Dowans: Another Richmond in making?

Dowans: Another Richmond in making?

Idrisa Rashid Dowans imekupa nini?

Na Mbasha Asenga
Mwanahalisi~Maslahi ya Taifa Mbele

TANZANIA yetu isiyoishiwa sakata, safari hii imethibitika kwamba lile sakata la Richmond ambalo lilirithiwa na Dowans katika mradi wa kuzalisha umeme wa dharura wa megawati 100, halijafa na kwa kweli limekataa kufa.

Ni jambo la kustaajabisha kusikia kwamba Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), Dk. Idriss Rashid, amewasilisha hoja mbele ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, akitaka uamuzi wa serikali utazamwe upya.

Serikali kupitia Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, ilitangaza kwamba imejitoa katika mchakato wa tenda ya kununua mitambo ya Dowans.


Ama kweli Dowans imekataa kufa. Haifi na wanaotaka kuiuwa watakufa wao! Naam. Juhudi zimeanza na sasa zimeshika kasi kuhakikisha kwamba kwa vyovyote Dowans haiwezi kupata hasara katika mkataba uliovunjwa.

Wanataka mambo mawili, Tanesco wakubali yaishe wanunue mitambo yake, au wasubiri kulipa fidia baada ya kesi iliyofunguliwa dhidi ya serikali kuamuliwa.

Awali, Richmond ilipouza mkataba wake kwa Dowans tena katika mazingira tatanishi, Watanzania waliambiwa habari ya Richmond imefungwa, hakuna tena tija kuijadili kwa sababu tayari umeme ulikuwa unazalishwa.

Waliokuwa na akili zao kichwani wakatulia na kutafakari, inakuwaje bwana mkubwa wakati huo, Edward Lowassa, anasema maneno hayo? Mambo yakafunikwa kama ambavyo imekuwa kawaida ya nchi hii.

Lakini mwishowe jipu likaiva na Richmond ikatumbuka vibaya. Baraza la Mawaziri lote likaenda na maji. Katika hali ya kawaida, Dowans ingeogopwa, ingekimbiwa kwa kuwa ni nondo mbaya, lakini wapi, watu wameendelea kuikumbuatia.


Miezi kadhaa ilipita tangu Februari 2008 maazimio ya Bunge yalipopitishwa hadi mkataba wake ulipovunjwa rasmi Agosti. Tangu kuvunjwa kwa mkataba huo, juhudi imekuwa ni moja tu, Tanesco ibebe Dowans kama si moja kwa moja basi hata kwa mlango wa nyuma.

Mwaka jana joto la Tanesco la kutaka kununua mitambo ya Dowans likapanda hadi pale wabunge walipotoa angalizo kwa Waziri wa Ngeleja, kwamba kununua mitambo ya Dowans ni kuvunja azimio la Bunge na kukiuka sheria ya manunuzi ya umma (PPRA).

Miezi mitatu tu imepita tangu serikali kupitia kwa Waziri Ngeleja itamke kwamba imejitoa katika mchakato wa zabuni ya kununua mitambo ya Dowans, lakini katika ujasiri wa aina yake Dk. Rashid anaweka wazi kwamba bado wana matamanio hayo. Je, ujasiri huu ni wa nini, na unatokana na nini?


Tanesco shirika ambalo linahemea hewa ya ziada kutokana na kukabiliwa na matatizo makubwa ya kiundeshaji, ikiwa haina hata uwezo wa kutosheleza wakazi wake wa mjini kwa umeme achilia mbali vijijini, inapata ujasiri wa kutaka kuendesha ligi ya kugombea mitambo ya Dowans ambayo ina kila shaka kwamba ni biashara chafu!

Kwa nini Dk. Rashid ana ujasiri huu? Si siri tena kwamba kiongozi huyu aliyepata kuongoza taasisi nyeti za fedha nchini, kuanzia Mkurugenzi Mkuu wa iliyokuwa Benki ya Taifa Biashara na hatimaye Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), amethibitika kushiriki katika mchezo mchafu.

Makachero wa Uingereza wa kikosi cha Kuchunguza makosa makubwa ya jinai (SFO) wamemtaja Dk. Rashid sambamba na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati wa utawala wa Rais Benjamin Mkapa na pia Waziri katika serikali ya Awamu ya Nne, Andrew Chenge, kuwa wana harufu ya rushwa ya rada ya Tanzania.

