Dowans: Another Richmond in making?

Dowans: Another Richmond in making?

safi sana,DR Slaa endelea kuzianika hizo wanazosema 'siri za serikali' mpaka mikataba ya kifisadi ikome na waogope kuiingia!
 
Ndugu yangu Kasheshe,

Kuna mambo yanafanyika Tanzania ambayo yanafanya nijiulize ni kwa kiwango gani viongozi wa serikali wanawaheshimu watanzania. Hii ya Dowans na dada yake richmonduli inapita kiwango cha kawaida cha dharau kwa watanzania.

Mwk dharau yote tuliyoipata kwa viongozi wetu in root kutoka kwetu watanzania wenyewe. Maana walishatusoma ujinga wetu na wanafanya wanavyotaka. Maana Ukiangalia watu kama makamba wanayofanya na watu wenye akili zao kabisa wamekaa nao wanawapigia makofi utasema nini????
Ebu fikiri wasomi tulionao katika siasa wanavyo behave na kisha angalia wakitokea vijijini wanavyoonekana miungu wadogo.
Ukifika wakati wa kura utasikia hao hao wanasema wazee wameniomba nigombee kuwakomboa na watu wanawapigia makofi. Lakini same people hawana credibility huko walikotoka, na no body cares tunawapa kura.
Hapo watatuheshimu saa ngapi?
Tumejipotezea heshima sisi wenyewe!🙁
 
Ni heading gani ingefaa kati ya hizi

1.Nchi iongozwayo na 'Muungwana' na Kashfa ya Dowans
2.Nchi iongozwayo na 'Mafisadi' na kashfa ya Dowans
3.Nchi iongozwayo na 'Ndondoncha' na kashfa ya Dowans

Mie nimemwelewa Mzee Mwanakijiji tofauti..
 
Hawa ni wezi kwani walikuwa hawajajua kuwa hakukuwa na mkataba kati ya TANASCO na Dowans why are they saying this now. Dowans was being paid every day why didnt they say we wont pay until the issue is solved.Someone somewhere has robbed us in a daylight we even gave them the key to rob the bank.
 
Next thing tutasikia kwamba pesa za Dowans zimefund Hizabullah au zimefund Al-Qaida. Hakuna check on balance sasa tutategemea nini?
 
Dowans wakamatwe

2008-07-02 09:49:36
Na Raymond Kaminyoge

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba, ameitaka serikali na menejimenti ya TANESCO kuibana kampuni ya kufua umeme ya Dowans kurudisha fedha iliyokwishachukua kwa mkataba ambao si halali.

Kampuni ya Dowans `ilichukua mikoba` ya Kampuni ya Richmond Development Company LLC iliyoingia mkataba wa kuiuzia umeme Tanesco.

``Naipongeza serikali na menejimenti ya TANESCO kwa uamuzi wake wa kuvunja mkataba na kampuni ya Dowans, wamesikia kilio chetu,`` alisema Profesa Lipumba jana jijini Dar es Salaam alipozungumza na Nipashe.

Alisema kitu cha kufanya sasa iwe ni kudai fedha walizokuwa wakichukua kila mwezi kwa sababu mkataba huo haukuwa halali na wameshachukua mamilioni ya fedha.

``Wameshachukua fedha nyingi za walipakodi wa Tanzania kupitia mkataba wa kisanii. Huu ni muda mwafaka wa kuelekeza nguvu za kuhakikisha fedha hizo zinarejeshwa,`` alisema.

Aliongeza kuwa sambamba na hatua hiyo, waliohusika katika mkataba huo wanatakiwa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria ili waweze kushughulikiwa kwa maovu waliyoyafanya.

Alisema walioingia mkataba huo ndiyo wamekuwa wakisababisha bei ya umeme kuendelea kupanda kila wakati na hivyo gharama za maisha kuendelea kupanda.

Aidha, Profesa Lipumba, alisema serikali kwa kutumia wanasheria wake waangalie namna wanavyoweza kuvunja mkataba mwingine wa kampuni ya IPTL na TANESCO.

``Mkataba huu pia unaonyesha ulikuwa na dalili za rushwa, hivyo ili kuwasaidia wananchi mkataba huu pia unatakiwa kuvunjwa na wahusika kufikishwa mahakamani,`` alisema.

