Dowans: Another Richmond in making?

Dowans: Another Richmond in making?

huyu waziri namfahamu tangu akiwa pale bot,ni mweupe pee kichwani, kwa hili atapata wachache sana. je nikisema kuwa huenda mitambo hiyo ya songas,imeharibiwa kwa makusudi na mafisadi wa richmond ili turudie dowans waendeleee kuneemeka haiwezekani?

Hiyo inawezekana kwani to suspect is your and our right kikatiba kabisa hasa tukiend kwa precedent! Inawezekana hata mimi na-suspect hivyo hivyo!
 
Kama serikali inalipa Tsh 240 billion kama capacity charge kwa hizo kampuni za kuzalisha umeme kwa mwaka, hata kama umeme hauzalishwi, kwa mradi huo serikali ingeweza kuondokana na tatizo la umeme kwa gharama hiyo hiyo kwa kununua mitambo yake yenyewe zaidi ya 6 (600 MW) ya MW 100 each ($40 million). na Tanzania tunatumia chini ya 1000 MW kwa nchi nzima.

Kokolo,

Naelewa lengo la hoja yako lakini pia inabidi tuwe waangalifu. Kununua mitambo ni kitu rahisi sana, tatizo liko kwenye kuiendesha hiyo mitambo. Angalia ndege ya rais, angalia rada, angalia mashangingi ya serikali. Yanaunguza pesa nyingi mno kiasi kwamba ni rahisi hata kwa mfano kutumia ndege za kukodi kuliko kununua ndege. Laiti tungejua operational costs za rada au ndege ya rais, huenda tunaungua mno hata huko.

Laiti hizo contract zingelikuwa zinajadiliwa na kusainiwa fairly, huenda free market ndio inaweza kusaidia kuondoa hili tatizo sugu la umeme TZ.

Serikali hii tunayoijua haina record nzuri kwenye project yoyote.

Tatizo la Tanzania ni huu ufisadi ambao unatufanya kwenye kila kitu tununue kwa bei ya juu mno ili hao middle class wetu wapate pesa za kuficha nje.
 
Hiyo mitambo uwa na warrant 3-5 years, na wakati huo wanawatrain watu wenu, kama ni operational cost (Labor, spare parts) hivyo ni vitu vidogo sana. Gas tunayo yakumwaga. nini zaidi ya hiyo.
 
Hivi long term plan ya Umeme Tanzania ndio hivi viji-kampuni vya mafungu? huyu Watts 100, yule sijui 150 etc.
Hivi kwa nini wasijenge Stigler Gorge?
Kwanza hata huo wa Songas/ Aggreko nafikiri kuna ufisadi . Is it the Best Option ya ku-generate electricity?
 
Mkuu, sidhani kama kuna mtu anafikiria long term power plan ya tanzania. Nenda pale tanmesco, hata hiyo plan ya miaka mitano unaweza usiipate. Ukiwaambia suala la kujenga stiglers unakuwa unawaudhi sana kwa sababu wananjua kuwa hiyo itakuwa ni miwsho wa hivi vimkataba uchwara am,bavyo wanapatia kula
 
Hivi hizi kampuni TAX na VAT zinalipa kweli??
Au ndo hivyo tena kwa vile wana deal naserikali hawaruhusiwi kulipa kodi??
 
Date::10/25/2008
Dowans kurudi kwa mlango wa nyuma

*Waitunishia misuli Tanesco kuhamisha mitambo

Na Waandishi Wetu
Mwananchi

MIEZI miwili baada ya serikali kusitisha malipo kwa kampuni kuzalisha umeme wa dharura kuna taarifa kuwa serikali inapanga kuinunua mitambo hiyo.

Habari zilizolifikia Mwananchi Jumapili zinasema kuwa lengo la kununua mitambo hiyo ni kupunguza upungufu wa nishati ya umeme unaolikabili taifa ambao mara kwa mara umekuwa ukisababisha mgawo wa umeme pale mtambo mmojawapo unapoharibika au kina cha maji kupungua.

Akizungumzia suala hilo jana Ngeleja alisema ni kweli taifa linaweza kuinunua mitambo hiyo endapo watalaamu wake wataridhika nayo.

Alisema hali hiyo inatokana na upungufu wa mitambo ya kuzalishia umeme unaoilazimisha serikali kununua mitambo yake ya kufua umeme.

