Miaka kadhaa iliyopita mawasiliano na watu waishio maeneo kama, Misozwe-Muheza, Nanjilinji, tandahimba, kibakwe, mgololo hawakuwa na mawasiano ya simu, lakini hivi sasa wanatesa masaa 24, unaweza kuwajulia hali bibi na babu zako hata usiku wa manane, shukrani ziwaendee mashirika ya simu za mikononi hawa jamaa wanafanya kazi kweli kweli minara yao inapanda kila kukicha, kama hadi sasa tungekuwa na TTCL pekee mambo kama haya yasingetokea ingebaki kuwa hadithi tuu, wacha yaje makampuni binafsi yaifundishe TANESCO jinsi yakusambaza umeme mpaka Misozwe-Muheza, Nanjilinji, tandahimba, kibakwe hadi mgololo..na kama DOWANS wanazosifa zinazohitajika basi nao wapewe nafasi hiyo.
Ni hayo tu.