.

Nani kati yetu hapa,ambaye atakuwa hai miaka 25 ijayo,hajui kwamba tarehe kama hii mwaka 2010 muda wa saa 2 usiku atahitaji sahani ilo shena msosi?
Kama jembe la mkono linaweza kutupatia shibe ya kiwango hiki kilimo cha Matrekta kitatupa shibe kubwa namna gani?, tukiwa na matrekta 10,000 yanayotifua ardhi ya kule Malinyi na Kondoa kwa yule Mzee Mzembe Mustafa hiyo njaa itajibanza wapi?
Unaweza ita dharura ru kama unapenda.

Wajerumani walifanyia utafiti wa kisayansi juu ya Stigler Gouge enzi hizo za 1800, sisi leo bado tunaona taabu hata kusoma kwa makini kile walichokifanyia utafiti??!!!
Tunapenda mambo laini, mambo ya muda mfupi na sifa za haraka haraka, wakati huo huo tunazaa sana tukitegemea wazungu na waarabu watatusaidia na matatizo yetu, tumelogwa??!

KWa taarifa yako sisi watanzania tuna tatizo la nishati kila siku kwa sababu watanzania zaidi ya 75% hawana nishati ya umeme hata hivi niandikapo maneno haya, japo ni kwlei kwamba wanafaidika kwa namna moja au nyingine na nishati hiyo lakini si moja kwa moja. Taabu ni pale wale wachache waanzapo kukosa nishati hiyo, neno dharura hupewa kipaumbele japo ukweli ni kwamba dharura ya nishati ipo siku zote.
Kma dharura ya umeme ipo leo ilikuepo jana na ilikuwepo siku tulipo pata Uhuru miaka 48 ilopita, vipi leo hii Wabunge na viongozi wa serikali na mashirika yake wanatuambia kuhusu dharura ya nishati??
Hii nidharura ya nishati au nidharura ya nishati mifukoni mwao??!
 
Ningekuambia nimepata fununu isingekuwa imani! once again it you are reasong borders the same line .. imani ni imani haina msingi katika facts au uthibitisho wa kihalisia. Nachagua maneno yangu vizuri.

Unaamini based on what?

Keshasema huyo Mkuu wa TANESCO kwamba umeme ukikatika asilaumiwe (according to what I am reading in here) kwa hiyo ina maana anaashiria yupo to stay.

Wewe unaamini ata quit within hours based on what?
 
that is the point.. kama ungetala waliongelee hilo wewe kimekushinda nini? Vinginevyo kama ulitaka watu hao wawili tu waliongelee, kwanini umeliweka public mngekuwa mnatumiana PM na kuzungumza huko chemba hizo topics ambazo wengine hawatakiwi kuzizungumzia!


Kwanza, unaonyesha jinsi gani ulivyo slow, Id ni mkurugenzi wa TANESCO na Bill ni waziri wa Nishati na madini. Wana mandate ya kulizungumzia hilo unalotaka nilizungumzie. Kwa vile wewe ni kuwadi wao uliyesema wanunue mitambo ya Dowans eti April kutakuwa na shida ya umeme, hutaki niwaulize maelezo kama wanayo au nini kingine kikuhangaishacho?

Pili acha uzushi, wapi nimesema wengine hawatakiwi kulizungumzia! Hii tabia yako ya uzushi na uchinganishi lini utaiacha?

Any way, naona umechukua kijiti kwenye tabia ya mwa fulani - arboreal in nature. Keep the spirit up.
 
Back
Top Bottom