Dowans: Another Richmond in making?

Dowans: Another Richmond in making?

Susuviri,
Kwanza kabisa nianze na swali lako ambalo umeuliza kama Dorwan's ni kampuni ya Rostam na Lowassa..
Mkuu, nitasema:- NB:- Hapana KISHERIA, na Ndiyo KIUJANJA...

Kuna mchezo ambao unatumiwa na viongozi wa Tanzania pamoja na nchi nyingi maskini..
Kama ilivyokuwa Richmond, hutafutwa mtu wa kuaminika mwenye uraia nje ambaye anaweza kuwa Mbongo au mtu wa nje ambaye anaweza kufungua kampuni huko nje kihalali kulingana na deal lilipo Tanzania. Shirika hufunguliwa na wanahisa ndio hao viongozi wenyewe lakini hakuna kabisa mikono yao ndani ya shirika hilo. Hata hapo Bongo kina Manji, Load Rajpar, Jeetu Patel na wahindi wengine wengi tu wametumiwa ktk masdeal kama haya.. nadhani unakumbuka ile list ya Mob ya Mkapa na M Bank.. ni ktk mchezo huo huo.

Sasa tatizo la uharamu wa deal la Richmond KISHERIA sio mkataba wenyewe isipokuwa ni shirika lenyewe. Richmond ni kampuni hewa kama ilivyobainika lakini mkataba wake ulifuata sheria zote pamoja na kwamba hazikuwa for the interest of our Country, yet kisheria mkataba wenyewe ni genuine kama ilivyo mikataba mingine such as Barricks.. Sasa kufungiwa kanyaboya ktk mkataba na tukakubali na kuweka sahihi inatufunga sisi ktk Mkataba huo isipokuwa tu tatizo likaja kwa shirika lenyewe Richmond... Na kama unakumbuka Mh. dr Slaa alipoanzisha vagi la Richmond tulikuwa na kila haki kisheria kuvunja Mkataba kwa sababu kwanza walishindwa ku deliver kisha tukaja gundua kuwa halikuwa shirika halali Marekani wala Tanzania...
Kwa Ujanja ujanja bila kufuata sheria na haki tukapigwa changa la macho, mkataba kuhamishiwa shirika la Dorwans (Halali)ambalo pia tayari lilikwisha pangwa ili kuvuruga ushahidi wa Richmond kama shirika feki..


Inawezekana vipi kusaini mkataba na "kampuni hewa" halafu mkataba uwe na uhalali kisheria?? Mkataba hufanywa kwa kuaminiana kwamba wewe ni X na mimi ni Y na kwamba katika muda wa mkataba, X ataendelea kutimiza majukumu yake kama X, na Y vivyo hivyo. Ikija kubainika kuwa X alitumia ulaghai kujifanya yeye ni X wakati ambapo yeye ni Z basi mkataba uliowekwa kati ya X na Y si unakuwa batili moja kwa moja??

Mnaposema Mkataba unasimama kama "independent entity" bila kuunganishwa na Richmond nashindwa kuelewa...naombeni mifano mingine kama hii ambapo mkataba ulisimama hata baada ya kubainika upande mmoja ulidanganya.
 
Yebo Yebo,
Nakubali maneno yako lakini unatumia sheria ipi hasa kwani huko Swiss wanataka kujua kuhusiana na Richmond!... Kama ilikuwa kampuni hewa swala sio kuuliza wao kwa nini ilikuwa shirika hewa bali kujiuliza sisi kwa nini tuliweka mkataba na shirika hewa Marekani ambalo kama sikosei lilisajiliwa Tanzania na account yao ilikuwa ikipokea malipo..Pili kisheria, kama lilikuwa shirika hewa waliweza vipi kuingiza nchini hizo generators na zikaanza kazi wakati tukifahamu ni shirika hewa..

Njew ya yoyte haya Dorwan's haihusiki na kabla hawajanunua mkataba sisi tuliwatazama uwezo wao na kupitisha mabadilishano..

Tulipokubali mabadiliko ni hatua ya kuonyesha hatua ama niseme hukumu yetu ktk kuliondoa shirika hewa badala ya kulifikisha mahakamani, hivyo Dorwan's kisheria tumeichagua sisi wenyewe...

Kwa lugha ya mtaani mkubwa wangu unaweza kumtumia ndugu ama rafiki yako kufunga ndoa hata kama yeye sio mme wa kweli.. Kisheria ndoa hiyo inakubalika maadam umeanguka na mke kaanguka sahihi na imekuwa registered..
 