Juzi TANESCO ilitangaza kuvunja mkataba na kampuni Dowans kuanzia Agosti mosi, mwaka huu baada ya kubaini kuwa haukuwa halali.

Wakati huo huo, Mary Edward wa PST anaripoti kutoka Dodoma kwamba baadhi ya wabunge wameipongeza serikali kwa hatua nzuri iliyochukua ya kuvunja mkataba na kampuni ya kuzalisha umeme ya Dowans.

Hata hivyo, wamesema hatua hiyo haitoshi bali inatakiwa pia kuwachukulia hatua wote waliohusika katika kuingizia hasara kubwa nchi kwa kupoteza mamilioni ya fedha.

Wakizungumza katika mahojiano maalumu na PST katika viwanja vya Bunge, baadhi ya Wabunge hao walisema, Watanzania wanasubiri kuona inakwenda mbali zaidi kwa kuhakikisha wale wote waliohusika katika utapeli huo wanafikishwa mahakamani, ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.

Mbunge wa Mkanyageni (CUF), Bw. Habibu Mohamed Mnyaa, alisema anaishukuru serikali kwa kuyafanyia kazi maoni ya Watanzania, lakini ni lazima ihakikishe uzembe wa namna hiyo haupewi nafasi tena.

Hata hivyo, alisema serikali ni lazima ijifunze sasa kwa hayo yaliyotokea ili isije ikafanya tena makosa katika mikataba mengine itakayokuja hapo baadaye.

Alisema serikali ilikuwa na uwezo wa kupata mitambo kama ile tena kwa bei nafuu na ikainunua na kuwa ya kwake, kuliko hasara kubwa iliyoingia.

Bw. William Shelukindo, Mbunge wa Bumbuli (CCM), ambaye pia alikuwa ni mmoja wa wajumbe wa kamati ya Mwakyembe, alisema kamati yao ilipendekeza kuvunjwa kwa mkataba huo kutokana na uchafu uliokuwepo.

``Tunashukuru serikali kuona kwamba imeyazingatia maoni ya kamati yetu japo wengine walianza kuzusha mambo kwamba tumewaonea, sisi tulifanya kazi tuliyotumwa, kama kuna watu wanasema tumewaonea basi waende mahakamani.``

Bw. Shelukindo, alisema hivi sasa hawazungumzii masuala ya Richmond kwa kuwa kazi hiyo imekwisha na kuahidi kuwa, wataendelea kuisaidia serikali pale inapoonekana kuna maovu.

Bw. John Cheyo, Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), alisema: ``Hatua iliyochukua serikali sio ya kuvunja mkataba kwa kuwa hapakuwa na mkataba wowote pale, isipokuwa wameamua kutekelezamambo ambayo tulikuwa tunayazungumza tangu zamani.``

Alisema baada ya hatua hiyo sasa iangalie namna ya kuwachukulia hatua wale wote waliohusika na udanganyifu huo.

Alisema hakuna kilichovunjwa kwani hakukuwa na mkataba. Hasara imeshapatikana na haijulikani serikali itafanya nini juu ya hao waliosababisha hasara.

Naye Mbunge wa Karatu (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa, alisema: ``Sawa, serikali imechukua hatua, lakini hiyo haitoshi. Tunataka kuona walioizamisha serikali katika hasara kubwa kama hii wanachukuliwa hatua kali za kisheria.``

Mbunge wa Jimbo la Nzega (CCM), Bw. Lucas Selelii, alisema serikali imechelewa kupata ukweli kuhusu Dowans Tanzania Limited kwani ilikuwepo tangu mwaka 2006.

Aidha Mbunge wa Bukoba Vijijini (CCM), Bw. Nazir Karamagi, ambaye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini, akizungumzia hatua hiyo aliendelea kukana kuwa hahusiki hata kidogo katika sakata hilo.

``Mimi nilirithi Wizara ya Nishati toka kwa aliyekuwa waziri wa Wizara hiyo (akimaanisha Ibrahimu Msabaha, Mbunge wa Kibaha vijijini -CCM) na wala sikuhusika kwa namna moja au nyingine katika kusaidia mkataba huo, hivyo kama serikali imechukua hatua ni vyema, nami naipongeza.

