Majuzi nilimsikia Dr. Mwakyembe akizungumza katika TBC kuwa Tanesco wasinunue mitambo ya Dowans. Hoja yake kuu ni kuwa wakinunua mitambo ya Dowans watakuwa wamekiuka taratibu za ununuzi. Hakutoa sababu nyingine yeyote ya kiuchumi.
Leo nimeskiliza Mh. Zitto Kabwe katika TBC hiyo hiyo. Yeye ameunga mkono ununuzi wa mitambo hiyo kwa sababu kuu tano za kiuchumi na kiutendaji:-
1. Mitambo hiyo ipo nchini na inazalisha umeme bila matatizo. Pia moja ya mtambo huo ni mpya kabisa.
2. Tanesco inaendeshwa kwa hasara kutokana na high capacity charges. Zaidi ya 80% ya mapato yake hutumika kununulia umeme toka kwa wazalishaji binafsi unaofikia 42% tu ya umeme wote unao gawiwa.
3. Hivi sasa Tanesco inaendeshwa kwa hasara. Ununuzi wa mitambo hiyo pamoja na mingine ya IPTL etc utaisadia Tanesco kuendeshwa kwa faida. Serikali/Tanesco imo katika mazungumzo na wazalishaji wote hao binafsi. Kwa hiyo, inaonyesha kuwa, zoezi hilo si la Dowans peke yake bali ndio sera ya serikali/Taneso hivi sasa.
4. Mitambo hiyo ikinunuliwa sasa itaepusha sokomoko la mgao wa umume baadae mwaka huu.
5. Katika sheria za manunuzi kuna kipengele cha waiver ikiwa kuna umuhimu wa kununua mitambo ambayo si mipya.
Sasa mimi najiuliza:-
1. Hivi kung'ang'nia kikataza Tanesco kununua mitambo hiyo kwa sababu tu ya kukiuka taratibu ambapo Mr. Zitto kisha eleza hapo kuwa kuna uwezekano wa waiver, ni kwa maslahi ya nchi au ni kwa maslahi ya kulinda heshima za kisiasa? Yaani kuonekana tu kama kichwa cha thread hii kuwa Dowans wataonekana wameshinda?
2. Surely katika jambo nyeti kama hili ni lazima mtu atoe hoja nzito za kiuchumi, kama alivyotoa Mr. Zitto. Sasa kweli hoja moja tu ya kukiuka taratibu ndio inatosha kuzuia project ya muhimu kwa taifa kama hii?
Jamani lazima tuwe serious. Tuachane na ubinafsi, chuki na kujijenga kisiasa na tuzingatie zaidi maslahi ya taifa na huduma kwa umma. I for one, hakuna kitu kinacho nikera na kunikasirisha kama kukatika kwa umeme.
Wakuu mimi hapa naona bado ni changa la macho.
Mitaambo hii wakati wa mchakato wa Richmond tuliambiwa ni kutoka "Pratt and Whitney" ambayo ni kampuni ya marekani halafu leo hii tunaambiwa kwamba eti kuna the so called "mtaalamu kutoka ujerumani" ameikagua na kuona ni safi hatuambiwi huyo mtaalamu ni kutoka kampuni gani, na je kampuni hiyo inatambulika na pratt & Whitney kama insperctors???????? Na after all huyo manayeitwa mtaalamu ana uzoefu gani na shughuli za ukaguzi wa mitambo kama hiyo.? Je is the guy insured kutokana na ukaguzi wake?
Well kuna hili la guarantee!!!! Guarantor wa hiyo mika kumi ni nani? na kama ni Dowans mbona kampuni yenyewe imekaa kisanii sanii, kwani ni wapi ina shughuli zingine kama hizi?
Halafu eti tunatishwa kwamba tusiponunua nchi itaingia gizani! wht a joke?????????? si kisingizio hiki hiki EL alitumia kuhalalisha Richmond?????? Hawa jamaa wamekuwa wapi miaka yote hii toka 2006?
