Dkt. Samizi aungana na wanamichezo kusaidia wenye uhitaji na kumuunga mkono Rais Samia

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
329
414
Jana Jumapili imekua siku nzuri kwa Mbunge wa Jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma, Dkt. Florence George Samizi kufurahi na wananchi wake wa Jimbo la Muhambwe ambapo alipata mwaliko wa uzinduzi wa tawi la Yanga SC pale Mukabuye.

Uzinduzi wa tawi hilo la Yanga SC umekuwa na shangwe na umati mkubwa sana wa watu ambapo Mbunge pamoja na mashabiki na wanachama wa Yanga walisaidia wahitaji, kupata chakula cha pamoja na kushuhudia mechi ya mpira wa miguu kati ya kata ya Mukabuye na kata ya Nyaruyoba.

Mbunge amefurahishwa na malengo mazuri ya tawi hilo ikiwamo Bima ya afya, kusaidiana kama wanachama, kujitolea kilimo cha pamoja na mengine mengi.

Mashabiki na wanachama wamemuahidi Mbunge Samizi kuendelea kuiunga mkono serikali yao ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan huku akiwashukuru waandaji wote kwa kumkaribisha kuzindua tawi hilo la Yanga la Mukabuye.


IMG-20230925-WA0046.jpg
IMG-20230925-WA0043.jpg
IMG-20230925-WA0044.jpg
IMG-20230925-WA0042.jpg
IMG-20230925-WA0041.jpg
IMG-20230925-WA0045.jpg
 
Back
Top Bottom