Du, mkuu Mkandara umeweka issue nzima kwa uwazi mkubwa sana. Itakuwa miujiza kama kina Rostam wasipopate hizo hela kutoka Tanesco sababu ujanja wa kumove mkataba kwa Dowans umeua soo la richmond kisheria na kwa kweli hapa ndio kazi ipo.

Swali rahisi, Kwani Dowans ofisi yao iko wapi?? Wameshafanya mkataba gani mwingine popote duniani???

Ukweli ni kuwa Dowans nayo ni kampuni hewa kwani haipo popote physically yaani inaexist kwenye makaratasi tu.

Kwa nini kila siku tunadeal na kampuni ambazo ndio wanafanya jambo kwa mara ya kwanza??
 
Kitu kimoja ambacho watu wengi hawajui ni kwamba Tanesco walipobid kununua mitambo ya Dowans,walikuwa wamekwishasuka dili na Rashid[Tanesco] na Ngeleja[Alikuwa mfanyakazi wa Rostam-Vodacom]; sasa kwa Tanesco[ read Rashid] kuweka injuction, na Dowans kufungua kesi Paris ni mpango uliosukwa na hao jamaa kutuangamiza wadanganyika kwani lawyers wa Tanesco will collude na hao wa Dowans ili Tanesco ishindwe na kuwalipa dowans mamillion ya dola!! Kitu cha msingi ni file countersuit kuonesha kwamba Dowans haikuwa kampuni halali kwaqhiyo haikustahili kulipwa fedha zote walizolipwa.
 
Sahihisho dogo tu mkuu Mkandara... aliyekuwa AG wakati wa Lowassa ni Mwanyika na si Chenge. lakini ufafanuzi wako ni mzuri sana, Umeweka wazi kwa kiasi fulani ni jinsi gani ambavyo Tanzania inaelekea kupoteza mchezo huu. Kosa tulilolifanya ni kutovunja mkataba wakati tulipobaini kuwa Richmond ni hewa. pale ndipo palikuwa pa kuchukulia point. lakini sasa tumeuvaa mkenge kwa sababu Dowans kama kampuni/shirika hawana matatizo yoyote, na mkataba waliorithi nao hauna matatizo yoyote. Ukichunguza kwa undani, katika kesi ambayo Dowans wamefungua, Richmond, ambayo sisi ndiyo tulikuwa na matatizo nayo, haihusishwi kwa karibu. Hivyo hapa sarakasi ni serikali vs Dowans, yale majigambo yetu kuhusu Richmond wala hayawezi kutusaidia kwenye kesi hii, tujiandae tu kuwalipa hawa wajanja fedha zetu

Watanzania tuache woga, hii sio kesi ya hoja. Tatizo sio mikataba ila ni ukweli usiofichika kwamba hii ni sinema inayoonyeshwa na serikali kwa wananchi wake, wanajua wanachokifanya. Richmond ilikuwa feki na maana yake mkataba wake kwa vyovyote ulikuwa batili, wakashindwa kutoa huduma kulingana na mkataba huo feki, kuhamisha mkataba kutoka Richmond kwenda Dowans nayo haikuwa halali pia. Huo uhalali wa mkataba wa Dowans unatokea wapi? "Uhalali wa mkataba unatatokana tu na uhalali wa misingi yake"
 
Yebo Yebo,
Nakubali maneno yako lakini unatumia sheria ipi hasa kwani huko Swiss wanataka kujua kuhusiana na Richmond!... Kama ilikuwa kampuni hewa swala sio kuuliza wao kwa nini ilikuwa shirika hewa bali kujiuliza sisi kwa nini tuliweka mkataba na shirika hewa Marekani ambalo kama sikosei lilisajiliwa Tanzania na account yao ilikuwa ikipokea malipo..Pili kisheria, kama lilikuwa shirika hewa waliweza vipi kuingiza nchini hizo generators na zikaanza kazi wakati tukifahamu ni shirika hewa..

Njew ya yoyte haya Dorwan's haihusiki na kabla hawajanunua mkataba sisi tuliwatazama uwezo wao na kupitisha mabadilishano..

Tulipokubali mabadiliko ni hatua ya kuonyesha hatua ama niseme hukumu yetu ktk kuliondoa shirika hewa badala ya kulifikisha mahakamani, hivyo Dorwan's kisheria tumeichagua sisi wenyewe...

