Dkt. Ndugulile: Uchaguzi wa 2020 ulikuwa na dosari ambayo hatuwezi kuificha, siungi Mkono kupita bila kupingwa

Kassim Majaliwa alipita bila kupingwa
2025 kama hajastaafu kuanza kula fuba la Waziri mkuu mstaafu, atashindanishwa.

Lakini mbinu alizozitumia 2020, ili kuwafanya waliokua na nia ya kugombea, warudi nyuma, ndiyo mbinu hizo hizo atakazozitumia akitaka kuendelea kuula uheshimiwa.

Mwenye kazi ya ziada ni Mbunge Kigwangala wa Nzega vijijini, maana raia washachoka naye.

ye'alikuwa akihonga wenye nia wanatoroka bila hata ya kurejesha fomu.
 
"Uchaguzi wa 2020 ulikuwa na dosari ambayo hatuwezi kuificha, haiwezekani wagombea wa upinzani tu ndio hawakujua kujaza fomu ipasavyo halafu wagombea wa CCM wakaweza kujaza fomu ipasavyo kila mahali” Dkt. Faustine Ndugulile.

Ndugulile amesema haungi mkono suala la wagombea kupita bila kupingwa “Mtu kama unajiamini kwa nini upite pasipo ushindani..?”

Hata hivyo Ndugulile amesema alikuwa na uhakika wa kuwashinda wapinzani wake kwenye uchaguzi wa ndani ya CCM akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw Paul Makonda, ambaye kwa sasa ni katibu muenezi wa CCM Taifa.

“Mimi sijawai kuwa na uchaguzi rahisi kigamboni na uwa sipendi uchaguzi mwepesi, hata 2015 niligombea na vigogo wengi akiwemo mtoto wa Rais Mkapa lakini nilishinda” Ndugulile.

Msg imefika, Mama 2025 hakuna kugombea peke yako,watu wanaanza kum challenge Mama na form yake moja ya urais!!
 
"Uchaguzi wa 2020 ulikuwa na dosari ambayo hatuwezi kuificha, haiwezekani wagombea wa upinzani tu ndio hawakujua kujaza fomu ipasavyo halafu wagombea wa CCM wakaweza kujaza fomu ipasavyo kila mahali” Dkt. Faustine Ndugulile.

Ndugulile amesema haungi mkono suala la wagombea kupita bila kupingwa “Mtu kama unajiamini kwa nini upite pasipo ushindani..?”

Hata hivyo Ndugulile amesema alikuwa na uhakika wa kuwashinda wapinzani wake kwenye uchaguzi wa ndani ya CCM akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw Paul Makonda, ambaye kwa sasa ni katibu muenezi wa CCM Taifa.

“Mimi sijawai kuwa na uchaguzi rahisi kigamboni na uwa sipendi uchaguzi mwepesi, hata 2015 niligombea na vigogo wengi akiwemo mtoto wa Rais Mkapa lakini nilishinda” Ndugulile.

Heri yenu mnaotambua na kukubali mapungufu yaliyojitokeza kwenye uchaguzi uliopita.lakini kwa namna moja au nyingine bado haiingii akiliini.ilikuwa vipi mkakubali dhambi hii?
 
Mbunge ni mpaza sauti tu, mleta maendeleo ni serikali.
Ndungulile sio bubu bungeni, anatetea mengi ya kigamboni
😂 Kumekucha.. yan kwa ulivyomtafsiri mbunge kirahisi hapo sidhani kama kungekuwa na umuhimu wa wabunge wa majimbo serikalini! Yan wangekuwa wanakutana wenyekiti na wangepaza sauti vizur kabixa kama ndio wabunge kazi yao n kupaza tu sauti...

We ndug yang kama n mkazi wa kigamboni mpe mitano tena! Ila kiukweli hana anachofanya kama mbunge wa hili jimbo tukamsifia
 
Makonda alipata kura nyingi kuliko Ndugulile ila Shujaa Magufuli akavuta waya na kuagiza Faustine awe namba 1 😂🔥

Hata yeye anajua hili
Magu alisimamia msimamo kuwa kama kakupa nafasi kisha ukajitia tamaa kugombea nafasi nyingine haupati.

Faustine anajitia kiburi tu..ila 2025 atamkumbuka Magu..pale wajumbe watakapomuambia bila millioni 00 asijisumbue kugombea..
 
Hata Samia nae watamkana.

Watakuja kusema ukopaji wa fedhs awamu ya Sita haukuwa unafuata sheria za fedha.na watamshushia tambala bovu

The only way ni wote hawa wakae pembeni.
Ila kila nikikumbuka upinzani nakosa nguvu

Upinzani huu wa mbowe ? Lema , ZZK? Wazee wa bahasha za kaki
 
"Uchaguzi wa 2020 ulikuwa na dosari ambayo hatuwezi kuificha, haiwezekani wagombea wa upinzani tu ndio hawakujua kujaza fomu ipasavyo halafu wagombea wa CCM wakaweza kujaza fomu ipasavyo kila mahali” Dkt. Faustine Ndugulile.

Ndugulile amesema haungi mkono suala la wagombea kupita bila kupingwa “Mtu kama unajiamini kwa nini upite pasipo ushindani..?”

Hata hivyo Ndugulile amesema alikuwa na uhakika wa kuwashinda wapinzani wake kwenye uchaguzi wa ndani ya CCM akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw Paul Makonda, ambaye kwa sasa ni katibu muenezi wa CCM Taifa.

“Mimi sijawai kuwa na uchaguzi rahisi kigamboni na uwa sipendi uchaguzi mwepesi, hata 2015 niligombea na vigogo wengi akiwemo mtoto wa Rais Mkapa lakini nilishinda” Ndugulile.

Ni kweli uchaguzi ulikua na dosari. Lakini ili tumuone ana nina njema atoe hoja Bungeni sheria ya uchaguzi iboreshwe. Nje ya hapa anatafuta kiki kwa jambo linalojulikana tayari.
 
Kweli kabisa,vitendo hivi vilikuwa vinaumiza sana kwani maamuzi ya wajumbe kumpitisha mgombea wanayemtaka yalidharauliwa na kukoswa mantiki ya kuwa wajumbe katika mchakato mzima wa kura za maoni.
 
Naamini haya ya 2020 hayatajirudia tena kwani CHAMA kinaonekana kinawenyewe,wenye kutaka namtaka mtu fulani nifanye naye kazi na ikawa.Hivyo tunakiomba CHAMA chetu tawala waone kuwa hayo yalikuwa ni mapungufu makubwa sana yasijirudie kwani yananaharibu taswira ya CHAMA na mtu kujiona kama mnyonge asiyefaa kupata nafasi ya kuchaguliwa nakuchagua kiongozi anayemfaa kumtumikia kwenye jamii yake.
 
Kaongelea uchaguzi wa ndani huko CCM, huku nje angeshindaje na tuliambiwa CHADEMA walishinda ndio maana matokeo yakaamuliwa nchi nzima CCM ishinde.
 
Back
Top Bottom