Dondoo za hatua za kupata hati ya umiliki wa ardhi hapa Tanzania kwa mwaka 2022

Kuna hasara gani kufatilia hati miliki ukiwa peke ako
Changamoto kubwa kufuatilia Hati mwenyewe ni kupoteza muda mwingi coz ili mchakato wa Hati ukamilike ni lazima
• Eneo Liwe limepimwa
•Eneo liwekwe beacons
•Town plan (ramani ya mipango mji) kutoka wizarani
•Mkataba wa mauziano
•Uhakiki wa mipaka na majirani

Sasa haya yote lazima ufanye kwa ushrikiano wa karibu na aliyekuuzia na majirani wa eneo ulilonunua,
Gharama za kulipia serikalini kwa kufanikisha mchakato wa Hati ni ndogo sana na inapanda au kupungua kutokana na ukubwa wa eneo lako au eneo kiwanja chako kilipo

•Note Usikubali kununua kiwanja kama hakija pimwa na hujaona Ramani ya mipango miji coz Kila eneo kwa Kila halimashauri Lina matumizi yake.
Jiridhishe eneo unalotaka kulinunua linendana na matumizi ya eneo husika ili kuepusha usumbufu hapo baadaye

Mfano Mimi kuna sehemu nashughulikia hati kwenye kiwanja changu nlilipa 71380 tuu, Lakini hiyo ni nje ya ile nliolipa kampuni ambayo iliniuzia kiwanja ili kunirahisishia mchakato mzima
IMG-20230718-WA0006~2.jpg
 
Utangulizi.

Cheti cha umiliki wa ardhi.

Ni nakala itolewayo kwa mtu ikionyesha haki yake ya kukodishiwa ardhi husika ndani ya miaka fulani.

Anayepewa hati hii anakuwa amekodishiwa ardhi na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ardhi hiyo husimamiwa na raisi wa Jamhuri kwa niaba ya watanzania wote.

Ardhi ni mali ya umma na raisi ndiye mmiliki au msimamizi wa ardhi yote kwa niaba ya Watanzania wote.

Hati ya umiliki wa ardhi ya kiserikali hutolewa kwa kipindi cha miaka 33, 66, au 99.

Kushindwa kutumia ardhi uliyokodishiwa kufuatana na matumizi husika ya ardhi yako hupelekea kunyang'anywa ardhi hiyo.

Hati hii hutolewa kwa ardhi ambayo imepimwa tu. Ardhi ambayo haijapimwa, haiwezi kupata hati ya hakimiliki ya kiserikali (granted right of occupancy).

Kwa mtu ambaye sio raia wa Tanzania, hupewa ardhi kama mwekezaji. Mwekezaji huyo atatakiwa kuzingatia utaratibu kutoka wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi ya Tanzania.

Wapimaji Wa Ardhi.

Viwanja na mashamba huweza kupimwa na makundi yafuatayo;-

✓ Wataalamu wa Halmashauri husika.

✓ Wataalamu wa makampuni binafsi yaliyo kwenye Halmashauri hiyo.

Mahitaji Ya Zoezi La Kupata Hati Miliki (Title deed).

(a) Kitambulisho cha muombaji au waombaji.

Kitambulisho cha mpiga kura, kitambulisho cha taifa, cheti cha kuzaliwa au cheti cha utambulisho wowote unaoruhusiwa.

(b) Mkataba wa umiliki wa ardhi.

Huu huonyesha kama ulinunua, ulipewa kama zawadi, ulirithi na kadhalika. Mkataba huu unatakiwa kuwa na mhuri wa mwanasheria.

(c) Fomu ya mipaka ya kiwanja (land form Number 92)

Hii huonyesha majirani ya wamiliki halali wa viwanja vinavyozunguka kiwanja chako. Mipaka inatakiwa kuonyesha pande zote nne kama ifuatavyo;-

Upande wa kaskazini ___________.

Upande wa kusini _______________.

Upande wa magharibi _____________.

Upande wa mashariki _______________.

Majirani wanatakiwa kuweka saini na kukubaliana mipaka ilivyo kwenye fomu hii.

Fomu inatakiwa kuwekwa sahihi na viongozi wa serikali ya mtaa husika.

(d) Fomu ya maombi ya hati (land form No.19).

Hii hujazwa taarifa za muombaji kama anavyotumia kwenye nyaraka zake zingine kufuatana na ushauri wa wakili wake.

(e) Ramani ya upimaji wa kiwanja.

Ramani iwe imeidhinishwa na wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi ya Tanzania.

Ramani iwe na mhuri na sahihi ya mkurugenzi wa ramani na upimaji.

(f) Ramani ya mipango miji.

Ramani hii huonyesha matumizi husika ya eneo ambapo kiwanja chako kipo. Ramani inatakiwa iwe na mhuri na sahihi ya mkurugenzi wa mipango miji na vijiji.

Ramani inatakiwa iwe imeidhinishwa na wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi ya Tanzania.

(g) Uwe na picha ndogo sita (6) ambazo zimepigwa hivi karibuni.

Gharama Za Kupata Hati Miliki (Title Costs).

Kwa ujumla gharama huwa kati ya tshs.100,000 hadi tshs.300,000. Hii ni kulingana na uzoefu wangu. Mchanganuo wa gharama zote za kupata hati miliki ya ardhi zinaweza kuwa ifuatavyo;-

✓ Gharama za upimaji (survey fee). Hii hutegemeana na Halmashauri husika.

✓ Gharama za usajili (registration fee). Utalipia 20% ya jumla ya kodi ya ardhi (annual land rent) ya mwaka mmoja. Mfano: kodi ya pango la ardhi ya mwaka ni tshs.50,000/=. Gharama za usajili zitakuwa ni 0.2×50,000=10,000.