Kwa lugha ya mtaani mkubwa wangu unaweza kumtumia ndugu ama rafiki yako kufunga ndoa hata kama yeye sio mme wa kweli.. Kisheria ndoa hiyo inakubalika maadam umeanguka na mke kaanguka sahihi na imekuwa registered..

Kikubwa kwa maelezo yako Mkuu Mkandara ni kwamba serikali imetuuza, ni yale yale kwamba serikali inakijua inachokifanya. Tunarudi palepale kwamba uongozi wetu umeoza na hata hii inayoendelea sasa ya kuwakamata kamata akina Yona na wenzake ni politics tuu hakuna lolote la haja hapo.

Mimi nina furaha kwa kiasi fulani kwamba wananchi wengi wasiojua nini kinaendelea katika nchi hii watapunguza hasira zao kwa kuona kwamba serikali inafanya kazi.
 
Thanks kwa wote mnaotufafanulia hii issue kwa undani hopefully will help to tackle mafisadi wote and to bring discipline to our leaders which was missing since our independence.
 
Hehehehe yangu macho maana naona movie ya kumkamata Lowassa na Rostam hiyooo ndio inataka kuanza tunamalizia hili trailer la Epa na Alex Stewart then movie lenyewe linaanza, noja nitafute coca yanngu mie mapemaaaa
Duh kama kulikuwa na kahuruma kidogo kutoka kwa muungwana naamini kataisha wamejichimbia kaburi let me take my wisky nibaki kusikiliza
 
I think Mr.Pesident has every tool to make or break the future of our country if he really care about the country but if his consern is for the party then we screwed because he can't be both.If the option is to take CCM to the toilet for the future of our children,then go ahead Mr.President.Rebuilding CCM is not an easy task once we have people like Kingunge.
 
Naona Gemu la RICMOND bado bichi, hivi kwanini Muungwana asiwaweke Rostam na Edo kwenye kachumba kadogo kwa kuhujumu uchumi?

Mkuu hiyo haisaidii kitu labda kwa kuwaonea au kuwatisha
Kwa kifupi washalikoraga, hiyo capacity charge ipo kwenye mkataba na walitakiwa walipe Tanesco hawajalipa obvious kuna chance Dowans kushinda kesi sasa wakihold hiyo mitambo hiyo fine yaketutatafutana
 
Akilimtindi,
Maneno yako safi kabisa na ndivyo wengi wetu tunavyoamini lakini kwa jinsi Kikwete anavyofanya mambo yake, sauti zenu na hasa hapa Jf zinaweza kabisa kumshtua.. Unajua tena yawezekana hana washauri wazuri..

Kuhusiana na swala la Kina Jeetu, Yona na Mramba mkuu wangu kusema kweli binafsi nayachukulia kama maajabu ya Kikwete.. iwe changa la macho ama laa siwezi kutoa hukumu maadam kesi bado ipo mahakamani, nitaendelea kujenga tumaini zaidi..

Sasa tukitumia lugha ya kiungwana nadhani tusitumie jina la CCM hivi sasa bali majina ya mahusika kama CCM wenyewe wanavyodai..Kesi ya Dorwan' kwenda Uswiss imetupa kila sababu ya kusimamisha kesi ya Richmond ndani ya nchi na kama kweli Kikwete amepania kusimamisha haki na sheria ndani ya nchi basi huu ndio mwanzo mzuri ambao kila mtu aliutegemea..

Lowassa na Rostam wasimame kizimbani, hapo atakuwa kasafisha dhana ya watu kama sisi na jina la chama chake halitatumika kama mhuri wa machafu yote yaliyotokea..
 
CCM wasiruke the fact is serikali imekuwa ikiendeshwa ki namna hii since tulipopata uhuru under CCM na wahusika wameweza kukwepa responsilities zao for so long,walijitokeza viongozi waadilifu wengi tu lakini system iliwabadilisha na wengine walibaki na uadilifu lakini majority walishindwa then guys we need a real change this is not a joke,we are suffering now and we shouldn't let our kids to suffer the same way we do for others mistakes and if we don't call mistakes there is no way we can correct them.
 
nafikiri ili suala , kamati ya zinazo husika katika bunge iwe kamati ya mashirika ya umma, sheria, fedha etc, waombe details zake na kuangalia uwezekano wa kushinda hizo kesi au ndio hivyo tunapelekwa machinjioni.bila kujijua. Maana wao angalau wata pewa details za kutosha kuliko sisi hapa tunavyo liona.
Pia naunga Mkono Rev, pale alipo sema Dr slaa naona unachungulia, sasa kupitia hilo tundu au dirisha naona ni wakati muuafaka wabunge kupitia kamati zao wakaliangalia hili suala kabla ya kikao kijacho cha januari na kabla mambo hayajaenda mrama.
 
