Done your proper research?! Kingereza cha ugoko cha Bashite

Hiyo lugha sio yetu , kinachoshangaza upo busy kumkosoa mtu kwa lugha ambayo sio asilia yake.
Usomi sio kujua kiingereza.
Tazama china, tazama India, Pakistan, Japan ENGLISH wanayoiongea ni mbovu sana ila.....
Utetezi sampuli hii kama yako huwa inanishangaza sana.Aisee!
 
swali ni je kwa nini aongee lugha ambazo haiwezi?
 
Kwani kalazimishwa kuongea kingereza, kama hajui si atafute mkalimani kuliko kuongea madudu.
Hata ingekuwa ni sehemu ya lazima yeye kuongea kiingereza bado watu wangecheka tu, ndio utamaduni tuliyojijengea. Kiswahili kibovu akiongea mzungu au muhindi huwa hatuna muda wa kucheka tunasikiliza ili kumuelewa na sio kutaka aongee kiswahili kizuri ila linapokuja suala la sisi kuongea kiingereza hapo ndipo ufasaha wa lugha unapozingatiwa.
 
Ujue hili tatizo ni la watanzania wote sio Makonda tu.

Tunaweza tukawa sahihi kwa kuwakosoa hawa viongozi hapa na pale, lakini tatizo linaishaje?

Nina uhakika mleta mada naye akipewa nafasi ya kujieleza kwa kiingereza ataboronga.
Hilo mbona liko wazi kabisa, wengi wanafikiri wabongo tungepaswa kuwa na uwezo mzuri wa kuongea kiingereza et kisa tu shuleni tunafundishwa kwa kiingereza.
 
Unaamini kusoma somo la kiingereza basi moja kwa moja kunafanya kuwa na uwezo mzuri wa kuweza kuongea kiingereza fasaha?
 
Are you that dumb??
Mzungu anayejifunza Kiswahili mtaani na Google miezi miwili mitatu unataka kumfananisha na Bashite aliyesoma Kingereza tangu primary mpaka chuo kikuu??
 
Ndio maana nikasema hiki kiswahili tunachoongea kuna kiasi kikubwa si kuswahili fasaha na wenyewe tushazowea hatujui kama si fasaha na kudhani hivyo ndivyo sahihi.
 
Unaamini kusoma somo la kiingereza basi moja kwa moja kunafanya kuwa na uwezo mzuri wa kuweza kuongea kiingereza fasaha?
Kama tumeshakubali kwamba sisi hata tukisoma Kingereza hatuwezi basi tuachane nacho kabisa, tusome Kiswahili secondary na chuo kikuu.

Kwa nini Kenya na Uganda wakisoma Kingereza wanakuwa na uwezo mzuri wa kuzungumza??
 
Ina maana hizo nchi hawana somo la english katika masomo yao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…