Umeanza kujibu vizuri ila huku chini umeharibu na umeharibu Kwa sababu umeingiza mafundisho ya DOGMA
Umesema baba ni Mungu na Yesu pia ni Mungu hii ni DOGMA
Jibu hili swali
Kati ya huyo Mungu baba na Mungu Yesu Kwa mujibu wa Maneno yako katika hao wewe
Umeumbwa na nani?
Na unamuabudu nani?
Kila nilichokuambia nimekupa na andiko la kukusaidia. At least unaanza kujua kwamba unajibiwa.
Na sasa umeongeza maswali ya ziada.
1) Nimeumbwa na nani?
Jibu ni Mungu. Hii ndiyo sababu wakristo tunaamini Mungu katika Utatu wake uliojifunua katika maandiko matakatifu ndiye anayehusika na uumbaji wa ulimwengu wote.
Mwanzo 1:26
"[26]Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi."
2) Ninamwabudu nani?
Jibu ni Mungu. Ukiamua ku address jina la Yesu katika ibada sawa, maana Yesu ni Mungu na anastahili heshima sawa na Baba
YOHANA 5:23
Ukiamua ku address kwa Baba ni sawa kabisa kimaandiko. Lakini mwenye kustahili ibada ni Mungu pekee.
Jambo muhimu la kukumbuka kuhusu Yesu ni;
*Alikuja duniani akivaa mwili wa kibinadamu