Kwa maelezo haya nakubaliana na Njia ya mkatao anayoshauri Kichuguuu, kwa sababu inaonyesha wazi baadhi ya watu ndani ya serikali wanataka bado kuhakikisha Dowans wananufaika na pesa na wavuja jasho wa Tanzania. Hivyo kwa kutumia sheria kuna uwezekano mkubwa tukauvaa mkenge. Afterall Wafaransa wana uchungu gani na nchi kama Tanzania? Hao majaji wakikatiwa na kuahidiwa mgawo baada ya kushinda kesi watakuwa na tatizo gani.Kama Uingereza walijua kuwa Rada wanayotuuzia sisi taifa masikini haikuwa tunayostahili na bei yake ilikuwa juu sana, lakini bado wakaona tuinunue,unategemea nini kwa Mfaransa??
Kama mkataba wa Richmond uligundulika ni feki kwa mujibu wa kamati then kuurithi mkataba huo hakuufanyi usiwe feki. Ni kuwa DOwans walirithi mkataba ambao ni batili

Mkuu sio majaji watakao tuhanithi ni hao hao waliopo Tanesco na Wizarani
Sasa Wanazuia hiyo mitambo kwa faida ya nani jee wakishindwa kesi itakuwaje kama ni kufuata ushauri wa mwanasheria wao ni bora watafute mwingine tuu
Hili tumeshalikoroga kabisa kwanza hata hiyo hasara waliyotupa watanzania inashinda hata ya Alex stewart
 
kwanza hawa TANESCO hawaeleweki!!! mara wanataka kuinunua mitambo walipokataliwa ndo wameizuia... wangeinunua wangezuia nini!!

pili there is very serious legal issue here which the government has decided to overlook!!! mkataba kati yake na Richmond ulikuwa batili maana Richmond haikuwepo kisheria na kwa hiyo Dowans hawawezi kurithi kitu ambacho hakipo. serikali kwa hasara iliyoingia ingetaifisha hiyo mitambo maana hakuna wa kuwashitaki as Richmond legally does not exist
 
Mkuu sio majaji watakao tuhanithi ni hao hao waliopo Tanesco na Wizarani
Sasa Wanazuia hiyo mitambo kwa faida ya nani jee wakishindwa kesi itakuwaje kama ni kufuata ushauri wa mwanasheria wao ni bora watafute mwingine tuu
Hili tumeshalikoroga kabisa kwanza hata hiyo hasara waliyotupa watanzania inashinda hata ya Alex stewart

Mkuu hapa mimi nilikuwa kwanza nazungumzia ushauri wa Mkandara wa kuwa akuanzae Mmalize. Tutakapokuabaliana kwenda huko Paris kwenye hii kesi tunauhakika gani kuwa tutapata haki kwa watu ambao hawana uchungu na nchi yetu nikatolea mfano Uingereza kwenye ununuzi wa RADA.

Kutaifisha hiyo mitambo ni suala ambalo mimi binafsi naliunga mkono na si kuinunua. Kwa kuwa ilionekana kuwa serikali iliingia mkataba na Kampuni hewa( huku wao wakidai ni kampuni halali).Kisheria mkataba uligundulika ni batili. Lakini kwa ubatili huo huo ikaja kampuni halali kurithi mkataba batili, hakujafanya ubatili wa mkataba uwe halali eti kwa kuwa tu DOWANS ni kampuni halali na ilifuata tararibu zote kurithi mkataba Batili. Sisi tuliingizwa mkenge na vilevile DOWANS wameingizwa mkenge. Sasa sisi lazima tushikilie hiyo mali.
 