✓ Gharama za kuandaa cheti (certificate of preparation). Hii utalipia tshs.50,000/=.

✓ Ada ya kupangilia ardhi (Deed plan fee). Hii utalipia tshs.20,000/=.

✓ Gharama za thamani ya kiwanja (premium fee). Utalipia 2.5% ya jumla ya thamani ya kiwanja chako. Mfano: premium fee=Mita za mraba×bei kwa mita moja ya mraba×2.5%.

Hatua Saba (7) Za Kupata Hati Miliki (Title Deed)

MOJA.

Kufanya ukaguzi wa ardhi yako.

Kazi hii hufanywa na mpimaji wa ardhi (land surveyor). Malengo la kufanya ukaguzi ni;-

✓ Kufahamu matumizi ya ardhi yaliyopo.

✓ Kupata ramani ya mipango miji kwenye Halmashauri husika.

Mpima ardhi atafika eneo la kiwanja chako akiwa na kifaa cha kupima ardhi (Handheld GPS) ili kupima mipaka kuzunguka eneo la kiwanja chako.

Mpima ardhi ataenda ofisi za Halmashauri au wizarani ili aweze kupata ramani ya mipango miji na afahamu matumizi ya ardhi yako.

MBILI.

Kupata Majibu Ya Mpima Ardhi (Land surveyor).

Mpima ardhi anaweza kukutana na mojawapo ya majibu yafuatayo;-

(a) Eneo lako kukosa sifa za kupimika.

Sababu ya eneo lako kukosa sifa za kupimika ni kama ifuatavyo;-

✓ Kutokuandaliwa matumizi kabisa (eneo lako halina mchoro wa mipango miji).

✓ Eneo kupangiwa matumizi ya kijamii kama vile makaburi, barabara, masoko na kadhalika.

(b) Eneo lako kuwa na sifa za kupimika.

Eneo lako linaweza kuonyesha sifa za kupimika na kuainisha mojawapo ya matumizi yafuatayo;-

✓ Ardhi kwa ajili makazi (residential).

✓ Ardhi kwa ajili ya makazi na biashara (residential and commercial).

✓ Ardhi kwa ajili ya viwanda (industrial).

✓ Ardhi kwa ajili ya biashara (commercial).

✓ Ardhi kwa ajili ya dini (makanisa na misikiti).

TATU.

Uandaaji Wa Michoro Ya Viwanja.

Wataalamu wa mipango miji (Town planners) wataandaa mchoro wa viwanja (Town planning drawing).

Wataalamu hawa wataambanisha mchoro wa viwanja na mchoro wa mipango miji na kutumwa kwenye wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi ya Tanzania.

Lengo la kutumwa wizarani faili lenye mchoro wa viwanja (Town planning drawing) na mchoro wa mipango miji ni kuidhinishwa rasmi kwa ajili ya upimaji.

NNE.

Kuomba Kibali Cha Upimaji Wa Ardhi.

Mmiliki halali wa kiwanja husika atatakiwa kutuma maombi kwa ajili ya kupimiwa kiwanja chake.

Barua itapitia serikali ya mtaa husika na Halmashauri husika.

TANO.

Upimaji Wa Ardhi Yako.

Mpima ardhi ataweka mipaka kwa kutumia nondo au mawe (beacons) kuzunguka kiwanja chako.

Mpima ardhi ataambanisha nakala muhimu kwenye faili na kuzituma wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi ya Tanzania kwa ajili ya kuidhinishwa tena.

SITA.

Kupokea Ramani Ya Upimaji Wa Kiwanja.

Mteja anayeiomba hatimiliki atatakiwa kupokea ramani ya upamaji wa kiwanja chake.

Muombaji ataipeleka ramani hii kwa Afisa ardhi ili aweze kuandaa hati miliki (title deed) ya ardhi iliyopimwa.

Ramani ya mpima ardhi inatakiwa kuonyesha taarifa muhimu kama ifuatavyo;-

✓ Namba ya kiwanja (plot number).

✓ Kitalu (Block).

✓ Eneo la kiwanja (location).

✓ Namba ya ofisi ya ardhi (land office number).

✓ vipimo vya kiwanja (measurements).

SABA.

Mteja Kukabidhiwa Hati Au Barua Ya Umiliki Wa Ardhi Yake.

Mteja (mmiliki halali) atapatiwa barua ya umiliki (letter of offer) wa kiwanja. Hivyo mmiliki muombaji atatakiwa kushirikiana na afisa ardhi wa Halmashauri husika.

Afisa ardhi wa Halmashauri husika ataendelea na zoezi la kuandaa jalada la hati miliki (title deed) ya eneo lako.

Hatua hii hufanyika baada ya mteja kukamilisha mambo mawili yafuatayo;-

✓ Kulipia gharama zote alizoelekezwa na mamlaka husika.

✓ Kupata ramani ya kiwanja kilichopimwa.

Nyaraka za kupeleka kwa kamishna wa ardhi wa Halmashauri husika ni kama ifuatavyo;-

✓ Barua ya maombi.

✓ Cheti cha kuzaliwa.

✓ Barua ya toleo (letter of offer).

✓ Rasimu ya hati.

✓ Barua ya historia (covering letter).

Ninaamini kwa maelezo haya utapata sehemu ya kuanzia kama unahitaji hati miliki (title deed) ya kiwanja au shamba lako.

Rafiki yako,

Aliko Musa.
Asante kwa maelezo yako mazuri juu ya hili swala. Nina swali, kama utaweza kunisaidia, au mtu yeyote mwenye uelewa juu ya haya mambo. Je, utaratibu upoje kwenye kubadilisha majina ya mmiliki wa kiwanja kwenye hati?
 
Back
Top Bottom