Dowans: Another Richmond in making?


Nadhani huu mjada unamiss one very important point. Hatuwezi kuendelea kumuweka Zitto kiti moto wakati hatujui maoni yake juu ya hili. Kama alivyoelezea kwa sasa hawezi kutoa msimamo wake. Nadhani tuvute subira ili tujue nani yuko upande gani kabla ya kurusha mawe.

Zitto umenifurahisha kuwa msimamo tayari unao, thats very important, na ulipaswa kuweka hili bayana tangu awali. Na wakati ukifika uwajulishe wananchi with evidence juu ya msimamo huo.

Subira yavuta heri...
 
Is being pragmatic means kununua zigo lililiopatikana kifisadi? Kwa hiyo kamati yenu inakubaliana na ufisadi? Kisheria inakuwaje?

maana ya kuwa pragmatic ni nini? labda mheshimiwa atumie neno la kiswahili naona limekuchanganya.
 
Hivi Zitto are you serious unaturushia changa machoni?
Zitto uliyejipatia umaarufu ambao wanasiasa wengi waliokaa madarakani miaka mingi hawana na wanautamani, leo unaamua kuupoteza kwa ajili ya Dowans (siyo taifa). Tanesco wameunda mgawo wa lazima ili kutulazimisha kununua mtando wa Rostam. Ndugu yangu Zitto nakusihi kwa kutumia kifungo cha Buzwagi achana na mpango huu.
 
Sijui. Mie sio mhandisi. Wamo humu, watajibu

Waliopo humu hawana uwezo zaidi ya kukariri waliyofundishwa darasani na kucheki kwenye google na wikipedia uwabanapo na maswali.

Watu humu ni cross section ya Watanzania kwa hiyo naamini kabisa kwa vile humu wahandisi tulionao wanauwezo mkubwa wa kuchonga domo na uwezo mdogo wa kutenda, ni vivyo hivyo ktk population ya Tanzania.

Anyway, tuendelee na mjadala. Leo umetega nini bungeni? Lol
 
maana ya kuwa pragmatic ni nini? labda mheshimiwa atumie neno la kiswahili naona limekuchanganya.

Kaka sijui kiswahili chake. Nimetoa mfano wa Mwalimu Nyerere na utaifishaji baada ya Azimio la Arusha. Williamson Diamond haikutaifishwa kwa sababu ya pragmatism ya Mwalimu. Au Mwalimu alipoamua kuita askari wa UK kumsaidia wanajeshi walipoasi badala ya kuita kutoka Ghana au Nigeria na hivyo kulaumiwa sana na wenzake wa Afrika kwa kuita jeshi la imperialists. Alikuwa Pragmatic. Tunapataje kiswahili chake?
 
Sema wewe kiazi, mitambo ya Dowans lazima inunuliwe kwani mwezi April kutakuwana shida ya umeme. Unaona bana, hivyo basi lazima hiyo kamati ya mheshimiwa Zitto iwe pragmatic, halafu na wadandiaji utawaona wakiuliza dola kumi. Hawana comment zaidi ya kwenda personal, so wary.
 
Ok, I will reserve my judgement.


Pamoja na hayo, nadhani MKJJ hukuweza kumuuliza kuwa hiyo Dowans ni ya nani kwani si mahali pake hapo, ila pia tujiulize:


Unaniwazia.. sasa kwanini unadhania wakati ni masaa tu yataamua kama nimemuuliza au la?

sikiliza mahojiano kwanza!

Katika kuuza na kununua, kuna mmoja humfuata mwenzie. Ama muuzaji humfuata mnunuzi au mnunuzi humfuata muuzaji. Hapa ni nani kamfuata nani
?

sikiliza mahojiano

Ama kweli kichwa cha mwendawazimu!

Na ndugu yangu Zitto naye, au basi nitasema zaidi baada ya Cheche ........


whistling
 
Kwa umasikini ulioko jimboni kwa zitto siamini anaweza kununua "hammer". Nadhani jamii ya mtikila wako wengi. Tupindishe sheria kisa Dowans. Acha tufe na mgao wetu isitoshe uchumi wa dunia unayumba tayari, huo umeme tunataka kuzalisha bidhaa gani na tukauze wapi? Kama ni stima ya majumbani wacha tuwashe kandili tu.

Kwanza urafiki wa zitto na masha unatia shaka sana.
 
Wahandisi wapo lakini hakuna kampuni ya kuunda.

Nadhani kuna technician tu wa Gas turbine, ni kwamba kutengeneza Gas Turbine ni sawa na kutengeza engine za ndege, zote ni sawa ila tofauti yake ni kwamba Jet engine (Aero) ni nyepesi, high maintenance cost, Run low hours until shutdown, na GAs Turbine ni Heavy duty( thick Metal), Low maintenance, high reliability and run many weeks with no shutdown. Hivyo kama tuna waandisi wa kutengeneza Jet engine na wa Turbine watakuwa haohao, kama hakuna wa kutengeneza Jet engine, pia wakutengeneza GAs turbine hawatakuwepo.

