Dowans: Another Richmond in making?

Dowans: Another Richmond in making?

Dowans is Rostum Aziz and Rostum Aziz is Dowans. Doesn't make sense? At the end of the day mitambo itanunuliwa, Rostam ataweka hela yake mfukoni, mambo kwisha.
 

MVUTANO mkali uliibuka jana katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma na maafisa wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuhusiana ombi la kununua mitambo ya kuzalisha umeme inayomilikiwa na Kampuni ya Dowans.

Baadhi ya wabunge wa kamati hiyo iliyokuwa chini ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe waliwabana maafisa wa Tanesco waliokuwa wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Dk Idrisa Rashid ili waeleze sababu iliyowafanya waamue kununua mitambo chakavu ya Dowans badala ya mipya.

Wabunge hao walionyesha wasiwasi wao kufuatia nia ya Tanesco kutaka kununua mitambo hiyo huku wakijua kuwa sheria ya manunuzi inazuia ununuzi wa mitambo chakavu.

Mbunge wa Bukombe, Emmanuel Luhahula, alihoji iwapo Tanesco na serikali hawana wazo mbadala zaidi ya kununua mitambo ya Dowans.

Zitto alimtaka Mkurugenzi wa Tanesco aieleze kamati mitambo ile inayotaka kununuliwa na shirika hilo ina ubora wa kiasi gani.

Akijibu baadhi ya hoja za wabunge, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dk Idriss Rashid kwa kushirikiana na timu ya wataalam wake, alisema mtambo mmoja ni mpya na mingine imetumika kwa takribani saa 800 kila mmoja.

Alisema mitambo hiyo inao uwezo wa kufanya kazi kwa miaka 10 bila kufanyiwa ukarabati na kwamba ikifanyiwa ukarabati inaweza kufanya kazi kwa miaka mingine 10 na kufikisha miaka 20.

Dk Rashid aliongeza kuwa shirika lake lilipata mkaguzi kutoka Ujerumani ambaye aliikagua mitambo na kutoa taarifa kuwa mitambo hiyo ni mizima na inao uwezo wa kuzalisha umeme.

Alisema jambo kubwa linaloisukuma Tanesco kushinikiza ununuzi wa mitambo hiyo ni hali ya ukame inayotarajia kuikumba nchi katika kipindi cha miezi kadhaa ijayo.

Zitto alipomtaka Mkurugenzi huyo aeleze mbadala endapo bunge halitaridhia ununuzi wa mitambo hiyo, Dk Rashid alisema hakuna chaguo jingine ni ama kununua mitambo hiyo au nchi kuingia katika giza.

“Nafikiri suala hili ni la kitaifa, tunapaswa kuliangalia kwa uzito wake, au tuendelee hivi tulivyo na kuwa na shortage (upungufu) ya umeme au kununua mitambo iwe ya Dowans au mingine yoyote, lakini tukumbuke kuwa tukiamua kukodi itabidi kuendelea kulipia capacity charges (gharama ya mitambo),” alieleza Dk Rashid.

Alisema mitambo hiyo inauzwa kwa Sh60 bilioni, huku wakiamua kununua mitambo mipya, mbali na kulipia Sh90 bilioni, lakini mchakato huo utachukua muda mrefu hadi kukamilika hali aliyosema italiingiza taifa kwenye uhaba wa umeme.

Kwa upande wake, Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), Peter Serukamba alitetea ununuzi wa mitambo hiyo akisema kuibana Tanesco ni kuionea kwani hali iliyopo ni kuwa shirika hilo limefungwa kamba na serikali.

“Tayari wametuambia, kuna shortage (uhaba) ya umeme, tunatakiwa kununua mitambo au tuingie kwenye shortage, sasa tunataka nini tena? Tatizo letu sisi tumeamua kuiacha siasa ndio itoe maamuzi, ukiisoma hii taarifa yao hutakuwa na swali lolote la kuwauliza,” aliongeza Serukamba.

Alipokumbushwa azimio la bunge lililokataza kununua mitambo hiyo, mwanasheria wa shirika hilo, Subira Wandiba alisema hana kumbukumbu zozote azimio hilo isipokuwa anachojua yeye sheria hairuhusu kununua mitambo chakavu.