``Mimi sikutetea mkataba huo isipokuwa nilikuwa najaribu kusema kwamba, wakati mkataba huo unafanyika nchi ilikuwa katika matatizo, hivyo katika hali ya kawaida, ilikuwa ni lazima watu wachanganyikiwe,`` alifafanua.

Akizungumzia hatua zitakazochukuliwa, Waziri wa Nishati na Madini, Bw. William Ngeleja, alisema: ``Hii ni hatua ya kwanza tuliyoichukua baada ya kujiridhisha, hatma ya wahusika ni hatua nyingine``

Aidha, alisema kilichofanyika kwa serikali sio kuvunja mkataba kwa kuwa hapakuwa na mkataba wowote walioingia kwa mujibu wa wanasheria na kwamba hapatakuwa na fidia yoyote ya kuwalipa Dowans kwa vile hakuna mkataba uliovunjwa.

``Msingi wa maamuzi haya ni kwamba, hakukuwa na kampuni yoyote ya Richmond Development Company LLC iliyokuwa imesajiliwa na kuingia mkataba na TANESCO... Haipo,`` alisema.

SOURCE: Nipashe
 
Kutimua Dowans bado hakutoshi


JUZI Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dk. Idrisa Rashid alitangaza rasmi kuvunja mkataba na kampuni ya kuzalisha umeme wa dharura ya Dowans.

Mkurugenzi alisikika akisema kuwa wao hawawatambui Dowans na mkataba wao ni batili kwa kuwa hapo awali TANESCO waliingia mkataba na kampuni tata ya Richmond.

Alisema Dowans endapo wana madai yoyote wawadai Richmond ambao ndiyo waliingia nao mkataba na kuwakabidhi kazi hiyo.

Hatua hiyo ya kuvunja mkataba huo mbovu imepokea kwa shangwe hasa na Watanzania wenye kipato cha chini ambapo ilikuwa ndiyo walikuwa wakitarajia kuumizwa zaidi na mkataba huo.

Kutokana na malalamiko na vilio vya wananchi kote nchini Wabunge waliliona hilo na ndipo walipoipenyeza hoja hiyo bungeni ambayo iliundiwa tume ikiwa chini ya Mwenyekiti Dk.Harryson Mwakyembe na ilibainika mapungufu makubwa ndani ya mkataba wa Richomond.

Hivyo kutokana na mapungufu yaliyobainika ndani ya mkataba huo kamati ya Mwakyembe ilipendekeza kupitia upya kwa mkabata huo na endapo ikibainika kuwa ni batili mkataba huo uvunjwe mara moja kwa maslahi ya wananchi.

Hoja hiyo ilizua mzozo ndani ya bunge hali iliyosababisha Waziri Mkuu wa Zamani Edward Lowassa pamoja na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi ambaye alikuwa waziri wa Nishati na Madini kwa wakati huo kujiuzulu mapema mwaka huu.

Sisi tunaungana pamoja na TANESCO kwa kuamua kuvunja mkataba huo hewa ambao ulikuwa ukiumizwa wananchi kwa muda mrefu.

Lakini kuuvunja tu haitoshi ila ichukuliwe hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuzifikisha mahakamani kampuni hizo na wahusika ikiwa na pamoja na wale viongozi walioingiza Taifa katika mikataba mibovu hatua kali zichukuliwe dhidi yao.

Kuvunjwa kwa mkataba huu mbovu iwe ni fundisho kwa baadhi ya viongozi wetu ambao wana uchu wa madaraka kwa kujinufaisha na fedha za umma kwa maslahi yao binafsi na kuwatesa wananchi.
 
Dowans : Hatuondoki
Faraja Mgwabati
Daily News; Friday,July 25, 2008 @00:02

Kampuni ya Dowans Tanzania Ltd imesema haiwezi kung’oa mitambo yake ya kuzalisha umeme na kuondoka kwa kuwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), halijawaambia kuondoa mitambo yao. Kampuni hiyo imetoa kauli hiyo huku muda ambao ilipewa na Tanesco kusitisha mkataba wa kutoa huduma ya umeme, ukikaribia kumalizika.

