Dodoma: Mavunde afanikisha huduma ya Bure ya wenye matatizo ya macho. Kijana aliyeacha masomo kwa tatizo la kutoona apona, aahidi kumsomesha

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
MAVUNDE AFANIKISHA HUDUMA YA BURE YA WENYE MATATIZO YA MACHO, KIJANA ALIYEACHA MASOMO KWA TATIZO LA KUTOONA APONA. AAHIDI KUMSOMESHA.



Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde kwa kushirikiana na Lion Club tarehe 24 na 25 waliendesha huduma ya kambi ya macho katika Kituo cha afya Makole ambapo walisaidia watu mbalimbali wenye matatizo ya macho.

Huduma hiyo ya kusaidia wenye matatizo ya macho ilikuwa ni Bure ambapo Kijana Chrispin Christopher ambaye alikuwa ameacha kuendelea na masomo kutokana na kupoteza uwezo wa kuona, kupitia huduma hiyo iliyoratibiwa na Ofisi ya Mbunge Mavunde Kijana huyo amefanyiwa upasuaji na sasa anaona vizuri na anatamani kurudi tena shuleni.

Baada ya kupona na sasa kuona, Mhe Mbunge Anthony Mavundeu ameahidi kumsomesha Kijana Chrispin Christopher kumalizia elimu yake yote.

#MtumishiWaWatu
 
Back
Top Bottom