Kuna mambo mengi yanahitajika kutengeneza Turbine (heavy duty Generator/Compressor heavy duty/ turbine engine/ many other parts plus testing facility, which I don't think we have in Tanzania.
 


Mnanunua mtambo uliopatikana kifisadi, kwa kisingizio cha kuwa PRAGMATIC!

Kwa nini msisuggest hiyo mitambo itaifishwe na serikali kufidia hasara iliyosababishwa na Dowans kwa Taifa? If that is being PRAGMATIC as ninaitafsiri kikurya!
 
==========

Mwalimu alikuwa pragmatic na kiswahili chake ni kigumu. Hii ya kamati ya Zitto siyo pragmatism, na kiswahili chake ni "kukosa msimamo" au kuwa na "ujasiri wa kifisadi".
 
Zitto,
Pragmatism ni kutambua hali halisi na kudeal nayo kama ilivyo.
 
==========

Mwalimu alikuwa pragmatic na kiswahili chake ni kigumu. Hii ya kamati ya Zitto siyo pragmatism, na kiswahili chake ni "kukosa msimamo" au kuwa na "ujasiri wa kifisadi".

kwi!kwi!kwi!
Umeniacha hoi.
 

Sitetei Dowans maana hata kuwajua siwajui. Sijui kuanzia mmiliki mpaka hata mlinzi wa Dowans.

Nataka Umeme. Sitaki uchumi utetereke tena kwa kukosa umeme. Tunaumia kwenye Utalii, Pamba na Maua hivi sasa. Makampuni makubwa yameanza kupunguza wafanyakazi na hata kwenye sekta madini. Mwezi Januari, circuit breaker iliharibika pale Kidatu na kusababisha mgawo. Circuit breaker tu - kisa hatuna reserve ya umeme bali tuna nakisi ya 150MW.

Madhara ya kukosa umeme ni makubwa mno na ndio yananitisha na hasa kwenye sekta ya viwanda (manufacturing) ambayo ndio pekee imebakia kutoumizwa na economic meltdown. Tunaposema giza watu wanafikiri ni giza la nyumbani. Hapana industrial production etc.

Ninapoyaona haya na sioni leadership being provided, ni bora umaarufu wangu ufutike wote lakini nchi yangu ibaki imara. Its a risk worth taking and i will triumph.
 

You're not even worth a dime. Hata unihonge shing'kumi sitakuachia uidandie. Nitakutemea mate..tuuuuuuuuuuuu
 
Kuhusu hili mimi nimenawa mikono, na sitacomment tena ila nitaendelea kuiombea Tanzania na Mungu akipenda tutasonga mbele tu ingawaje power ya maadui imeongezeka sababu wanatumia njia za kila namna kuwarubuni watu wapende wasipende, kwa kutumia hata mbinu chafu.

Personally sasa hivi nitaweka matumaini zaidi kwa wabunge wa CCM kama kina Mwakyembe, Seleli, Mama Kilango sababu wao wako kwenye firing lane kutoka mafisadi which then implies wanatutetea watanzania.

Hawa wapinzani nakuwa forced kuconclude kuwa ni opportunistic na walevi wa madaraka ambayo hata hawajayapata.

Upinzani wakweli utatoka CCM, kwa hiyo hata kama nafanya makosa kwenye hii conclusion potelea mbali, nitajua mbele kwa mbele, maana hawa wapinzani nimegundua kuwa wana misimamo yao wenyewe na hawatusikilizi sisi wananchi.

Kama wajanja wa humu JF tunaburuzwa hivi, wale ndugu zangu kule milimani si watatukanwa mchana kweupe.

Mzee ES naomba mkuu ufikishe ujumbe huko kwa hao wana CCM kina Mwakyembe, Mama Kilango na wengine kuwa sasa tutabase support zaidi kwao na mategemeo yetu yako kwao sababu wakitutupa na wao tutakuwa hatuna pa kwenda.

May God Almighty Bless Tanzania.
 
Last edited:

Viwanda gani hivyo? na kama that is the case kwa nini msiopt kununua mitambo mipya mmeng'ang'ania hayo mamitambo ya Dowans?

Hiyo hasara itakayosababishwa na kukosekana kwa umeme italingana na gharama ya kununua, kugharamia maintanance ya mitambo mikuu kuu? And what if hiyo mitambo ikafa baada ya mwaka mmoja, mtakuwa na garantee ya aina yeyote?

Kuweni cost effective!
 

Moelex, don't give up man....
 
Zitto said......(akimjibu Keil)....ya kwamba
Capacity charge haihusiani kabisa na mitambo ya Dowans kwa sasa na hili limelieza katika maelezo yangu hapo awali. Capacity charge inayokwepwa hapa ni iwapo TANESCO itatangaza zabuni ya makampuni kuleta mitambo ya dharura na hivyo kujikuta katika tatizo la capacity charge.

........nafikiri hapo ndio kuna tatizo.......hivi hatuna chombo cha serikali ambacho kinaweza kufanya hayo manunuzi?.........naomba kuelimishwa jamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…