DKT. Samizi amshukuru Rais Samia kumtua Mama ndoo kichwani Muhambwe

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
Jana Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amefika Jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma kukagua miradi ya maji ambapo Mbunge wa Jimbo hilo, Dkt. Florence George Samizi amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Maji kwa namna wanavyofanikisha kumtua ndoo kichwani Mama na Wananchi wa Muhambwe.

Kwenye ziara hiyo, Waziri Aweso ameahidi kutoa pikipiki nane na gari moja kwa ajili ya shughuli za maendeleo kwenye sekta ya maji kwenye Jimbo la Muhambwe pamoja na milioni 300 kwa ajili ya kulipa deni la Umeme na milioni 200 kumalizia tanki la Maji Lita Milioni moja na laki tano kwenye mradi wa maji Muhambwe.

Hii unahusisha ujenzi wa chujio wenye gharama ya milioni 560 ambao umebadilisha maji katika Jimbo la Muhambwe kutoka majitaka mekundu kwenda maji meupe masafi na salama.

Pili, uwezeshaji wa Mradi wa pili utakaohusisha uzinduzi wa maji kijiji cha Kitahana wa milioni 360

Wananchi wa Muhambwe wamemshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyozidi kumtua Mama ndoo kichwani.

IMG-20230720-WA0027.jpg
IMG-20230720-WA0026.jpg
IMG-20230720-WA0025.jpg
IMG-20230720-WA0023.jpg
IMG-20230720-WA0024.jpg
IMG-20230720-WA0022.jpg
IMG-20230720-WA0021.jpg
IMG-20230720-WA0020.jpg
IMG-20230720-WA0019.jpg
IMG-20230720-WA0017.jpg
IMG-20230720-WA0016.jpg
 
Back
Top Bottom