==========
Ni kweli kauzoefu kanapungua kwa kijana huyu. Lakini tufanyeje, in the absence of ... hata mwenye jicho moja tunamshangilia.
KGM,
Una ushahidi gani wa hiyo accusation yako? I disagree with Zitto kwa jinsi alivyolishughulikia hili suala la TANESCO-DOWANS, lakini ku-conclude kuwa yeye ni fisadi kwa vile tu amesema ambacho Rostam anataka kusikia, ni kuonyesha kuwa ulikuwa una nia ya kumpa hiyo branding no matter what na ulikuwa unatafuta tu nafasi ya kufanya hivyo kwani hakuna ushahidi wowote wa ufisadi wa Zittto.
Wakuu,
Hivi kelele zote hizi bado hakuna anayesema mtambo mpya wa kununua huu hapa?
Angalau Zitto ameonyesha hafuati upepo na yuko tayari kukosa umaarufu wa kisiasa kwa kitu anachokiamini.
Wanasiasa wote wamehamia Dar kupiga kelele za mtambo, hakuna uamuzi unachukuliwa, nchi giza totoro baada ya muda tunajiuliza eti kwanini hatuendelei?
Haya makundi yanayopingana yangeliweza kukaa pamoja na kujadiliana kwa wiki na kisha kuamua cha kufanya sio kama sasa wanasiasa wamegeuka watalaamu wa umeme.
Wacha wengine tuwajibike!
Mitambo tayari ipo ni $39million for 100MW mipya pamoja na warranty ya miaka 7 from the world biggest company of manufacturing Turbine and Jet engine ni kwenda kuchukua na kuwasha, hakuna kununua second hand kwa $60million.
===============
Breaking News: 100% verified.
Tayari keshapata taarifa kwamba mitambo mipya ipo tayari kutoka kwa biggest manufacture of Gas turbine na bei yake ni $39million for 100MW ndo maana hakupenda kusema uongo mbele ya waandishi wa habari maana angejimaliza moja kwa moja. Mitambo hipo tayari ni kwenda kuchukua tu na kuwasha. Warranty ni 7 years with commissioning for 30 years. hiyo mitambo Serikali watakaa nayo kwa miaka 40-50. hiyo mipya toka kwa huyo manufacture . Mtambo mpya kwa hali ya kawaida ni $35-46million na siyo $90million labda kama inatengenezwa mbinguni.
Zitto, huyo anaeitwa Omary Ambaye kila saa anajitia kukusafisha ama kukutetea hafai hata kidogo kuwa mshauri wako kwani ni kama wale ambao wanaweza kumwambia mfalme umependeza kumbe yuko uchi.
Huyu jamaa anapaswa kuwashauri watu wapenda sifa kama Mzee wa kiraracha pamoja na Mtikila ambao wanapenda kusifiwa kila wanalolifanya ila ukimwendekeza atakupotezea mbali sana .
Huyu jamaa anajifanya kujua kuwa wewe unamsimamo gani ,na anafika mbali zaidi kuwaona wengine ambao wanajaribu kukuonyesha upande wa pili wa shilingi kuwa hawajui wanalolifanya , jiepushe na washauri wa aina hiyo kwani ni watu hatari na hata siku moja ukikosea hawatakuwa tayari kukueleza ukweli wa mambo.
Sijawahi kujiunga humu Jf ila tangu mjadala huu uanze , nimekuwa nikisoma na nimemwona kuanzi thread za mwanzo kabisa akimshambulia kila mtu ambaye anajaribu ama kukuonyesha feeling za jamii na haswa watanzania wengi ambao walikuamini.
Anafika mahali anaandika eti wewe uko tayari kuchukua maamuzi magumu , na anaita hilo unpopular decisions , kwenye ulimwengu huu anayechukua maamuzi magumu sharti awe na uwezo wa kuyatekeleza , wewe unauwezo gani wa kuamua kununuliwa kwa hiyo mitambo kama huo ndio uamuzi mgumu?
Bush alichukua unpopular decisions , na alikuwa na mamlaka ya kufanya yatekelezeke, wewe hizo mamlaka huna mpaka sasa , sasa hao wanaokushauri hivyo jua kuwa ni watu ambao hawakutakii mema , jitahidi sana kuwa msikivu,mpole ila mwerevu kama nyoka .
Nimejiunga humu leo ili niweze kuandika ujumbe huu, niko mbali sana na huko nyumbani ila leo niliongea na watanzania walioko huko na wamenieleza kusononeshwa sana na msimamo wako huo, tafuta njia ya kutoka kwenye mtego.
Namshukuru aliyeanzisha mtandao huu kwani ni wa afya pamoja na wengine kujiandikia tuu kwa sababu wanajua kuwa majina yao sio halisi hivyo hawako responsible kwa chochote watakachoandika.
===============
Breaking News: 100% verified.
Tayari keshapata taarifa kwamba mitambo mipya ipo tayari kutoka kwa biggest manufacture of Gas turbine na bei yake ni $39million for 100MW ndo maana hakupenda kusema uongo mbele ya waandishi wa habari maana angejimaliza moja kwa moja. Mitambo hipo tayari ni kwenda kuchukua tu na kuwasha. Warranty ni 7 years with commissioning for 30 years. hiyo mitambo Serikali watakaa nayo kwa miaka 40-50. hiyo mipya toka kwa huyo manufacture . Mtambo mpya kwa hali ya kawaida ni $35-46million na siyo $90million labda kama inatengenezwa mbinguni.
Zitto, huyo anaeitwa Omary Ambaye kila saa anajitia kukusafisha ama kukutetea hafai hata kidogo kuwa mshauri wako kwani ni kama wale ambao wanaweza kumwambia mfalme umependeza kumbe yuko uchi.
Huyu jamaa anapaswa kuwashauri watu wapenda sifa kama Mzee wa kiraracha pamoja na Mtikila ambao wanapenda kusifiwa kila wanalolifanya ila ukimwendekeza atakupotezea mbali sana .
.
ooopps kumbe alishakujibu hapo juu......haya sasa Mtanzania washauri hao wakulu basi
Na wewe nawe unataka ushahidi gani ndugu yangu?.
Unataka nikwambie nimemshudia akipewa Burungutu la wekundu wa msimbazi.????. He He He He He He He.
Hata Ubunge amekwambia hana haja nao tena unafikiri ni BURE+Maneno yanayomtoka utafikiri mgonjwa wa maleria iliyopanda kichwani.
Ahsante Mkuu. Huyo Omary ni mmoja wa makuwadi wa Rostam, hivyo lazima amtetee Zitto pale ambapo Mbunge huyo kijana anamwekea kifua "ndugu" yake Rostam. Tumeshasema awali kuwa Zitto ni rafiki mkubwa wa Rostam na diyo maana Zitto yuko tayari kumcriticise mtu yeyote awe Kikwete au Sitta laki hwezi hata kidogo kumgusa Rostam.

kipi usichokielewa hapo?
Naona huyo Mama anawachezesha mdumange anapiga filimbi na nyie mnacheza kweli kweli.
Duh, kama vile mko kwenye mbio za rilei washkaji, poleni sana.