Dowans: Another Richmond in making?

Dowans: Another Richmond in making?

...hakuna haja ya kukomoana hapa,kama serikali wana kesi wapeleke mahakamani kwa kufuata utaratibu sio kuangalia Paris wameamua nini na sisi ndio tuamue,unachotaka kufanya seems ni kukomoa sio kutaka haki ipatikane,haya mambo ya ujanja ujanja na mikato hayasaidii na hayana tofauti na ufisadi wa aina nyingine hata kama tumeibiwa!

Serikali ina kesi nzuri sana dhidi ya hawa mafisadi ambao walilipwa mabilioni wakati hawakuweza kuzalisha hata tone ya umeme. Hivyo kama serikali inataka kufanya kweli basi ni kulala nao mbele na lazima ishinde na kisha kudai mafisadi wa Richmond/Dowans walipe gharama zote za kesi ambazo serikali imeingia. Na kama hawana uwezo wa kulipa gharama hizi basi serikali inataifisha mtambo wao na kuuza mnadani.

Inasikitisha sana kuona wanachi wanataka kuikomoa nchi yao ili kukidhi uroho wao wa utajiri wa haraka haraka.
 
mi naona ifikie pahala Muungana atumie nguvu ya dola hata kama watasema ni Dictetorship lakini heshima kama Taifa irudi na sio kucheza na watu wawili tu kama wao ndio wenye akili sana, wakati taifa lina watu wanao kerwa na hayo mambo yao.

I tafikia hatua sisi wananchi tutaandamana kwenda kuingoa kama mabati yaliozungushwaga Mnazi mmoja si unakumbuka?
 
Serikali ina kesi nzuri sana dhidi ya hawa mafisadi ambao walilipwa mabilioni wakati hawakuweza kuzalisha hata tone ya umeme. Hivyo kama serikali inataka kufanya kweli basi ni kulala nao mbele na lazima ishinde na kisha kudai mafisadi wa Richmond/Dowans walipe gharama zote za kesi ambazo serikali imeingia. Na kama hawana uwezo wa kulipa gharama hizi basi serikali inataifisha mtambo wao na kuuza mnadani.

Inasikitisha sana kuona wanachi wanataka kuikomoa nchi yao ili kukidhi uroho wao wa utajiri wa haraka haraka.

...tuko pamoja na i wish to recoup back every single cent + fine kutoka kwa hawa matapeli na ikibidi kuwaweka jela as a punishment,ninachokataa ni kuwa reactionary na kufanya vitu kwa influence ya wengine,we have the law, i believe,sasa why wait Paris wameamua nini ndio na sisi tuchukue hatua nafikiri that idea ni ufisadi mwingine tuu maana sheria zetu hazisemi hivyo!
 
Wana JF, Nafikiri hawa Tanesco hawana cha kupoteza, wako katika nafasi nzuri ya kutumia sheria za Tanzania kuitaifisha mitambo ya Dowans kama walidhulumiwa kwa namna moja au nyingine kutokana na utafiti uliofanywa na tumwe ya Bunge ya Dr Mwakyembe.

Kwa kawaida kampuni zinapo-sign mikataba ya kimataifa huwa zime sign pia choice of forum, in case of disputes resolutions kwa maana ya kwamba kama gogoro litatokea, basi parties to the contract either watatumia sheria ya Nchi Fulani mfano Tanzania, au watatumia arbitration procedures mfano ICC Paris au ICC London. Hawawezi tu kuamka na kusema hey tunafungua case ICC Paris kama hawakuichagua tangu Mwanzo. Na kama itakuwa hivyo yafuatayo itabidi yazingatiwe.

ICC Paris inasema kwamba it is a standard arbitration clause that any dispute arising out of or under this contract shall be settled by arbitration in accordance with the rules of the CHAMBRE ARBITRALE DE PARIS (61, Bourse de Commerce, 2, rue de Viarmes, 75040 PARIS cedex 01, Tel:+ 33 (0)1 42 36 99 65, Fax : + 33 (0)1 42 36 08 54), of which both the Parties hereto declare to be cognisant and which they hereby accept .

