Mbunge Mavunde aishukuru Serikali kwa utekelezaji wa Miradi ya Elimu jijini Dodoma

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
210
500
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde ameishukuru Serikali kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa madarasa na matundu ya vyoo kwa shule za msingi nne za Dodoma Jiji ambazo ni Shule ya Msingi Kisasa,Medeli,Kizota na Mlimwa C.

Mradi huu ambao unagharimu kiasi cha Tsh 1,902,000,000 (Shilingi Bilioni Moja Milioni Mia Tisa na Mbili) umelenga katika kutatua changamoto ya madarasa ya kusomea na matundu ya Vyoo katika Shule hizo.

“Ninaishukuru Serikali chini ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha za ukarabati na ujenzi wa matundu ya vyoo ambazo kwa kiasi kikubwa zitapunguza adha kwa wanafunzi wetu wa Shule za Msingi.

Mradi huu umekuja wakati wa muafaka hasa ikizingatiwa kwamba kwa sasa mahitaji ya vyumba vya kusomea kwa wanafunzi ni makubwa sana hali inayosababishwa na muitikio wa sera ya Elimu bure na kuhamia kwa serikali Jijini Dodoma.

Natoa rai kwa kamati za shule kuhakikisha wanasimamia ipasavyo fedha za mradi huu kwa uaminifu na uadilifu mkubwa ili matokeo ya mwisho ya lengo lililokusudiwa yaonekane”Alisema Mavunde

Akishukukuru kwa niaba ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma Prof. Davis Mwamfupe ameishukuru serikali kupitia TEA kwa mradi huu mkubwa na kuahidi kuendelea kutenga bajeti kubwa ya Elimu kwenye miradi ya maendeleo ili kupunguza changamoto za kwenye sekta ya Elimu.

Akitoa maelezo ya awali Mkurugenzi Mkuu wa TEA Bi. Bahati Geuzye amewata wadau wote wahusika wa usimamizi wa mradi huo kuhakikisha kazi yote inakmilika ndani ya miezi minne(4) ili kuwapa fursa wanafunzi kuanza kutumia miundo mbinu hiyo kwa wakati.

IMG-20210507-WA0006.jpg

IMG-20210507-WA0005.jpg

IMG-20210507-WA0008.jpg
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
49,061
2,000
Awashukuru na wakoloni kwa kutujengea barabara, reli, shule na makanisa.
 

Bunsen Burner

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
586
1,000
Sasahivi wajibu wa serikali umegeuzwa kuwa ni hisani
Yaani kweli aisee,huo ni wajibu wa serikali kuwahudumia wananchi na sio fadhila kwani pesa ya kazi ilyofanyika ni kutokana na kodi za wananchi. Ni wajibu siku zote wa serikali kuhakikisha hayo yanafanyika manake hata hao wafanyakazi hulipwa kutokana na kodi za wananchi.

Yaani mfanyakazi uwe unamlipa mshahara kwa huduma anayoitoa, halafu unalazimika tena kumshukuru kwani imekuwa fadhila....??? Kazi iendelee.
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
49,061
2,000
Yaani kweli aisee,huo ni wajibu wa serikali kuwahudumia wananchi na sio fadhila kwani pesa ya kazi ilyofanyika ni kutokana na kodi za wananchi. Ni wajibu siku zote wa serikali kuhakikisha hayo yanafanyika manake hata hao wafanyakazi hulipwa kutokana na kodi za wananchi. Yaani mfanyakazi uwe unamlipa mshahara kwa huduma anayoitoa, halafu unalazimika tena kumshukuru kwani imekuwa fadhila....??? Kazi iendelee.
Mwendazake alivyokuwa anasema nimetoa 60B sijui ngapi kama vile ametoa mfukoni kwake.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom