DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

Sina maneno mengi ila napenda kutafakurisha kidogo, hili shambulio lina kila dalili za kisiasa. Limepangwa na upo uwezekano waliofanya shambulizi ni watu walioletwa kutoka nchi za jirani, zenye uzoefu wa kufanya matukio km haya..!

Kwa namna lilifanyika ni wazi kuwa limefanywa na watu wasio na uzoefu mkubwa na mazingira ya Tanzania kama nchi na wannchi wa Tanzania.

Kufyatua risasi nyingi hivi ni ishara ya uoga na kutoamini sehemu wanapofanyiwa tukio kwa maana walikuwa ni waoga na hawakujua vyema nature na hali ya hewa ya wananchi wa Tanzania.

Narudia tena, washambulizi wa Lissu watakuwa wamekuwa imported kutoka nje. Usiniulize nani kawaleta hilo jambo lingine ambalo linaweza kufanyiwa utafiti wake.
......
......I smell your point Sir also the Map readers?
 
Ivi kwanza umeshatoa mchango wako?kama bado ebu zichange then fanya kuzituma achana na porojo uungwana ni vitendo.
 
Let's be serious,taifa la walalamikaji. Mambo yetu bado no magumu mbona tunashupaza shingo kwa mambo ya majirani? Mara PK mara UJK, hii hali yetu tunapambana nayo vipi jamani.

Sent using Jamii Forums mobile app

We do not live in isolation. A wise learns from others' mistakes but a fool always wait to learn from his own failures. Hapo huwa hakuna uwezekano wa tahadhali tena. Ni mwendo wa majeraha kama si mauti kwa kwenda mbele!.
 
Kuna makubaliano ya kitaarifa kati ya Bunge na Jeshi la Polisi kuwa Mbunge Lissu ameshambuliwa kwa risasi kati ya 28-32. Kati ya hizo,amepatwa na risasi tano: moja mkononi,mbili mguuni na mbili tumboni

Risasi husika hazikupigwa sehemu moja. Inaarifiwa kuwa baada ya kuona wanaowafuatilia,Lissu alishauriwa kutoshuka garini na dereva wake na akatii. Kiintelijensia,garini 'alitake cover' kulingana na nafasi iliyokuwepo.

Kufanikiwa kukoswa na risasi 23-27 si jambo dogo. Hakika,Lissu amethibitisha ukamanda wake katika kutetea uhai wake. Naamini,Lissu amesaidiwa na mafunzo ya kiulinzi na kiusalama huko JKT. Kamanda Lissu akirejea,atakuwa imara zaidi!

Bunduki za kivita kwa Wabunge ni za nini tena jamani!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (safarini kwenda Dodoma)
Where was bashite yesterday. Tukio lilipotokea
 
Wakuu,

Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, ajeruhiwa kwa risasi.

Kwa sasa wapo hospitali ya Mkoa, mjini Dodoma.

Ameshambuliwa kwa risasi wakati akishuka nyumbani kwake Area D Mjini Dodoma, alikuwa akitokea Bungeni na alienda Nyumbani kula chakula cha mchana.

Lissu amepigwa risasi 5, miguuni na tumboni.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema hali ya Mbunge huyo aliye hospitalini sasa ni mbaya!




56d494001b8e52eca1b71490ff9635e4.jpg


9f94cea0e0708e5fafb57915caf1dd27.jpg

abc21fedd617180297c6247f403b7362.jpg


Updates to follow

=======

UPDATES:

=======

Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini ameeleza jinsi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alivyopigwa risasi nyumbani kwake mjini Dodoma.

Selasini amesema kuwa maelezo aliyopata ni kuwa alikuwa akifuatiliwa na gari tangu anatoka bungeni na dereva wake alilishtukia. Amesema kuwa alivyoona wanamfutilia alipofika nyumbani, dereva alimsihi Lissu asishuke ndani ya gari.

"Hao watu walipoona hawashuki walijifanya kuna kitu wanaangalia walivyoona kuna utulivu walisogeza gari lao ambalo ni tinted na kuanza kurusha risasi upande wa Lissu." amesema.

Selasini amesema, “Risasi zilimpata mguuni, mkononi na tumboni lakini daktari anasema anaendelea vizuri."

Lissu amepigwa risasi leo Alhamisi na kupelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma.

Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, wabunge na viongozi wengine wa ulinzi wa Bunge wamefika katika hospitali hiyo kujua kinachoendelea.