Hata hivyo, baada ya mvutano mkali kamati hiyo iliamua suala hilo lijadiliwe na Kamati ya Nishati na Madini ili waweke msimamo wa pamoja kuhusu mitambo ya Dowans, IPTL, Mradi wa Umeme wa Upepo Singida, Mradi wa Kinyerezi na ule wa Mtwara.


Stupid: Mtambo mpya wa 100 MW ni $40 million=Tshs 48billion na siyo Tshs 90 billion. Piga simu GE, huu ni upumbavu sana tena sana. Dr Idrisa acha huo wizi, utaendelea kuiba mpaka lini. Mtambo mpya twaweza kuutumia miaka 30 kwa gharama ya $40 million na siyo miaka 10, upuuzi kabisa huu. angalia riport ya Mwakyembe gharama zake ni kiasi gani, leo wameshasahau. Idiot.
 
Stupid: Mtambo mpya wa 100 MW ni $40 million=Tshs 48billion na siyo Tshs 90 billion. Piga simu GE, huu ni upumbavu sana tena sana. Dr Idrisa acha huo wizi, utaendelea kuiba mpaka lini. Mtambo mpya twaweza kuutumia miaka 30 kwa gharama ya $40 million na siyo miaka 10, upuuzi kabisa huu. angalia riport ya Mwakyembe gharama zake ni kiasi gani, leo wameshasahau. Idiot.


...Couldn't have said it any better! Thanks.
 
............watufanyie CBA...........tuone faida/hasara ya kununua mitambo michakavu/mipya............however hiyo isije ikawa precedence ya kununua mitambo chakavu...........we don't wanna go there


Kinachonichosha zaidi ni MD, Dr. Rashid, kutokuwa na plan B. ''...Zitto alipomtaka Mkurugenzi huyo aeleze mbadala endapo bunge halitaridhia ununuzi wa mitambo hiyo, Dk Rashid alisema hakuna chaguo jingine ni ama kununua mitambo hiyo au nchi kuingia katika giza''...... Jamani hivi kunahsida gani na watalaamu hawa? Should we say professional omision, self centeredness, or Uvivi wa kufikiri?. It appears TANESCO hawana long tema plan. Nilishauri kwenye thread moja juu ya namna ya kuleta ushindani katika sector hii nyeti. Approach tuliyo nayo so far haiko sawa. Naamini ushauri ukifanyiwa kazi hatutakuwa na shortage ya umeme Tanzania.

Nilishawahi sikia kuwa kulikuwa na project kubwa sana ''Stigla gorge'' sina uhakika kama spell zipo sawa. Huu ni mradi ambao naambia serikari iliupiga chini na ulikuwa uwe na uwezo wakuzalisha umeme wakutosha TZ by that time na supplus for export. Kama kunamwenye maelezo sahihi juu ya mradi huu atuhabarishe na je kama project bado ipo feasible or la. Unajua serikali yetu inahitaji kukumbushwa kila kitu nadhani ipo busy sana kiasi chakushindwa kuplan na kureview plan zake thus making adhoc decions with no Plan B '' Altenative Plan''
 
Jamani haya mazingaombwe yataisha lini? Hii ilikua ikifahamika ya kwamba swala la mitambo hii baada ya kuvunja mkataba sio mwisho. Tangu awali ilionekana kwamba walioshiriki katika sakata la mitambo hiyo bado watafanya mbinu kuizia serikali mitambo hiyo, kilichosubiriwa ni wakati.Hapa ninamaswali ya kujiuliza.

1. Baada ya serikali naTanesco kuvunja mkataba ilichukua hatua gani kutafuta alternative ya kupata mitambo au njia nyingine ya kupata umeme? Ni kitendo cha uzembe kama baada ya kuvunja mkataba usitafute alternative.

2. Ni lini serikali ilipata taarifa ya utabiri wa hali ya hewa inaoashilia ukame? Kwa sababu naona utabiri wa ukame katika miezi michache ijayo inataka kutumiwa kama shinikizo kwa serikali kununua mitambo hiyo.

3. Ni lini serikali yetu itakua na mipango ya muda mrefu kuhusu swala la umeme na mipango mingine. Kulikuwa na ulazima gani kwa kamati hiyo kukutana kama ortenative ni moja KUNUNUA MITAMBO HIYO au TAIFA KUBAKI GIZANI? Au ilikua formality kama tulivyo zoea.