"Nchi yetu imebarikiwa kwa rasilimali mbalimbali, lakini hatuna mitambo, hivyo serikali iko kwenye mchakato wa kununua mitambo kwa ajili ya umeme wa dharura, si tu ya Dowans hata tukiipata mingine kutoka nje, lakini kama wataalamu wetu wakijiridhisha na mitambo hiyo (ya Dowans) serikali itafanya hivyo," alisema Ngeleja.

Alisema endapo serikali ikinunua mitambo yake itakuwa imepunguza gharama kubwa za uzalishaji wa umeme ukizingatia kuwa matumizi ya nishati hiyo yanaendelea kuongezeka siku hadi siku kutokana na kukua kwa miji.

"Umeme unaozalishwa kwa sasa ni megawati 1,200 tu, ambao umekuwa ukitumika katika maeneo ya mijini, lakini vijijini hakuna huduma hii ingawa nao wanaihitaji, kwa hiyo tunalazimika kununua mitambo mingine ya kusaidiana na hii iliyopo," alisema Waziri Ngeleja.

Wachambuzi wa mambo wanasema kwa kufanya hivyo serikali itakuwa inaendelea ‘kuwawekea mwavuli’ waliohusika na mkataba wa Richmond ili wasipate hasara ya mitambo yao kubaki bila kazi yoyote

Kauli hiyo ya Ngeleja imekuja siku chache baada ya naibu wake, Adam Malima kukaririwa akisema kwamba endapo mgawo wa umeme ungendelea wangeweza kuruhusu Dowans iuzie Tanesco umeme.

Malima alisema hayo wakati akizungumzia mgawo wa umeme ambao uliikumba nchi baada ya mitambo mitatu ya Kampuni ya Sogas kuharibika.

Wakati huo huo, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), limepanga kuondoa mitambo ya Dowans kwenye eneo lake Ubungo, jijini Dar es Salaam, huku kampuni hiyo imetunisha msuli ikisema haitafanya hivyo kwa kuwa haina mahali pa kuipeleka.

Hatua hiyo imekuja wakati tayari Tanesco imekwishasitisha malipo kwa Dowans ambayo ilirithi mkataba wa tata wa Richmond.

Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud amelieleza gazeti hili kwamba shirika lake litaondoa mitambo hiyo muda wowote kuanzia sasa.

"Tupo mbioni kuondoa mitambo ya umeme ya Dowans,na sasa tunaandaa mikakati hiyo halafu tutatoa taarifa kamili wiki ijayo kuhusiana na uondoshwaji wake,"alisema Masoud.

Lakini tamko hilo limepata upinzani kutoka kwa Dowans wanaosema kuwa hakuna kitu kama hicho kwa kuwa hawana pa kuipeleka mitambo hiyo.

Afisa mwandamizi wa Dowans ambaye aliomba kutotajwa jina lake gazetini, alisema wao hawana pa kuipeleka mitambo hiyo, hivyo wataiacha katika eneo hilo mpaka watakapoamua wao.

"Kwa sasa hatuna mawazo ya kuondoa mitambo hiyo katika eneo la Tanesco, kwa sababu hatuna pa kuiweka wala pa kuipeleka, hivyo itabaki pale pale," alisema afisa huyo.

Akizungumzia suala hilo, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alisema suala la kuhamisha mitambo hiyo liko mikononi mwa Tanesco.

Kulingana na mkataba huo uliositishwa, Tanesco ilikuwa inatakiwa kulipia gharama za kuhamisha mitambo hiyo kwenda popote atakapotaka mwekezaji baada ya muda wa mkataba huo kumalizika.
 
Ama kweli nchi hii haina uongozi wala utawala wa sheria! Utanunuaje mitambo iliyoingizwa nchini kitapeli? Dowans ni Richmond hao hao ambao juzi walifutwa na Msajili wa Makampuni. Sasa msingi wa kudeal na Dowans uko wapi? Ngeleja na Malima wamevuta kiasi gani kutoka kwa hawa matapeli?
 
Uchaguzi mkuu wa 2010 unakaribia wakati wa wanasiasa kula haramu na kuuza nchi, tusipokuwa na watu makini nchi itauzwa na watu tulio wadhani ni waadilifu
 
Ama kweli nchi hii haina uongozi wala utawala wa sheria! Utanunuaje mitambo iliyoingizwa nchini kitapeli? Dowans ni Richmond hao hao ambao juzi walifutwa na Msajili wa Makampuni. Sasa msingi wa kudeal na Dowans uko wapi? Ngeleja na Malima wamevuta kiasi gani kutoka kwa hawa matapeli?