Pia kuna hili la kuchekesha zaidi eti kwamba Tanesco inaidai Dowans kama USD 11m, na kwamba eti tukinunua hiyo mitombo tutakatana humo humo. Huu ni utani tena utani wa masuala ya nguoni!!!!!!!! Yaani ina maana Tanesco inaogopa kumdai Dowans ambaye ana mitambo kwenye yadi ta Tanesco???????? Deni ni Deni hata Tanesco isiponunua hiyo mitambo bado Dowans anadaiwa.
Halafu juzi nimemsikia yule Mkurugenzi Idris aking'aka kwamba mitambo lazima inunuliwe na eti watu wengine wanafikiri wengine hawakwenda shule. Hv huyu jamaa anafahamu kwamba ana questionable credibility?
Hivi hawa wakulu wanatuonaje watanzania?????? Wanatuona sisi mafala sana eeh??? Wanatuona sisi ni kuku????
Pia nashindwa kumshangaa mtu nayemuheshimu Zitto kushabikia ununuzi huu. Yeye ni mwanasiasa anafahamu nini kuhusu mitambo ya umeme? These people should know kwamba huwa tunawasapoti pale wanapokuwa na facts na si kwamba we have just aligned to them. When they are wrong wanapaswa kukosolewa!!!!! Na katika hili nnaamini opinion ya Zito si sahihi!!!!!!
1. Mitambo hiyo ipo nchini na inazalisha umeme bila matatizo. Pia moja ya mtambo huo ni mpya kabisa.
2. Tanesco inaendeshwa kwa hasara kutokana na high capacity charges. Zaidi ya 80% ya mapato yake hutumika kununulia umeme toka kwa wazalishaji binafsi unaofikia 42% tu ya umeme wote unao gawiwa.
3. Hivi sasa Tanesco inaendeshwa kwa hasara. Ununuzi wa mitambo hiyo pamoja na mingine ya IPTL etc utaisadia Tanesco kuendeshwa kwa faida. Serikali/Tanesco imo katika mazungumzo na wazalishaji wote hao binafsi. Kwa hiyo, inaonyesha kuwa, zoezi hilo si la Dowans peke yake bali ndio sera ya serikali/Taneso hivi sasa.
4. Mitambo hiyo ikinunuliwa sasa itaepusha sokomoko la mgao wa umeme baadae mwaka huu.
5. Katika sheria za manunuzi kuna kipengele cha waiver ikiwa kuna umuhimu wa kununua mitambo ambayo si mipya.
Sina tatizo na hiyo hoja, lakini je ameishajua kwamba Dowans wanauza mitambo hiyo kwa bei gani? Incentive ya kununua mtumba ni kwamba unaweza kuununua kwa bei ambayo ni nusu ya bei halisi ama pungufu ya nusu ya bei yake, lakini kwa Dowans tusitarajie kitu kama hicho.
TANESCO walitender kununua mitambo hii na sio wao waliotangaza zabuni ya kutaka kuuziwa. Dowans ndio waliotangaza katika magazeti kuuza mitambo. TANESCO wakabid kutaka kununua. Bei Kamati imeambiwa ni kati ya 50bn na 60 bn minus tunachowadai. Naomba ikumbukwe kuwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma mpaka hapa tunapoongea haijaamua kama mitambo ya kununuliwa ni ya DOWANS. Kamati ilikubaliana na maoni ya TANESCO na kwa kuwa kamati nyingine ilikwishamua tukaona ni busara kamati mbili zikutane ili kuweka harmony. Uamuzi wa Kamati yangu bado ni huo kwamba kamati mbili zikutane ili kupima hoja za TANESCO na maswali kama haya ya bei nk yanapaswa kuulizwa
Kununua mitambo ya Dowans hakutaondoa gharama za capacity charges anazoziongelea Mh. Zitto. Mkataba wa Dowans na Tanesco ulivunjwa tangu mwaka jana mwezi Agosti na hivyo TANESCO hawalipi capacity charges kwa Dowans. Capacity charges anazoongelea Mh Zitto ni za IPTL, Songas na AGGREKO ambao mikataba yao bado iko hai na hata tukinunua mitambo chakavu ya Dowans leo hii, hao akina IPTL na ndugu zake bado wataendelea kudai hizo capacity charges bila kujali wamezalisha umeme au la. Kwa hiyo kununua mitambo mipya ama mitambo chakavu hakutapunguza hasara wala mzigo wa capacity charges kwa TANESCO.