Dk. Rashid anatuhumiwa kupokea kutoka kwa Chenge Dola za Marekani 600,000 zinazohisiwa kuwa mgawo wa watu walioshiriki kufanikisha ununuzi wa rada hiyo iliyogharimu serikali ya Tanzania fedha za walipa kodi Sh 40 bilioni.


Je, kweli kiongozi wa nama hii, yaani Dk Rashid pamoja na kujua wazi kwamba anachunguzwa kwa tuhuma hizo, na hata baada ya kuelezwa na kusoma magazetini kuhusu tuhuma hizi, amemaua kukaa kimya, lakini kibaya zaidi akiendelea kukalia ofisi umma.

Dk Rashid anadaiwa kuwa na uhusiano wa karibu na mmiliki wa Dowans, mbunge wa Igunga na mfanyabiashara, Rostam Aziz. Uhusiano wao unakwenda ndani katika uendeshaji wa shughuli za kibiashara kwenye kampuni moja nyeti nchini.


Kwa maana hiyo kuendelea kwa shinikizo la kutaka Dowans inunuliwe bila kuzingatia maslahi ya taifa, ni kielelezo kwamba mbinu chafu zimejichimbia ndani ya Tanesco.

Ujasiri huu pia wa Tanesco kupitia kwa Dk. Rashid wa kutaka kununua Dowans, ni sawa na jaribio la kutikisha Bunge.

Ndiyo kutikisa Bunge! Jaribu kutafakari. Bunge limetoe azimio kutaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Johnson Mwanyika, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Edward Hosea na waliokuwa mawaziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha wachunguzwe.

Je, kama sio kile kinachoitwa, "ujasiri wa kifisadi" Dk Rashid anapata wapi ujasiri wa kuendelea na matamanio ya Dowans?

Huu ni ujasiri ambao hauwezi kuelezewa katika sura ya kiuwajibikaji ndani ya shirika la umma, ni jambo linalohitaji utafiti zaidi kubainisha nguvu hizi zimejiegemeza wapi?

Kwa upeo wangu ni nguvu za fedha, ni nguvu za kutaka kuvuna, liwe liwalo ni lazima Tanesco ikamuliwe hadi ibaki hoi bin taaban.

Inawezekana Dk. Rashid na Tanesco yake wana hoja, lakini katika dunia hii hivi mitambo ya kufua umeme kwa kutumia gesi ni ya Dowans tu? Kwa nini anaing'ang'ania Dowans kwa kiwango hiki?

Je, kuna asilimia ngapi za kamisheni kama za rada? Ipo shida moja ndani ya nchi hii. Ujasiri wa ajabu; kukosa soni; kufanya uhalifu wao kweupe kana kwamba wamepewa kibali cha kutokuwajibishwa kwa maovu yao.


Hali hii ndiyo inawafanya wote wanaotuhumiwa makosa makubwa ya kuikosea jamii, kujitafutia njia nyepesi na za kitoto kabisa kujisafisha; wengine kusajili magazeti ili kujisafisha na kuandama wengine eti kulipiza kisasi; wengine kutaka jamii iamini kwamba Tanzania haina mtu safi hata mmoja.

Nafikiri wakati sasa umefika kuamua kuzaliwa upya kwa taifa hili, na hakika halitazaliwa bila kwanza wahalifu wote, watuhumiwa wote waikosoe jamii katika mikataba kama ya rada, Richmond, IPTL na mingine mingi kufikishwa mahakamani na kufilisiwa ili kutoa ujumbe mmoja tu kwamba WIZI HAULIPI.

Hatua ya Dk. Rashid na serikali kung'ang'ana na Dowans ni dalili tosha ya kwamba kuna "Wizi mtupu."
 
Dowans imeibuka tena katika vyombo vya habari na mmiliki/wamiliki wake wanampush yule fisadi ailiyepekwa kuiongoza Tanesco ainunue mitambo yake. Hili ni gumu kutokana na kesi zilizo mahakamani, ingawa kwa mafisadi hili litawezekana tu.

Swali langu ni hili: Hawa wamiliki wa Dowans ni kina nani, mbona hata hawatajwi katika sakata linaloendelea. Huyo Dr Idris Rashid, na zile kamati mbili za Bunge zinazopingana hazielezi ni nani wamiliki ambao wanasimama kidete kutaka kuiuzia mitambo hiyo mibovu kwa Watanzania kwa bei ya kifisadi. Katika habari zote za Tanesco kutaka kununua mitambo ya Dowans, magazeti hayataji nani mmiliki isipokuwa katika makala moja ya Mwanahalisi la wiki hii ilimtaja kuwa ni Rostam.

