BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 328
- 414
Mbunge wa Jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma, Dkt. Florence George Samizi akiambatana na mkuu wa wilaya ya Kibondo Agrey John Magwaza, leo tarehe 03/10/2023 amekuwa Mgeni rasmi katika zoezi la kampeni ya usajili wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5(0-5) ambao umefanyika katika Viwanja vya ofisi ya Kata - Kitahana.
Katika Uzinduzi huo amehudhuria Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Kibondo, Hamis Salum Tahilo na viongozi mbalimbali wa chama na serikali. Viongozi wote wamempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Saluhu Hassan kwa namna anavyoendelea kuwahudumia Watanzania na kuwasogezea wananchi huduma hii muhimu tena kwenye ngazi ya chini kabisa ya zahanati na kijiji.