Sitashangaa kama watainunua mitambo hiyo kwa bei kubwa kuliko hata bei ya mitambo mipya. Tanzania inajengwa na wenye moyo na kuliwa na wenye meno.
 
Sikio la kufa.......

Hapa sasa inakuja kashfa nyingine. Richmond ambaye alikuwa mwenye mkataba ilikuwa kampuni hewa. Hiyo hewa ikawauzia Dowans matatizo yao. Na Dowans tayari imefutwa na msajili au mimi ndo sina kumbukumbu nzuri?

Sasa kama Dowans imeshafutwa, huyu Waziri na Naibu wake wanaongelea mitambo ya kampuni gani wakati sasa kwenye orodha ya msajili hakuna tena kampuni kama hiyo? Haya ngoja tusubiri hili tena la kufanya biashara na kampuni hewa!!
 
Kama mitambo inafaa na nchi ina matatizo mimi sioni shida kwanini tusiinunue. Labda jambo la kuangalia hapo ni transparency, kuhakikisha mchakato mzima wa kuamua kununua au kutokununua hiyo mitambo unakuwa wa wazi.

Mitaani hakuna umeme, viwanda na huduma zingine zinaanza kuwa affected, kweli kuna haja ya kuangalia hiyo mitambo inanunuliwa toka wapi?

Hiyo mitambo kama hakuna ufisadi inaweza kupatikana kwa bei ya chini sana maana wenye nayo wako kwenye uamuzi wa kuingia hasara kwa asilimia 100 au kuokoa pesa kidogo.

Muhimu hapo ni kwa wahusika kufanya maamuzi kwa faida ya nchi.
 
Nadhani akina Mwakyembe walifuatilia bei ya mitambo wakakuta ni bei rahisi sana direct toka kwa manufacturers. Kama ni mitambo nadhani TANESCO wakanunue mipya direct toka kwa manufacturers ili kuepuka matatatizo ya kuuziana makanyaboya kwa inflated price watu wakijaribu kukusanya chao mapema. Maana 2010 tayari imepiga hodi na hawa jamaa hawana uhakika kama watafanikiwa kurudi.
 
Kama mitambo inafaa na nchi ina matatizo mimi sioni shida kwanini tusiinunue. Labda jambo la kuangalia hapo ni transparency, kuhakikisha mchakato mzima wa kuamua kununua au kutokununua hiyo mitambo unakuwa wa wazi.

Mitaani hakuna umeme, viwanda na huduma zingine zinaanza kuwa affected, kweli kuna haja ya kuangalia hiyo mitambo inanunuliwa toka wapi?

Hiyo mitambo kama hakuna ufisadi inaweza kupatikana kwa bei ya chini sana maana wenye nayo wako kwenye uamuzi wa kuingia hasara kwa asilimia 100 au kuokoa pesa kidogo.

Muhimu hapo ni kwa wahusika kufanya maamuzi kwa faida ya nchi.

Mafisadi hawana hata chembe ya haya maana 2010 imekaribia. Wanataka kufunga magoli ya haraka haraka maana hizi ni dakika za majeruhi.
 
Kama mitambo inafaa na nchi ina matatizo mimi sioni shida kwanini tusiinunue. Labda jambo la kuangalia hapo ni transparency, kuhakikisha mchakato mzima wa kuamua kununua au kutokununua hiyo mitambo unakuwa wa wazi.

Mitaani hakuna umeme, viwanda na huduma zingine zinaanza kuwa affected, kweli kuna haja ya kuangalia hiyo mitambo inanunuliwa toka wapi?

Hiyo mitambo kama hakuna ufisadi inaweza kupatikana kwa bei ya chini sana maana wenye nayo wako kwenye uamuzi wa kuingia hasara kwa asilimia 100 au kuokoa pesa kidogo.

Muhimu hapo ni kwa wahusika kufanya maamuzi kwa faida ya nchi.

Tatizo hapa sio uzima au ubovu wa mitambo. Issue ni kwanini tuinunue wakati tulitapeliwa? Dawa ni kuitaifisha na kuwa mali ya serikali kwa kuwa tuliibiwa tangu mwanzo na kampuni hewa. Kuinunua au hata kujadili suala la kuinunua ni wizi mwingine ambao tunataka fanyiwa.Hakuna cha kuiacha iondoke ndani ya nchi wala kuinunua.
 
Ngeleja ni kijana mwenzetu na tunatazamia awe na akili za vijana, yaani google.com, GE : imagination at work, Wärtsilä - Home ni website ambazo anaweza kuzitembelea na kujua generators gani za kununua.