Bado tuna kazi.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Kwa maoni yangu nashauri serikali inunue mtambo mmoja wa Dowans wenye uwezo wa kutoa 40MW kwa sababu wakwti wowote kuanzia sasa kama maji yakikauka basi baadhi ya maeneo ktk nchi yetu tajua giza,huo mtambo wenye uwezo 40MW ni wa kisasa kabisa zaidi ya ile inayo tumika pale SONGAS nao pia unatumia gesi asilia,na ndio uliokua unatumika na Dowans kuzalishia umeme katika kipindi cha nyuma, hivyo licha ya kwamba mtambo huo umetumika kiufundi mtambo huo bado unaweza kutumika ktk kipindi zaidi ya miaka kumi
 
Hivi huyu si ndiyo mnasema kuwa ......... Ahh, nisiseme sana.

Kwa upande wake, Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), Peter Serukamba alitetea ununuzi wa mitambo hiyo akisema kuibana Tanesco ni kuionea kwani hali iliyopo ni kuwa shirika hilo limefungwa kamba na serikali.

“Tayari wametuambia, kuna shortage (uhaba) ya umeme, tunatakiwa kununua mitambo au tuingie kwenye shortage, sasa tunataka nini tena? Tatizo letu sisi tumeamua kuiacha siasa ndio itoe maamuzi, ukiisoma hii taarifa yao hutakuwa na swali lolote la kuwauliza,” aliongeza Serukamba
 
Hivi huyu si ndiyo mnasema kuwa ......... Ahh, nisiseme sana.

Tuachane na .....................Ahh. Huko majuu watu..........Ahh wanaendesha nchi na shughuli zao kwa ufanisi na bila kubaguliwa.

Katika hili, mawazo yake huyo huyo ......Ahh ni ya busara sana kuliko hao straights.

1. Mitambo yote iliyo nchini kwa sasa inafanya kazi. Mitambo hiyo ilinunuliwa ikiwa mipya na imezeekea humu humu nchini ikitumiwa na Tanesco. Kwa hiyo hiyo sheria ya kununu mitambo ya zamani hai apply hapa. Ingekuwa ilikuwa ikitumiwa na mtu mwingine nje ya nchi, hapo ingekuwa issue.

2. Tunajua milolongo iliyopo ya ku order mitambo mipya. Mpaka ifike hapa si chini ya miaka miwili. Kwanza ufanyike upembuzi yakinifu, ziitwe tenda, kamati ya zabuni ikae, majadala wa waziri mhusika kuingilia tenda process ufuate, mwishowe oda ifanywe, kampuni iliyopata tenda ichelewe utekelezaji, etc. By the time mradi unaanza kazi si chin ya miaka miwili. Wakati huo wote Tanesco inalipa capacity charges. Sasa badala ya kutumia hizo pesa za capacity charges kununulia mitambo zinakuwa zinapotea bure. Kama si ujuha ni nini?

3. Jamaa wakikatalia mitambo yao, nyie hao hao ndio mtakao anza kulalamikia mgao.

4. Tuache siasa jamani. Tuwaachie wataalam akina Dr. Rashid, wafanye kazi yao.
 
tk,
Hili tatizo la umeme halijaanza leo. Hii mitambo ya Richmond ilikuwa ije na ifanye kazi mwaka mmoja. Wakati huo hawa jamaa wa serikali ya Kikwete walikuwa wafanye kazi ya kutosha na hadi leo wangelikuwa wameshaweka mikakati ya kumaliza hii shida.
Hivi kama ingelikuwa nchi za wenzetu, huyu Rais/Waziri/Boss wa Tanesco wangelikuwa bado wako kazini? Maneno ya NYANI yanajisema yenyewe....
 
Dowans = Kikwete + lowassa + Rostam... ndio maana nguvu yake kubwa kushinda chochote Tanzania
 
Stupid: Mtambo mpya wa 100 MW ni $40 million=Tshs 48billion na siyo Tshs 90 billion. Piga simu GE, huu ni upumbavu sana tena sana. Dr Idrisa acha huo wizi, utaendelea kuiba mpaka lini. Mtambo mpya twaweza kuutumia miaka 30 kwa gharama ya $40 million na siyo miaka 10, upuuzi kabisa huu. angalia riport ya Mwakyembe gharama zake ni kiasi gani, leo wameshasahau. Idiot.