Kutokana na hapo Juu ni wazi kwamba Tanesco hawana cha kujibu hapa kama hawaikubali au hawaikukubali tangu mwanzo hiyo ICC Paris , na kama wasipoikubali au kutoitambua basi ina maana kwamba hiyo kesi ya Dowan Hakuna , case ni Void ab nitio.

Kama TANESCO wanaikubali ICC Paris, ndani ya article 7 ya ICC Paris, wanachotakiwa ni either kujiwakilisha wenyewe na kutoa facts za case kama ambavyo Bunge la Tanzania chini ya Mwakembe lilivyogundua madudu ya Dowans au kumteua mwanasheria toka popote pale duniani na kuwawakilisha , na hili likisha fanyika basi hawa waliochaguliwa inabidi pia chini ya Arbitration Chamber of Paris organise arbitration in conformity with its legal status and follow regulations that define the different applicable rules during arbitration proceding.

Kama Tanesco ikishindwa kujiwakilisha au kumchagua mtu wa kuiwakilisha na pia Tanesco ikiwa imekubali jurisdiction ya ICC Paris basi, should they parties fail to appoint an arbitrator, the ICC Paris shall make an appointment on their behalf.
Tanesco inabidi tu wasiitambue ICC Paris unless kama disputes kama hiyo ilisha wahi kupelekwa na Tanesco wenyewe na kuamliwa na hao wa paris , Tanesco itakuwa kwa njia mja u nyingine imekubali jurisdiction yab Icc Paris.

Kwa hayo machache napenda tu kusema kwamba Tanesco hawana cha kupoteza, ni hawo tu Dowans wanaotaka kuiendesha Tenesco kicha kichwa toka bongo mpaka France wakati sheria wanazijua kwamba kama walichagua bongo inabidi wa-stick na bongo, pia kwamba penye ukweli uongo hujitenga, yale aliyosemwa Dr Mwakyembe kama yalikuwa ya uongo yatajulikana huko huko hivyo Tanesco kaeni mkao wa kushinda case kwa maoni yangu na hakuna haja ya kuondoa injuction hiyo maana hata huko Paris itawabidi kila parties waweke bond kama arbitral award kwa mshindi na atakayeshindwa basi ICC Paris would not intertain the case .

Serikali pia yaweza kutaifisha mali za Dowans au Richmond chini ya nationalising process na hatuna obligations yeyote kuilipa kampuni yeyote inayokuja Tanzania kufanya madudu, na nafikiri hii itakuwa precedent nzuri itakayo-send good message kwa wawekezaji wote uchwara ili waache ufisadi la sivyo mali zao zitataifishwa. Inabidi tufuate mfano wa Hugo Chavez wa Venezuela ambaye hana machezo na wawekezaji ushwara!!! Tutakuwa kichwa cha mwendawazimu hadi lini, kila siku ni kunyoa nywele tu na kwenda kupokea ma-Phd for conflict resolutions wakati wenyewe tumeshindwa ku-resolve conflict kati na ndani ya nchi yetu kwa kutumia sheria zetu mpaka twende Paris?

Kwa maelezo zaidi kuhusiana na ICC Paris soma hapa chini.
Chambre Arbitrale de Paris
 
This is the best thing to happen.. kwa sababu itatakiwa kujibu swali la msingi:

Dowans ilirithi mkataba toka Richmond; Richmond imegundulika kwa sheria zetu siyo kampuni na haipo. Sasa Dowans watarithi vipi mkataba wa kampuni ambayo haipo. Kama Paris watasema kuwa mkataba wa Dowans na Richmond ni illegal maana yake makubaliano kati ya Dowans na Tanesco hayapo vile vile na hela ambazo tayari tumewalipa tutazidai.

So kwangu, ni kufungua kesi nyingine (counter suit) huko huko Paris na kuidai Dowans kwa kudanganya walipoingia mkataba kwa sababu mikataba yote inaingia in good faith. Dowans hawakuingia na good faith.
 
