Done your proper research?! Kingereza cha ugoko cha Bashite

Done your proper research?! Kingereza cha ugoko cha Bashite

Tungeona kama tunavyoona kwenye kiingereza.
Huwa tunacheka. Huoni hapa JF wanaoshindwa kuandika tunavyobagaza? My take ni kuwa, kama wewe hujui kiingereza kwa nini unajifanya kuweka maneno ambayo hujui hata maan yake? Huyo Bashite alikuwa na ulazima gani wa kusema ''dene your research''? Si angeseme tu fanya uchunguzi/utafiti wako?
 
Makonda is neither smart upstairs nor good in communication skills,
It takes him a week to hardly construct a sentence in English language ,
This local language swahili has denied Tanzanians alot of opportunities abroad Kenyans have carried the day several times in Communication skills

Makonda love Queen's language but whenever He opens his mouth the language deny him.
Practice will make him perfect (read books and Newspapers and listen to more English programs from Citizen TV Kenya, He might Improve his speech,
 
Nje ya mada,

Hivi kwanini ni rahisi zaidi mtu kukosolewa anapokosea neno la kingereza kuliko kukosolewa pale anapoongea neno/sentensi kwa lugha ya Kiswahili na kukosea?

Mfano unakuta humu JF mtu akisahihishwa kuandika Kiswahili kwa ufasaha anakua mkali!

leo dada
Mtu akikose kuongea kiingereza Mimi siwezi kumcheka hata siku moja. Sijui kwa nini, labda kwa sababu kiingereza changu nacho ni broken 😂.
 
Tatizo ni kwamba elimu yetu ya Pili na vyuoni ni ya Kiingereza, hivyo ni mategemeo yetu, kuwa angekuwa ana kijua hicho kiswa -inglish, tofauti na MTU mwingine aliyesimea lugha nyingine Shule ya upili na vyuoni. Kama Rio Angejaribu Kiswahili akakisea watu wangemuwelewa.
Kwahiyo unataka kusema kwamba hajui kiingereza na kwa sababu elimu yetu ya pili na chuo hufundishwa kwa kiingereza hivyo hakuwa akielewa masomo?
 
Hauwezi kujitetea udhaifu wako kwa sababu nchi nyingine zimekwama.Umeanza kujifunza kuongea kiswahili tangu ukiwa na wastani wa miaka miwili/mtoto hadi miaka mitano uliweza kuongea vema.Kiingereza umejifunza kuanzia ukiwa na miaka minane/darasa la tatu hadi miaka 23 chuoni/miaka 15 kwa wastani.Nini shida hapo kama siyo uzuzu sugu aka ukilaza?Jitetee.
Shida ni kwamba kuna watu hawajasoma sana ila wanaongea kiingereza vizuri na kuna waliyosoma sana na wana elimu nzuri ila hawawezi kuongea vizuri kiingereza.
 
Huwa tunacheka. Huoni hapa JF wanaoshindwa kuandika tunavyobagaza? My take ni kuwa, kama wewe hujui kiingereza kwa nini unajifanya kuweka maneno ambayo hujui hata maan yake? Huyo Bashite alikuwa na ulazima gani wa kusema ''dene your research''? Si angeseme tu fanya uchunguzi/utafiti wako?
Unadhani hiki kuswahili tunachoongea ni fasaha?
 
Hivi tujiulize kama kweli kutumika kwa kiingereza masomo yetu ndio kunaweza kumfanya mtu aweze kuongea kiingereza vizuri na kwa ufasaha sasa kwanini watanzania tuna shida ya kuongea vizuri kiingereza?
 
Ni Bora angeongea Kwa Kiswahili maana uko nchini kwako Tanzania na media ni za kiswahili, hata hivyo watz wengi kwenye ishu ya kuongea kiingereza kilichopangiliwa ni mziki, hiyo lugha ni Tia maji wala tusidanganyane na watu wanajua kuwa hatujui, tena inawezekana Jamaa kajitahidi Sana, ugumu unaweza usiuone Kwa kuwa unaweza Kuongea peke yako utajiona unakiweza Sana, siku uambiwe kuna kundi la watu inabidi ukaongee nao Kwa kimalkia ndio utajua ugumu unatokea wapi, ww kila siku unaongea kiswahili lazima kimalkia hata cha maji kikupige chenga.
 
Ni kweli usomi sio kujua kiingereza. Ila msomi anajua aongee nini, wakati gani na aongeeje. Kama hujui kiingereza huna haja ya kujiongelesha lugha usioielewa vyema wakati unaweza ukatumia lugha unayoielewa vyema (Kiswahili) ukaeleweka?
 
Hivi tujiulize kama kweli kutumika kwa kiingereza masomo yetu ndio kunaweza kumfanya mtu aweze kuongea kiingereza vizuri na kwa ufasaha sasa kwanini watanzania tuna shida ya kuongea vizuri kiingereza?
Sasa hapa umeanza kupata akili, huu ni mjadala muhimu.

Hizi zinaweza kuwa sababu,

1. Ubora wa elimu yetu ni mdogo sana kwa sasa, kiwango kimeshuka tangu enzi za Mkapa na JK baada ya serikali kujikita katika kujali wingi wa majengo na kupuuza quality ya walimu, na hii sio kwenye lugha tu bali elimu kwa ujumla. Wengi waliohitimu vyuo kuanzia 2000s hata uwezo wao wa kujenga hoja, kujieleza na kuelezea jambo hata kwa lugha ya Kiswahili ni mdogo sana. Shule nyingi na vyuo vingi duniani vinavyotumia lugha ya Kingereza huwa kunakuwa na debate clubs ambazo ni sehemu ya kuberesha oratory skills, lugha na uwezo wa kujenga hoja, Tanzania hakuna hili.

2. Mfumo wa elimu yetu shule za umma hauweki msingi mzuri au ku support wanafunzi kujua Kingereza, cha kufanya sasa ni kuzifanya shule zote za umma English medium kwani tuna ushahidi wa wanafunzi wanaosoma shule za English medium za msingi Tanzania, Kenya na Uganda kuwa na uwezo mzuri wa kuzungumza Kingereza bila kubabaika.

3.Uongozi mbovu umeua utamaduni wa kujisomea katika nchi. Kuna mahusiano makubwa sana kati ya kusoma vitabu na uwezo wa kuzungumza lugha, hii nchi suala la kujisomea vitabu ni kama liliisha na Mkapa, na sidhani kaman kuna serikali tofauti na serikali ya Nyerere huko 1960s na 1970s zimewahi kujihusisha na maktaba za umma.
 
Shida ni kwamba kuna watu hawajasoma sana ila wanaongea kiingereza vizuri na kuna waliyosoma sana na wana elimu nzuri ila hawawezi kuongea vizuri kiingereza.
Hiyo nayo ipo.Kuna watu wana vipaji na wepesi kujua lugha mbalimbali.Wepesi mnoo.Mfano mmoja ninao chini ya paa ninalooshi.Anaweza kuzungumza lugha za asili na za mataifa kadhaa tena kwa madaha sana.Ipo hivyo muda mwingine.
 
Back
Top Bottom