Second kama wanauwezo wa kuwekeza kwa kununua Mitambo kama hiyo kwanini, wasitueleze p[ia Mipango/Miradi mingine kama ya Stigler Gorge etc. Watakwambia sera ya sasa ni kununua kwa mafungu, yakiwashinda au wakiona kuna manufaa mahali ndio wanakuja na idea za kununua hiyo mitambo. Ndio maana nauliza nini energy policy yetu? au mikakati yetu ya baadae? na kwanini wasiombe mkopo either WB etc wajunge miradi moja mkubwa?
 
Tanesco imeiambia kamati ya BUNGE kuwa haina njia mbadala ya kuepuka kuiingiza nchi gizani zaidi ya kununua mitambo chakavu ya DOWANS.

Hayo yalisemwa na Bw Idrissa alipo kutana na kamati ya bunge ya ukaguzi wa mahesabu ya mashirika ya UMMA.,Iddrisa aliendelea kusema kuwa mitambo hiyo ilikaguliwa na mtaalamu kutoka UJERUMANI na kuwa mtaalam huyo alisema,mitambo hiyo inaweza kufanya kazi kwa hali iliyonayo sasa kwa miaka kumi bila kufanyiwa matengenezo na pia Itakapo fanyiwa matengenezo inaweza kudumu kwa miaka mingine kumi hivyo kufanya miaka ishirini.

Aidha kamati hiyo ya bunge ilitofautiana juu ya kwamba mitambo hiyo inunuliwe tu huku wakikiuka sheria za manunuzi na zabuni au sheria hiyo itumike halafu taifa liingie kwenye giza.

Kwa mujibu wa Bw. Iddrisa ni kuwa mitambo hiyo ina thamani ya sh.60bilion na mitambo mipya kama hiyo ni sh.90 bilion.Pamoja na hayo anasema kwa hali ya ukame ilivyo,wakiamua kufuata utaratibu wa kukodi au kununua mitambo mipya, basi lazima nchi iingie gizani kwa sababu mchakato wa kumpata mzabuni wa kuleta mitambo hiyo ni mrefu sana.

Wabunge hawakufikia makubaliano zaidi ya kusema kuwa watalipeleka kwenye kamati ya bunge inayo shughulika na nishati na madini ili wapate jibu kamili

SOURCE:Mwananchi newspaper
 
I now can see... Kina Rostam wanacheza kwelikweli... Kuna wabunge watajikuta hawaelewi mchezo huu.

Inasikitisha SANA. Masikini Bongo!

Zitto kama unasoma hapa, jaribu kusoma between the lines. Tunaweza kupata mitambo mingine bila kuwanufaisha wasanii hawa... Wanahakikisha wanahonga kila sehemu ionekane haya makampuni yao yalikuwa ya maana na kutaka kuifanya serikali yetu iliyo madarakani ionekane inababaisha na ilichukua maamuzi ya kukurupuka!

Yaani iko hivi, hata wataalam wote watahongwa waandike reports ambazo zinaweza kuoenekana za kweli kuonesha kuwa hali ni mbaya sana kuliko ilivyo hali halisi.

Sikatai kuwa hali ni mbaya, lakini nadhani DOWANS hatuwahitaji... That's it!
 
I now can see... Kina Rostam wanacheza kwelikweli... Kuna wabunge watajikuta hawaelewi mchezo huu.

Inasikitisha SANA. Masikini Bongo!

Zitto kama unasoma hapa, jaribu kusoma between the lines. Tunaweza kupata mitambo mingine bila kuwanufaisha wasanii hawa... Wanahakikisha wanahonga kila sehemu ionekane haya makampuni yao yalikuwa ya maana na kutaka kuifanya serikali yetu iliyo madarakani ionekane inababaisha na ilichukua maamuzi ya kukurupuka!

Yaani iko hivi, hata wataalam wote watahongwa waandike reports ambazo zinaweza kuoenekana za kweli kuonesha kuwa hali ni mbaya sana kuliko ilivyo hali halisi.

Sikatai kuwa hali ni mbaya, lakini nadhani DOWANS hatuwahitaji... That's it!

Huu utaifa kila mtu na lwake. Kuna haja ya kuangalia tulitafuta vipi uhuru.....
 
Kifupi tunawaomba Zitto na Dr. Slaa wasikubali kabisa kanyaboya hili na kama wanataka details za mitambo hiyo wawasialiane na vijana wetu wanaoishi Marekani watapawa kila kitu toka manunuzi hadi usafirishaji na muda utakao tumika..