Mzee mwanakijiji, ama kweli umenena!! Hawa wa Dowans hawawezi kurithi mali ya kampuni uchwara!!

sheria pia inasema kwamba the one who comes to seek justice (in equity) must come with clean hands, je hizo clean hands za Dowans ziko wapi? Ni mafisadi yanayotaka kui-pressurise Tanesco ili walipwe hiyo capacity charge au wainunue mitambo yao chakavu, nafikiri Dowans kwa kufungua Case Paris wanataka kufnya Dili na Tanesco ili baadae tuambiwe kwamba aah imedidi tuwalipe kulipo kwenda France maana ni ghrama sana, Gharama za kutetea case paris ni kubwa kuliko malipo kwa Dowans hivyo ni vema walipwe, hii ni likely outcome ya mcheo mchafu toka kwa Tamesco unavyowezwa kuchezwa na hao akina Ngereja wanaong'ang'ania kununua mitambo chakavu maana tayari walikisha jua habari za ICC PARIS kupelekwa huko na akina Dowans...

Pia counter suit si possible maana ICC Paris haiwezi ku-intertain case nyingine wakati case ya msingi bado haijamliwa, ngoja kwanza waamue hiyo ya msingi, ambayo kwa mtazamo wangu kisheria Dowans isubiri tu kunyeshewa mvua za mawe halafu Ndipo Tanesco wakongelee Msumari wao kwenye donda ndugu ndipo Dowans watajua nini maana ya who comes to seek justice must come with clean hands.
 
Hehehehe yangu macho maana naona movie ya kumkamata Lowassa na Rostam hiyooo ndio inataka kuanza tunamalizia hili trailer la Epa na Alex Stewart then movie lenyewe linaanza, noja nitafute coca yanngu mie mapemaaaa
 
Asanteni waungwana wote mliotangulia kusema mpaka sasa. Nimewapata vizuri sana. Waswahili wa pwani wanasema "ngoma inogire". Maana yake "mchezo umeiva". Iwapo ni kweli inavyosemwa kuwa Dowans ni Rostam/Lowasa, basi hawa watu si watanzania kabisa. Ni adui zetu. Inasemekana Ngeleja ameinuliwa kisiasa na haya mafisadi Rostam/Lowasa. Sasa inaanza kuingia akilini kwanini Ngeleja alitaka kutuingiza mkenge kununua mitambo chakavu ya Dowans kinyume cha Procurement Act na maamuzi ya Bunge kwa manufaa ya makuwadi wake kisiasa. Kamati ya bunge ya akina Shelukindo ingezubaa tu, tungekuwa saa hii Rostam/Lowasa wanakenua macho, na watanzania wanalia. Kumbe ni mchezo mchafu ulisukwa na huyo Ngeleja wao. Sasa nadhani ni serikali ku"act"tu bila kuoneana huruma. Haya kina Rostam na Lowasa si wenzetu. Tuwashughulikie mapema kabisa. Tunamuomba kikwete atoe upenzi wake kwa haya majamaa kama kweli ana nia thabiti ya kusafisha nchi.
 
...hivi kwanini Lowassa/Rostam/Karamagi etc bado ni wabunge na bado wanatembea mjini freely bila hata na kuwa na kesi ya kujibu? nilifikiri bunge lina uwezo wa kumfukuza mbunge yeyote aliyefanya act kama hizi..walimfukuza Zitto kwa kumsingizia tuu,sasa vipi hawa matapeli wakubwa walioleta disaster na hasara ya mabilioni kwa kutumia ubunge huo huo,cha ajabu the bogus speaker of the house kazi yake ni kuangalia maslahi ya mafisadi na kusimamisha wapiganaji kama Zitto...Sitta must go!
 
lakini kwanini Tanesco wafungue kesi sasa hivi baada ya kushindwa kuinunua hiyo mitambo. Mbona hiyo kesi ya kuidai Downs hatukuisikia toka mwanzo? na kwanini wasi-kamate account yao Bank ambayo walikuwa wakiwa lipa Downs. Halfu kamati ya Bunge hawakuweza kuwataja wamiliki wa RICH/Downs, je sasa hivi sio wakati wa kuvua-buibui, ilikujua ni nani aliye jificha chini ya huyu mtu-kampuni Rich/Downs, kwa kupitia Brela au Bank ambako hiyo kampuni ina Account.
 