Yebo Yebo,
Nakubali maneno yako lakini unatumia sheria ipi hasa kwani huko Swiss wanataka kujua kuhusiana na Richmond!... Kama ilikuwa kampuni hewa swala sio kuuliza wao kwa nini ilikuwa shirika hewa bali kujiuliza sisi kwa nini tuliweka mkataba na shirika hewa Marekani ambalo kama sikosei lilisajiliwa Tanzania na account yao ilikuwa ikipokea malipo..Pili kisheria, kama lilikuwa shirika hewa waliweza vipi kuingiza nchini hizo generators na zikaanza kazi wakati tukifahamu ni shirika hewa..
Njew ya yoyte haya Dorwan's haihusiki na kabla hawajanunua mkataba sisi tuliwatazama uwezo wao na kupitisha mabadilishano..
Tulipokubali mabadiliko ni hatua ya kuonyesha hatua ama niseme hukumu yetu ktk kuliondoa shirika hewa badala ya kulifikisha mahakamani, hivyo Dorwan's kisheria tumeichagua sisi wenyewe...
Kwa lugha ya mtaani mkubwa wangu unaweza kumtumia ndugu ama rafiki yako kufunga ndoa hata kama yeye sio mme wa kweli.. Kisheria ndoa hiyo inakubalika maadam umeanguka na mke kaanguka sahihi na imekuwa registered..


Huu ndio umafia haswa...unatengeneza dili linalokupa hela hata kila kona, yaani sisi hapa watawala wetu wameiweka nchi katika mazingira ya kulipa tu. Hawa Dowans wapo kwenye winning side all the way.
 
ICC Paris inasema kwamba it is a standard arbitration clause that any dispute arising out of or under this contract shall be settled by arbitration in accordance with the rules of the CHAMBRE ARBITRALE DE PARIS (61, Bourse de Commerce, 2, rue de Viarmes, 75040 PARIS cedex 01, Tel:+ 33 (0)1 42 36 99 65, Fax : + 33 (0)1 42 36 08 54), of which both the Parties hereto declare to be cognisant and which they hereby accept .

Kutokana na hapo Juu ni wazi kwamba Tanesco hawana cha kujibu hapa kama hawaikubali au hawaikukubali tangu mwanzo hiyo ICC Paris , na kama wasipoikubali au kutoitambua basi ina maana kwamba hiyo kesi ya Dowan Hakuna , case ni Void ab nitio.

Kama TANESCO wanaikubali ICC Paris, ndani ya article 7 ya ICC Paris, wanachotakiwa ni either kujiwakilisha wenyewe na kutoa facts za case kama ambavyo Bunge la Tanzania chini ya Mwakembe lilivyogundua madudu ya Dowans au kumteua mwanasheria toka popote pale duniani na kuwawakilisha , na hili likisha fanyika basi hawa waliochaguliwa inabidi pia chini ya Arbitration Chamber of Paris organise arbitration in conformity with its legal status and follow regulations that define the different applicable rules during arbitration proceding.

Kwa maelezo zaidi kuhusiana na ICC Paris soma hapa chini.
Chambre Arbitrale de Paris

Mkuu heshima mbele ningeomba msiweke cheap conclusion kwa hii issue kwani ni nzito inaweza kuwa kama ya Valambia.

Kwa taarifa yako TANESCO lazima watakuwa walikubali hich kipengele kama wakishindwa kuelewana waende ICC Paris na Tanzania ni signatory wa ICA kesi ya msingi ni capacity charge amayo walikubaliana wote sasa hivyi Tanesco hawataki kulipa wana jamii wenzangu mnaonaje hili.

Kuhusu uhalali wa Richmond ni kitu kidogo kwani ilihalalishwa Tanzania na kupata certificate of incentive from TIC kwa hiyo ni kampuni halali.

Kwa maono yangu hii itakuwa kama kesi Magufuli na Mansour wa mwanza kiwanja sio halali lakini kina hati halali.

Isitoshe kuna chance kubwa sana ya kutiwa dole na watendaji wa sasa kwani walitaka kununua kwanza baada ya kushikiwa bango wanaanza hayo mambo ya kuzuia mali za watu.

According to my experience kesi ikienda ICC kuna kipengele cha mshitaki kuweka Bond kama akishindwa hakuna haja ya kujua kwingi na kuzuia mitambo yao.
 
Mitambo ya Dowans yawavuruga wabunge

Na Joyce Mmasi
Mwananchi
Date::2/21/2009

MVUTANO mkali uliibuka jana katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma na maafisa wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuhusiana ombi la kununua mitambo ya kuzalisha umeme inayomilikiwa na Kampuni ya Dowans.

