Sheikh wa Mkoa Mwanza (Kuhusu Mjadala wa Bandari): Walaaniwe wote wenye nia ovu na Rais Samia

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,925
30,273
TAMKO LA SHEIKH WA MKOA MWANZA KUHUSU MJADALA WA BANDARI

Utangulizi

Kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja kumekuwa na mjadala kuhusu uwekezaji na uendeshaji wa bandari zetu na kampuni kutoka Dubai. Mjadala ulianzishwa na wanasiasa na wanasheria lakini baadae ukachukua sura mpya na ya hatari ambayo nchi yetu haijawahi kushuhudia.

Hoja na mwelekeo wake

Wakati mjadala ulipoanza, hoja kubwa ilikuwa Wazanzibari wawili wanauza bandari za Tanganyika. Baada ya muda si mrefu, mjadala ukachukua sura mpya na kusisitizwa kuwa ni waarabu ndio waliouziwa nchi. Wakati mjadala unaendelea, ulihama kutoka sura ya kisiasa na kuingia udini.

Sote tumeshuhudia viongozi mbalimbali waandamizi wa dini ya kikristo walivyokuwa mstari wa mbele kupinga suala hili na wengine wamediriki kumkejeli Rais Samia Suluhu Hassan. Hii sio mara ya kwanza kwa viongozi wa dini ya kikristo kumkejeli Rais Samia.

Baadhi ya viongozi wa dini ya kikristo wamedai kuwa Rais Samia amevunja Katiba na kwa maana hiyo anastahili kuondolewa madarakani. Mmoja wao ameenda mbali zaidi kwa kutishia kufanyike Mapinduzi ya kumuondoa Rais Samia madarakani. Jambo la ajabu ni kuwa mpaka sasa hakuna hata mtu mmoja ambaye ameupinga mkataba wa bandari kwa hoja za kiuchumi.

Wote waliozungumza na hasa viongozi wa dini ya kikristo wamezungumza kwa jazba na kumshambulia Rais Samia bila sababu za msingi. Kama viongozi hawa wana uchungu na wananchi, tuliwatarajia kupaza sauti zao wakati wa utawala uliopita ambao tumeshuhudia watu wengi kupoteza maisha yao bila maelezo. Pia tumeshuhudia serikali iliyopita imeingia kwenye miradi mikubwa kinyume cha utaratibu. Sote ni mashahidi, hakuna kiongozi hata mmoja wa kiislamu aliyeushambulia uongozi uliopita.

Wito

Mimi ninaamini kuwa mjadala huu umetawaliwa na UDINI na una lengo la kumtoa Rais Samia madarakani kabla ya muda wake. Hivyo basi, kama sheikh wenu wa Mkoa, natoa wito kwa kila mwislam popote alipo katika Mkoa huu, afunge kwa siku 3 na katika kila swala ya Ijumaa kuanzia Ijumaa hii ya tarehe 7 Julai 2023 misikiti YOTE 700 ya Mkoa wa Mwanza isome dua ya kunuti kuwalaani WATU WOTE wenye nia ovu na Rais Samia.

Sheikh Hassan Kabeke ………………………………..

Sheikh wa Mkoa, MWANZA

Tarehe 6 Julai 2023
 
Shehe ubwabwa, amejaa naye kaingia kwa vile hata uelewa tu wa mambo hajui zaidi ya mihemuko, angejenga hoja juu ya mkataba angeonekana wa maana, hakuna mtu asiyetaka mwekezaji inshu ni mkataba, mkataba mbovu haufai kila mwenye akili na mwenye kuipanda hii nchi hawezi akakubali aina hii ya mkataba.
 
Shehe ubwabwa,amejaa naye kaingia kwa vile hata uelewa tu wa mambo hajui zaidi ya mihemuko,angejenga hoja juu ya mkataba angeonekana wa maana,hakuna mtu asiyetaka mwekezaji inshu ni mkataba,mkataba mbovu haufai kila mwenye akili na mwenye kuipanda hii nchi hawezi akakubali aina hii ya mkataba.
... lengo lake ni KIKRISTO; hayo mengine geresha tu.
 
Kweli ufinyu we elimu ni mzigo kwa hawa masheikh ubwabwa. Nayeye kaamka kwa kubwatuka na jazba pasina sababu za msingi wala hoja. Ni viongozi gani hao wa kikristo waliomtukana samia suluhu hassan au nae anazusha taharuki.