Koba,
Mkuu swala la Paris wala usilichukulie kuwa dogo na hakika nilitazama bao tumepigwa vibaya vibaya..Richmond hata kama ni kampuni feki walichonunua wao ni Mkataba na sio Richmond kisha Dorwans ni kampuni iliyosajiliwa kihalali. Unaponunua Mkataba hakuna haja ya tender kufanywa na serikali wala longolongo zote tunazoweza kudai kwa Richmond..Kila kitu kiimefanyika kiujanja ujanja wakitumia sheria kama kivuli.

Matatizo ya Richmond yatabakia Richmond na Dorwans yatawakabili wao, up to now hawa jamaa wanatushinda!. suggest yangu ya kutazama matokeo ya Paris ni ktk kuona nani atakuwa wa kwanza kurusha jiwe!..Kikwete hawezi kumsimamisha Lowassa wala Rostam bila sababu, hilo ondoa kabisa akilini na hakuna rule of law nchi zetu, Ni ujanja ujanja mtupu hata hizo kesi za kina Mramba kunatumika Ujanja zaidi kuliko sheria..

Kwa hiyo Paris tunaendeshana na Dorwans kama shirika Incorporated hata kama wamiliki ni Rostam/Lowassa, na Tanzania inabidi tuwe wajanja kutumia sheria..

Katika dunia ya leo Ujanja ni kupata maswala ya haki na sheria ni baada ya matukio. Hapakuwepo na haki wala, sheria ya kuivamia Iraq wala Afghanstan...

Wakati Marekani na NATO wanajaribu kuweka defence missile huko Poland, mrusi naye kasogea Cuba wakisema:- Watawekaje defence missile Poland kama hawafikirii kuwa Russia ni adui yao...those defence missile against who! -kwa hiyo wanasubiri tu Mmarekani (NATO) waanze wao watamalizia.
 
Mkuu, kwa heshima zote, naomba tusichanganye apples and oranges, kutumia invasion of Iraq and Afghanistan, to justify ubabe wa Kikwete's government is really reaching that stage. Alfu ukaleta tena Cuban missile crisis. Labda sijaelewa point yako maana so far all the examples you brought up is foreign relations wakati DOwans vs Tanesco ni inetrnal affairs. Ungeleta hapa kesi ya Blago kwa mfano ingekuwa ni mfano bora zaidi.
Mimi binafsi nafurahi wanapopelekana mahakamani iwe hapa au nchi yoyote. Kwa nini? kwa sababu proceedings zinakuwa wazi na wananchi tunapata information nyingi, na si hadithi kuishia behind closed doors.
 
Rostam/Lowassa wanajua hamna mnunuzi yeyote duniani anayeweza kununua hiyo mitambo na hawana pa kuipeleka, kwa kuogopa kulazimishwa kutoa mitambo kwenye ardhi ya Tanesco wamewatumia viongozi uchwara through Mahakama.

Dowans suffers another setback

Mambo hayo, it would be interesting to know how much these turbines cost. And if they borrowed any money to buy them. Hawa jamaa waishie jela, kufilisiwa na kufa maskini....
 
Susuviri,
Mkuu huwezi kunielewa ikiwa utayachukulia maelezo yangu kwa mifano ya karibu kuhusiana na Dorwans isipokuwa wahusika wake yaani Lowassa na Rostam. Kwa bahati mbaya sina imani na Haki wala Sheria ktk dunia ya leo, kwa maana nyingine mwenye nguvu na uwezo ndiye mwenye haki na sheria..