Fununu nyingine zinasema ni Rostam -- na kama hii ni kweli, inakuwaje wahusika wanapata courage ya ku-deal naye tena mtu huyu anayetajwa katika Richmond na Kagoda?
 
Dhamira ya Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) ya kutaka kununua mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura yenye uwezo wa kutoa megawati 100 inayomilikiwa na Kampuni ya Dowans, imezua mambo.

Hiyo imetokana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Dk. Harrison Mwakyembe, kutofautiana kuhusu suala hilo.

Tofauti kati ya Zitto, ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) na Dk. Mwakyembe Mbunge wa Kyela (CCM), imeibuka siku sita baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, William Shellukindo kutamka hadharani kuwa kamati yake haikubaliani na dhamira hiyo ya Tanesco inayoonekana kuungwa mkono na Kamati ya Zitto.

Shellukindo, ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli (CCM), alitangaza msimamo huo wa kamati yake, siku moja baada ya Tanesco kuripotiwa na vyombo vya habari ikiendeleza dhamira yake mbele ya Kamati ya Zitto ya kutaka kununua mitambo hiyo.

Tofauti kati ya wabunge hao, ambao katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, wametokea kuwa kivutio kikubwa kwa Watanzania kwa ujasiri wao wa kupambana na ufisadi na mafisadi nchini, imedhihirika baada ya Dk. Mwakyembe, ambaye kueleza hisia zake kwamba, ameshangazwa na hatua ya Kamati ya Zitto kuzungumzia suala la Dowans wakati si kazi yake.

``Kazi ya Kamati ya Zitto ni kuangalia mahesabu na siyo sera. Nadhani Zitto anapaswa kusoma kanuni za Bunge aelewe,`` alisema Dk. Mwakyembe katika mahojiano maalum na Nipashe juzi.

Dk. Mwakyembe alisisitiza kuwa maamuzi yaliyofikiwa na Kamati ya Madini na Nishati kuhusu suala hilo, hayawezi kamwe kupingwa na kamati yoyote hivyo, akamshauri Zitto kusoma kanuni za Bunge.

Naye Zitto, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, alisisitiza kuhusu uamuzi wa kamati yake wa kumuomba Spika wa Bunge kibali ili aruhusu kuitisha kikao cha kamati zote mbili (ya Hesabu za Mashirika ya Umma na Nishati na Madini), serikali, Tanesco na Mamlaka ya Usimamizi wa Manunuzi ya Umma (PPRA) ili wajadili na kufikia muafaka wa pamoja kuhusu suala la kununua mitambo ya Dowans ili kuepuka kamati kupingana.

Alisema wazo la Dowans lilikuja baada ya kamati yake kukagua matumizi ya Tanesco na kugundua kuwa katika kila Sh. 100 inazopata shirika hilo, Sh. 84 zinakwenda kwa makampuni yanayoiuzia umeme.

``Hivyo, ndio tukaamua kuomba kukutana na Kamati ya Nishati na Madini tujadili hiyo hali kwa pamoja ili nchi isije kukumbwa na giza,`` alisema Zitto.

Alisema kazi ya Bunge si kuingilia utendaji wa serikali bali kusimamia.

``Hata hivyo, inaonekana Bunge linataka kuingilia utendaji wa serikali, linatakiwa lisimamie tu,`` alisema Zitto na kuongeza: ``Kamati ya kina Mwekyembe haikusikiliza Tanesco, hivyo tunaiomba ifanye hivyo``.

Zitto alisema suala lolote lenye maslahi ya umma yuko tayari kukosolewa, hawezi kamwe kuingiza siasa.

``Hivi kweli Watanzania wako tayari kukaa katika giza? Kamati yangu ina nia njema kwamba kamati zote mbili ziwasikilize ndio tutoe uamuzi ambao utakuwa na maslahi kwa taifa kuliko kulumbana,`` alisema

Alisema kwa hali ilivyo sasa taifa linakabiliwa na upungufu wa megawati za umeme zaidi ya 100, hivyo haoni sababu gani nchi iingie katika gharama kubwa za kuweza kuangiza mitambo wakati tayari ipo ya Dowans.

