Dkt. Samizi ashiriki kupokea madawati 50, washuhudia mamilioni ya Rais Samia ujenzi wa shule

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
Jana Jumatatu Septemba 25, 2023 Mbunge wa Jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma, Dkt. Florence George Samizi ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Col. Aggrey Magwaza pamoja Mkurugenzi wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Seka Urio katika mapokezi ya madawati 50 yenye thamani ya milioni tano kutoka NMB katika shule ya msingi Busunzu B.

Mgeni rasmi katika shughuli alikuwa DC Magwaza ambapo baadae walitembelea shule msingi mpya inayojengwa na serikali ya awamu ya 6 ambapo Rais Samia Suluhu Hassan ametoa jumla ya milioni 561 ambapo madarasa 16, matundu ya vyoo 21, na jengo la utawala vinaendelea kujengwa katika kijiji cha Nyankwi kata ya Busunzu.

Mbunge Samizi ameendelea kuishukuru serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa mambo makubwa anayoendelea kufanya Jimboni na kwa Taifa zima huku akiushukuru pia sana uongozi wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi hasa Meneja wa benki hiyo NMB tawi la Kibondo Bi. Asha Kwa ushirikiano anaotoa na kutoa misaada mbalimbali.

IMG-20230926-WA0036.jpg
IMG-20230926-WA0037.jpg
IMG-20230926-WA0038.jpg
IMG-20230926-WA0040.jpg
IMG-20230926-WA0039.jpg
IMG-20230926-WA0041.jpg
IMG-20230926-WA0041.jpg
IMG-20230926-WA0041.jpg
 
Back
Top Bottom