Dowans wanatoa umeme wa megawati 100 kwa Tanesco, lakini mkataba huo ulitangazwa kuwa utasitishwa ifikapo Agosti mosi mwaka huu, kwa madai kwamba mkataba wa mwanzo ambao ulihusisha kampuni nyingine ya Richmond haukuwa halali. Zikiwa zimebaki siku sita tu kufikia hiyo, Dowans imesema haina mpango wa kuondoa mitambo yake kwenye maeneo ya Tanesco kwa sababu hawajaambiwa kufanya hivyo, bali waliambiwa waache kuwauzia umeme Tanesco.

Akizungumza na HabariLeo jana ofisini kwake, Ofisa mmoja wa ngazi ya juu wa kampuni hiyo ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini, alisema kampuni yake inaendelea na biashara kama kawaida kwa kuwa pia Tanesco bado wanahitaji umeme kutoka kwa Dowans. “Sisi tuliambiwa mkataba unasitishwa, hatukuambiwa tuondoke… hatuwezi kuondoka wakati Tanesco wanaendelea kuomba umeme kwetu,” alisema ofisa huyo.

Alisema ikifika Agosti mosi, kama Tanesco watagoma kuchukua umeme wao (Dowans), kampuni hiyo itaanza kuwauzia wateja wengine walioonyesha nia ya kupata huduma yao. Alisema viwanda na machimbo ya migodi ndani na nje wameonyesha nia ya kupata huduma hiyo ya umeme na soko la umeme Tanzania bado ni kubwa, hivyo wataendelea na kazi.

Kuhusu mitambo ambayo ipo katika viwanja vya Tanesco Ubungo, alisema mpaka sasa Dowans haijazungumza na Tanesco juu ya suala hilo, lakini wanaweza kukubaliana kukodisha mitambo hiyo au wao Dowans kulipia gharama mitambo hiyo kukaa pale. Ofisa huyo hata hivyo hakusema kama watachukua hatua za kisheria dhidi ya Tanesco kwa kukatisha mkataba mwezi uliopita kwa kusema “tusubiri ifike tarehe mosi Agosti.”

Hata hivyo, Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud alipozungumza na gazeti hili jana, alisema Dowans walipewa taarifa ya kuondoa mitambo, lakini hakuna makubaliano zaidi yaliyofikiwa kati ya pande hizo mbili kuhusu namna ya kuitumia mitambo hiyo. Masoud alisema ni vyema kusubiri hadi muda huo ufike kwa kuwa sasa hivi muda waliopewa Dowans kuondoka haujafika.

Hakusema hatua gani zitachukuliwa kama Dowans hawataondoa mitambo hiyo. Hata hivyo, alisema wananchi wasiwe na wasiwasi kwa kuwa umeme wa megawati 100 ambao ulikuwa ukitolewa na Dowans, sasa utapatikana kupitia mitambo ya Watsila ya megawati 100 ambayo inamilikiwa na shirika hilo. Kampuni ya Dowans ilirithi mkataba kati ya serikali na Richmond miaka miwili iliyopita baada ya Richmond kushindwa kuzalisha umeme kama ilivyokubaliwa kwenye mkataba.

Mkataba huo baadaye ulionekana ulikuwa na walakini na Bunge likaamua kuunda Kamati Teule ambayo iliongozwa na Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe kuchunguza mkataba huo ambapo ulionekana haukuwa na maslahi kwa nchi. Kutokana na ripoti ya Kamati hiyo, aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa alijiuzulu na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Nazir Karamagi na Ibrahim Msabaha aliyerithiwa na Karamagi, na baadaye kuhamia Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, walijiuzulu pia.
 
Dowans wanafikiri bado WTZ wamelala.
 
Wanaona nchi yenyewe mambo yamekaa kimchoromchoro tu, basi na wao wanaweza kutumia michoro hiyo hiyo kuendelea na utapeli/ufisadi wao.
 
Hivi kweli kiburi hiki wanakitoa wapi? Je wanataka tuwakamatie mapanga, mikuki na mrungu ndipo wajue hatuwataki kabisa?
 
kichunguu wenzio kiburi wanapewa na watu wa ofisi kuu......unafikiri wanakitoa wapi?
 
Nani atawapatia tena kibali cha kuuza huo umeme huko machimboni,Huyo mchawi akamatwe na asulubiwe mchana kweupe.
 