``Kwanza tukianza kuagiza mitambo kutakuwa na gharama kubwa ambazo tutalipa, mawazo yangu ni kwamba tuangalie uwezekano wa kununua mitambo ya Dowans ili nchi isije kuingia katika giza kama Tanesco walivyotuambia. Tukiingia katika giza uzalishaji utakupungua na uchumi utatetereka,`` alisema Zitto

Mimi Jumatatu wiki hii, Nipashe ilimkariri Shellukindo akisisitiza msimamo wa kamati yake wa kupinga dhamira hiyo ya Tanesco kwa vile inakiuka taratibu na haina maamuzi ya kununua mitambo hiyo.

Shellukindo, alisema mwenye maamuzi ya kununua mitambo hiyo ni serikali kama imeona kuna dharura ya kufanya hivyo.

Hata hivyo, alisema taratibu zilizopo zinataka suala hilo lifikishwe kwanza bungeni ili likajadiliwe na kupata baraka za Bunge.

Alisema ipo pia, sheria ya manunuzi inayozuia kununua mitambo chakavu kwa vile hatua hiyo ni ya hatari.

Kutokana na hali hiyo, alisema haoni kuwa ni busara kung’ang’ania kutaka kununua mitambo ya Dowans kabla taratibu zinazohusika hazijafuatwa na kwa kuzingatia pia, kwamba, mitambo ya kampuni hiyo haijulikani ilitumika kwa muda gani.

``Tanesco wanadai kuwa Dowans wanalo jenereta jipya. Lakini mitambo yao (Dowans) iliingizwa nchini mwaka 2006 na utekelezaji ulianza Desemba 2007. Sasa hilo jenereta linaweza kuwa jipya? Na hata yale (majenereta) mengine hatujui kama ni mapya,`` alisema Shellukindo.

Alisema inashangaza kuona Tanesco iking`ang`ania kutaka kununua, huku mkononi mwake ikiwa na amri ya mahakama iliyoomba kuzuia kuuzwa kwa mitambo ya Dowans kwa vile inaidai kampuni hiyo.

``Hatuna uhakika Tanesco wanaidai nini Dowans, hilo haliko wazi, tunataka tujue kwanza hilo. Hata hivyo, kama hilo lipo basi si wangekubaliana wabadilishane badala ya kununua,`` alisema Shellukindo.

Tanesco iliifikisha dhamira yake hiyo kwenye Kamati ya Zitto miezi miwili baada ya Kamati ya Nishati na Madini inayoongozwa na Shellukindo, kupinga suala hilo mbele ya Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja Desemba, mwaka jana.

Awali, Zitto alikaririwa na Nipashe Jumatatu wiki hii akisema kuwa katika kikao kati ya kamati yake na Tanesco kilichofanyika jijini Dar es Salaam Jumamosi wiki iliyopita, uongozi wa shirika hilo walitoa hoja za msingi kuhusu dhamira ya shirika ya kutaka kununua mitambo ya Dowans.

Zitto alitaja sababu nyingine ya kamati yake ya kuomba kibali hicho kwa Spika, ni kwa vile Kamati ya Nishati na Madini, haikutoa nafasi ya kukutana na Tanesco ili waeleze kwanini wanataka kununua mitambo hiyo ya Dowans.

``Walikutana tu na Waziri Ngeleja wakapinga Tanesco kununua mtambo huo wa Dowans,`` alisema Zitto, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Alisema pia, watatumia fursa ya ruhusa hiyo Spika kujadili kuhusu hatma ya umeme wenye megawati 300 wa Mtwara baada kampuni ya Barick kujitoa na umeme wa upepo wa Singida.


SOURCE: Nipashe
 
Suala ninojuliza Hivi tangu waone huo upungufu wa uzalishaji umeme Miezi miwili iliyopita(tangua shellukindo na kamati yake ilipotembelea) wamefanya
nini ili kununua mitambo mmbadala kabla ya kiza kuingia nchini??

Je wanasubiri siku za mwisho ili wapate kisingizio kwamba ndio njia pekee ya klinusuru taifa????

Dowans walisema walishapata mnunuzi mbona hawajamuuzia hadi leo????? ama aliingia mtini

Kuna wakati nilisikia TRA walizuia Dowans kutoa mitambo kwa sababu ya kodi, je walishalipa kodi waliokuwa wanadaiwa????? Je serikali inashirikianaje na watu wasiolipa kodi????

Kuna shida kwenye uongozi wa Tanesco na hawa dowans wana mkono mrefu serikalini kiasi cha kuwafanya watu washindwe kutimiza wajibu wao,
Hivi kina Dowans ni Nani???????
 
