Lwiva
JF-Expert Member
- Apr 17, 2015
- 21,157
- 29,775
Hoja ya kwanza 👉Siku ya kiama hakuna kufa bali hata walio kufa watafufuliwa na kuwepo kama ulivyo sema wewe ...Mkuu watu wote watakuwepo siku ya kiama hata wewe 😃
Hoja ya pili 👉kama yesu akufa na kuja siku ya kihama vipi auishwe na kutwaliwa mbinguni ...maana imeandikwa kuwa mungu atakuuisha na kukutwaa mbinguni
Quran 3:55
"Pale Mwenyezi Mungu alipo sema: Ewe Isa! Mimi nitakufisha, na nitakunyanyua kwangu, na nitakutakasa na wale walio kufuru, na nitawaweka wale walio kufuata juu ya wale walio kufuru, mpaka Siku ya Kiyama. Kisha marejeo yenu yatakuwa kwangu, nikuhukumuni katika yale mliyo kuwa mkikhitalifiana" (hapa kuna maswali mengi na makuu mno na ya msingi sana )
Sasa tuje kwenye hoja zaidi kuhusu 👉👉sura hii
Quran 3:55
"Pale Mwenyezi Mungu alipo sema: Ewe Isa! Mimi nitakufisha, na nitakunyanyua kwangu, na nitakutakasa na wale walio kufuru, na nitawaweka wale walio kufuata.
💥hapa tunaona maneno
1) KUUISHA
2)NITAKUNYANYUAA
3)KUFUATA(nitaweka wale walio kufuata juu ya walio kufuru)
Sasa hapa tunaona hayo maneno matatu yanayo zua maswali mengi sana nayo ni
1)waislamu wanasema Yesu akufa bali alitwaliwa mbinguni ....ila hapo kwenye hiyo sura tunaona neno KUFISHA sasa tunajiuliza Kwa mujibu wa waislamu wanadai yesu atakuja mara 2 duniani ila akija mara ya pili atawaelekeza watu wote kumfuata MUNGU NA MTUME MUHAMMAD SIYO KUMFUATA YEYE ...hivyo hiyo sura inazungumzua nyakati gani za Yesu duniani.