Sheikh inatakiwa ajue maslahi ya rasilimali za nchi sio swala la waislam au wakristo au wasio na dini bali ni suala la watanzania wote.

Ukosoaji wa uwekezaji huo sio kwa wakristo tu bali hata umma wa waislam nao hawaridhii mkataba huo.

Sheikh inatakiwa afahamu kuwa hata utawala wa bwana magufuli ulikabiliwa na ukosolewaji mkubwa kutoka Kwa viongozi wa kanisa. Pastor mwingira, pastor James makulo, wito wa Tec kwa serikali au sheikh alikuwa asikilizi kipindi hicho! Miradi mingi ilikosolewa ikiwemo ule uwanja wa chato hatukusikia anasema anakosolewa kisa ni mkristo.

Viongozi wa dini na watu baki baada ya mh. Lissu kushambuliwa kwa risasi na nchi kusimama kwa muda huku umma wote wa watanzania ukilaani huku kila mmoja wetu akitoa matamko sheikh huyo akuwepo!. Katika utawala uliokabiriwa na ukosolewaji mkubwa basi ni wabwana magufuli, amini mtu yule alikataliwa na mamilioni ya Watanzania lakini hakuna hata mmoja aliefungua kinywa na kusema anakosolewa kisa ni mkristo au kuna dalili ya udini kwene ukosoaji, huenda sheikh alikuwa kalala.

Umma wa watanganyika hauupingi uwekezaji bali unapinga aina ya mkataba kwa maana watu wanahitaji kujua mashali ya tanganyika katika mkataba. Ni suala dogo tu, Watu wanahitaji mkataba ulio na maslahi kwa taifa. Utampaje mtu uhuru wa bandari zote na hata zitakazo kuwepo si baharini tu hata ziwani au mtoni au iwapo kutatokea fursa za bandari basi DPW wajulishwe.

Suala hili halina chembe ya udini hata kidogo, bali kuna watu wanazusha taharuki za udini ikiwemo sheikh mwenyewe, tawala zote zilizopita zilikumbwa na ukosolewaji lakini watu hawakuona ukosoaji huo kwa minajili ya udini bali kwa maslahi mapana ya taifa.

Ni juzi tu rais Samia alipongezwa na kusifiwa na umma wa watanzania ikiwemo mamilioni ya wakristo nchini, hakuibuka mtu akasema wanamsifia kwasababu ni muislam, Leo kuna ukosolewaji ambao ni jambo la kawaida hata kwa tawala zote zilizopita gafla mtu anasema kuna udini, ohhhh watu wanataka mh raisi eti ajiuzuru, huu ni upuuzi na ujinga unaopaswa kupuuzwa na kila mtanzani mwene akili timamu.

Mtu akisifiwa watu wapo kimya, akikosolewa watu kwa vinywa tena vipana wanasema kisa ni muislam. Pumbafu.
 
Mohamed Said salam sheikh
Naanza kwa tahadhari kwamba unapoleta jambo ni vema ukajiridhisha na uthabiti wake.

Bandiko kutoka kwa Sheikh Hassan halibebi uzito sana isipokuwa kwa kuletwa nawe kwa umaarufu wako.
Chukua tahadhari ili usinasibishwe na 'mzigo' kwavile tu umesimama karibu nayo

Sheikh Said, sidhani kama Sheikh Hassan kafanya 'homework' yake vizuri na ikiwa ni hivyo kuna tatizo .

Kwanza, Hassan anasema hoja ilianza kwamba bandari za Tanganyika zinauzwa.
Ni kweli kwasababu Zanzibar imesema bandari zake hazihusiki hivyo zilizobaki ni za Tanganyika.
Neno bandari zimeuzwa linaweza kuwa na ' semantic '. Sheikh Hassan aelewe bandari zilihusu Tanganyika

Pili, kwamba MoU imesainiwa na Wazanzibar wawili, ni Ukweli na sahihi zipo. Kwanini Wazanzibar wanatajwa? Jibu, wizara husika si suala la muungano lakini kubwa zaidi ni kuondolewa kwa bandari za Zanzibar.
Wazanzibar wanaolalamika mambo ya muungano kuongezwa, wanaposaini yasiyowahusu inatia shaka.
Lakini pia wapo wataalamu wanahoji, sahihi ya Mwanasheria mkuu ipo wapi?