Mbali na hivyo kuna mitambo ya mashirika mengi sana ikiwa swala ni mitambo ya muda kwanza habari za kutumia generators zimepitwa na wakati...Population inazidi kuongezeaka kila mwaka..

Wasitufanye majinga watu hawa tumeweza kusubiri ndani ya kiza kwa miezi kibao kabla ya hao Richmond na ahadi zilikuwa hizi hizi..Na kama walifahamu hivyo kwa nini wasiagize mapema miezi kibao iliyopita kama sio mwaka mzima sasa toka Bunge lipindue mkataba wa Richmond..
 
Wakati Richmond ikiletwa tuliambiwa kwamba hilo lilikuwa ni suluhisho la muda mfupi wakati serikali ikiangalia namna ya kupata ufumbuzi wa muda mrefu. Je, TANESCO na serikali walifanya nini kwa kipindi cha miaka 3 ili kuwa na ufumbuzi wa muda mrefu?

Hivi kuna sababu gani ya kununua mitambo ambayo ilishatumika? Kusema kwamba imetumika kwa masaa 800, hatuna uhakika kama kweli imetumika kwa masaa hayo tu. Kwanini serikali isitangaze tenda ya kununua mitambo mipya? Dr. Rashid anaposema kwamba mchakato wa kununua mitambo mipya kwamba itachukua muda mrefu, tunarudi kule kule kwenye mkenge wa Richmond, kwamba mambo yalifanyika kwa dharura na hivyo hakukuwa na umakini wa kutosha, je bado tunarudia kutumia same excuses kwamba hali ni mbaya sana na hatuwezi kusubiri?

Ni vyema TANESCO na serikali wakaanza mchakato wa kununua mitambo mipya, maana naona yanatengenezwa mazingira ya kutuingiza kwenye mkenge mwingine.
 
Wakuu Mkandara na Keil,

Ndo hapa ninapofikia kufikiria uwezekano wa kuwapo vichwa vingine vipya Bungeni kuongeza nguvu.

Kuna mambo yamesitirika kwa waheshimiwa wabunge. Nafurahi mpaka sasa tunao wabunge zaidi ya 20 wanaoitembelea JF mara kwa mara, naamini wanasoma tunachoandika na wanaelewa kuwa tuna machungu na taifa letu.

Wakti mwingine huwa nahisi machozi kunitoka, kuna watu hawana huruma hata chembe kwa watanzania. Nadhani wana uraia wa nchi nyingine na ndo kinachowapa kiburi kwani wakishaharibu wanajiondokea zao.

Masikini Tanzania!
 
Fununu zinasema zimetumika fedha nyingi sana kuwahonga watu mbalimbali ili safari hii ununuzi wa hii mitambo usikwame!!!!!! (hasa baadhi ya wabunge na waandishi wa habari). Nasikia hata Tanzania Daima wamo kwenye listi na kampeni imeshaanza rasmi....
 
Kwanini tununue hiyo mitambo wakati tunawadai fedha zetu?

Kama ni kweli hawa jamaa waliondoka na shilingi bilioni 23 zetu, wakaacha kulipa shilingi bilioni 4 ambazo serikali iliwawezesha kununa hiyo mitambo, wakakiuka mkataba na hata kudanganya...naamini haya yote ni mianya ya serikali kutaifisha hiyo mitambo na kuanzan kuitumia muda wowote kuanzia sasa halafu waende mahakamani na serikali ikajitetee na kuwadai fidia zaidi na ziaidi.....

Na huyu Peter Serukamba wakati mwengine namuonea huruma na hili jukumu la kukuwadia MAFISADI kiasi hiki.....kaka soma nyakati usije zama wakati unaowatetea wanaendelea kupaaa..

omarilyas
 
Kifupi tunawaomba Zitto na Dr. Slaa wasikubali kabisa kanyaboya hili na kama wanataka details za mitambo hiyo wawasialiane na vijana wetu wanaoishi Marekani watapawa kila kitu toka manunuzi hadi usafirishaji na muda utakao tumika..

Wakisha pata detils hizo wafanye nazo nini? Mbona walipata details za ndege ya Rais (Gulfsteam) na bado ndege ikanununliwa kwa bei ile ile ya serikali..
 
Back
Top Bottom