Upo sahihi kabisa na kwa kweli ninafurahi sana angalau wewe unaelewa na una knowledge na kinachoongolewa na Kamati yangu. Capacity charge haihusiani kabisa na mitambo ya Dowans kwa sasa na hili limelieza katika maelezo yangu hapo awali. Capacity charge inayokwepwa hapa ni iwapo TANESCO itatangaza zabuni ya makampuni kuleta mitambo ya dharura na hivyo kujikuta katika tatizo la capacity charge. Iwapo TANESCO itanunua mitambo yake yenyewe (sio lazima hii ya dowans) maana yake ni kwamba itaongeza idadi ya umeme unaozalishwa na wao wenyewe bila gharama za manunuzi (cost of sales). Hivi sasa kama nilivyoeleza 80% ya mapato ya TANESCO inanunua 42% ya umeme wote. Wakiwa na gas turbines zao ina maana proportion ya umeme unaozalishwa na wao wenyewe itaongezeka. Ununuzi wa IPTL na kuigeuza kuwa gas ndio utakaoipinguzia TANESCO mzigo mkubwa sana. Renegotiation ya SONGAS ili kupunguza gharama za uwekezaji nayo itapunguza gharama. Haya ndio masuala ambayo kamati ilijadili na kutolea mapendekezo kama sehemu ya kuifanya TANESCO ianze kupata faida na kujiendesha kibiashara
Hapa Mh. Zitto anachanganya somo. Anaongelea ununuzi wa mitambo ya Dowans ambao hatuna mkataba nao kwa sasa na pia tuna option ya kukubali ama kukataa na hivyo kununua mitambo mipya. Majadiliano yanayoendelea sasa hivi na akina IPTL ni kwa kuwa mikataba yao bado iko hai na hivyo capacity charges bado ziko pale pale. Kwenye mikataba hai TANESCO haina ujanja inabidi kuwabembeleza hao wazalishaji binafsi wakubali kuuza mitambo yao iendelee kuoza huko iliko ili kupunguza mzigo wa capacity charges ambazo TANESCO wanalipa.
Nakubaliana nawe
Kiuchumi, kwenye issue ya IPTL na ndugu zake kinachotakiwa kufanyika ni CBA kati ya kuendelea kulipa capacity cherges mpaka mikataba itakapoisha ama kununua hiyo mitambo na hivyo kuondokana na gharama za capacity charges, whichever is cheap ndicho kitatoa unafuu kwa TANESCO na ndiyo maana mazungumzo yanaendelea huku serikali ikiendelea kuwabembeleza maana akina IPTL ambao wameshika mpini kwa kuwa wana mikataba hai.
Kwenye issue ya Dowans ni kufanya CBA ya aidha kununua mitambo mipya ama kununua mitambo ya Dowans. Hapo kinachotakiwa kuangaliwa ni running cost ya mitambo ya Dowans vs mitambo mipya na uwezo wa mitambo hiyo, pia bei ya mitambo mipya vs bei ya mitambo ya Dowans, life span ya mitambo mipya vs life span ya mitambo ya Dowans. Kwa kufanya hivyo ndiyo watakuwa wanatenda haki. Dowans wala hatuhitaji kuwabembeleza kwa kuwa hatuna mkataba nao, lakini giza likianza tutaanza kuwapigia magoti na ndicho kinachosubiriwa. Subiri speech ya JK ya mwezi March atasema nchi inaingia gizani kwa hiyo hatuna jinsi inabidi tu tununue mitambo ya Dowans hata kama tutakuwa tunakiuka sheria ya ununuzi. Na hapo ndipo tutapewa na kipengele cha waiver.