Tatu, Mh Mbowe alizungumza kwa kuchagua maneno yake kwa umakini mkubwa sana.
Kwa mtu aliyesikiliza video hakuna mahali alileta taharuki zaidi ya kutahadharisha kile alichokiona na kinachoweza kutafsiriwa kinyume na hali ilivyo. Ukiisikiliza video utabaini nia ovu ya wanaojaribu kuipotosha, sina hakika sheikh Said na Sheik Hassan wameiona na kuidurusu kwa kina na utulivu hiyo video!

Tatu, hoja ya bandari haikuanza na bandari za Tanganyika bali MoU iliyovuja kutoka serikalini na haikuwa katika ratiba za Bunge kwa mujibu wa Wataalam. Kuvuja huko na yaliyomo kumeibua hisia na mjadala mkali ukihusisha wanasheria, wanasiasa na hata viongozi wa dini zote akiwemo Sheikh Ponda.

Kwamba waliozungumza ni viongozi wa Kikristo, hilo si kweli kwani wapo wa dini zote na wana haki kama Raia wengine. Sheikh Hassan akitazama mijadala kwa jicho la dini hatakosa hoja hata siku moja kwasababu Tanzania ina dini mbali mbali na Raia wana haki ya kushiriki mijadala bila kutumia dini zao.

Nne,Kwamba viongozi wa Kikristo walikuwa kimya wakati wa utawala wa JPM, ni hoja yenye ukweli nusu.
Ukweli uliokamilika ni kwamba viongozi wa dini zote akiwemo sheikh Hassan walikaa kimya wakati uovu ukitendwa, watu kupigwa risasi au kuokotwa katika viroba.

Hivyo, kukaa kimya halikuwa suala la dini moja, lilikuwa la viongozi wote na hapa umma ulifikia mahali kutilia shaka uadilifu na uongofu wa viongozi wa dini kwa kushangilia na kuombea viongozi dua za biashara za madini na ujenzi wa madaraja bila kujali utu na uhai wa Raia wao. Sheikh Hassan anakumbuka vizuri hili

Tano, kwamba hoja haijaangaliwa kiuchumi si kweli. Sheikh Hassan anataka kuaminisha umma kwamba tatizo ni mkataba wa uchumi. Ukiwasiliza watu wote wakiwemo Wabunge hakuna anayepinga uwekezaji, watu wanapinga kilichomo ndani ya mkataba ambacho viongozi wa serikali wanapaswa kutetea kwa hoja.

Sheikh Hassan atakumbuka Bunge letu lilijadili kauli ya Mbowe zaidi badala ya Mkataba aui hoja za kiuchumi.
Tulitarajia Sheikh Hassan aanze kusota vidole kwa Bunge kuliko kushambulia watoa maoni kwa imani zao.

Sita, Bunge la JMT lina watu wa aina na imani zote. Bunge limepitisha Mswada bila kuangalia kingine, na hivyo Sheikh Hassan amekuwa na jicho chongo la kutoona Wabunge walioko ni akina nani.

Saba, kwamba Rais SSH anashambuliwa kwa udini ni hoja dhaifu . Sheikh atueleze ni Rais gani alipata ''immunity' ya kutoshambuliwa ? Urais ni taasisi inayobeba sera na maono ya Taifa.

Ni jambo la ajabu kama Rais awaye atapewa ufaulu tu kwa kuangalia jinsia, asili au dini.
Hilo halikuwepo na wenye fikra ongofu hawalifikirii hata kidogo.

Nane, inaonekana Sheikh Hassan alichukizwa na neno Tanganyika. Neno hilo linasemwa kila siku kule Zanzibar tena kwa indhara, kashfa na matusi, leo likitumiwa na Watanganyika linakuwa tusi! Sheikh Hassan na jicho chongo.

Tisa, kwavile Sheikh Hassan ameeleza kuna faida za kiuchumi, ni yeye mwenye dhima ya kueleza faida ni zipi.
Kutuhumu wanaotoa maoni tofauti na matarajio yake wakati hana alichoweka mezani si jambo sahihi.

Kumi, hoja ya Sheikh Hassan inajengwa katika misingi ya udini badala ya uhalisia. Sheikh arudi na kupitia video ya Mbowe, apitie mkataba na malalamiko ya wananchi wakiwemo viongozi wote wa dini, arejee katika mkataba na kufafanua vifungu vinavyolalamikiwa na aeleze faida za uchumi. Bila hayo andiko lake lina sura tofauti

Ni kwa msingi huo tunamshauri tena Mohamed Said kuwa mwangalifu wakati wa 'kubeba mizigo' ambayo mingine inachuruzika shombo na hivyo kuichukiza kanzu yake nadhifu achilia mbali kuweka mshangao kwa macho ya mamia ya Wapendwa wake wanaomtazama kwa mahaba, mfano na wivu mkubwa!