Matatizo yote kati ya Marekani na Iraq alikuwa Saadam, na Afghanstan alikuwa Mullah Mohammed Omar kutokana na maamuzi yao against interest za serikali ya Marekani, hawa wote wakatafutiwa dawa bila haki wala sheria. Hata Russia problem kubwa ya Marekani ni Putin hivyo fitna inaundwa kwa sababu ya kiburi chake..

Sisi, matatizo na Dorwan's yanatokana na Lowassa/ Rostam pamoja na kwamba ni maswala ya ndani lakini hawa jamaa wamelamba dume hadi sasa hivi. Na wana kiburi hivyo fitna lazima ijengwe nje ya haki na Sheria kisha itumike kisheria kuhalalishwa...Ni ujanja ujanja kama alivyosema Koba, lakini ndivyo dunia ya leo inavyokwenda. Ukiujua huu wenzako wanakuja kwa mlango wa nyuma.. Mchezo ni ule ule kuzua FITNA ktk kumtafuta mchawi..

Well, yawezekana nimekwenda nje ya utaratibu ambao wengi wenu mngependelea kuuona lakini mimi binafsi kutokana na kutokuwa na imani na hizo haki na sheria bali ushenzi kwa malipo ya Ushenzi ndio maana nimezua fitna hiyo..

Mkuu hata kama ingekuwa mfano wa ndani bado ningeonyesha fitna na ushenzi ambao Koba hakubaliani nao isipokuwa haki na sheria itumike. Ningependa sana niamini kama nyie, lakini mdudu wangu ananipa kuwa Mkataba wa Richomond na Tanesco umepatikana kiujanja, kihuni na hapakuwepo na haki wala sheria. Wakatufumba macho na kumwingiza Dorwan's ambaye kwa mtazamo wangu wana kila haki na sheria tofauti na Richmond lakini bado tuna karata mkononi kuweza kuzua fitna.

We can turn the table around!
 
Nimekuelewa sasa, mkuu, na machoni kwangu ni kama umekata tamaa kidogo, but it is your prerogative, mkuu!

Naomba kwanza niulize hivi Dowans ni 100% ya Lowassa and Rostam? Tunajua nini kuhusu Dowans? Ndo maana nasema wanapoenda mahakamani kuna information ambazo lazima zitatoka na tutapata insight zaidi.

We have to respect private property and private ownership in Tanzania vinginevyo hatutaendelea. We also have to learn to respect the rule of the law. Ni kweli kabisa kama ulivyosema kuwa unfortunately wapo watu wenye nguvu za pesa au kisiasa watakaojaribu kupinda sheria (si Bongo tu bali nchi yeyote duniani) but it is our duty as citizens to usher them back to the legal framework. How can that be done? By public pressure and by the ballot box. Mfano mzuri ni Bush and his cronies.

I truly believe that this attitude ya kudhani ujanjaujanja works is the curse that our society suffers from. Because even in other countries, vitu hivi vipo but in Western societies even posthumously, things are re-assesed within legal framework and justice is done (even after 200 years). These are my thought, mkuu.
 
Tuwe makini na huu mchezo unaochezwa hapa. Ni serikali hiyohiyo ndiyo iliyoingia mkataba na Richmond, ambayo maelezo yanaonyesha wazi kabisa ilikuwa kampuni hewa. Ni serikali hiyo hiyo iliendeleza mkataba wa Richmond uliorithiwa na Dowans. baadaye ni serikali hiyohiyo iliyo katika mkataba na Dowans kwa maelezo ambayo ni magumu kuyaelewa kuwa kampuni iliyoingia nayo mkataba awali (Richmond) ilikuwa hewa. Lakini baadaye naibu waziri wa Nishati, Adam Malima alianza kuonyesha hisia za serikali kuwa inaweza kuitumia Dowans kama hali italazimu, hapa ulikuwa ni muda mfupi tangu serikali ikatishe mkataba wake.