Baadhi ya wabunge wa kamati hiyo iliyokuwa chini ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe waliwabana maafisa wa Tanesco waliokuwa wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Dk Idrisa Rashid ili waeleze sababu iliyowafanya waamue kununua mitambo chakavu ya Dowans badala ya mipya.

Wabunge hao walionyesha wasiwasi wao kufuatia nia ya Tanesco kutaka kununua mitambo hiyo huku wakijua kuwa sheria ya manunuzi inazuia ununuzi wa mitambo chakavu.

Mbunge wa Bukombe, Emmanuel Luhahula, alihoji iwapo Tanesco na serikali hawana wazo mbadala zaidi ya kununua mitambo ya Dowans.

Zitto alimtaka Mkurugenzi wa Tanesco aieleze kamati mitambo ile inayotaka kununuliwa na shirika hilo ina ubora wa kiasi gani.

Akijibu baadhi ya hoja za wabunge, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dk Idriss Rashid kwa kushirikiana na timu ya wataalam wake, alisema mtambo mmoja ni mpya na mingine imetumika kwa takribani saa 800 kila mmoja.


Alisema mitambo hiyo inao uwezo wa kufanya kazi kwa miaka 10 bila kufanyiwa ukarabati na kwamba ikifanyiwa ukarabati inaweza kufanya kazi kwa miaka mingine 10 na kufikisha miaka 20.

Dk Rashid aliongeza kuwa shirika lake lilipata mkaguzi kutoka Ujerumani ambaye aliikagua mitambo na kutoa taarifa kuwa mitambo hiyo ni mizima na inao uwezo wa kuzalisha umeme.

Alisema jambo kubwa linaloisukuma Tanesco kushinikiza ununuzi wa mitambo hiyo ni hali ya ukame inayotarajia kuikumba nchi katika kipindi cha miezi kadhaa ijayo.

Zitto alipomtaka Mkurugenzi huyo aeleze mbadala endapo bunge halitaridhia ununuzi wa mitambo hiyo, Dk Rashid alisema hakuna chaguo jingine ni ama kununua mitambo hiyo au nchi kuingia katika giza.

“Nafikiri suala hili ni la kitaifa, tunapaswa kuliangalia kwa uzito wake, au tuendelee hivi tulivyo na kuwa na shortage (upungufu) ya umeme au kununua mitambo iwe ya Dowans au mingine yoyote, lakini tukumbuke kuwa tukiamua kukodi itabidi kuendelea kulipia capacity charges (gharama ya mitambo),” alieleza Dk Rashid.

Alisema mitambo hiyo inauzwa kwa Sh60 bilioni, huku wakiamua kununua mitambo mipya, mbali na kulipia Sh90 bilioni, lakini mchakato huo utachukua muda mrefu hadi kukamilika hali aliyosema italiingiza taifa kwenye uhaba wa umeme.

Kwa upande wake, Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), Peter Serukamba alitetea ununuzi wa mitambo hiyo akisema kuibana Tanesco ni kuionea kwani hali iliyopo ni kuwa shirika hilo limefungwa kamba na serikali.

“Tayari wametuambia, kuna shortage (uhaba) ya umeme, tunatakiwa kununua mitambo au tuingie kwenye shortage, sasa tunataka nini tena? Tatizo letu sisi tumeamua kuiacha siasa ndio itoe maamuzi, ukiisoma hii taarifa yao hutakuwa na swali lolote la kuwauliza,” aliongeza Serukamba.

Alipokumbushwa azimio la bunge lililokataza kununua mitambo hiyo, mwanasheria wa shirika hilo, Subira Wandiba alisema hana kumbukumbu zozote azimio hilo isipokuwa anachojua yeye sheria hairuhusu kununua mitambo chakavu.

Hata hivyo, baada ya mvutano mkali kamati hiyo iliamua suala hilo lijadiliwe na Kamati ya Nishati na Madini ili waweke msimamo wa pamoja kuhusu mitambo ya Dowans, IPTL, Mradi wa Umeme wa Upepo Singida, Mradi wa Kinyerezi na ule wa Mtwara.
 
Last edited:
............watufanyie CBA...........tuone faida/hasara ya kununua mitambo michakavu/mipya............however hiyo isije ikawa precedence ya kununua mitambo chakavu...........we don't wanna go there
 
Back
Top Bottom