Baadhi ya ndugu na wagonjwa wamefurika katika chumba cha upasuaji cha hospitali ya mkoa wakitafakari huku wengine wakilia.

UPDATE: Ndege imeshawasili Dodoma ili kumchukua Tundu Lissu kumpeleka Muhimbili kwa matibabu zaidi

Katibu wa Bunge amethibitisha kufika kwa ndege Dodoma kumchukua Tundu Lissu kumpeleka hospitali ya Muhimbili ili kuokoa maisha yake

DODOMA: RPC amesema watu waliomshambulia Tundu Lissu walikuwa wakitumia gari aina ya Nissan la rangi nyeupe

Freeman Mbowe: Ndugu Lissu kwa sasa yuko katika chumba cha upasuaji anajaribu kuokoa maisha yake, nitazungumza baadaye.
View attachment 583459
UPDATES: Miongoni mwa waliofika hospitali kumuona Lissu ni Spika Job Ndugai, Waziri Ummy Mwalimu na katibu mkuu wa bunge, Dkt. Thomas Kashilila

Rais Magufuli ametoa pole na kutaka Vyombo vya Dola kuchukua hatua:

CCM imetoa pole

Waziri wa zamani, Mark Mwandosya naye ametoa pole
View attachment 583477

UPDATES: 2235HRS
Ndege iliyokuja kumchukua Tundu Lissu ndo inatua Uwanja wa Dodoma. Ni ndege binafsi, imetoka Dar Es Salaam na itampeleka Mh. Lissu Nairobi Kenya kwa matibabu zaidi.
6a0df0d4014896f500bc344cb3ddcb26.jpg

TunduLissu akipakiwa kwenye ndege usiku huu tayari kwa safari ya Nairobi kwa matibabu zaidi
3c38765220348b8a8712fc343f512797.jpg


*Rais wa Chama cha Mawakili Kenya(LSK), Isaac Okero amesema Lissu amelazwa Hospitali ya Aga Khan, Nairobi.

TAARIFA YA AWALI KUHUSU SHAMBULIO LA KUPIGWA RISASI MHE. TUNDU LISSU

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kupigwa risasi Mwanasheria Mkuu wa Chama ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Tundu Antipus Lissu baada ya kikao cha Bunge mchana wa leo.

Shambulio hilo limetokea majira ya mchana nyumbani kwake Area D Dodoma na kujeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika Hosiptali ya Mkoa wa Dodoma.

CHADEMA tunalaani vikali kitendo hicho, na tunafuatilia kwa karibu hali yake.

Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

Imetolewa na Kurugenzi ya Uenezi, Mawasiliano na Mahusiano ya Nje.

CHADEMA MAKAO MAKUU

DAR ES SALAAM.

=====

Preliminary Press Statement on the incidence of Hon. Tundu Lissu being shot

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) has received with great shock the report on the shooting of the Attorney General of the Party who is also the Chief Whip of the Official Opposition in Parliament and MP of Singida East, Hon. Tundu Antipus Lissu just after a Parliamentary session today.

The attack took place at his Dodoma residence at midday and was seriously wounded and had been rushed to the Dodoma Regional Hospital.

CHADEMA strongly condemns this act, and we are following up closely on his condition.

We will continue to update as we get more information.

Issued by the Directorate of Ideology, Publicity, Communications and Foreign Relations.
 
Mimi ni miongoni mwa watu walioguswa mno na kupigwa risasi kwa Mh Tundu Lissu,kuna mwizi alivamia nyumba yangu nilimkamata kwa kushirikiana na majirani.Baada ya kupata habari za kupigwa risasi kwa Tundu Lissu nilijiic kufa gani na kwa kuwa alichoiba ni mali yangu nilijikuta siangaiki naye tena..Inauma sana mungu hakika atamponya.
 
Mimi ni miongoni mwa watu walioguswa mno na kupigwa risasi kwa Mh Tundu Lissu,kuna mwizi alivamia nyumba yangu nilimkamata kwa kushirikiana na majirani.Baada ya kupata habari za kupigwa risasi kwa Tundu Lissu nilijiic kufa gani na kwa kuwa alichoiba ni mali yangu nilijikuta siangaiki naye tena..Inauma sana mungu hakika atamponya.
Pole mkuu, tuzidi kumwombea TL
 
Back
Top Bottom