Mag3 Fundi Mchundo JokaKuu Pascal Mayalla
 
TAMKO LA SHEIKH WA MKOA MWANZA KUHUSU MJADALA WA BANDARI

Utangulizi

Kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja kumekuwa na mjadala kuhusu uwekezaji na uendeshaji wa bandari zetu na kampuni kutoka Dubai. Mjadala ulianzishwa na wanasiasa na wanasheria lakini baadae ukachukua sura mpya na ya hatari ambayo nchi yetu haijawahi kushuhudia...
Hivi mtu mwenye upeo kiduchu au AKILI-MBILIKIMO namna hii alipataje hiyo nafasi ya ushehe, achilia mbali ushehe wa mkoa?

Mtu mwenye akili ndogo namna hii ambayo inamtosha yeye mwenyewe katika kuvukia barabara tu hakupaswa kuchangia hoja yoyote kwenye mijadala pevu kama huu mjadala wa bandari, anapaswa akae kimya ili kutunza heshima yake kidogo iliyobakia.
 
TAMKO LA SHEIKH WA MKOA MWANZA KUHUSU MJADALA WA BANDARI

Utangulizi

Kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja kumekuwa na mjadala kuhusu uwekezaji na uendeshaji wa bandari zetu na kampuni kutoka Dubai. Mjadala ulianzishwa na wanasiasa na wanasheria lakini baadae ukachukua sura mpya na ya hatari ambayo nchi yetu haijawahi kushuhudia.

Hoja na mwelekeo wake

Wakati mjadala ulipoanza, hoja kubwa ilikuwa Wazanzibari wawili wanauza bandari za Tanganyika. Baada ya muda si mrefu, mjadala ukachukua sura mpya na kusisitizwa kuwa ni waarabu ndio waliouziwa nchi. Wakati mjadala unaendelea, ulihama kutoka sura ya kisiasa na kuingia udini.

Sote tumeshuhudia viongozi mbalimbali waandamizi wa dini ya kikristo walivyokuwa mstari wa mbele kupinga suala hili na wengine wamediriki kumkejeli Rais Samia Suluhu Hassan. Hii sio mara ya kwanza kwa viongozi wa dini ya kikristo kumkejeli Rais Samia.

Baadhi ya viongozi wa dini ya kikristo wamedai kuwa Rais Samia amevunja Katiba na kwa maana hiyo anastahili kuondolewa madarakani. Mmoja wao ameenda mbali zaidi kwa kutishia kufanyike Mapinduzi ya kumuondoa Rais Samia madarakani. Jambo la ajabu ni kuwa mpaka sasa hakuna hata mtu mmoja ambaye ameupinga mkataba wa bandari kwa hoja za kiuchumi.

Wote waliozungumza na hasa viongozi wa dini ya kikristo wamezungumza kwa jazba na kumshambulia Rais Samia bila sababu za msingi. Kama viongozi hawa wana uchungu na wananchi, tuliwatarajia kupaza sauti zao wakati wa utawala uliopita ambao tumeshuhudia watu wengi kupoteza maisha yao bila maelezo. Pia tumeshuhudia serikali iliyopita imeingia kwenye miradi mikubwa kinyume cha utaratibu. Sote ni mashahidi, hakuna kiongozi hata mmoja wa kiislamu aliyeushambulia uongozi uliopita.

Wito

Mimi ninaamini kuwa mjadala huu umetawaliwa na UDINI na una lengo la kumtoa Rais Samia madarakani kabla ya muda wake. Hivyo basi, kama sheikh wenu wa Mkoa, natoa wito kwa kila mwislam popote alipo katika Mkoa huu, afunge kwa siku 3 na katika kila swala ya Ijumaa kuanzia Ijumaa hii ya tarehe 7 Julai 2023 misikiti YOTE 700 ya Mkoa wa Mwanza isome dua ya kunuti kuwalaani WATU WOTE wenye nia ovu na Rais Samia.

Sheikh Hassan Kabeke ………………………………..

Sheikh wa Mkoa, MWANZA

Tarehe 6 Julai 2023
Mtaje huyo kiongozi aliyesema Rais apinduliwe.
 
Back
Top Bottom