Mbaya zaidi, ni serikali hiyo hiyo, iliyogundua kuwa mkataba na Dowans ni batili, ikaonmyesha dhamira ya kuinunua mitambo ya kampuni hiyo hadi ilipozuiwa na Bunge kwa maelezo ambayo Mwanasheria Mkuu alipaswa luyafahamu na kumshauri waziri kabla hajapeleka ombi la srikali kwa kamati ya Bunge.

Sasa serikali hiyo hiyo imerudi tena kuishitaki Dowans baada ya Dowans kuishitaki serikali.
Inavyoonekana, serikali inakuwa kama haijui inachokifanya katyika molongo wa matukio haya yote kwa maana iliyemkataa kuwa hafai. kama serikali ingekwua inamaanisha inachokisema, basi wakati ule ule ilipokatishja mkataba ya Dowans, (kwa mujibu wa sababu walizozitoa) walipaswa kuwahi pia mahakamani kudai fedha walizoilipa kampuni hewa kupitia mkataba hewa.

lakini angalia kinachotokea, waliorithi mkataba hewa ndio wa kwanza kwenda mahakamani na serikali sasa inajikuta katika upande wa kujitetea badala ya yenyewe kuwa ndiye mdai.
Na sinema bado inaendelea...
 
Kwa maelezo haya nakubaliana na Njia ya mkatao anayoshauri Kichuguuu, kwa sababu inaonyesha wazi baadhi ya watu ndani ya serikali wanataka bado kuhakikisha Dowans wananufaika na pesa na wavuja jasho wa Tanzania. Hivyo kwa kutumia sheria kuna uwezekano mkubwa tukauvaa mkenge. Afterall Wafaransa wana uchungu gani na nchi kama Tanzania? Hao majaji wakikatiwa na kuahidiwa mgawo baada ya kushinda kesi watakuwa na tatizo gani.Kama Uingereza walijua kuwa Rada wanayotuuzia sisi taifa masikini haikuwa tunayostahili na bei yake ilikuwa juu sana, lakini bado wakaona tuinunue,unategemea nini kwa Mfaransa??
Kama mkataba wa Richmond uligundulika ni feki kwa mujibu wa kamati then kuurithi mkataba huo hakuufanyi usiwe feki. Ni kuwa DOWANS walirithi mkataba ambao ni batili
 
Dr. Slaa, naona unachungulai huku, naomba nikutupie swali.

Ikiwa mkataba kati ya Tanesco/URT na Richmond ulikuwa una utata na hivyo kuwa ni batili, kwa nini tumeendelea kuilipa Dowans au kuafiki kuwepo kwa mkataba kati ya Tanesco/URT na mrithi wa Richmond ambaye ni Dowans?

Kwa nini kuna utata na ubutu kutoa kauli moja kuwa mkataba wa Richmond hautambuliki kutokana an Richmond kuwa kamouni hewa iliyodanganya wasifu wake?

Ni mpaka lini tutaendelea kuwa waoga na kuendekeza wanaotuhujumu?
 
Susuviri,
Kwanza kabisa nianze na swali lako ambalo umeuliza kama Dorwan's ni kampuni ya Rostam na Lowassa..

Mkuu, nitasema:- NB:- Hapana KISHERIA, na Ndiyo KIUJANJA...

Kuna mchezo ambao unatumiwa na viongozi wa Tanzania pamoja na nchi nyingi maskini..
Kama ilivyokuwa Richmond, hutafutwa mtu wa kuaminika mwenye uraia nje ambaye anaweza kuwa Mbongo au mtu wa nje ambaye anaweza kufungua kampuni huko nje kihalali kulingana na deal lilipo Tanzania. Shirika hufunguliwa na wanahisa ndio hao viongozi wenyewe lakini hakuna kabisa mikono yao ndani ya shirika hilo. Hata hapo Bongo kina Manji, Load Rajpar, Jeetu Patel na wahindi wengine wengi tu wametumiwa ktk masdeal kama haya.. nadhani unakumbuka ile list ya Mob ya Mkapa na M Bank.. ni ktk mchezo huo huo.