Serikali yasitisha kuinunua Dowans
Mwandishi Wetu
Daily News; Wednesday,December 17, 2008 @21:15


Serikali imesimamisha mpango wake wa kununua mtambo wa kufua umeme wa Kampuni ya Dowans ambayo mkataba wake umefutwa. Uamuzi huo umetokana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, kupinga mpango huo kupitia kikao kilichofanyika kati yake, Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme (Tanesco) Jumapili iliyopita.

Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alisema pamoja na kwamba kikao hicho kilielezwa faida ambazo walidhani zingepatikana kutokana na kununua mtambo huo, lakini wameona kuwa penye mjadala lazima pawapo makubaliano.

Ngeleja aliyekuwa akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, alisema wametafakari maoni ya Kamati hiyo ya Bunge na kujiridhisha kwamba ni vyema Tanesco wasishiriki kwenye zabuni ya ununuzi wa mtambo huo wenye mashine tano.

Akinukuu hoja za Kamati ya Bunge, Waziri huyo alisema wizara yake ina imani kubwa na kamati hiyo na kuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo kwa ustawi wa taifa. Alisema wamekubali ili kwenda pamoja katika kukabili changamoto zinazokabili utoaji huduma ya umeme na siyo kuwakanganya wananchi kwa mijadala.

Kwa mujibu wa Ngeleja, pamoja na faida au sababu zilizoelezwa katika kikao hicho kuhusu ununuzi wa mtambo huo, kamati ilipinga kwa kusema kuwa kufanya hivyo ni kukiuka maelekezo ya Bunge na Sheria ya Manunuzi ya Umma kwa vile mitambo hiyo siyo mipya.

“Serikali tayari imeshaiagiza Tanesco kutoshiriki kwenye zabuni ya kununua mtambo wa Dowans,” Ngeleja aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake na kusema walidhamiria kutumia Sh bilioni 70 katika ununuzi. Katika kuelezea mchakato wa kutaka kununua mtambo huo, Ngeleja alisema kabla ya wizara yake kuiruhusu Tanesco, ilipata kwanza ushauri kutoka Wizara ya Katiba na Sheria.

Alisema waliona pia ni busara kuishirikisha Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ili kushauriana juu ya suala hilo. Alisema, “Serikali ilifanya hivyo kwa nia njema na kwa kutambua umuhimu wa dhana shirikishi kati ya Serikali na Bunge na hasa kwenye maamuzi muhimu na nyeti yanayohusu maslahi ya taifa.”

Miongoni mwa sababu ambazo serikali ilitarajia kuzipata kutokana na kununua mtambo huo ni pamoja na kuziba pengo la uhaba wa umeme unaolikabili taifa. Kwa mujibu wa Ngeleja, kuna ongezeko la mahitaji ya umeme kwa wastani wa megawati 70 kwa mwaka.

Alisema mtambo huo wa Dowans wenye uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 112.2 ni sawa na mbadala wa umeme wote unaozalishwa na mabwawa ya Mtera, Hale na Nyumba ya Mungu kwa pamoja. Faida nyingine ilikuwa ni kupunguza gharama za kununua umeme kama kampuni binafsi itanunua mitambo hiyo na kuiuzia Tanesco kwa utaratibu wa Capacity Charge.

Awali akielezea hali ya uzalishaji umeme nchini, alisema haikidhi mahitaji yaliyopo. Wastani wa uwezo uliopo wa mitambo ya kuzalisha nishati hiyo ni megawati 542 ikilinganishwa na wastani wa mahitaji ya megawati 570. Alisema mfumo wa umeme wa gridi ya taifa unaendeshwa katika hali ya kutokuwa na nafasi ya kupumua; jambo linalosababisha kukatika kwa umeme mara kwa mara itokeapo hitilafu ndogo kwenye mifumo ya usafirishaji na usambazaji.
Dah,

Sometimes mambo haya yanachanganya akili sana.

Anyway, thanks to Daily News!
 
Haya jamani!tuwe tunaangalia na vyanzo vyetu vya habari.Tunaweza kuwapoteza wanajamii
 
Hivi ukinunua mitambo ya Dowans iliyoridhi Richmond kesi itakuwepo tena?Umegundua tapeli wako halafu unanunua vitu alivyotumia kukutapeli,mimi naona tamaa ya mali itatupeleka pabaya kwani sasa hivi kinachoangaliwa na viongozi wetu ni maslahi tu.Kama wabunge wanaowawakilisha wananchi nao wameingia kwenye mtego huu sasa nani mtetezi.Wabunge wa upinzani nao wanatetea kitu walichohusika kuweka azimio baada kama teule ya bunge kutoa ripoti kuhusu Richmond.
 