Ngeleja wasikuingize mkenge hao kina Lowassa umeona yaliyomkuta Msabaha na Karamagi.

Issue hapa ni very simple, Tanesco wanahitaji MW ngapi in total?? So generators ngapi za 50MW au 100MW zinahitajika?? Ukishapata jibu hapo ni kulog in to kwenye websites za wartsila na GE na kuwapambanisha wakupe bei nzuri kwa reliable generators zenye warranty!!

Si umeona SONGAS generators zao zikiwa na issue wanapiga simu to GE sababu ya warranty?? Sasa Dowans wa nini?? wanasema hawana mahali pa kuzipeleka hizo generators, that should tell u everything, yaani hiyo si biashara yao. Mbona Aggreko contract ikiisha wanapeleka generators zao sehemu nyingine???

Yaani ni kama mtu amekodi nyumba, contract imeisha unamwambia mwenye nyumba siwezi kuondoka sina pa kwenda!! Hiyo inamuhusu nini??

Naona gear ya kuharibu Songas na agrreko generator ili kuwe na giza nchini watu walishtukia.

Jk kwani wewe vipi mkuu?? Au huwezi kulog in huku JF sababu wamekuibia ile laptop?? tsk tsk tsk
 
Tutanunua mitambo ya Dowans tukishauriwa – Ngeleja
Mwandishi Wetu
Daily News; Monday,November 03, 2008 @22:45

Serikali imesema itakuwa tayari kununua mitambo ya Kampuni ya Dowans Tanzania Ltd endapo Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), litaishauri kufanya hivyo. Dowans Tanzania Ltd jana ilitangaza rasmi zabuni ya kuuza mitambo yake ya kuzalisha umeme ikiwa ni miezi mitatu baada ya serikali kukatisha mkataba wake na Tanesco.

Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja aliiambia HabariLeo jana kuwa kimsingi serikali haitakuwa na tatizo na mitambo hiyo endapo wataalamu wa Tanesco watashauri hivyo. “Tanesco ndiyo wataalamu wetu, tutawauliza wakisema tununue tutanunua, lakini kwa kufuata taratibu na sheria za manunuzi ya mitambo hiyo,” aliongeza Ngeleja.

Endapo serikali au Tanesco watanunua mitambo hiyo, itasaidia kupunguza uwezekano wa kutokea mgawo wa umeme mara mitambo mingine ikipata hitilafu. Mwezi uliopita, Tanesco ililazimika kutangaza mgawo wa umeme baada ya mashine moja ya Kampuni ya Songas yenye uwezo wa kuzalisha megawati 40 kuharibika.

Hata hivyo, Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud alisema jana kuwa shirika hilo halijaamua kama watanunua au la. Alisema watatoa taarifa uamuzi ukifikiwa. Dowans Tanzania Limited ilirithi mkataba wa kuiuzia umeme wa megawati 120 Tanesco kutoka kwa Kampuni ya Richmond Development LLC ambayo baadaye iligundulika kuwa ni kampuni hewa.

Serikali ilifikia uamuzi wa kusitisha mkataba huo Agosti mosi mwaka huu baada ya kuridhika kuwa mkataba huo haukuwa halali wala haukuwa na nguvu kisheria. Tangazo lililotolewa jana na kampuni hiyo lilimtaka mtu yeyote, taasisi, kampuni itakayotaka kununua mitambo hiyo ipange bei inayoona inaweza kutoa kuipata mitambo hiyo.
 
Tangazo lililotolewa jana na kampuni hiyo lilimtaka mtu yeyote, taasisi, kampuni itakayotaka kununua mitambo hiyo ipange bei inayoona inaweza kutoa kuipata mitambo hiyo.
 
“Tanesco ndiyo wataalamu wetu, tutawauliza wakisema tununue tutanunua...” aliongeza Ngeleja.

Endapo serikali au Tanesco watanunua mitambo hiyo, itasaidia kupunguza uwezekano wa kutokea mgawo wa umeme mara mitambo mingine ikipata hitilafu.

Alah, kumbe TANESCO wana uwezo wa kumiliki na kuendesha mitambo hiyo hiyo ya Dowans/Richmond ambayo walienda kuwa contract Dowans/Richmond ?

Hivi kumbe hizi contract - hata zile zilizokuwa halali - basi mi miradi ya watu!!!

I mean, unaweza kuingia mkataba wa kukodisha gari kulitumia mwaka mzima wakati una hela za kununua likawa lako ?

Somebody ask Ngeleja this question.
 
Back
Top Bottom