Sasa tatizo la uharamu wa deal la Richmond KISHERIA sio mkataba wenyewe isipokuwa ni shirika lenyewe. Richmond ni kampuni hewa kama ilivyobainika lakini mkataba wake ulifuata sheria zote pamoja na kwamba hazikuwa for the interest of our Country, yet kisheria mkataba wenyewe ni genuine kama ilivyo mikataba mingine such as Barricks.. Sasa kufungiwa kanyaboya ktk mkataba na tukakubali na kuweka sahihi inatufunga sisi ktk Mkataba huo isipokuwa tu tatizo likaja kwa shirika lenyewe Richmond... Na kama unakumbuka Mh. dr Slaa alipoanzisha vagi la Richmond tulikuwa na kila haki kisheria kuvunja Mkataba kwa sababu kwanza walishindwa ku deliver kisha tukaja gundua kuwa halikuwa shirika halali Marekani wala Tanzania...

Kwa Ujanja ujanja bila kufuata sheria na haki tukapigwa changa la macho, mkataba kuhamishiwa shirika la Dorwans (Halali)ambalo pia tayari lilikwisha pangwa ili kuvuruga ushahidi wa Richmond kama shirika feki..

From the beggining ingewezekana kabisa Tanesco kuchukua mitambo ya Richmond badala ya Dorwan's lakini kwa sababu hawa jamaa walikuwa bado na tamaa ya fedha wakatafuta njia ya mkato ambayo ingeweza kuua ndege wawili kwa jiwe moja. yaani kuua kesi ya Richmond wakati huo huo wanaendelea kukatiwa chao na Dorwan's. Dorwan' by any means ina mkono wa Rostam ndio maana walitumia address yake lakini tukitumia haki na sheria hatuna ushahidi wa mkono wake...Him and Lowassa were/are silent Partners... sijui kama tupo pamoja!

Kwa hiyo, hapa tunafungwa na vitu viwili, Dorwan's kama shirika - A legal entinty (Incorporated) na sio shirika feki kama Richmond haina makosa kabisa na wala hakuna kitu walichoshindwa kulingana na mkataba wetu as a company..Na kibaya zaidi ni kwamba shahidi wao wakubwa ni toka serikali yetu Mh. waziri mkuu mstaafu Lowassa, ambaye mbali na kuwa na interest zake ndani ya Dorwan's ana hasira na utawala huu.. Ndiye alitoa Order ya kuhamisha mkataba toka Richmond kwenda Dorwan's baada ya kupata ushauri wa Mwanasheria mkuu (Chenge) nadhani sijakosea kulingana na report ya Mwakyembe.

Hivyo tumejiweka ktk nafasi mbaya zaidi kama nchi against shirika halali ya Dorwan's lenye wazalendo wenye uchu wa fedha na hasira za kutotawala...Kinachoendelea hapa ni kukomoana tu hakuna tena haki wala sheria..

Kama nilivyosema mchezo wote huu umechezwa kiujanja ujanja wakitumia kivuli cha sheria na haiwezekani kabisa kutumia sheria tupu kuweza kuhakikisha hatupotezi zaidi fedha..Now it's about survival of the fittest!..

Ndio nikasema huko Paris hatuna Ujanja wala hatuwezi kutumia ujanja isipokuwa sheria na bila shaka Dorwan's ni washindi, bila hata kuhonga mtu..

Lakini kwa sababu sisi tunafahamu ni akina nani waliotufungia kanyaboya la Dorwan's tuwape kibano hapa nyumbani.. Rostam na Lowassa wafunguliwe mashtaka wao na sio shirika la Dorwan's..Kesi yao kuhusiana na Richmond iko huru kabisa na tumekuwa na shida kubwa kuifikisha mahakamani kwa sababu aidha ni washikaji wa Kikwete, ni sangara nyavu zetu ndogo au bunge limekwisha kubali hasara hivyo wanafikiria gonjwa limekwisha..