Hata mitambo mipya ikinunuliwa itatuepusha na mgao wa umeme. Badala ya kuendeleza huu mjadala ambao ulianza tangu mwaka jana, sasa hivi wangekuwa walishanunua mitambo mipya na imeishafungwa, ila kwa kuwa wanataka kutulengesha kwenye mkenge ndiyo maana wanasubiri mgao ukianza na tukionja joto ya giza ndipo tuanze kutengeneza Richmond nyingine. Na ninawahakikishia kwamba Dowans watatuuzia mitambo hiyo kwa bei ya mitambo mipya maana tutakuwa hatuna jinsi na hatuna muda wa kuanza kufikiria kununua mitambo mipya kwa kisingizio cha mchakato kuchukua muda mrefu.
Waiver ni nzuri kama taratibu za kisheria zinafuatwa kwamba eveluation ya mitambo hiyo ifanyike chini ya makubaliano ya kisheria. Ili ikitokea kwamba mitambo hiyo imekufa after 2 yrs wakati tuliambiwa ina uwezo wa kufanya kazi kwa miaka 10 basi tuwe na mtu ambaye tutamshika shati kwa ajili ya kulipa hasara/gharama za kufanya tathimini ambayo haikuwa sahihi. Kutumia mfano wa ATCL ambapo ndege waliyokodi tayari ni mzigo kwao hata kabla haijaanza kufanya kazi ni kuendelea kukumbatia mifano ya kijinga. Tatizo ni kwamba hata hiyo waiver ikitolewa tutafanya mambo kienyeji ili kukwepa kushitaki mtu iwapo mitambo itakuja kuwa fake huko mbeleni.
I feel sorry for Hon. Zitto K.
I cannot figure out how he got trapped on this.I think he needs to reconsider his decision. My question to him is, "What will happen with the case which was filled by Dowans?
Also, can you tell us who are the owners of Dowans?
nitaelezea zaidi badae
nitaelezea zaidi badae
Zitto hapa hakuna maelezo zaidi unachoweza kufanya ni kuja na na kauli kama za huyo Idris au Mramba kuwa mitambo itanunuliwa mtake msitake ila wewe uongezee hata ikibidi mle majalalani. VInginevyo maelezo yanayotakiwa nikuwa uliteleza kuunga mkono ujambazi huu.
Ushauri wa bure kamisheni yako kwa ajili ya kutetea si umeshachukua? Hujachelewa bado badilisha mawazo yako hayo potofu vinginevyo "you are a number one public enemy"
Kwa nini Serikali wasinunue mitambo mipya kabisa toka GE ambao wanazo tayari tena wangepata 200MW kwa $50-60million badala ya mtambo mmoja chakavu toka Dowan: Pia wangepata Warranty for 5 years and services comissioning for 20-30 years.
GE Energy - Heavy Duty Gas Turbines & Combined Cycle
Hawa Wabunge wengi ni mitambo most of them are idiot and flip flop.
Kama wewe ni zito Piga simu GE waombe quotation, ndo utajua gharama za hii mitambo, kuliko kuongea tu bila kujua gharama halisi.
Siungi mkono ujambazi wowote.Pia nipo tayari kusimama mwenyewe na kuelezea ninachoamini. Nipo tayari kubaki peke yangu iwapo ninachofanya ninaona ni sahihi na nipo genuine. Katika hili mimi na kamati yangu tupo genuine na hatuna maslahi yeyote zaidi ya kuona shirika linaendeshwa kwa faida na hivyo nasi kuwa na national champion.
I stand with the decision of my committee kwamba Kamati mbili zikutane na kujadili suala hili. Kiongozi lazima awe tayari kuchukua maamuzi magumu. nipo tayari kuwajibika kwa hili.