Dowans : Hatuondoki
Faraja Mgwabati
Daily News; Friday,July 25, 2008 @00:02



Hata hivyo, alisema wananchi wasiwe na wasiwasi kwa kuwa umeme wa megawati 100 ambao ulikuwa ukitolewa na Dowans, sasa utapatikana kupitia mitambo ya Watsila ya megawati 100 ambayo inamilikiwa na shirika hilo. Kampuni ya Dowans ilirithi mkataba kati ya serikali na Richmond miaka miwili iliyopita baada ya Richmond kushindwa kuzalisha umeme kama ilivyokubaliwa kwenye mkataba.

.

Hiyo Watsila ndio hao hao? Mkataba wao ni wa Kirichmund pia? Siwaamini hata kidogo.
 
Suala kama hili hakuna haja ya kutumia manguvu, muhimu ni kwa TANESCO kufuata sheria zote ili tusije tukaingizwa kwenye mtego wa kulipa mabilioni mengine ya bure.

Hao Dowans watakuwa na watu wanaowashauri, ni muhimu TANESCO nao kutumia sheria kupambana nao.
 
Suala kama hili hakuna haja ya kutumia manguvu, muhimu ni kwa TANESCO kufuata sheria zote ili tusije tukaingizwa kwenye mtego wa kulipa mabilioni mengine ya bure.

Hao Dowans watakuwa na watu wanaowashauri, ni muhimu TANESCO nao kutumia sheria kupambana nao.
The "Bakhresa Issue" unanikumbusha. Kukurupuka kokote kunaweza kutupeleka pabaya SANA.

Good observation either...
 
Hiyo Watsila ndio hao hao? Mkataba wao ni wa Kirichmund pia? Siwaamini hata kidogo.


Richmond, Dowans, Watsila....?! I am totally confused!

Wanasema watasambaza umeme migodini??!!! Kwa kutumia grid ya nani??!!! Inamaana wanaingia mkataba mwingine na tanesco ili watumie grid ya tanesco kusambazia wateja wao??!! And how is that possible!!??? Yaani grid moja kutumiwa na distributors wawili wenye different interests (private & pubric)???!! Tanesco...dowans....same grid!!?? How are they going to account for their revenues??!! Power distribution engineers, please, help me on this. I am totally confused!

Na hao tanesco leo wanatueleza habari za watsila!!!!? Hivi naye ni munyama gani huyo watsila??!! Au ndo wanampango wa kuchukua hiyo mitambo ya dowans halafu waingie mkataba mwingine wa kisilisili kulipa mabilions mengine kwa dowans??!! Kweli nchi hii ni ya wadanganyika! Tutaendelea kudanganywa mpaka watz wote tuihame nchi yetu. La sivo tutegemee tena kurudi kwenye ujima wetu wa duka la kaya!

This is very interesting....dowans power plant produces 100MW, and now tanesco is coming with another power plant named watsila able to produce the same 100MW????!!! I can't believe this sort of a perfect coincidence!!! It is realistically impossible!!! DOWANS and WATSILA must be the same company!

Ikuulu wanacheza na akili za watz. Inabidi sasa watoe tamko rasimi juu ya hili la dowans!
 
MD wa Dowans hana sababu ya kujificha tena mawazo yake mazuri sana, soko la umeme tz ni pana sana wanaweza uza umeme sambamba na tanesco na kuleta ushindani wa kibiashara katika sekta ya umeme, wazo lao la kuuzia umeme viwanda na migodi ni strategical plan nzuri.

Wanaweza simika mitambo ya makaa ya mawe nyamongo na geita mine ambapo tanesco hawapo, wakanunua makaa ya mawe toka kiwira na kuzalisha umeme wa bei nafuu na kujipatia faida nono.

Kwa dar wanaweza suply umeme twiga cement, alaf steel mill ukizingatia umeme huo wanauzalisha kwa kutumia ges ya songosongo basi wanaweza kujiendesha kibiashara zaidi, kuwa wapangaji wa tanesco niwazo zuri kwani tanesco watapata kodi ya pango.

Hakika siku moja tutanunua vocha za umeme kama tunavyonunua vocha za simu.
 
Back
Top Bottom