Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566

Ili kuiwezesha Nchi kuwa na Sera za Kodi zinazotabirika na kuweka mazingira bora ya uwekezaji, Serikali imependekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Ushuru Kwa kuanzisha utaratibu wa kurekebisha viwango vya Ushuru wa Bidhaa kila baada ya miaka mitatu (3)

Kuanzia mwaka wa fedha 2023/24 kutakuwa na msamaha wa Bidhaa unaotozwa kwa mujibu wa uwezo wa Injini (Engine Capacity) kwenye magari yanayotumia Nishati ya Umeme pekee yanayotambulika kwa HS Code 8702.40.11; 8702.40.19; 8703.80.10; na 8703.80.90 pamoja na magari yanayotumia Nishati ya Gesi Asilia (CNG) pekee

Lengo la hatua hii ni kuhamasisha matumizi ya nishati ya umeme na gesi asilia nchini na hivyo kuokoa matumizi ya fedha za kigeni inayotumika kuagiza nishati ya mafuta kutoka nje ya nchi.
 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba leo June 15,2023 amewasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 Bungeni Jijini Dodoma ambapo moja ya mambo aliyoyapendekeza kwenye hotuba yake ni kusamehe ushuru wa bidhaa unaotozwa kwa mujibu wa uwezo wa injini (engine capacity) kwenye magari yanayotumia nishati ya umeme pekee yanayotambulika kwa HS Code 8702.40.11; 8702.40.19; 8703.80.10 na 8703.80.90 na magari yanayotumia Nishati ya Gesi Asilia (CNG) pekee.

“Lengo la hatua hii ni kuhamasisha matumizi ya nishati ya umeme na gesi asilia nchini na hivyo kuokoa matumizi ya fedha za kigeni inayotumika kuagiza nishati ya mafuta kutoka nje ya Nchi”
 
Kama unafuatilia budget iliosomwa leo, kuanzia July 1, 2023; magari ya umeme na gesi hayatakua na kodi.

Karibu kwa ushauri kwa wenye uzoefu eneo hili, gari gani bora, linaloenda umbali mrefu na muda wa kuchaji.
 
Kama unafuatilia budget iliosomwa leo, kuanzia July 1, 2023; magari ya umeme na gesi hayatakua na kodi.

Karibu kwa ushauri kwa wenye uzoefu eneo hili, gari gani bora, linaloenda umbali mrefu na muda wa kuchaji.
Tesla
 
Kila mtanzania akichangia elfu 2 tu tutapata pesa ya kutosha kuendeshea na kununulia mashine za kisasa kuweza kuendesha bandari yetu badala ya kuwauzia warabu milele.

Watanzania walioaminishwa na Hayati Magufuli kwamba wanaweza na nchi yao ni tajiri na wakaanza kujenga miradi ya matrillioni ya fedha kama ndege, SGR, bwawa la umeme, kuhamia Dodoma, elimu bure, madaraja marefu Afrika mashariki na ya kati etc, ghafla sasa upepo umebadilika viongozi wote wanahubiri watanzania hawawezi na hawajiwezi kwa lolote kabisa! Bunge linasema kila kitu kipitishwe kwa sababu watanzania hawana uwezo wa kifedha wala akili ya kuendeleza miradi mikubwa kama ya bandari. Wapo pia wanasema hata taasisi za bunge na urais nazo zibinafisishwe ili ziweze kutoa matokeo chanya na ya haraka kwa wananchi.
 
Back
Top Bottom