Dkt. Massaga: Uzalishaji Maji tiba Hospitali ya Bugando kuokoa fedha ambazo zingetumika kununua maji tiba kutoka sehemu nyingine

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
F500Xw9WoAAJjIc.jpeg

Idara ya famasi imefanya maboresho makubwa kupitia kitengo cha uzalishaji maji tiba, (Infusion Unit).

Akizungumza katika makabidhiano Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, Dkt. Fabian Massaga amewapongeza Idara ya Famasi kwa jitahida kubwa wanazofanya ili kuongeza uzalishaji na kuipunguzia Hospitali gharama za kuagiza maji tiba nje kwa gharama kubwa.

Dkt. Massaga ametoa wito kwa viongozi na wanaidara kwa jumla kutunza mitambo mipya pamoja na sehemu zilizofanyiwa ukarabati bila kusahau kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni na miongozo ya nchi.

Ameeleza adhima ya Taasisi hapo baadaye kuwa na kiwanda kikubwa cha uzalishaji maji tiba kwa kutumia teknolojia mpya “Sisi kama Hospitali ya Rufaa ya Kanda, tunaowajibu wa kuhakikisha wagonjwa wanapata tiba stahiki na kwa wakati pia kuokoa gharama za matibabu kwa wananchi, kitengo hiki cha maji tiba kinazalisha kwa asilimia 90, ya mahitaji ya maji tiba ndani ya hospitali, kwa kuwa tunaendelea na maboresho mbalimbali niombe Wadau kushirikiana nasi tuweze kutumia teknolojia mpya ili kuongeza uzalishaji zaidi.”
F500aNnWMAA1Pkd.jpeg

Pia Dkt. Massaga ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kutupa kibali cha kufanya ubunifu wenye tija katika uboreshaji wa Huduma za Afya katika taasisi zetu, kwani ubunifu huu utaipunguzia Serikali mzigo wa kununua dawa na vifaa tiba kutoka nje ya nchi, pia itapunguza gharama za matibabu kwa Mwananchi.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Uzalishaji Maji Tiba, Mfamasia Deus Sinibagiye amesema: “Tumeongeza uzalishaji kutoka Chupa 400 hadi chupa 720 kwa siku, tumefikia vigezo vya TMDA na hivyo kuruhusiwa kuzalisha na kuuzia taasisi nyingine ndani ya nchi, tumepunguza tatizo la ukosefu wa maji tiba ambayo hayapatikani kirahisi sokoni mfano Hypertonic saline 3%, Dextrose 50%, Dextrose 25%, Neonatal fluids, Methylene blue pamoja na distilled water kwa matumizi ya mashine za maabara, Kitengo cha Saratani na Endoscope.
F500YPvXcAAvmlq.jpeg

“Pia tumeipunguzia taasisi gharama za manunuzi ya maji tiba ambayo kwa wastani Chupa moja hununuliwa kati ya Shilingi 850 hadi 950 kutegemea aina ya maji,” amesema Mkuu wa Kitengo.
 
Back
Top Bottom