Hii habari sasa hivi itageuka kuwa kama ile ya LIYUMBA. CONTROVERSY OVER CONTROVERSY!

Sasa hapa ieleweke vp wananunua au??????
 
Hii habari sasa hivi itageuka kuwa kama ile ya LIYUMBA. CONTROVERSY OVER CONTROVERSY!

Sasa hapa ieleweke vp wananunua au??????
Nilichofanya hapa mkuu ni kuwakumbusha tulikotoka... Yani just connecting the dots! Hopefully wanisoma vema tu.

Kununua kwa sasa inavyoelekea HAKUKWEPEKI... Haijalishi outcome itakuwa nini lakini we have to face it (Ili nchi isiingie kwenye giza mwezi wa nne mzima!)
 
Nilichofanya hapa mkuu ni kuwakumbusha tulikotoka... Yani just connecting the dots! Hopefully wanisoma vema tu.

Kununua kwa sasa inavyoelekea HAKUKWEPEKI... Haijalishi outcome itakuwa nini lakini we have to face it (Ili nchi isiingie kwenye giza mwezi wa nne mzima!)


Nakupata vzuri mkuu, lakini si mkulu wa nchi na Hosea walituambia kipindi kile kwamba nchi haikuingia hasara yeyote. Sasa serikali/ Tanesco wanaogopa nini sasa?
 
Why not DOWANS: legal opinion
Among the factors which vitiate under The Law of Contract Act (LCA)is FRAUD and MISREPRESENTATIO. Effects of these two will render the contract to be voidable. The contract will be void ab initio once you discover there was a fraud or misrepresentation Ss. 17 and 18 LCA.

For anyone to enter into a contract there is something which we call capacity. S. 11 of LCA provides for who is competent to enter into a contract. Sub-section 2 says;

“an agreement by a person who is not hereby declared to be competent to contract is void.”

In the contract between RICHMOND and TANESCO there was a fraud and misrepresentations on then part of the Richmond. Second since Richmond was not in existence it had no capacity to enter into any form of contract. Since DOWANS inherited the Richmond’s contract, and since there was no legal contract, Dowans inherited un-existed contract which is not enforceable anywhere.

My stand; since the government incurred very big loss because all deeds which involved Richmond, and since Richmond has no legal existence, government has to confiscate the so called DOWANS turbines. Dowans has to sue Richmond and Richmond has to sue government. Since Richmond can’t sue or be sued there is no case.

Kwa hiyo hili la kununua mitambo halipo bali ni kuitaifisha. Maana ililetwa hapa kwa garama zetu na insurance tulilipia sisi na umeme hatukupata tukaingia hasara kubwa. Hii case serikali inipe niisimamie nitashinda tu

 
Ochu,

Unadhani haya mambo serikali yetu haijui! Wanajua sana lakini huu ni mwendelezo tu wa ufisadi.

Ingekuwa Uchina, hili lingekuwa limeisha zamani na wengine tumeshawazika! Nakumbuka Mh. Ndesamburo aliligusia hili bungeni!
 
Nimesoma gazeti la Nipashe nakastushwa na uungaji mkono wa Zitto kuwa serikali ni vema inunue mitambo hiyo. Kwa kuwa ni mwanachama wa JF, na kwa status yake miongoni mwetu, ni vema atufafanulie. Visingizio vya nia njema, nchi kuingia gizani havieleweki kwa madhara tuliyokwisha sababishiwa na richmond/dowans.
 
Why not DOWANS: legal opinion
Among the factors which vitiate under The Law of Contract Act (LCA)is FRAUD and MISREPRESENTATIO. Effects of these two will render the contract to be voidable. The contract will be void ab initio once you discover there was a fraud or misrepresentation Ss. 17 and 18 LCA.

For anyone to enter into a contract there is something which we call capacity. S. 11 of LCA provides for who is competent to enter into a contract. Sub-section 2 says;

“an agreement by a person who is not hereby declared to be competent to contract is void.”

In the contract between RICHMOND and TANESCO there was a fraud and misrepresentations on then part of the Richmond. Second since Richmond was not in existence it had no capacity to enter into any form of contract. Since DOWANS inherited the Richmond’s contract, and since there was no legal contract, Dowans inherited un-existed contract which is not enforceable anywhere.