Sasa tukifuata sheria pamoja na kwamba Richmond ni shrika feki bado itatuuwia vigumu sana kumhusisha Lowassa na Rostam kwa sababu hawa ni watu nje kabisa kulingana na mchezo niliousema huko mwanzani. Richmond ni shirika hewa hatuwezi kuwafikisha mahakamani kama shirika kwa sababu halikusajiliwa Marekani. Na kibaya zaidi Tanzania mkubwa akikwambia ruka unatakiwa kuruka bila kuuliza!.. pia kiongozi hahitaji kuandika kitu chochote anaweza kumtuma hata dereva wake acha mbali kufuata sheria na utaratibu wa kazi..

Kama unakumbuka Meghji pia alisema aliingizwa mkenge na Balali kwa simu tu bila supporting document, fedha zikatoka..Behind all this, kilichotembea Tanzania ni nje kabisa ya sheria na haki lakini ndio utaratibu uliokuwepo na huwezi kum pin mtu ktk madhambi ikiwa mambo yote yalikuwa yakiendeshwa kiholela..

Kwa hiyi leo hii sijui hata tutaanzia wapi kuhusiana na Richmond kwa sababu kwanza ni shirika hewa, pili wahusika wakubwa ni pamoja na Waziri mkuu mstaafu, Mwanasheria mkuu na vigogo wote ambao wamejiuzuru.. Mara nyingi kwa viongozi ngazi zao hii ndio huwa adhabu kubwa sana na huonekana kuwa ni ujasiri mkubwa kwa kiongozi kuachia ngazi..

Lakini kwa kutumia street justice inawezekana kabisa kuwamaliza hawa wote waliotakla kuifilisi nchi yetu..

Na tukitumia haki na sheria inawezekana pia lakini mkuu wangu ikiwa Richmond ni shirika hewa na Lowassa au Rostam sio walioweka sahihi isipokuwa wao wamesimama upande wa Richmond ambayo ni shirika hewa na walihakikisha hakuna mkono wao kisheria unaoweza kuwafunga, tutawavuta vipi ndani ya mashtaka kisheria!...

Trust me, Lowassa anajua alichokifanya na anafahamu kabisa hatuwezi kuwa na ushahidi wa yeye kuhusika moja kwa moja zaidi ya hearsay!..Kujiuzuru kwake hakuna maana anahusika isipokuwa kosa limefanyika akiwa waziri mkuu hivyo ni uzembe na aibu kwake...kajiuzuru. Unakumbuka hata India baada ya mabomu ya zile Hotel viongozi wake walijiuzuru haina maana walihusika na kulipua mabomu hayo!..

Na wale wote waliosema Lowassa ndiye aliyetoa order ndio leo wanaonekana wenye hatia kwa sababu hakuna ushahidi kimaandishi kumhusisha Lowassa..Na tukifuata haki na sheria hatuwezi kumfunga Lowassa kwa sabau kahakikisha yuko nje, kuna scapegoats wale waliokubali kufunga mkataba na Richmond..All evidence point to them!
 
Sahihisho dogo tu mkuu Mkandara... aliyekuwa AG wakati wa Lowassa ni Mwanyika na si Chenge. lakini ufafanuzi wako ni mzuri sana, Umeweka wazi kwa kiasi fulani ni jinsi gani ambavyo Tanzania inaelekea kupoteza mchezo huu. Kosa tulilolifanya ni kutovunja mkataba wakati tulipobaini kuwa Richmond ni hewa. pale ndipo palikuwa pa kuchukulia point. lakini sasa tumeuvaa mkenge kwa sababu Dowans kama kampuni/shirika hawana matatizo yoyote, na mkataba waliorithi nao hauna matatizo yoyote. Ukichunguza kwa undani, katika kesi ambayo Dowans wamefungua, Richmond, ambayo sisi ndiyo tulikuwa na matatizo nayo, haihusishwi kwa karibu. Hivyo hapa sarakasi ni serikali vs Dowans, yale majigambo yetu kuhusu Richmond wala hayawezi kutusaidia kwenye kesi hii, tujiandae tu kuwalipa hawa wajanja fedha zetu
 
Back
Top Bottom