My stand; since the government incurred very big loss because all deeds which involved Richmond, and since Richmond has no legal existence, government has to confiscate the so called DOWANS turbines. Dowans has to sue Richmond and Richmond has to sue government. Since Richmond can’t sue or be sued there is no case.

Kwa hiyo hili la kununua mitambo halipo bali ni kuitaifisha. Maana ililetwa hapa kwa garama zetu na insurance tulilipia sisi na umeme hatukupata tukaingia hasara kubwa. Hii case serikali inipe niisimamie nitashinda tu


Asante

Pia tuwaombe wanasheria wengine kaeni vizuri na mjipange vizuri .

Kesi hii inaweza kutumika kuitimua serikali iliyoko madarakani.Kinachotakiwa kufanyika endapo Tanesco na serikali wataridhia kununua hiyo mitumba wananchi kupitia mawakili kama wewe wamburuze kila aliyehusika kushabikia na kuidhinisha kununuliwa mitambo mitumba ya Dowans mahakamani kwa matumizi mabaya ya madaraka na kulitia hasara taifa na walipa kodi kwa kununua mitambo mitumba..Kesi hiyo inatakiwa iwe kama ile ya akina Liyumba,Yona ,Basil MRAMBA n.k na iongezwe vikorobwezo vingine.

Wakuwaburuza mahakamani iwe ni pamoja na wabunge kama Zitto Kabwe na kamati yake ya POROJO YA HESABU ZA SERIKALI,Waziri Ngereja,Mkurugenzi wa Tanesco,Raisi Kikwete na baraza lake la mawaziri (Kwa kuchekelea na kuachia uozo upite) na tume na kamati zao zinazojifanya zinajua kujenga hoja za utapeli za kuliza wananchi kwa maneno ya kijanja ambayo yamejaa misamiati ya uwongo.

Nitashereheka kuona Kikwete naye akipanda basi la magereza na kwa staili kama ile ya akina Yona,Mramba na Liyumba kama dili hili la Dowans serikali ikilipitisha.
 
Nimesoma gazeti la Nipashe nakastushwa na uungaji mkono wa Zitto kuwa serikali ni vema inunue mitambo hiyo. Kwa kuwa ni mwanachama wa JF, na kwa status yake miongoni mwetu, ni vema atufafanulie. Visingizio vya nia njema, nchi kuingia gizani havieleweki kwa madhara tuliyokwisha sababishiwa na richmond/dowans.

Gagnija,
Una hoja yenye mashiko. Haiwezekani suala hili ambalo limeumiza watanzania kiasi cha kutosha, leo Zito aje na kisingizio cha giza na msalahi ya taifa kushadadia ununuzi wa mitambo ya daowans. Kama aliyeanziasha hii thread alivyosema na inavyojulikana huu ulikuwa mkataba wa kifisadi na ambao hausimami kisheria.

Tumeozeoa mara nyingi kutishiwa kuwa kutakuwa na mgawo wa umeme ili watu wapate njia za kupitisha dili zao. Tanzania hakuna umeme wa uhakika tangu hapo, na wala hiyo mitambo chakavu ya dowans haitaondoa tatizo la umeme leo.

Hakuna, hakuna na hakuna busara hata kidogo katika hoja ya zito na kamati yake kuizinisha kununua mitambo hii ya Richmond. Zito katika hili amewaangusha Watanzania wenye kupenda nchi inayoendeshwa kwa misingi na utawala wa sheria. NAAMINI HAPA KUNA JAMBO.

HII MIPANGO YA ZIMAMOTO HAITALIONDOA HILI TAIFA KATIKA UMASIKINI MKONGWE
 
Cha kukumbuka pia hapa ni kwamba tatizo lile lililosababisha tukawaita akina Richmond, Aggreko,.., bado lipo. Pamoja na kumsulubu EL na wenzake hakuna hatua nyingine mbadala zilizochukuliwa kulishughulikia tatizo lile. Mambo ya kiufundi kabisa yakaamuliwa kisiasa, visasi vikalipwa, tatizo likaachwa vilevile!
 
Hivi watanzania nani 'ameturoga'? Huyu RA ni nani hasa? Mbona anatuendesha hivi? Ama ni maandalizi ya uchaguzi mwakani? - Wakipata kidogo kupitia Dowans na zingine kwenye mradi wa vitambulisho..nk, zinawatosha 'kushinda' kwa kishindo 2010.
 
Kwa muda sasa wa zaidi ya majuma mawili kumetokea maneno mengi sana ambayo Kamati mbili za Kudumu za Bunge zimekuwa zikisema kuhusiana na ununuzi wa mitambo chakavu ya Dowans , ambayo ni masalia ya Richmond.

Kamati ya Nishati na madini inayoongozwa na Mh. Shelukindo ambaye ni miongoni mwa wabunge wakongwe na wasiokuwa na madoa ya ufisadi yanayoonekana wazi wakipinga TANESCO kununua mitambo hiyo chakavu kwani ni kinyume na sheria za manunuzi ya umma .

Na sababu ya pili wakitoa kuwa mitambo hiyo bei yake imeongezwa maradufu na wamiliki wa Dowans yaani price imekuwa infleted.

Kamati hii ambayo ndio yenye wajibu wa kusimamia masuala ya kisera kuhusiana na mambo ya Nishati na madini , ikiwa na msimamo huo ambao kwangu nauona kuwa ni sdahihi na unalinda masilahi ya Taifa letu ili kutokuendelea kuangamizwa na wezi hawa ambao tunakumbuka jinsi walivyoliingiza Taifa kwenye matatizo makubwa na hata kufikia mahali Taifa letu likakaa siku nne bila kuwepo kwa Serikali.

Kamati nyingine ya Hesabu za Mashirika ya Umma inayoongozwa na mbunge kijana wa Kigoma Kasikazini Zitto imejitokeza na kuwa kama wasemaji wa Dowans na kuitaka serikali inunue mitambo hiyo chakavu na kwa bei ambayo inasemekana kuwa imeongezwa makusudi na wamiliki wa Dowans .

Kamati hii ya Zitto kwa mujibu wa kanuni za Bunge toleo la 2007 ina majukumu yafuatayo,

1.kushughulikia taarifa za kila mwaka za hesabu zilizokaguliwa za mashirika ya umma .

2.kushughulikia maeneo yenye matatizo sugu ya matumizi mabaya ya fedha za Mashirika ya Umma yaliyoainishwa katika taarifa za kila mwaka za hesabu zilizokaguliwa za mashirika hayo na kutoa mapendekezo na ushauri wa namna ya kuyaondoa matatizo hayo.3.kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo yaliyokwishatolewa na kamati hiyo ili kuondoa matatizo hayo.

4.kutathimini ufanisi wa mashirika ya umma .

5.kufuatilia utekelezaji wa sera ya ubinafsishaji wa mashirika ya umma .

Nimeona ninukuu vifungu vya kanuni za Bunge ili kuweka hoja yangu iweze kueleweka kwa wengi .

Wakati kamati ya Zitto ikitakiwa kushughulikia mashirika yenye matatizo sugu ya matumizi mabaya ya fedha kama lilivyo shirika letu la Tanesco na kutafutia ufumbuzi , Kamati hiyo sasa imegeuka na kusahau majukumu yake na kuanza kuwa wasemaji wa Dowans na sasa wanataka kuliingiza shirika hilo kwenye matumizi mabaya ya fedha za umma na hata kununua mitambo chakavu kwa bei iliyoongezwa.

Kamati hii ya Zitto imepewa nini?
Nini kinamsukuma Zitto hata kufikia mahali pa kusahau majukumu ya kamati yake ?
Je?kinachomsukuma ni sawa na kile walichofanya wakina Karamagi na Msabaha badala ya kuwa wasemaji wa serikali wakawa wasemaji wa Richmond?
Nini kinaendelea kwenye suala hili?
Zitto ana masilahi binafsi kwenye suala hili?
Je?ni kweli kuwa anasimamia masilahi ya Taifa kwenye hili hata kama ni kwa kununua mitambo chakavu?

Nimeuliza maswali haya ili kuweza kumrudisha mbunge huyu kijana kwenye mstari kwani ununuzi wa mitambo hii ni mkakati maalum wa kujipatia fedha za kampeni kwa wanamtandao hapo mwakani 2010.

Nitaweka mengine hapa hapo baadae.
 
wait on a minute........hapo unamzungumzia Zitto as Zitto...au unaizungumzia kamati ambayo Zitto yumo............

.........kama sikosei kauli ya Zitto kwenye hii issue alikuwa against kununua mitambo michakavu.......kutokana na sheria za manunuzi...........ndani ya kamati kuna wajumbe waliokuwa wanakubali maneno ya Dr Idris........au mimi ndio sielewi
 
Back
Top Bottom